
Mtunzi: Yozz Piano Maya
SEHEMU YA PILI
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
alitimua mbio kama mwanariadha kuelekea kule alipomuona chales pamoja na watu wengine wamebeba jeneza..alipofika alipaza sauti jamani mimi sijafa nipeni kiwiliwili changu.. lakini chales pamoja na wale watu hawakumjali peto""""
IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI
ENDELEA...
Wala hawakuonekana kumsikiliza kabisa.. aisee peto alichanganyikiwa…watu wale walielekea kwenye gari na kuliweka jeneza ndani ya gari… kisha wote wakapanda ndani ya gari hilo…. aisee msinitanie acheni mchezo na kiwiliwili changu.. alisema peto kwa hasira… lakini bado watu wale hawakumjali.. peto aliamua na yeye kupanda ndani ya gari hilo…..alijaribu kufungua jeneza lakini hakuweza kulifungua… peto alianza kulia… hivi nyinyi watu mbona hamna huruma… jamani hata wewe mwanangu wa kumzaa mwenyewe unajifanya husikii kabisa ninacho ongea!!!! nakufukuza nyumbani kwangu….alisema peto huku akilia.. lakini chales hakumjali baba yake.. safari ileendelea na hatimae walifika nyumbani kwa peto.
peto aliwashangaa wamama lilipokuwa wakilia baada ya maiti yake kuletwa nyumbani.. watu wote walishuka kutoka nadani ya gari na kulibeba jeneza kulipeleka upande wa ndani kunako nyumba.. peto alikuwa sambamba na jeneza lake… hakutaka kuwa mbali kabisa… kichwani mwake alikuwa na mpango mmoja tu… asubiri wakilifungua jeneza aungane na kiwiliwili chake""
alipotazama upande wa nje kwa kupitia mlango wa sebuleni ulikuwa wazi… alimuona yule mkubwa wa wachawi aliyemkaribisha kwenye chama chake cha wachawi… peto alifuragi sana akapata matumaini…kisha peto akatoka nje huku akizipiga hatua za harakaharaka kuelekea kule alipokuwa ameketi yule mkubwa wa wachawi" peto alipofika alimwambia yule mkubwa wa wachawi…aisee ni bora nimekuona embu fanya mpango nirudi kwenye kiwiliwili changu…. yule mkubwa wa wachawi alikuwa na uwezo wa kumuona peto…..lakini alishindwa kumjibu peto kwa sababu alikuwa kwenye mkusanyiko wa watu.. hivyo wangemshangaa kuona anaongea peke yake…
aliamua kutoka na kuelekea upande mwingine akajitenga peke yake…. ili peto amfuate ampe maelekezo jinsi ya kurudi kwenye kiwiliwili chake… peto alipo ona yule mkubwa wa wachawi akizipiga hatua kutoka hapo alipokuwa… peto aliamini hata kuwa hata huyo mkubwa wa wachawi hamsikii wala hamuoni.. peto alinyong'onyea.. akazipiga hatua kurudi kule lilipokuwepo jeneza lake… yule mkubwa wa wachawi alikasirika sana kwa kitendo kile cha peto kutomfuata kule alipojitenga…. huyu ni mtu mjinga sana anadharau kumbe… sasa ngoja nimuache wakizike kiwiliwili chake… alijisemea hivyo huyo mkubwa wa wachawi" kisha akazipiga hatua na kuondoka zake hilo eneo la nyumani kwa peto..
peto alikuwa akilitazama jeneza lake…huku akisikitika na kuonekana kuwa na wasiwasi mkubwa.. ilipofika majira ya saa saba za mchana jeneza la peto lilitolewa nje kwa ajili ya kuuaga mwili wa marehemu… peto alizidi kuchanganyikiwa alipaza sauti.. jama mimi sijafa fungueni jeneza nirudi kwenye kiwiliwili changu… hakuna mtu aliye msikiliza peto wala kumjali.. jeneza lilitolewa nje na kuwekwa juu ya meza tayari kwa kuuaga mwili wa marehem… peto alimfuta mwanae chales na kumwambia ebu fungua jeneza mwanangu… nitakupa kila kitu unachokitaka…. chales hakumjali baba yake alibaki kimya""
jeneza lilifunguliwa upande wa kichwani… na watu wakajipanga kwenye mstari mmoja kwa ajili ya kuuaga mwili wa marehemu peto… peto alipo ona jeneza limefunguliwa alifurahi sana alitimua mbio kuelekea pale jeneza lilipokuwepo ili aungane na kiwiwili chake…. alipofika alijaribu kuingia lakini alistahajabu sana.. kashindwa kuungana na kiwiliwili chake… kisha akasema ""jamani kiwiliwili changu mimi ni nafsi yako…..nihurumie""" mmh!! inamaana nazikwa huku najiona hivi hivi…. yani hata kiwiliwili changu kinanikana mimi nafsi yake..
kumbe ili nafsi ya peto iungane na kiwiliwili ni lazima kiwiliwili kirudishwe pale kitandani kilipokuwa…
peto alianza kulia kwa uchungu….baada ya watu waliohudhulia msiba wa peto walimaliza kuaga mwili wa marehem peto…. na kujiandaa kuelekea makaburini kwa ajili ya kuuzika.. peto alizidi kuchanganyikiwa.. baada ya kuona jeneza lake likibebwa kupelekwa ndani ya gari.
Peto alianza kuangua kilio… alipiga mayowe ya kuomba msaada bila mafanikio yoyote… alimshi dereva… ili ahairishe kuendesha gari kuelekea makaburini.. dereva hakumjali peto… alibaki kimya huku akionesha wazi kutomsikia peto anaongea nini"" kisha dereva akazipiga hatua kuelekea upande mwingine… jamani mbona binadamu hamna huruma… alijisemea peto huku akilia kwa uchungu… peto hakukata tamaa aliendelea kuwasihi watu waliohudhuria msiba wale wasizike kiwilwili chake… aliamini huenda wakamsikia… peto aliamua kuchukuwa mawe mawili na kuyaweka chini ya matari ya gari ili lisiondoke…. kwa mbali alimuona chales akiingia upande wa ndani ya nyumba…. peto alitimua mbio kuelekea mule ndani alimoingia chales…peto alipofika alimwambia chales mwanangu tazama mimi baba yako ninavyoangaika!!!! nionee huruma mwanangu… ebu fikiria kama watazika kiwiliwili changu itakuwaje? ni nani atakaye kutunza zaidi ya mimi baba yako….ebu jaribu kuwaambia watu warudishe kiwiliwili changu kitandani kwangu hienda kikakubali kuungana na nafsi yangu" peto aliyasema maneno hayo huku akilia kwa uchumgu mkubwa…. wakati huo chales alikuwa kaketi chumbani kwake huku kashika tama akilia huku akimkumbuka marehemu baba yake…..hakika nilikupenda sana baba yangu lakini mungu kakupenda zaidi…alijisemea moyoni chales""huku akilia kwa uchungu… jamani mwanangu unalia nini mimi sijafa… alisema peto"" chales alionekana kuwa kimya bila kujibu chochote…
kisha akanyanyuka pale alipokuwa ameketi na kuelekea upande wa nje… Peto alianza kuingiwa matumaini huwenda sasahivi mwanae kamsikia alichokuwa akimwambia ndio maana anatoka nje… asante mwangu kawaambie" peto alisema hivyo.. kisha akazipiga hatua kumfata chales kule upande wa nje.
peto alipofika nje alistahajabu sana..kumuona chales akipitiliza na kwenda kuketi…. agh inamaana hakusikia yale yote niliyokuwa nikimwambia!!!! peto alijisemea moyoni""sasa hapo peto alianza kumkumbuka mungu aliamini mungu anao uwezo kuliko binadamu…….peto. alipiga magoti na kuanza kumuomba mungu huenda wakahairisha kizika kiwiliwili chake…. peto aliomba huku akilia kwa uchungu.. uso na macho yake yalionesha wazi kujutia..masanja umeniponza mimi laiti ningejua nisingekubaliana na wewe kunipeleka kujiunga na chama cha wachawi… tazama sasa hata nyinyi wachawi wenzangu mmeshindwa kunisaidia mimi mwenzenu!!!!! alisema peto huku akilia na kugalagala chini…..alipo ona hakuna msaada wowote aliamua kunyanyuka pale chini… aliona wakina mama wakilia kwa uchungu…hata yule jirani aliyetaka kuuliwa kichawi na mke wa peto naye alilia kwa uchungu mkubwa… pete alizidi kuchanganyikiwa alipo ona watu wengine walilia mpaka kuzimia…. peto aliweka mikono kichwani huku akiwatazama watu wakilia…. hivi hawa akinamama nahisi akili zao sio nzuri uani wanamlilia mtu ambaye hajafa!!!! alijisemea moyoni peto,,, kisha akapaza sauti jamani tusikilizane mimi sijafa embu acheni mchezo na kiwiliwili changu… watu hawakuonesha kumjali peto…. kisha akaona watu wakiingia ndani ya magari ili waelekee makaburini….. peto alizidi kuchanganyikiwa..watu wote waliingia ndani ya magari na wengine wakitembea kwa miguu kuelekea makaburini… alipotazama huku na kule aliona watu wanazidi kupungua…. aliamua kuzipiga hatua za haraka akaingia ndani ya gari lililobeba kiwiliwili chake…. na safari ya kuelekea makaburini ikaanza
