MAMA ALISHIKWA KALIO MBELE YANGU (46)

0

SEHEMU YA AROBAINI NA SITA
TULIPOISHIA...
Hatimaye walifika hospitali na kukaa kwenye foleni ambapo baada ya muda kidogo alikuja Nesi na kutoa tangazo…
“Walioambatana na waume zao wasogee mbele”

IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI

TUENDELEE...
Verity na Gwakisa walinyanyuka na kusogea mbele na kujikuta wakiwa wa Kwanza kwenye foleni na kisha kuingia ndani…
“Hongera sana Baba kwa kuambatana na mkeo…”
“Asante sana, mimi ni mwanaume ninayetambua wajibu wangu…” alijibu Gwakisa kwa mbwembwe…
Haya kabla ya kila kitu itabidi mpime afya zenu wote kwa pamoja…

Sam alijiona mwenye hatia sana, aliumia moyoni kwa jinsi ambavyo amemtenda mkewe huku akiwa hana hatia,
“Hivi huyu mwanamke atanielewa kweli? Hii ni mara ya ngapi namfanyia ukatili wa kutisha kiasi hiki?”
Sam alijiuliza mwenyewe bila kupata majibu ya wapi anakoitoa roho mbaya kiasi hicho.
Alijiuliza ataingia na gia gani kwa mkewe mpaka amuelewe,
“Hivi ni mzima wa afya lakini, alikufa ama alipona” haya ni maswali ambayo Sam alikuwa anaendelea kujiuliza peke yake.

“Ngoja nimtafute Glory”
Alichukua simu yake akaitafuta namba ya Glory na kuipiga, alipiga zaidi ya mara tano lakini ilikuwa haipatikani.
Hofu ilikuwa kubwa kwani alitamani sasa ajue kuhusu hali ya nyumbani kwani ameshajua kuwa yeye ndie mkosaji.

Mawazo yalikuwa yanapita na kurudi kisha likaja la kumtafuta mkewe…
Huku mapigo ya moyo yakienda mbio alianza kuipiga namba ya mke wake lakini hali ilikuwa kama kule kwa Glory, nayo ilikuwa haiko hewani.
Alizidi kuumia kwa mara nyingine, hapo hapo akili yake ikamkumbuka “NISHA”
“Ah ngoja nimpigie na huyu nione”

Alitafuta namba ya Nisha akaipiga na kwa bahati nzuri ikawa inaita, ndani ya sekunde kadhaa ikapokelewa
“haloo”
“Nani Mwenzangu?”
“Samahani naongea na NISHA?”
“ndio wewe ni nani?”
“Oh Nisha, mimi SAM”
“Mchyuuu, ukome kunipigia!” hapa Sam alishtuka vilivyo.
“Unasemaje NISHA?”
“Nasema hivi ukome kunitafuta, na nakwambia utanijua mimi ni nani”
Baada ya NISHA kusema hivyo akakata simu na kuizima kabisa, Sam alijaribu kuipiga tena na tena lakini ilikuwa haipatikani akajua imezimwa.

Hofu ilianza kumjaa alijiuliza ikiwa NISHA tu ambaye sio mke wake lakini amekasirika kiasi hicho itakuwaje kwa Rafiki.

Aliamua tena kumtafuta Mdogo wake (Glory)
Furaha ililipuka ghafla baada ya kusikia simu ya mdogo wake ikiita…
“Glory mdogo wangu”
“Shkamoo kaka”
“Marahaba habari za huko?”
“Nzuri tu…”
“Mbona nimekupigia ulikuwa hupatikani?”
“NIlikuwa kwenye mtihani”
“Mbona unajibu shoti shoti kiasi hicho”
“Hapana niko sawa tu”
Sam aligundua kuwa hata mdogo wake alikuwa na hasira nae, hapo ilibidi ahoji vizuri.
“Glory niambie ukweli una tatizo gani?”
“Sina tatizo kaka ila nawaza tu kuwa kwa ukatili unaomfanyia wifi ipo siku utauhamishia hata kwangu”
Hapo sasa Sam alielewa anachomaanisha Mdogo wake…
Ilibidi Sam amuelezee Glory kinagaubaga chanzo chakile alichokifanya, alijieleza mno kuanzia matatizo yake na jinsi ambavyo alihisi kuwa anachakachuliwa,
Kwa mbali Glory alimuelewa lakini alimlaumu kwanini anachukua maamuzi bila kutafakari kwanza…
“Hivi kwa mfano kama ungemuua unahisi nani angekuelewa?”
“Nisamehe mdogo wangu, naomba unisamehe sitorudia tena”
“Sasa kaka naomba tu nikwambie ukweli … Wifi alifariki”
“Unasemaje Glory”
“Ndio kaka Wifi alifariki na ameshazikwa”
“Kaka, kaka ….” Glory aliita lakini ukimya ulitanda kaka yake hakujibu kitu na hatimaye simu ilikatika.
Alijaribu kuipiga tena lakini ilikuwa haipokelewi, Glory alianza kujuta kwanini kamdanganya lakini alipotaka amwambie ni uongo simu ilikuwa haipokelewi na badae ikawa haipatikani kabisa.
………………………..
Sam baada ya kusikia ile taarifa alisikia kama kitu kimemkaba kifuani akaanza kutetemeka…
Mikono iliishiwa nguvu na pumzi ikawa haitoki na hatimaye akadondoka chini na kupoteza fahamu.
……………………………..
Glory alipoona kaka yake hapatikani ilibidi aende nyumbani kwa wifi yake na kumkuta amekaa sebuleni anaangalia tv..
“mke mbona mbio mbio hivyo”
“Mke acha tu, nimeyatimba”
“Nini tena?”
“Kaka kakupigia simu?”
“MH hiyo simu nilivyoitupa hata chaji haina”
“amenipigia ananiomba nimuombee umsamehe si kwa hasira nikamdanganya kwamba ulifariki….”
“Haaaa wifi! Kwahiyo ikawaje?”
“Nilimsikia tu akitoa mshtuko na hakuongea tena hata sasa simu yake haipatikani”
………………………..
Vipimo vya damu vilichukuliwa kati ya Verity na Gwakisa kisha wakakaa kusubiri majibu.
Ndani ya muda mfupi majibu yao yalikuwa yamekamilika na hivyo kutakiwa kupatiwa majibu yao.
Kabla ya kupewa majibu ilibidi ushauri nasaha kwanza utolewe…
Wataalamu wale wa ushauri nasaha na kupima walitoa ushauri mrefu huku wakiwauliza maswali mengi lakini swali moja ndilo liliwashtua lakini likiwa limemshtua Verity zaidi…
“Ikitokea mmoja wenu ana Virusi vya UKIMWI alafu mwingine hana je ? mtachukua uamuzi gani? ”
Hapo ilibidi wote wamtolee macho muuliza swali bila kujua kila mmoja ajibu nini, lakini kabla hawajajibu Yule dokta alianza kuwashauri kuhusu ikitokea mmoja wao ana maambukizi alafu mwingine hana,
Aliwashauri namna ya kuishi na kuendelea kuwa wanandoa huku wakisaidiana na kuendeleza maisha yao bila mwingine kupata athari.

Kwa ushauri ule tayari walishahisi kuwa kuna mmoja wao ana maambukizi lakini sasa ni nani kati yao … hapo ndio ilikuwa kitendawili.

“Mjibu ya vipimo yanaonesha kuwa Mrs Gwakisa una maambukizi ya virusi vya Ukimwi ”
Baada ya kusema tu sentensi hiyo kabla haijamalizikia vizuri Verity alijishika kifuani na hatimaye almanusura kama asingeshikiliwa angeanguka chini.

Gwakisa alimshikilia mkewe na kumlaza kwenye miguu yake ambapo ilibidi ahudumiwe kwanza kwani alikuwa ameshalegea na hajitambui.

“je? Vipi kuhusu mimi Dokta?” gwakisa ilibidi aulize kwani yeye alikuwa hajapewa majibu yake.
“Majibu yako haya hapa, kama huelewi useme”
Gwakisa alichukua ile karatasi akaisoma na kugundua kuwa yeye ni mzima.

Hapo sasa mawazo yalianza kumuandama akilini, ina maana huyu VERITY amenisaliti mpaka akaambukizwa jamani? Alijiuliza Gwakisa.
“Inakuwaje mimi sijaambukizwa? Inakuwaje kuhusu hii mimba, ni yangu kweli?”
Hasira zilikaba koo la Gwakisa na hakutaka kusubiri zaidi. Taratibu alianza kuondoka zake.
Hatua ya kwanza ya pili yatatu akavutwa shati, alivyogeuka akakutana na sura ya Yule dokta…

“Unakwenda wapi? Njoo kwanza.”
“niache niondoke”
Watu waliokuwa pale mapokezi walistaajabu wakawa wamemtolea Gwakisa macho wakijiuliza ni kitu gani kimetokea.

Baada ya Gwakisa kurudi ilibidi akalishwe kitako na kushauriwa upya, alibembelezwa kwa namna nyingi mpaka akaelewa na kuridhia kuendelea kuishi na Verity.
………………………….

Sam aliokotwa na wenzake waliomuona akiwa anaanguka na kumchukua hadi kwa daktari ambaye almpa huduma na baadae akaamka.

“Naomba simu yangu” ndio kitu cha kwanza Sam aliongea baada ya kuamka tu.
“Msimpe simu” dokta ndie alitoa ushauri.

Ikawa hivyo kwamba Sam hakupewa simu hata baada ya kuomba sana, dokta aliamini kuwa simu ndio ilisababisha yote, hivyo basi ilibidi apatiwe dawa za usingizi ambapo alilala hadi kesho yake akawa ameamka akiwa mzima.

Ilibidi ahojiwe vizuri kuwa nini ni hasa kilimpata mpaka akafikia hatua ile lakini hakutaka kuweka wazi ninini hasa aliambiwa akiamini kuwa ataonekana mtu wa ajabu hivyo akatoa sababu za uongo kwamba ameambiwa nyumba yake imeungua.

Mambo yalipokaa sawa walirudi kwenye ratiba za kawaida na hapo ndipo alipopewa simu yake na kuiwasha.

Moyo wake ulijaa simanzi mno kiasi kwamba alijiona hana maana ya kuishi duniani kwani aliyoyafanya atayajutia maisha yake yote.

Ndani ya moyo wake alikuwa anampenda sana mke wake, kitendo cha kuambiwa amefariki alijikuta ameumia sana, ni afadhali hata angefariki kwa hali ya kawaida tu lakini alijiona kuwa ana hatia mbele zake na mbele za Mungu.
Kila alipokuwa anaingia kwenye masomo yao ilibidi kuwa anazima simu na kuiwasha anapokuwa anatoka.
Kwakuwa mafunzo yalikuwa kwenye hatua za mwishomwisho walikuwa wanapewa muda wa kupumzika mapema na hata kufanya mambo mengine kama vile kutembea mtaani.
Siku moja akiwa amejilaza chumbani kwake akitafakari maisha jinsi yatakavyokuwa bila ya mkewe wenzake walimfwata chumbani wakimtaka wakatembee mtaani kwa ajili ya kupata mbili tatu lakini Sam aligoma akidai kuwa anapumzika.

Akiwa amejilaza kitandani aliona simu inaingia, kilichomshtua ni ile namba iliyopiga… ilikuwa namba ya Rafiki (mke wake).
Mapigo ya moyo yalimwenda kasi kuliko kawaida kiasi kwamba hata akawa anatetemeka akiamini kuwa huenda ni mzimu.

Kwakuwa alikuwa amewahi kutazama sinema zinazoonyesha watu waliouawa wanavyowarudia waliowaua kimiujiza nayeye akajua ndio kinachotokea na hivyo akaogopa kupokea simu.

Alitamani akimbie pale chumbani lakini akajikaza, kabla hajakaa vizuri simu yake ikaita tena kwa namba ileile ya mke wake.

Alijishtukia mkojo ukimtoka bila kujua, alisubiri ikaita mpaka ikakatika, ilivyokatika tu akaiwahi ili aizime kabisa asipatikane.

Kabla hajaizima iliita tena lakini alipoangalia vizuri jina halikuwa la mkewe isipokuwa lilikuwa la Glory mdogo wake.

Hapo roho ikatulia kidogo na kuamua kupokea,
“Haloo Glory”
“Sio Glory mimi ni mke wako Rafiki”
Hapo sasa ndipo Sam alichoka kabisa na kuitupa simu chini.
…………………………
Hakuna kitu kilimuuma Rafiki kama kumpigia Sam alafu asipokee mpaka akaamua kumpigia kwa Simu ya wifi yake ndio akapokea lakini aliposikia kuwa mpigaji ni yeye akakata simu.

Akili yake ilimwambia bila wasiwasi kuwa Sam ana chuki bado nayeye na ndio maana hataki kumsikia.
Taratibu machozi yalianza kumbubujika mashavuni mwake akijua kuwa kwa SAM hana lake tena, alijutia kuolewa nae na kutamani siku zirudi nyuma awe sio mke wa Sam.
“Wifi mbona unalia?”
“Kaka yako ananichanganya sana wifi”
“Kwani imekuwaje tena?”
Ilibidi rafiki amuelezee Glory kila kitu jinsi ambavyo alimpigia bila kupokea hadi akaamua kuchukua simu yake ambayo ilikuwa kwenye chaji na kupiga ikapokelewa lakini baada ya kujua kuwa mpigaji n yeye akamkatia simu.

Glory alishusha pumzi ndani akitafakari jambo, hakutaka kuamini kuwa kaka yake hataki kumsikia wifi yake wakati mara ya mwisho walipoongea alionekana kujutia sana hadi kumuomba amuombee msamaha kwa wifi yake ila akamdanganya kuwa amefariki.

Glory aliamini kuwa kaka yake anaogopa kupigiwa simu na mtu aliyeambiwa amefariki na wala sio kwamba hampendi.

“Wifi nimegundua kitu”
“Kitu gani?”
“Kaka anaogopa kuongea nawewe kwasababu nimemwambia umefariki, anahofia kuongea na mtu ambaye ameambiwa kafa”

Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

JIUNGE KWA UPDATE NA BURUDANI ZAIDI
WhatsApp Channel=> CnZ Media(Follow)
Telegram Channel=> CnZ Media(Join)

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)