
Mtunzi: Yozz Piano Maya
SEHEMU YA TATU
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
watu walianza kuchukua makoleo na kuanza kufukia kaburi la peto… mara ghafla….ilisikika sauti ya mngurumo mkubwa ikiambatana na upepo uliovuma kwa kasi ya ajabu… watu walianza kuogopa hata peto iwoga ilianza kumuingia….
IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI
ENDELEA...
Watu waliokuwa wakilifukia kaburi la peto waliacha kufukia… huku wakistahajabu upepo huo unaovuma kwa kasi isiyo ya kawaida… mara ghafla peto aliona watu wakija ule upande wa kaburi alipoangalia kwa umakini aligundua ni wale wachawi wenzake wakiongozwa na Magembe ambaye ni mkuu wa wachawi… walipokaribia mara ghafla jeneza la peto lilianza kutoka kunako ndani ya kabiri likija upande wajuu na kujiweka kando ya kaburi…. watu walitimua mbio hakibaki hata mtu mmoja""""hata yule mchungaji alitimua mbio kutokana imani yake kuwa ndogo… peto alipo ona mpaka mchungaji katimua mbio ilibidi na yeye atimue mbio peto alikimbia utadhani alishawahi kushiriki mashindano ya mbio za mita mia….
magembe na wachawi wenzake walilifiata kaburi kisha wakasimama karibu na jeneza la peto… mara ghafla….
peto alikimbia mara ghafla akasita kuendelea kukimbia.. akasimama… dah!! hivi mimi ni mjinga kiasi gani? huenda wamekuja kunisaidia… alipogeuka atazame ule upande lilipokuwepo kaburi lake… aliona Magembe…Masanja pamoja na wachawi wengine watatu wamelizunguka jeneza lake….. ghafla wakatoweka pamoja na jeneza….peto alichanganyikiwa akapaza sauti huku anakimbia kurudi kule lilipokuwepo jeneza lake… jamani eee mbona mmenisahau nipo huku"" Magembe unapeleka wapi kiwiliwili changu??peto alisema maneno hayo huku anakimbia kwa kasi kama kafungwa mota miguuni… alikata tamaa na kuamua kuondoka haraka aende nyumbani kwa magembe. …akiwa njiani anazipiga hatua aliona mtu anasukuma mkokoteni huku kabeba mzigo..alipotazama vizuri aligundua ni mkokoteni wake .. alimfata mtu huyo… kisha akamwambia…. mbona unatumia kitendea kazi changu bila ruhusa yangu??? mtu yule alibaki kimya hakumjibu peto….peto alikasirika sana.. akaanza kukunja mikono ya shati yake ili aanzishe ugomvi… ghafla akakumbuka kiwiliwili chake… akaanza kutimua mbio kielekea kule nyumbani kwa magembe… alipofika hakumkuta magembe…. hivi hawa watu mbona wanafanya mchezo na kiwiliwili changu!!!? peto alijisemea moyoni"""" punde magembe ambaye ndiye mkuu wa wachawi alikuja nyumbani kwake…..huku akiwa amemuacha masanja na wale wachawi wengine wapeleke kiwiliwili cha peto nyumbani kwa peto pale juu ya kitanda ili peto aweze kuungana na kiwiliwili chake"""magembe alikuwa na iwezo wa kumuona peto… kisha akamwambia ndani ya masaa matatu.. inatakiwa uwe umeshaungana na kiwiliwili chako…. sharti… itabidi utoe kafara la damu ya mtoto wako…. peto alichanganyikiwa baada ya kusikia masharti ya magembe….. peto aliamua kukubali….. kisha akajisemea moyoni…..nikiungana na kiwiliwili changu tu…..naacha uchawi na sitoweza kumtoa mtoto wangu kafara…."""""" magembe alimwambia peto waweza kwenda…. peto alianza kutimua mbio kuelekea nyumbani kwake..
uleupande mwingine.. Masanja na wale wachawi wengine waliwasili nyumbani kwa peto… wakatokezea upande wa nyuma ya nyumba ya peto…kisha masanja akaingia kichawi ndani ya nyumba ya peto ili aangalie mazingira yamekaaje…. alipoingia kwenye chumba cha peto masanja alistahajabu kukuta chumba cha peto hakuna kitu ndani hata kitanda ambacho inatakiwa iwekwe maiti ya peto…ili peto aweze kuungana na kiwiliwili chake…kumbe chales alikifungua kitanda hicho na kukiweka stoo ili atandike mkeka mkubwa ipatikane nafasi ya kulala wageni waliosafiri kuja msibani……
wakati huohuo peto alikuwa njiani akitimua mbio kuja nyumbani kwake.. punde alifika.. alipitiliza moja kwa moja chumbani kwake ili aungane na kiwiliwili chake…. alikutana uso kwa uso na masanja… masanja hakuwa na uwezo wa kumuona peto isipokuwa Magembe pekee. ..peto alistahajabu kuona hakuna kitanda wa kitu chochote….kisha akamuuliza masanja kiwiliwili changu kikowapi?? masanja hakujibu kitu.. alitoweka kichawi….wee rudi hapa nipeni kiwiliwili changu""alisema peto kwa sauti ya ukali"""
masanja alitokezea upande wa nyuma ya nyumba kule alipowaacha wachawi wenzake na kiwiliwili cha peto. …..na kusema hii kazi itakuwa ngumu sana kisha wakatoweka kichawi kuelekea kwa mkuu wa wachawi Magembe….huku wakiliacha hapo chini jeneza la peto…
Peto alitoka mule chumbani na kuelea upande wa nje.. alimuona mwanae chales akamfata na kumwambia kitanda changu kikowapi??? chales alibaki kimya…peto alizidi kuchanganikiwa aliamua kurudi ndani na kutazama saa ya ukutani ilikiwa ni saa kumi na moja… lisaa limojs limshakwisha…..peto alianza kuingiwa na uwoga wa hali ya juu aliamua kutokea mlango wa nyuma… alistuka kuliona jeneza lake… akazipiga hatua za taratibu kulifiata jeneza lilipokuwa….. alipofikaara ghafla..
Aliona jeneza linafunguka peke yake bila kufunguliwa na mtu…. peto aliona kiwiliwili chake alipojaribu kurudi aungane na kiwiliwili chake alishindwa""" dah! yani hata wewe unanikataa mimi nafsi yako embu kuwa na huruma!!!! tazama yamebaki masaa mawili tu…. niliyopewa ili nirudi kwenye kiwiliwili changu""" alisema peto akikiambia kiwiliwili chake….. huku akionesha sura ya upole….na huzuni kubwa.. peto aliamua kutoka upande ule na kuelekea upande wa mbele ya nyumba…… alianza kupiga mayowe kwa sauti kubwa… jamani eee nimebakiza masaa mawili tu…..nyinyi ndio mtasababisha mimi nife!!!!! watu hawakumjali ndio kwanza waliendelea kunawa mikono na kula chakula….aisee inamaana nakufa hivihivi nikiona!!!!!? alijiuza kimoyoni kisha akakunja suruali akaanza kutimua mbio kurudi nyumbani kwa mkubwa wa wachawi ambae ni Magembe… peto alikimbia bila kugeuka nyuma"" alipofika alichanganyikiwa baada ya kutomkuta magembe…. Mbona mnaniangaisha hivi… haki naapa nikifanikiwa kurudi kwenye kiwiliwili changu.. naokona na kuanza kumtumikia Mungu""" Eee Mungu nisaidie tazama navyoteseka!!!!!!
kumbe wakati peto alipokuwa njiani kuelekea kwa Magembe..kumbe ndio muda ambao magembe pamoja na wachawi wenzake walikuwa wamekwenda nyumbani kwa peto..
