
Mtunzi: Yozz Piano Maya
SEHEMU YA NNE
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
baada ya dakika kumi peto alifika nyumbani kwa magembe…. alipoangalia mlango wa nyumba ya magembe ulikuwa umefungwa… peto alizidi kuchanganyikiwa akaanza kutimua mbio kurudi nyumbani kwake huenda akamkuta magembe ili amsaidie aungane na kiwiliwili chake…. baada ya muda kidogo alifika nyumbani kwake…
IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI
ENDELEA...
Alipitiliza mpaka sebuleni akaitazama saa ya ukutani zilikuwa zimebaki dakika 45…..katika yale masaa matatu aliyopewa…..peto aliondoka sebuleni na kuingia chumbani kwake"""alifurahi baada ya kumkuta chales akifunga kitanda chake…… peto alitoka nje kwa kupitia mlango wa nyuma alimkuta magembe peke yake….kisha magembe akamwambia huu ndio muda wa kuungana na kiwiliwili chako…rudi chumbani kwako… peto alitimua mbio na kuingia chumbani kwake… punde magembe aliingia kichawi pamoja na jeneza la peto…. magembe aliuliza godoro liko wapi???? peto alizidi kuchanganyikiwa…
kumbe muda huo wale wezi wawili walikuwa wamerudi kulifuata godoro la peto kule walipolificha…… peto alitoka nje na kuanza kutimua mbio kuwatafuta wezi wale…..alikimbia kwa hatua kadhaa mara ghafla…
Mara ghafla kwa mbali aliwaona wale wezi wawili wakija nyumbani kwake huku wakiwa wamelibeba godoro lake….aliamua kutimua mbio na kurudi nyumbani kwake alipitiliza moja kwa moja mpaka sebuleni kisha akatazama saa iliyokuwa ukutani… zilikuwa zimebaki dakika30kl katika yale masaa matatu aliyopewa…. peto alizidi kuchanganyikiwa.. akaamua kutoka nje ili achungulie aone wale wezi wamefika wapi?? aliona bado hatua chache wafike kwake….peto akatimua mbio akaingia chumbani kwake….alistahajabu magembe hakuwemo chumbani humo..alipotazama pale chini aliliona jeneza lake….. peto alitoka chumbani na kutimua mbio kuelekea upande wa nyuma ya nyumba…. alimkuta magembe kaketi peke yake… peto alianza kuwa na amani…. kisha akamwambia magembe kuwa godoro limeshaletwa….. magembe akasema nenda chumbani kwako nakuja mimi nakuja""" peto akatimua mbio kurudi chumbani kwake…alipoingia alikuta magembe kaishafika…….kwa sababu magembe aliingia chumbani humo kichawi……peto akatoks chumbani akaelekea nje ilahakikishe kama godoro lipo… alihisi kichanganyikiwa baada ya kumuona mwanae chales amelibeba godoro hilo na kuelekea stoo…. peto akatimua mbio kurudi chumbani" kamwambia magembe kuwa godoro linapelekwa stoo"" tafadhali fanya uwezavyo godoro liletwe humu""
magembe alitoka kichawi mule chumbani…… na kitokezea upande wa nje..akazipiga hatua kumfuata chales… alipomkaribia… magembe alinyanyua mkono wake na kutema mate juu ya kiganja chake… kisha akamgusa chales mgongoni""" punde chales aligeuza na kuanza kuzipiga hatua kuelekea kwenye nyumba na kuimgia ndani…akapitiliza moja kwa moja mpaka chumbani kwa baba yake"" akaliweka godoro juu ya kitanda… kisha akatoka nje….. wakati huo peto alikuwa na shauku kubwa ya kuungana na kiwiliwili chake macho yalikuwa yamemtoka……punde magembe alifika……akasema inabidi iletwe ile shuka iliyokuwa imetandikwa sikuile….. peto alizidi kuchanganyikiwa akatimua mbio kuelekea sebuleni akatazama saa ya ukutani… aliona zimebaki dakika kumi na saba(17) jamani mbona nateseka hivi huyu mtoto sijui kaweka wapi hiyo shuka…. peto alitia mbio akatoka nje…. akamuona chales anazipiga hatua kuondoka pale nyumbani… wewe chales"" peto alimuita chales…lakini chales hakuitika wala hakumjali baba yake… aliendelea kuzipiga hatua…..peto aliamua kutimua mbio kurudi chumbani kwake… akamwambia magembe kuwa akamwambie chales alete ile shuka…magembe alitoka kichawi kisha akajitokeza nyuma ya chales na kuyabadilisha kichawi mawazo ya chales ili arudi kuitafuta shuka ile…..
ghafla chales aligeuza na kutimua mbio kurudi nyumbani….. akaanza kuitafuta shuka ile kwenye kabati la nguo… wakati huo peto naye alikuwa akitafuta pia… ghafla kumbukumbu ilimjia chales alikumbuka juzi walipopeleka mochwari kiwiliwili cha bababa yake walikuwa wamemfunga ndani ya shuka hiyo kwa hiyo shuka ilisahaulika kule mochwari…. magembe aliweza kutambua kile alichokuwa anafikiria chales katika akili yake…. mara ghafla magembe alimshika mkono chales na kutoweka naw kichawi kuelekea mochwari..peto alitimua mbio kuelekea sebuleni akatazama saa ya ukutani zilikuwa zimebaki dakika 10. ….peto alichanganyikiwa… jamani nakufa hivihivi najiona aisee hiki ni kifo cha kujitakia…peto alisema maneno hayo huku akilia kwa uchungu……. punde magembe alirudi peke yake bilala chales!!!!! kisha akaanza kutandika shuka lile pale kitandani… alipomaliza alilifungua jeneza na kutoa kiwiliwili cha peto na kukilaza pale juu ya kitanda"" mara ghafla
mara ghafla magembe alikumbukakuwa kaacha mkia wa ng'ombe ambao huwa anautumia katika mambo yake ya kichawi…. punde alitoweka kichawi bila kumuaga peto… magembe mbona unanikimbia rudi unisaidie nakuomba tafadhali….peto alijaribu kungana na kiwiliwili chake lakini hakufanikiwa…akatimua mbio kuelekea sebuleni… akatazama saa ya ukutani… zilikuwa zimebaki dakika nane…. uuuwi nakufa hivi hivi huku najiona…..yani masaa matatu yamekuwa kama karne alijisemea moyoni"""kisha akatimua mbio kuelekea upande wa nje… alipofika nje alitazamahuku na kule hakumuona magembe…. aliamua kutimua mbio na kurudi chumbani kwake…. kwanini utaki kuungana na nafsi yako eee eti wewe kiwiliwili changu"" tafadha embu sema na mimi!!!!! peto alisema maneno hayo akikiambia kiwiliwili chake…. dah!! mpaka umrbadilika rangi… mimi sio mweusi kiasi hicho… embu punguzaasihala unanichosha tazama siku ya tatu leo sijaoga wala sijala… peto alizidi kuongea akikiambia kiwiliwili chake…. aliona magembe anacbelewa….. peto. akatimua mbio kuelekea sebuleni… alipotazama saa ya ukutani zilikuwa zimebaki dakika tano(5) peto alizidi kuchanganyikiwa… macho yalimtoka akatimua mbio kurudi chumbani kwake…. ile anafika na magembe akatokea…..
magembe aligusa kiwiliwili cha peto kwa kutumia ule mkia wa ng'ombe… hivi magembe mbona unanichelewesha kuungana na kiwiliwili changu….maana yake sikuelewi kabisa!!!! alisema peto huku macho yake yakimtazama magembe kwa msisitizo….. magembe alisema haya panda juu yakiwiliwili chako… kabla magembe hajamaliza kuongea peto alikuwa kaisha panda….
magembe alistahajabu muona bado peto hawezi kuungana na kiwiliwili chake…. macho yaljmtoka magembe huku jasho likimtiririka…. mmmh!!! haiwezekani… magembe alijisemea moyoni" kisha anza kukizunguka kitanda cha peto…. wakati huo peto alikuwa akimtaza magembe…peto aliona kama muda unakwisha alinyanyuka na kutimua mbio kuelekea sevuleni akaitazama saa ya ukutani zilikuwa zimebaki dakika mbili… peto alizidi kuchanganyikiwa akatimua mbio kurudi chumbani….akapanda juu ya kiwiliwili chake… magembe alitoa kachupa kadogo akafungua na kumwa unga mweupe kwenye kiwiliwili cha peto….mara ghafla peto aliungana na kiwiliwi chake…. aisee peto alifurahi sana alinyanyuka kitandani kisha akaanza kucheza staili aina ya KIDUKU…..alimkumbatia magembe kwa kumsaidia…. aised wewe kiboko kweli wewe ni mkuu wa wachawi… alisema peto…. magembe alikuwa akimtazama peto wakati akiongea maneno hayo……. kisha magembe alikohoa kidogo….. akabaki kimya kwa sekunde kadhaa kisha akamwambia peto…. kwa kuwa umeweza kuungana na kiwiliwili chako… itabidi utimize ahadi ya kumtoa kafara mtoto wako chales….peto alichanganyikiwa kisha akamwambia magembenakusihi tafadhali msimchukue mwangu chales sina mtoto mwingine zaidi yake….. magembe akasema haiwezekani ni lazima utoe kafara uzawa wa chimbuko la damu yako…kisha magembe akatoweka kichawi….. peto aliamua kutoka nje ili ahakikishe kama kweli ni yeye…. ile anatoka nje mara ghafla
alihisi kama miguu yake haikanyagi chini…. aliogopa sana…. akasita kutoka nje akarudi ndani…
mmmh!! jamani eee mbona kama bimemuona peto.. katokeza mlangoni kisha akarudi ndani…. alisema mtu mmoja kati ya watu waliobaki kwenye matanga….
peto alichukua ndoo na kuchota maji kutoka kwenye diaba akayamimina kwenye ndoo.kisha akazipiga hatua kutoka nje…. watu walipomuona peto waliogopa sana…. ilikuwa kama sinema…. au mlipuko wa mabomu mbagala yani watu walitimua mbio kila mtu alipita njia yake na kutokomea kusikojulikana….. ndani ya dakika moja hapakuwepo mtu hata mmoja aliyebaki hapo…. peto alistahajabu kisha akajisemea moyoni kwenda zenu huko… kwanza mlitaka kunizika mzimamzima…. kisha akaendelea kuzipiga hatua kuelekea bafuni…
baada ya kumaliza kuoga peto alirudi chumbani kwake…… akapanda kitandani na kuanza kuutafuta usingizi… ghafla wazo lilimjia… huenda akilala anaweza akapitiliza moja kwa moja aisiamke tena..alinyanyuka haraka kitandani…kisha akazipiga hatua kutoka nje ya nyumba.. na kuzipiga hatua kuelekea mjini…. kila alipokuwa akipita watu walitimua mbio……
ilipofika majira ya usiku……magembe alijiandaa mwenda kwenye shughuli zake za kichawi…….na ilipofika mida ya saa sita za usiku magembe alitoweka kichawi…alikwenda kwenye mti mkubwa wa m-buyu mti huo huwa anautumia na washirika wake kwenye vikao vyao vya kichawi…..alipofika alikuta tayari wale wachawi wengine wameshafika… kisha akasema leo ni siku maalumu ya kutimiza ahadi ya mwenzetu peto… hivyo inatakiwa chales aletwe usiku huu kwa ajili ya kafara.
ule upande mwingine alionekana peto akiwa nyumbani kwake…. alikuwa na wasiwasi kuhusu mwanae chales peto aliamua kuelekea mpaka kule kwenye mbuyu… alipofika alijipaka mafita ya binadamu… mafuta hayo ni ya kutoka kwenye mwili wa mtoto mchanga… upande wa katikati ya moyo….. baada ya peto kujipaka mafuta hayo punde alianza kuwaona wenzake alizipiga hatua mpaka pale walipokuwa…..alitoa salamu kwa ishara kisha akajumuika na wachawi wenzake..
punde magembe sliamuru chales aletwe… peto alichanganyikiwa alianza kulia huku akimsihi magembe asimdhuru….hakuna namna hili ni agano la mungu wetu wa kuzimu""magembe alijibu""
punde chales aliletwa…… chales alistahajabu kumkuta baba yake pale….. kisha magembe alimgusa kichani chales akawa hawezi kusema wala hakuweza kuona tena yale yanayoendelea…kisha magembe aliamuru chales alazwe juu ya gogo lililokuwa chini…… kisha peto apewe kisu amchinje mwanae ili kafara lifanyike.
peto aliamua kutimua mbio akatokomea kusikojulikana…..
Peto alionekana akielekea kwa mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la KANGALA…..akaomba msaada… kangala amsaidie kumuokoa mwanae… kangala alikuwa ni moto wa kuotea mbali alikuwa ni mchawi kutoka SUMBAWANGA…..alikubali kumsaidia peto… kisha akampa kipande cha mkia wa FISI iwe kinga kwa peto..
ule upande mwingine kule alipokuwepo magembe na wachawi wenzake..
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi Shawishi Wapenzi wa Simulizi Wapakue(Install) App ya CnZ Media