MAMA ALISHIKWA KALIO MBELE YANGU (47)

0

SEHEMU YA AROBAINI NA SABA
TULIPOISHIA...
“Wifi nimegundua kitu”
“Kitu gani?”
“Kaka anaogopa kuongea nawewe kwasababu nimemwambia umefariki, anahofia kuongea na mtu ambaye ameambiwa kafa”

IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI

TUENDELEE...
Nisha alikuwa amejilaza kitandani ameshikilia tumbo lake anawaza jinsi Sam alivyomtenda, hasira ilikuwa imemkaba kooni kiasi cha kumfanya awe anatetemeka.

Hapo hapo alichukua simu yake na kutafuta baadhi ya namba na kuzipiga…
“Haloo”
“sema bosi”
“Kuna kazi nataka muifanye”
“Lete kazi bosi maana njaa kali sana saivi umetutupa kweli siku hizi hutoi kazi kabisa”
“Ndio nawapa kazi sasa”

Waliongea mengi sana na hao watu wake lakini mwisho NISHA alimalizia kwa kuwaambia kuwa …
“Baada ya wiki mbili watamaliza mafunzo hivyo muwe makini akishuka tu hapo airport mmalizeni kabisa”
“Usijali Bosi kazi ndogo sana hiyo”
Wale watu wa NISHA kwa shida ya pesa walizokuwa nazo walijipanga vizuri ili kumkabili mtu ambaye waliambiwa atatua Dar es Salaam baada ya wiki mbili,
Walikuwa na silaha za kutosha kwakuwa walishaambiwa mtu mwenyewe ni mtu wa mazoezi na ana mafunzo, walijua jinsi ya kuwakabili watu wa aina tofauti kwani ni kazi waliyoizoea hivyo walijipanga vyema kwa kila kitu.
Wakati NISHA ametoa maagizo kuhusu mtu wake anayetaka amalizwe simu yake iliita tena akaichukua na kuiangalia, hasira zilimkaba baada ya kugundua mpigaji ni SAM, pamoja na hasira alizokuwa nazo lakini aliamua kuipokea tu.
“wewe Mbwa unataka nini kwangu?”
“Mimi Mbwa Nisha?”
“Wewe ni zaidi hata ya huyo Mbwa”
“Kwahiyo na mwanangu utakayemzaa pia ni Mbwa?”

Hapo NISHA alishtuka kidogo, hakutegemea jibu hilo kutoka kwa SAM,
“Mtoto yupi unayemsemea wewe ambaye nitamzaa”
“Tafadhali NISHA hata kama nimekukosea kiasi gani naomba usitoe Mimba yangu, natamani sana kumuona mtoto wangu atakayetoka kwenye tumbo lako”
Nisha hakujibu kitu ikabidi SAM aendelee…
“Najua nimekukosea lakini msamaha upo kwa ajili ya wanaokosea, nisamehe NISHA, mwenzio nilikuwa na matatizo ambayo nikija nitakueleza vizuri, nakupenda na nampenda mtoto wetu atakayezaliwa”
“Its too late SAM (Umechelewa SAM)”
Baada ya NISHA kusema hivyo akakata simu huku akabaki analia tu kwa hasira…
Moyoni mwake alimpenda sana SAM ila hasira za mtu unayempenda huwa ni kali kuliko kwa mtu usiyempenda.
Nisha alikuwa na hasira zilizochanganyika na mapenzi, alimpenda sana SAM na ndio maana alijikuta akikasirishwa nae sana.
“Lazima nitimize nilichopanga” alijisemea NISHA!
……………………..
Glory aliamua kutumia simu nyingine na kumpigia kaka yake ambaye aliona alipokewa japo alikuwa na hofu kwani alishajua ni namba ya Tanzania.
“Haloo”
“Habari yako ”
“Nzuri kaka, Mimi Glory mdogo wako”
“Ah Glory ,mwenzio naogopa sana, leo nimepigiwa simu na mzimu”
“Mzimu gani kaka?”
“Sasa mtu aliyekufa akikipigia simu utasema ni nani?”
“Nani huyo aliyekufa amekupigia simu?”
“Wifi yako Rafiki”
“Mh kaka nisamehe kwa kukudanganya, wifi hajafa ni mzima kabisa, nilikudanganya tu ila nawewe ukakurupuka hukutaka kunisikiliza zaidi”
“Glory unasema kweli?”
“Ndio kaka, wifi yuko hapa”
“Mungu wangu…jamani mke wangu, naomba niongee nae”