Alionekana derva akiingia ndani ya gari lililobeba kiwiliwili cha peto.. dereva alipoliwasha gari peto alichanganyikiwa… safari ikaanza"" makaburi hayakuwa mbali sana iliwachukuwa dakika 45 kufika makaburini… walipofika.. Peto alikuwa wa kwanza kushuka… kwa mbali aliona mafundi wajenzi wakiwa wanachanganya zege…. peto alizidi kuchanganyikiwa aliamini bila shaka mafundi wale walikuwa wakiandaa zege kwa ajili ya kaburi lake… alitimua mbio mpaka pale walipokuwepo mafundi.. alipofika alichungulia ndani ya shimo… jamani mbona hamna huruma inamaana ndio mnazika humu kiwiliwili changu… kisha akawatazama mafundi wale alimuona fundi mmoja aliyekuwa akimfahamu alimsogelea na kumsihi wasizike kiwiliwili chake""'" fundi eee kwani haunikumbuki??? mimi peto na sijafa….aliongea peto huku uso wake ukionekana kuwa na huzuni kubwa… fundi yule hakumjibu peto aliendelea kuchanganya simenti na mchanga vikiambatana na kokoto" huku akipiga stori na mafundi mwenzake…..yule fundi mwingine alisikika akisema ongeza simenti zege iwe kali…peto aliposikia hivyo alitamani amnyang'anye koleo fundi. alijaribu kufanya hivyo lakini alishindwa….. alipotazama upande wa kushoto aliona watu wakiwa wamebeba jeneza wakija huo upande aliokuwepo peto… peto alianza kulia.. alibaki akiwatazama watu wale… jamani hivi kweli hawanisikii au wanataka kunikomoa tu!!!! eti fundi hamnisikii??? alisema peto"" mafundi wale hawakumjibu kitu waliendelea kufanya kazi yao. nakuonekana kutomjali.. punde jeneza lililetwa likawekwa kando ya kaburi… peto aliweka mikono yake kichwani…. na kuangua kilio kwa kupiga mayowe…. lakini haikusaidia kisha alionekana mchungaji akija upande wa kaburi ili auwombee mwili wa marehem peto……. watu wote walifumba macho kisha mchumgaji akaendelea na maombi.. peto aliona huo ndio muda mzuri wa kufingua jeneza aingie kwenye kiwiwili chake. alipojaribu kulifungua jeneza alishindwa..
punde mchungaji alimali maombi…. peto aliona watu wanachukua kamba na kuziweka katijeneza kisha wakaanza kulishutaratibu kuliingiza nadani ya kaburi… aisee peto aliangua kilio…alijaribu kuwazuia watu wale wasiliingize jeneza kaburini lakini alishindwa…. punde walimaliza kuliingiza jeneza kisha mchungaji akasema mtoto wa marehemu ataanza kuweka mchanga kwenye kaburi la baba yake huku akifatiwa na ndugu na jamaa wa karibu na peto… chales alichota mchanga na kutupa ndani ya kabiri.. huku akilia kwa uchungu.. baba yangu inamaana sitokuona tena?? chales alisema huku analia""" peto alipaza sauti mwanangu mimi sijafa yani hata wewe unakubali kubali kunizika mzimamzima hivi najiona"""" chales aliendele kutupa mchanga ndani ya kaburi na kuondoka.. walifuta ndugu na jamaa pamoja na marafiki wa peto…. walipo maliza""" watu walianza kuchukua makoleo na kuanza kufukia kaburi la peto… mara ghafla….ilisikika sauti ya mngurumo mkubwa ikiambatana na upepo uliovuma kwa kasi ya ajabu… watu walianza kuogopa hata peto iwoga ilianza kumuingia….
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi Shawishi Wapenzi wa Simulizi Wapakue(Install) App ya CnZ Media