baada ya peto kumkosa magembe.. peto aliamua kutimua mbio kurudi nyumbani kwake alipokuwa njiani alikutana na mkusanyiko wa watu wamebeba jeneza wakielekea makaburini kuzika…. peto alistuka sana alihisi ni lile jeneza lililokuwa na kiwiliwili chake alipowakaribia watu wale aligundua kuwa sio jeneza lake…. kisha akaendelea kutimua mbio…. punde alifika nyumbani kwake alipitiliza mpaka nyuma ya nyumba yake…..alipokuwa ameliacha jeneza lake… alopofika aliwakuta wale wachawi wengine isipokuwa Mgembe.. alianza kuwauliza jamani mnanisaidiaje??? muda unazidi kwenda…..wale wachawi hawakujibu kitu kwa sababu hawakuwa na uwezo wa kumuona peto….. peto aliamua kutoka na kuelekea upande wa mbele ya nyumba yake….. kwa mbali alimuona magembe akiongea na chales"" peto alisita kwenda pale alipokuwepo magembe na chales… alisimama kando akitazama kinachoendelea…. nakuaminia magembe fanya mambo… peto alijisemea moyoni huku uso wake ukionekana kujawa wasiwasi…
aliendelea kuwatazama kisha aliona magembe akimshika chales kichwani… kisha aliona chales akianza kuzipiga jatua na kuelekea upande wa stoo…. kumbe magembe alipomshika chales alipandikiza mawazo kichawi ya kumuongoza chales aingie stoo na kukirudisha kitanda ndani ya chumba cha baba yake…
peto alipofika stoo alistahajabu sana hakukiona kitanda…. kumbe siku waliyokwenda makaburini kuzika….. kunawezi walikuja nyumbani kwa peto na kuingia stoo wakaiba baadhi ya vitu kikiwemo kitanda na godoro la peto…
chales aliendelea kushangaa kisha akatoka mule stoo na kuelekea upande wa nje…..alimfuata magembe na kumueleza kuwa kitanda hakipo kimeibiwa…….macho yalimtoka magembe kisha akazipiga hatua na kurudi ule upande wa nyuma ya nyumba..kule lilipokuwepo jeneza la peto…. peto alistahajabu kumuona magembe akizipiga hatua za haraka peto alimfuata magembe ule upande wa nyuma ya nyumba…. alipofika alikuta magembe akiongea na wale wachawi wengine… peto aliwasogelea…. alisikia magembe akisema… kitanda kimeibiwa…kabla hajamaliza kuongea peto alidakia na kusema" magembe acha masihala mbona mnanitenda hivi?? kisha peto akatimua mbio kuelekea ndani ua nyumba alipitia mlango wanyuma akaenda moja kwa moja mpaka sebuleni.. kisha akaitazama saa ya ukutani.. lilikuwa limebaki lisaa limoja…. peto alizidi kuchanganyikiwa…. alitoka nje haraka nakurudi ule upande walipokuwepo wachawi wenzake….
upande mwingine walionekana watu wawili wakiwa njiani kuelekea nyumbani kwa peto ni baada ya kukamatwa na ulinzi shilikishi… walikati wanajaribu kuuza kitanda cha peto….waliekuwa wanamuuzia ni yule jirani wa peto kumbe alikuwa ni mlinzi shilikishi…. alipowahoji wamekitoa wapi walijichanganya kutoa maelezo kila mmoja alisema kauli yake….jirani yake peto alistuka baada yakuona maelezo yao ni tofauti aliamua kuwaweka chini ya ulinzi…alipowabana waliamua kusema ukweli…
kule nyumbani kwa peto mambo yalizidi kuwa magumu magembe alionekana kuwa na wasiwasi mkubwa…. alimtazama peto kwa macho ya huruma…..peto alikuwa akilia kwa uchungu na kuonekana kukata tamaa ya kuungana na kiwiliwili chake……..magembe na wachawi wenzake waliondoka na kumuacha peto pamoja na jeneza lililokuwa na kiwiliwili chake…jamani eee mbona mmenikimbia!!!! kunatatizo gani… alisema peto kwa kupaza sauti baada ya magembe na wachawi wenzake kutoweka kimiujiza…. peto alikimbia na kuelekea upande wa mbele ya nyumba yake… mara ghafla aliona watu wawili wakiwa wamebeba kitanda alistuka sana""" alipotazama vizuri alimuona jirani yake akiongozana na watu hao kuja nyumbani kwake….. peto alitimua mbio kuwafuata.. alipowauliza wale wezi wawili hawakumjibu kitu…peto alikasirika sana"" yani mmeiba kitanda changu alafu nawauliza hamtaki kunijibu… kisha peto alirusha ngumi ili kuwapiga wale wezi… lakini hawakuguswa na ngumi hizo alizokuwa akizirusha peto…. ghafla alikumbuka kuwa watu wale hawakuwa na uwezo wa kumuona peto kwa sababu yupo katika hali ya nafsi…. peto aliwaacha watu wale na kuanza kutimua mbio kuelekea nyumbani kwa magembe…. ili akamwambie magembe kuwa kitanda kimerudishwa na wale wezi…. baada ya dakika kumi peto alifika nyumbani kwa magembe…. alipoangalia mlango wa nyumba ya magembe ulikuwa umefungwa… peto alizidi kuchanganyikiwa akaanza kutimua mbio kurudi nyumbani kwake huenda akamkuta magembe ili amsaidie aungane na kiwiliwili chake…. baada ya muda kidogo alifika nyumbani kwake…
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi Shawishi Wapenzi wa Simulizi Wapakue(Install) App ya CnZ Media