Hapo hapo Sam aliunganishwa na mke wake ambapo hakuna alichosema zaidi ya kusisitiza msamaha na kuapa viapo vya kutorudia huku akidai Kuwa anampenda sana mke wake na hatakuja kumuacha mpaka kifo…
“Mke wangu nisamehe sana, nisamehe mke wangu…nimeishi maisha mabaya sana yaliyokosa matumaini, wewe ni kila kitu kwangu…nakuhakikishia nikija nitaokoka ili Mungu aniondolee pepo la hasira za kukurupuka”
“Wewe mwenyewe unajua mke wangu, unajua tatizo nililokuwa nalo alafu ukaniambia ni mjamzito…wivu ulizidi kipimo mke wangu kwasababu nakupenda sana”

Rafiki alikuwa hajibu chochote anasikiliza tu…
“Mke wangu naomba usije ukafa kabla yangu, naomba Kama ni kufa nianze mimi, nimegundua siwezi kuishi bila wewe, nakupenda sana”!
Wakati Rafiki anaongea na Sam simu iliwekwa Loud speaker hivyo Glory alikuwa anasikia kila kitu, kila alipokuwa anamsikia SAM anaomba msamaha ilibidi awe amepiga magoti mbele ya wifi yake akisisitiza kwa ishara huku mikono ikiwa kifuani akiomba kaka yake asamehewe.

Rafiki alikuwa amewekwa mtu kati, hakuwa na ujanja ikabidi atoe msamaha…
“OOOOH mke wangu, siamini mimi kama tutakuwa wote tena, ”
“Ndio uamini sasa”
“Yani nikija Dar siku hiyohiyo nitakodi hata Helikopta nije Mbeya nikuone mke wangu”
“Baba usiharakishe hivyo ukapata matatizo wewe njoo kawaida tu”
“Hapana mke wangu siwezi, natamani nije hata saivi, nitakuletea zawadi nzuri sana…vipi kitumbo kikubwa eeenh”
“Bwana weee utakiona ukija”
Waliongea mengi na hatimaye wakaridhika na kuagana.
……………………….
Siku ya siku ilifika Sam akawa ndani ya ndege anakaribia Tanzania, aliposhuka tu kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa JK NYERERE aliburuza mizigo yake akaketi sehemu ili ampigie mkewe kumjulisha kuwa anaunganisha ndege nyingine mpaka Mbeya siku hiyo hiyo…
Kabla simu haijapokelewa alishtuka mwanamke Mrembo amesimama mbele yake anamuita kwenye gari ambayo ilikuwa milango wazi…

Sam alibaki ametoa macho akimtazama Yule dada anayemuita ndani ya gari, alijiuliza amewahi kumuona wapi kwani alijionyesha Kama anamfahamu.
Taratibu sam alianza kumsogelea huku akiendelea kutafakari kama anamfahamu ila kila alipokuwa anamkaribia ndio sura yake ilionekana kuwa ngeni kabisa. Yule dada alizidisha tabasam lililozidi kumvutia sam ambaye alikuwa anautazama urembo wa Yule dada.
Alikuwa ni msichana mrefu mweupe mwenye uso kama wasichana wa Rwanda, alikuwa amevaa gauni jeusi lenye mpasuo uliosababisha sehemu ya paja lake la kuvutia liwe wazi na kumtoa Sam udenda.
Ndani ya lile gari kulikuwa na wanaume wanne waliolala kwenye siti wakisubiri Sam akaribie hata kwenye mlango tu wamvutie ndani waondoke nae kama maagizo ya bosi wao yanavyosema. Ni kama mate yalikuwa yanawatoka walivyokuwa wanamuona Sam anakaribia kufikia kwenye lengo lao.

Akili ya Sam ilikuwa inafikiria mambo zaidi ya mia ikiwemo kuwa Yule dada amewahi kumuona wapi, kwanini anamuita kwenye gari na lililomchanganya zaidi ni urembo wa Yule dada uliomtoa ufahamu.
Wakati anamkaribia alianza kukumbuka baadhi ya mafunzo ya upelelezi aliyoyapata na jinsi mbinu ya kutumia wanawake warembo inavyotumika kunasa watu. Hapo akili yake ikawa inaanza kufanya kazi kama kawaida, hali ya uso wa Sam ilivyobadilika ilianza kumshtua Yule mdada aliyekuwa ameegemea mlango wa gari na kutoa signal kwa wenzake.
Kwakuwa Sam alikuwa ameshasogelea Sana lile gari wale jamaa kule ndani wakawa wanapanga namna ya kufanya ili wasije wakapoteza lengo.

“Wewe ni nani?” sam alimuuliza Yule dada.
“Sam yani umenisahau? Mimi ni PC eveline tumetumwa tukuchukue tukupeleke makao”
Yule dada alijua kabisa ile hoja haitamkamatisha Sam lakini lengo lake lilikuwa ni kumzubaisha Sam ili watumie mbinu nyingine.
Wale vijana ndani ya gari walichukua kitambaa chenye dawa za kulevya kisha mmoja akashuka kwa kutumia mlango wa upande mwingine kisha akazunguka na kuwa anakuja nyuma nyuma huku Sam akiwa hamuoni.
Kwa mwendo wa haraka lakini wa kunyata Yule kijana alimwendea Sam ili amfunike na kile kitambaa usoni, Sam alikuwa anamtazama Yule dada ambaye ni kama aliacha kuongea na kuhamishia mawazo na macho yake nyuma ya Sam kitendo kilichomfanya Sam ahisi huenda kuna kitu nyuma yake…
……………………………………
Maisha ya Gwakisa na Verity hayakuwa na mvuto tena, wasingeweza kushiriki tendo la ndoa kama mwanzo kwani Gwakisa hakutaka kuambukizwa. Hata hivyo mvuto kwa mkewe hakuuona tena.
Hili lilimsumbua sana Verity, alijiona ananyanyapaliwa hata kwa haki zake za msingi, alijiona thamani yake haionekani na mbaya zaidi Mimba aliyonayo ilimfanya atamani ngono kuliko wakati wowote kwenye maisha yake.
Kila alipojaribu kuonesha hisia zake kwa Gwakisa ndio kwanza alimkuta na stress zisizopimika, kila Gwakisa aliporudi nyumbani alikuwa hana hata muda wa kuongea na mke wake. Hata kula alikuwa anakula huko mtaani akirudi ni kulala tu.

“Mme wangu” verity alimuita Gwakisa
“Unasemaje” Gwakisa badala ya kuitika alirusha swali.
“Hivi ninafaa kweli kuwa mkeo tena?”
Gwakisa alishindwa kujibu hili swali kwani hakulitarajia na lilikuwa gumu kwake.
“Mme wangu naomba unijibu”
“Unamaanisha nini?”
“Namaanisha hivi, kwa hali yangu na mabaya yote niliyokufanyia nastahili kuwa mkeo tena na kulala nawewe chumba kimoja?”
Gwakisa usingizi ulikatika na kujigeuza.
“Kwani mbona maswali yako siyaelewi, unataka kuamua nini?”
“Nakuomba mme wangu, nakuomba mimi uniache tu ili upate mwanamke mnayeweza kuishi kama mme na mke, mimi sifai tena”

Nikweli Gwakisa alikuwa na hasira juu ya Verity lakini sio kwa kuanzwa yeye eti aombwe kumuacha mkewe, tena anayeomba ni mke mwenyewe.
“Alafu utaenda kuishi wapi?”
“Mimi nina kazi yangu sitaweza kuishi na kujitegemea, kama pia utataka kunipa chochote kama mgao kwenye mali zetu unaweza ila sikulazimishi mme wangu”
“Tutaongea basi vizuri kesho, kwa sasa lala kwanza”
Sio GWAKISA wala verity ambaye alipata usingizi wa maana kwa usiku ule, kila mmoja alikuwa anawaza namna mambo yatakavyokuwa ikiwa kila kitu kikiwa kulingana na ombi lilivyotolewa.
Gwakisa alikuwa hayuko tayari kumuacha Verity, alimpenda sana na uwepo wake ulikuwa una maana kwake hata kama walikuwa hawashirikiani kwa chochote.
Verity nae alikuwa anawaza huenda ametoa ombi ambalo endapo litakubaliwa atakuwa hana uwezo wa kulihimili, alikuwa anawaza sana huku akitamani Gwakisa aseme amemkatalia ombi lake nayeye angekuwa tayari kukubali kuishi nae hata kwa kuuhadaa ulimwengu.
……………………………
Asubuhi na mapema Gwakisa aliamka akamuona Verity bado yupo usingizini, hakutaka kumuamsha ila yeye alijiandaa haraka haraka na kuondoka zake akielekea kazini.
Alipofika huko alijifungia ofisini kwake huku akiwaza mambo mengi sana, aliwaza jinsi ambavyo ataishi bila ye mkewe aliyemzoea, aliwaza jinsi ambavyo jamii itamchukulia na kugundua kuwa maisha hayatakuwa kama awali.

Pamoja na yote lakini aliona huenda Verity hana mapenzi nae tena hivyo kumng’ang’aniza abaki wakati alikuwa ameomba yeye mwenyewe kuachwa itakuwa ni kuendleza uzoba. Alijiuliza ni kipi mkewe alikikosa kwake mpaka akaamua kumsaliti na kuishia kuambukizwa ukimwi na leo anaomba kuachwa… hii ilimpa picha kamili kuwa Verity hampendi.

“Hakuna shida, naenda kuridhia ombi la kuachana nae” alijisemea Gwakisa.
Alichokifanya ni kupanga ninini amuache nacho Verity, yaani ampe nini kwenye mali zao, aliandika mali zao zote pamoja na zile alizochuma katika ushirika wake na Nisha kisha akaamua cha kumpa ili waachane.

Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

JIUNGE KWA UPDATE NA BURUDANI ZAIDI
WhatsApp Channel=> CnZ Media(Follow)
Telegram Channel=> CnZ Media(Join)

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)