Mtunzi: Omary John Mndambi
SEHEMU YA AROBAINI NA TANO
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Alipofika alienda moja kwa moja hosteli kwao kwani giza lilikuwa limeshaingia, alimpigia Simu na kumuomba atoke waonane.
IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI
TUENDELEE...
“Vipi kaka mbona Kimya kimya leo, hata kuntaarifu kabla kwema kweli“
“Kwema tu, vipi masomo yanaendaje?”
“Yako poa, ”
“Ingia kwenye gari tukaongee kidogo”
Glory ambaye ni mdogo wake Sam aliingia kwenye gari kisha wakaondoka wakaelekea kwenye sehemu inayouzwa vyakula na vinywaji wakakaa humo.
“Nipe Whisky alafu msikilize na huyu” Sam aliagiza Pombe
“Naomba savannah ya Baridi” aliagiza Glory.
“Agiza chakula unachotaka ule”
Glory aliagiza Chipsi Kuku kisha wakaendelea kunywa na kuzungumza…
“Vipi Wifi hajambo?”
“Hajambo yupo”
“Mbona leo hujatoka nae?”
“Anasema amechoka”
Waliendelea kunywa hadi pale chakula kilipoletwa wakala na kuendelea kunywa, Sam alikuwa amemaliza ile Whisky na sasa alikuwa anakunywa nyingine.
“Mdogo wangu mimi naenda kozi huko Israel”
“Haaa hongera sana kaka”
Sam alimuachia mdogo wake kadi zake za benki na PASSWORD zote akamuelekeza kisha akamrudisha hostel na kuondoka zake.
Kesho yake alielekea kazini na kuchukua kila kilichotakiwa na kuanza safari yake ya Dar es Salaam ili apae kwenda Israel.
Safari yake ya Dar es Salaam ilieda vizuri na hatimaye akawa yuko ndani ya ndege ya shirika la ndege la Qatar anaelekea Israel.
Safari yake ilichukua siku nzima na nusu na hatimaye akashuka kwenye uwanja wa ndege wa Jerusalem na kupokelewa na wenyeji wake kwa ajili ya kozi kuanza.
Hakutaka kabisa kukumbuka mambo ya nyumbani maana yalikuwa yanampa kizungumkuti, aliyemkumbuka ni mdogo wake tu.
……………………………..
Kule hospitali Rafiki aliendelea kupatiwa huduma na hatimaye akawa amezinduka. Aliangaza huku na kule kisha akagundua kuwa yuko hospitali akaanza kurudisha kumbukumbu zake nyuma akawa amekumbuka kila kitu na machozi yakawa yanammwagika.
Nesi aliyekuwa zamu baada ya kumuona kaamka alienda kumuita Doctor ambaye alikuja moja kwa moja pale alipolazwa Rafiki.
“Pole dada, unajisikiaje?”
“Najisikia vizuri”
“sawa sasa pumzika, tumegundua kuwa mimba yako ilikuwa inatishia kutoka ila tumeidhibiti kwa hiyo unatakiwa upate mapumziko muda wote wa Mimba yako kwani inaonekana iko kwenye riski ya kutoka”
Baada ya Rafiki kusikia vile machozi yalizidi kummwagika…
“Usilie na usijipe mawazo kwani kwa mimba ya aina hii hutakiwi kuwa na stress, naomba umpigie mme wako simu aje”
Rafiki alivyosikia jina la Mme wake alizidi kuumia na machozi yakammwagika zaidi, hakuwa na jinsi aliomba simu ili ampigie mme wake lakini kila alipopiga ilikuwa haipatikani….
Hisia mbaya sana zilimjia kuhusu mme wake, alijua lazima mme wake ameamua maamuzi mabaya, hofu ilimjaa moyoni akajikuta anaemia sana…
Glory akiwa chuoni siku moja aliishiwa fedha ya stationary akaamua kwenda kuchukua fedha kwenye akaunti ya kaka yake.
Alipofika alitoa shilingi laki moja kwenye ATM kisha akachukua risiti na kutoka nje ili arudi chuoni, akiwa kwenye bodaboda alijiuliza jambo flani.
Iweje kaka yake amuachie kadi zake za benki ili hali mkewe yupo? Alipata wasiwasi na kwasababu hakutaka kuingia kwenye mgogoro na wifi yake aliamua kumtafuta kwenye simu ili amrudishie zile kadi na akitaka fedha basi atamuomba wifi yake.
Alichukua simu akatafuta namba ya wifi yake ambayo aliisevu “mke wangu” akaipiga lakini haikupatikana.
Aliipiga tena na tena lakini haikupatikana pia, hapo hapo alimwambia Yule bodaboda ageuze pikipiki ampeleke nyumbani kwa kaka yake.
“Utaniongeza buku lakini”
“usijali”
Pikipiki ilienda mpaka nyumbani kwa kaka yake akashuka nje ya geti akagonga na kuingia ndani, alimkuta mlinzi pale kwenye kibanda chake akasalimiana nae na kuingia ndani.
Kule ndani alimkuta msichana wa kazi ambaye alimuuliza alipo wifi yake akamjibu kuwa aliondoka na Kaka yake kwenda hospitali lakini hajarudi hadi muda ule.
Hapo hapo Glory wasiwasi ulimzidia, alijiuliza kwanini mambo yawe hivyo, siku aliyotajiwa kuwa kaka yake alimpeleka mkewe hospitali hadi kufikia siku ile ni kama wiki imepita.
“Ina maana wifi kalazwa siku zote hizi na mbona kaka hajaniambia?” alizidi kujiuliza maswali.
“alipelekwa hospitali gani?”
“Sijui”
“Ina maana hujawahi kwenda kumuangalia?”
“Sijawahi kuambiwa niende kumuangalia”
Glory baada ya kusikia hivyo hakutaka kusubiri zaidi, alienda moja kwa moja kwenye hospitali ambayo huwa wanaitumia sana mara kwa mara ili kujaribu bahati kama atamuona wifi yake.
Alipofika alipita moja kwa moja mapokezi na kuulizia kama kuna mgonjwa mwenye jina la Rafiki Mndeme…
“Ngoja niangalie”
Yule nesi wa mapokezi alipekua kwenye daftari lake kisha akauliza tena…
“Ameletwa lini hapa?”
“Ahhhh … kama wiki moja hivi imepita”
“Anhaaa kama ni huyo yuko wodi ya Sokoine nenda utamuona”
Haraka haraka Glory alipiga hatua kuelekea kwenye wodi aliyotajiwa, alipofika aliangaza macho yake kwenye baadhi ya vitanda huku akitoa pole kwa baadhi ya wagonjwa aliowaona wamelazwa pale.
“Poleni jamani”
“asante”
Kila alipokuwa anapita alikuwa anatoa pole…
Hatimaye alifika kwenye kitanda ambacho alimuona Verity amekaa akajua hapo alipokaa lazima ndipo alipo Rafiki kwani hawa ni mtu na dada yake.
Aliwaendea akakuta wakiwa wanaongea taratibu kisha akawasalimu, walishtuka sana kumuona lakini kwa hali ya kushangaza Verity aliachia msonyo mkubwaaa ambao ulimshtua sana Glory…
“Mchyuuuuuuuuuu” baada ya kutoa huo Msonyo aligeuza shingo yake kando.
Rafiki yeye hakuweza kusema chochote isipokuwa alilengwa na machozi tu….
“Jamani mke wangu…yani unalazwa hospitali hata huniambii mmeo jamani…” aliongea Glory huku akikaa kitandani na kumshika wifi yake mkono…
Hapo hapo Verity aliamka na kuchukua pochi yake…. “Dada nitakuja badae madikteta wako wakiondoka”
Kauli hii ilimshtua Glory lakini hakujali….
“Wifi mbona sielewi, unaumwa nanini?”
Rafiki kwa mara nyingine hakuweza kujibu kitu akabaki anatokwa machozi tu, Glory alihisi jambo ambalo sio la kawaida akakaa vizuri akamshikilia wifi yake viganja na kuwa anavisugua sugua.
“Niambie wifi yangu, nyamaza usilie niko hapa kwa ajili yako…”
“Wifi Glory…!”
“Niambie Mke wangu”
“Kaka yako ana roho ngumu sana…!”
“Basi wifi, naomba usiniambie kwasasa, ugua kwanza upone tutaongea yote wifi, naomba unipe dakika moja narudi”
Glory alienda moja kwa moja mpaka kwa dokta wa zamu ili ajue ninini kinamsumbua wifi yake mpaka akalazwa pale…
“Umesema ni nani yako Yule…?”
“Ni wifi yangu…mke wa kaka yangu kabisa”
“Mlikuwa wapi siku zote mpaka anabaki hana wa kumhudumia?”
“Mimi sikujua kwasababu niko chuo nasoma, hata leo nimebahatisha tu baada ya kurudi nyumbani na kumkosa kwani mme wake ameenda masomoni nje ya nchi”
“Sawa…wifi yako ana Mimba ambayo inatishia kutoka, hivyo yuko Bed Rest hadi tutakapokuwa na uhakika wa hali yake, ama kama kuna mtu wa kumhudumia nyumbani bila yeye kufanya kazi yeyote tunaweza kumruhusu…”
“Sawa, ngoja mimi nikaongee nae…”
Glory akiwa anajisikia hatia sana kwenye moyo wake alirudi pale alipolazwa wifi yake na kukaa tena kitandani.
Alimsihi sana wifi yake kuwa akubali kurudi nyumbani kwani atahama hosteli na kukaa nyumbani ili amhudumie…
Ilikuwa ngumu sana kwa Rafiki kukubali lakini mwisho alikubali na hivyo taratibu za kuruhusiwa zilipokamilika waliondoka kurudi nyumbani.
Walipofika nyumbani Glory alihakikisha wifi yake anaoga na kula vizuri kisha akachukua nguo chafu za wifi yake akazifua, akasafisha chumba vizuri na kuhakikisha kila kitu kiko sawa ndipo akaenda kukaa na wifi yake ili waongee haswa nini kilichotokea.
Wifi mtu hakuacha neno, alisimulia kila kitu kilichotokea mpaka akajikuta amelazwa hospitali na kuachwa bila msaada. Sio siri maelezo yale yalimchoma sana Glory na kujikuta akilia.
Hakuamini kuwa kaka yake ndio anaweza kuwa na roho ngumu kiasi kile…
“Kaka Sam ndio ana roho ngumu ngumu kiasi hicho?”
“Basi wifi…usilie wewe tulia tu, mungu yupo upande wako na wala usilalamike. Nipo kwa ajili yako na hata kaka atajirudi tu”
“Yani wifi isingekuwa wewe nilishaamua niondoke zangu pindi tu nitakapokuwa buheri wa afya, hata hivyo sijui atarudi na lipi?”
“Usitie shaka wifi kwani hata hizi kadi zake za benki aliniambia nikupe” hapa Glory ilibidi adanganye.
………………………….
Sam alikuwa amemaliza miezi mitatu akiwa Israel, na alikuwa kwenye hatua za mwisho za kumaliza kozi yake na kwa wakati wote huo hakupiga simu nyumbani kuulizia hali za huko.
Moyoni mwake alikuwa na kinyongo kikubwa mno cha kuhisi amesalitiwa na mke wake na Hawara yake (NISHA) wote kwa pamoja.
Aliwalaani wanawake na kuwaona mashetani, iweje najijua kabisa kuwa nina matatizo alafu niembiwe nimewapa Mimba…?
Siku hiyo kwasababu walikuwa off aliamua kwenda kwenye hospitali bora ili aangalie afya yake ya Uzazi kwani aliamini kule kuna hospitali bora zaidi.
Kwakuwa alikuwa raia wa kigeni ambaye alikuwa anaishi kwa kibali maalumu alipewa kipaumbele na hata huduma yake ilikuwa bora kabisa.
Ndani ya dakika kadhaa aliitwa kwa ajili ya majibu ya vipimo ambayo yalimshtua sana, Dokta aliyempa majibu alishangaa kwa kuona Sam ameduwaa huku yeye alitegemea kuwa angemkuta akiwa mwenye furaha lakini ilikuwa tofauti.
“Ina maana nilishapona? Ina maana hata zile mimba inawezekana ni za kwangu?” alijiuliza maswali ndani yakichwa chake…
………………………….
Miezi mitatu ilikuwa imekatika kama utani ambapo ilikuwa ni wakati wa Verity kuhudhuria kliniki, kwakuwa inapaswa kwenda Kliniki na mme wake, Gwakisa hakusita kuambatana na mke wake ili wahudhurie wote kliniki hususani hii ya kwanza.
Ndani ya gari Gwakisa alikuwa amefungulia mziki wa taratibu akisikiliza wimbo ulioimbwa na Mark Antony…. ‘You Sang to me’
Ndani ya moyo wake alikuwa na furaha ya kutosha kwani aliamini kwa umri wa Mimba ya mkewe uliofiikia ni muelekeo mzuri wa ukuaji wa mimba.
Alijiona akiwa na dalili za kuitwa Baba ndani ya miezi kadhaa ijayo na hiyo ilitosha kabisa kumfanya ajione mwanamme kamili.
“Umekaa sawa sweetieee” aliuliza Gwakisa kabla ya kuondoa Gari…
“Mh twende bhana…” alijibu Verity
Safari ya kwenda hospitali ilianza ambapo Taratibu na kwa mwendo wa pole Gwakisa aliendesha gari akihofia kumuumiza mtoto wake aliye tumboni huku akijitahidi kukwepa mashimo.
Hatimaye walifika hospitali na kukaa kwenye foleni ambapo baada ya muda kidogo alikuja Nesi na kutoa tangazo…
“Walioambatana na waume zao wasogee mbele”
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
JIUNGE KWA UPDATE NA BURUDANI ZAIDI
WhatsApp Channel=> CnZ Media(Follow)
Telegram Channel=> CnZ Media(Join)