NILILALA NA MAITI 20 ILI NIOLEWE NA RAIS (10)

Zephiline F Ezekiel
0

SEHEMU YA KUMI
ILIPOISHIA...
Macho yake yalikuwa na rangi tofauti tofauti. Yalikuwa yakibadilika kama taa za disco kila alipokuwa akinisogelea. Kichwani hakuwa na nywele hata moja zaidi ya kuwa na manundu manundu na aliponikaribia karibu zaidi ndipo nikagundua kuwa kichwani kuna sehemu za siri za wanawake wengi zimeganyanyika gawanyika.

IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI

ENDELEA...
Akanifikia karibu.

Adela mke wangu mpya!”

Aliongea kwa sauti ya kutetemesha hali ilionifanya mwili kudhoofu kwa muda. Mkono wake ulikuwa umenakshiwa kwa midomo ya watu wa duniani. Nikageuka nyuma kumuangalia Diana.Patupu! hakukuwa na Diana na hata wale watu wapambe pembeni walikuwa kama wameganda kwa mshangao mithili ya mtu aliyeganda kwenye barafu.

“Mimi ndiye rais wa wachawi wote hapa Tanzania na leo nipo na mwanamke mzuri kama wewe. Nipo tayari kufunga ndoa na wewe. Kwanza nataka kuona utamu wako Adela!!”

Akaendelea kuongea kwa sauti ya kukwaruza na ya kiubabe. Akanishika mkono mpaka katika eneo kubwa lililokuwa limekaa mithili ya kitanda. Lakini ilionesha kuwa kitanda kimetengenezwa kwa kutumia ngozi ya binadamu hawa wa duniani. Akanilaza mpaka kwenye hicho kitanda. Akavua ngozi ya binadamu ambayo alikuwa amejiziba eneo la sehemu za siri. Tahamaki! Macho yangu yakakutana na mioyo ya watoto wachanga mingi mingi ikiwa imezunguka kwenye sehemu zake za siri uku uume wake ukionekana kwa mbali sana. Akanilalaia kwa juu nakutoa ulimi ambao nao ulikuwa umetanda kucha kucha hizi za bandia ambazo wanapenda kuzibandika sana kinadada wa duniani.

Nilijitahidi kuvumilia, moyo wangu ulikuwa tayari umejawa na ujasiri wa ajabu. Ujasiri wa kuvumilia lolote mbele yangu. Adela mimi nikajikuta nikikubaliana na yote. Yule Rais akanikumbatia kwa nguvu katika kile kitanda. Akachomoa yale makucha yake marefu nakuyapitisha mpaka katika sehemu zangu za siri nakuzitoboa toboa. Ile mikucha yake yote ikalowa damu, damu za kutoka katika sehemu zangu za siri. Akaanza kulamba zile damu.

“Hakika wewe mtamu sana Adela.. Haya inuka uanze kuninyonya..”

Aliongea yule Rais wa wachawi kwa sauti ile ile ya kukwaruza. Nilimwangalia mara mbili mbili. Akili yangu ikapingana na moyo, moyo ukasita nakukataa kutii amri ya yule Rais. Amri ya mimi kumnyonya eneo la sehemu zake za siri, Sehemu zake za siri ambazo zilikuwa zimezungukwa na mioyo ya watoto wachanga.

“Haiwezekani!!” Nikabisha kwa kuusemea moyo.

Nikauchukua mikono yangu miwili nakuielekeza moja kwa moja mpaka katika sehemu za siri za Rais. Nikaanza kuvuta ile mioyo ya watoto wachanga. Kadri nilivyokuwa nikiivuta ndivyo na Sauti za watoto wachanga zilivyokuwa zikipaa zaidi. Ndani ya muda mchache eneo lote likatapakaa damu. Yale maji niliyodhania niko chini ya bahari yakawa yamesalimiana na hizi damu za mioyo ya watoto wachanga kutoka kwa huyu rais wa wachawi. Bahari yote ikatapakaa damu. Hofu! Giza likaanza kutanda eneo lote kunizunguka mimi. Rais akabaki kumetameta peke yake. Nikashuhudia ile mikono ya Rais ambayo ilikuwa imezungukwa na midomo ya watu ikitoa sauti kali uku ikitetemeka.

“Adela, Adela kwanini unataka kumuua Rais wetu..”

Ile mikono ikaanza kutoa maneno yakijirudia rudia mara mbili mbili. Sepa! Nikaanza kurudi kinyume nyume nikitaka kukimbia katika eneo la wachawi. Yule rais hakuwa na uwezo wakunifuata hata kuningelesha tena zaidi ya kunitazama tu kwa macho. Nikaendelea kupiga hatua moja baada ya nyingine nikirudi kinyume nyume. Nikiwa bado katika hali ya kumshangaa Rais wa wachawi. Tahamaki! Mara ghafla nikapokea vibao kupitia mashavu yangu yote mawili. Nikaigeuza shingo yangu kuangalia ni nani. Patupu! Hakukuwa na mtu yeyote. Ujasiri! Nikaacha kurudi kinyumenyume nakuanza kwenda mbele sasa.

“Liwalo na liwe!” Niliusemea moyo

Huku nikizidisha kasi ya kuelekea mbele alipokuwa yule Rais akimetameta. Hatimaye nikamfikia kwa ukaribu mpaka pale kwenye kile kitanda aliniweka awali kwa ajili ya kufanya mapenzi na mimi. Hasira! Nikatoa mikono yangu miwili nakupeleka mpaka shingoni mwake. Nikaanza kumkaba, Kumkaba kwa kutumia nguvu zangu zote nilizokuwa nazo. Rais akaanza kuweweseka. Akaghafilika kwa ujio wangu tofauti. Nikazidisha nguvu zaidi ya simba dume.

“Huu ndio mwisho wako mchawi mkubwa wewe, Wewe ndio chanzo cha mimi kuwa hivi. