MAMA ALISHIKWA KALIO MBELE YANGU (48)

0

SEHEMU YA AROBAINI NA NANE
TULIPOISHIA...
“Hakuna shida, naenda kuridhia ombi la kuachana nae” alijisemea Gwakisa.
Alichokifanya ni kupanga ninini amuache nacho Verity, yaani ampe nini kwenye mali zao, aliandika mali zao zote pamoja na zile alizochuma katika ushirika wake na Nisha kisha akaamua cha kumpa ili waachane.

IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI

TUENDELEE...
Kwa upande wa Verity aliamka akiwa mchovu sana, aliangalia pembeni na kugundua kuwa mme wake ameshaondoka kwani hakuwepo pale.
Machozi yalimtoka usoni kwa jinsi ambavyo maisha yamemgeukia vibaya, aliiwaza aibu inayomuwinda mbele ya jamii. Alikuwa anasubiria jibu kutoka Kwa Gwakisa lakini alitamani ampigie simu amuambie kama vipi apuuzie ombi alilompa.
Baada ya kuona anakosa jibu jawabu la mawazo yake alitamani kupata mtu wa kumshirikisha kuhusu lile jambo na hakuona mwingine isipokuwa dada yake.
Alijiandaa haraka haraka na kwenda hadi kwa dada yake Rafiki ili amwambie kinachomsibu.

Alipanda gari lake hadi nyumbani kwa Rafiki na kupiga honi ambayo ilisababisha geti lifunguliwe na kuingiza gari ndani. Alipofika ndani alipaki na kushuka kisha akaelekea moja kwa moja mpaka chumbani alikolala dada yake.
“Kumbe wewe aaah”
“Haaa Dada ina maana sina maana”
“Una maana gani sasa” alijibu Rafiki bila kijua kuwa jibu lile lilikuwa na pande mbili kwa Verity ambaye alikuwa na mawazo ya kunyanyapaliwa.
Kilichomshtua rafiki ni kilio cha mdogo wake VERITY. Rafiki alibaki anamtolea macho tu asielewe ninini kinamsumbua.

Vipi tena jamani mbona unalia” aliuliza rafiki lakini Verity hakumjibu isipokuwa alifungua mlango na kutoka, Rafiki hakuvumilia akanyanyuka bila kujali hali yake na kumfwata.
“Mdogo wangu unalia nini?” rafiki alijitahidi kumrudisha mdogo wake na hatimaye akakubali kurudi ndani na kuketi japo bado aliendelea kulia.
“Mbona unantisha mwenzangu na hali yangu hii, nyamaza basi uniambie kinachokutatiza mdogo wangu”

Hatimaye Verity alinyamaza na kumwambia dada yake jinsi alivyojisikia kwa kumwambia kuwa ana maana gani…
“Maskini mdogo wangu, mimi sina maana hiyo, ungejua kuwa namsubiria mme wangu anakuja leo hivyo kila gari inayoingia nahisi niyeye”
“Haa shemeji anakuja leo?” aliuliza kwa hamaki Verity.
“Ndio yani hapa moja haisimami wala mbili haikai, natamani aje nimemmisi sana”
“Linda sana ndoa yako dada, kabla hujafika muda wa kujutia, Mimi mwenzio najuta saivi”
“Unajuta nini tena mdogo wangu, mbona mambo ya mitihani kwenye ndoa ni kawaida tu”
“Hujui tu lakini mimi mwenzio hapa saivi sina thamani tena, nimeathirika dada, mbaya zaidi Gwakisa yeye ni mzima wa afya”
“Unasemaje Verity?”
“Usipaniki dada, kilichonileta hapa nataka unisaidie mawazo kwani naona bila msaada kwasasa naweza kufa kabisa japokuwa mimi ni mfu ninayeishi tayari”

Verity alimsimulia dada yake kila kitu na hakubakisha wala hakuongeza, alimwambia tangu mwanzo alipoanza kutembea na Sam na kuzaa nae kisha akamuomba sana kwa machozi amsamehe.
Alimsimulia jinsi alivyoisaliti ndoa yake na kutembea na Dr Kelvin na kuishia kupewa mimba na UKIMWI juu, alimsimulia pia jinsi ambavyo ameomba kuachana na mme wake japo ombi hilo linamtesa kwani anaona halikuwa ombi sahihi.
Rafiki alimsikiliza mdogo wake kwa umakini mkubwa huku akishangazwa na kila alilosikia kutoka kwa Verity. Aliumia sana lakini hakutaka kuonyesha, alionyesha sura ya kutoshtuka ili mdogo wake asijione ana majanga makubwa sana.
“Usijali mdogo wangu, maisha bado yanaendelea na nivyema kwa ulichoomba kwa mmeo ili msije mkakaa huko ndani huku mnasimangana, atakuua mapema”

“Lakini dada mbona kama nampenda bado mme wangu?”
“Sio kweli, ungekuwa unampenda usingekuwa unamsaliti, na ndio maana inabidi kuolewa na mwanamme unayempenda na ikitokea tofauti inabidi ujitahidi sana kumpenda hata kwa kujilazimisha kitu ambacho wewe kimekushinda mpaka ukafikia huko”
“Sidhani dada, naona sitaweza kuishi bila Gwakisa”
“Si umekuja kwangu kuomba ushauri?”
“Ndio dada”
“Basi nisikilize”
Kabla RAFIKI hajaanza kuongea walisikia kengele ya getini ikilia ikabidi wanyamaze kwanza, walichungulia getini wakaona gari inaingia baada ya geti kufunguliwa, wote walitoa macho huku RAFIKI akifikiri ni mmewe amerudi lakini VERITY yeye alishaitambua ile gari kuwa ni ya Gwakisa

Verity alianza kuhisi hofu ndani ya nafsi yake akijiuliza kwanini Gwakisa ameamua kumfwata pale kwa dada yake ilihali wangeweza tu kuzungumza hata jioni yake.
Rafiki alikuwa anahaha akidhani huenda atakayeshuka ni Sam lakini Verity yeye alishajua kuwa ujio ule ni wa GWAKISA.
Gwakisa alishuka kwenye gari na kuelekea moja kwa moja mpaka sebuleni alikokaribishwa na kukaa huku akiwaulizia wenyeji na kuambiwa wako ndani kisha wakaenda kuitwa.

Rafiki alikuwa na mfadhaiko baada ya kujua kuwa ujio ule pia haukuwa wa mme wake lakini aliungana na Verity kukaa pale sebuleni wakiwa na Gwakisa.
“Vipi mme wangu mbona umeamua kunifwata huku?”
“Nimekuja pia kumtembelea sshemeji yangu”
“Sawa karibu, niliamua kuja kumtembelea dada baada ya kuona sijisikiii vizuri pia nahitaji walau mtu wa kunichangamsha kwa maongezi”
“Ni vizuri tu haina shida”
Gwakisa alikaribishwa kifungua kinywa lakini alisema ameshakula hivyo asingerudia tena, uso wa Gwakisa ulionekana kabisa kutokuwa na furaha, hili Rafiki alilitambua na kwakuwa mdogo wake alishamsimulia kila kitu alishajua chanzo cha ile hali.
Gwakisa alitulia kwa muda kisha akafungua kibegi chake kidogo na kutoa baadhi ya karatasi chache na kumpa Verity azisome.

Huku Verity akiwa anatetemeka mikono alizichukua zile karatasi na kuzipitia kisha akamalizia kwa kilio kilichomshtua kila mtu pale walipokaa.
“Yani kwli Gwakisa umeamua kuniacha kwasababu ya UKIMWI wangu”
Verity alitamka maneno haya huku akiwa analia kwa kwikwi, kitendo kile kilimshangaza Gwakisa kwani aliyeomba kuachwa ni Verity Mwenyewe, iweje sasa analalamika kiasi kile.
“Mme wangu kweli? Unaniacha mimi nilikuwa natania tu mme wangu ”

Hali ile ilimfanya Gwakisa anyanyue mdomo na kumwambia VERITY…
“Nani aliyesema kuwa una UKIMWI?” Mbona unapenda kujichulia wewe” gwakisa alisema vile akidhani kuwa Rafiki hajui chochote.
“Usijali chochote shemeji, Verity amenieleza kila kitu na hakuna haja ya kuficha chochote”
“Lakini yeye mwenyewe ndie aliyeomba hili litokee yaani tuachane”
“Najua ila nadhani anaiogopa hali ya upweke na hiyo hali ya ujauzito aliyo nayo”

Kibarua cha kumbembeleza Verity kilianza na hatimaye akanyamaza na kuruhusu maongezi kuendelea.
Waliongea mengi na hatimaye Verity akakubali kuachana na Gwakisa kwa kuachiwa Nyumba moja na viwanja viwili pamoja na milioni sitini ambazo aliwekewa kwenye akaunti yake.
Makubaliano pia yalionyesha kwamba watashirikiana kulea mimba ya Verity mpaka mtoto azaliwe na kuwa Gwakisa atamlea mwanae kwa kushirikiana na Verity, baada ya kila kitu kukamilika kila mtu alienda kivyake huku wakiyaanza maisha mapya.
…………………………….
Kwa mbinu kali alizokuwa nazo Sam alijigeuza kama roboti na kuachia shuti kali lililotua kifuani mwa mtu na kumtupa mpaka kwenye seng’enge zilizozunguka uwanja huu.
Hapo aligeuka vizuri na kumtazama Yule mtu na kumfwata kabla hajaamka, alimnyanyua na kumsindilia na ngumi mfululizo zilizomfanya ateme damu nzito mdomoni.
Wale wenzake waliokuwa kwenye gari waliamua kuondoka ili kukwepa msala lakini wakasita baada ya kuuona Sam akimburuza mwenzao isijulikane anampeleka wapi.
Waliogopa endapo mwenzao akikamatwa atataja mtandao wao kitendo ambacho kingemaanisha bosi wao atawapoteza nao pia.

Hapo ilibidi washuke wakapambane kuondoka na mwenzao au ikibidi wamuue ili kupoteza ushahidi wa mtandao wao.
Walikuwa ni vijana watatu huku kati yao akiwemo Yule dada mrembo wakiwa wanamfwata Sam wakimtaka amuachie mwenzao ama wammalize.
Wakati hayo yanaendelea tayari watu walikuwa wanashuhudia sinema ile huku wengine wakirekoodi na kuchukua picha.
Katika hatua iliyowashangaza watu ni jinsi Yule dada alivyoruka sambasoti na kumrushia Sam mateke mazito japo alikuwa anavukwa na gauni kiasi cha kuifanya kufuli yake nyeupe iwe nje nje lakini hakujali.
Hapo sasa Sam alijua ana wakati mgumu kwani aliyekuwa anapambana nae sio Yule dada pekee bali hata wale jamaa nao walikuwa wanamjia wakimtaka amuachie mwenzao waondoke nae. Sam nae hakutaka kukubali kirahisi. Hapo hapo alimpiga Yule jamaa ngumi ya kichwa chini ya kisogo na kumfanya alegee na kuzimia kabisa kisha akamuachia na kupambana.

Katika mateke zaidi ya nane aliyorusha Yule dada ni moja tu ndilo lilimpata. Baadhi ya mashuhuda walidhani huenda ni maigizo ya filamu haswa baada ya kuona watu wameshikilia simu wanarekodi bila wasiwasi.

Mapigo aliyokuwa anayatoa Sam yalimtisha kila mtu na kuwafanya watu waliokuwa pembeni kumshangilia mno ngumi zilipigwa kwa zaidi ya dakika ishirini na kumuacha Sam akiwa amewaziidi wale jamaa kitendo kilichowafanya wakimbie na kumuacha mwenzao.

Hapo sasa polisi walikuja na kumkamata Sam huku watu wakimzonga mpaka kituo cha polisi pale uwanja wa ndege na wengi wao wakimpiga picha kwa jinsi alivyoonyesha uwezo wa ajabu wa kupambana.
Baadhi ya watu walichelewa hata safari zao wakitazama yale mapigano huku kivutio kikubwa akiwa ni Sam. Walipofika pale kituoni na watu kuwa wameondolewa Sam alitoa vitambulisho vyake na kuwaonyesha wale polisi ambao walianza kupiga saluti.

“Huyu mtu mhifadhini na nitataka kujua walitumwa na nani kunifanyia hili tukio” Sam aliacha maagizo na kuondoka zake kwenda kupanda ndege ambayo ilikua inakaribia kuondoka.

Alipofika aliingia kukaguliwa na kisha akazama ndani ambapo baada ya masaa kadhaa ndege ikapaa hadi Songwe –Mbeya ambapo alishuka na kuchukua tax kuelekea nyumbani kwake.
“Ilikuwa ni furaha isiyo kifani kwa Sam kuonana na mke wake, walikumbatiana na kupigana mabusu kama wenda wazimu”
Jambo moja tu lilishindikana kufanyika “Ngono” na hii ni kwasababu Rafiki alikuwa na Bed Rest kutokana na mimba yake iliyokuwa na hatari ya kutoka. Lakini hii haikutosha wao kutoridhishana bila kuingiliana.

Walifanya walivyoweza ili mradi kila mtu akawa ameridhika na kufikia mshindo, raha na vicheko vilitawala nyumba yao kwa siku mbili nzima ambazo Sam alilala na kuamka bila kutoka huku akiwa na mkewe mda wote.
Glory nae baada ya kusikia kaka yake amerudi alienda haraka sana na kuonana nae huku kaka mtu akishangaa jinsi ambavyo mdogo wake amebadilika, amekuwa mrembo na kukua mno. Ukweli kaka mtu alijua kabisa kuwa maisha ya Glory yamepatana sana na hali ya Mbeya na chuo kimempenda pia.
“Mdogo wangu kumbe wewe ni mzuri kiasi hiki?”
“Sasa je? Ulitaka uwe mzuri peke yako tu eenh..hata mimi nawatingisha eti”

Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

JIUNGE KWA UPDATE NA BURUDANI ZAIDI
WhatsApp Channel=> CnZ Media(Follow)
Telegram Channel=> CnZ Media(Join)

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)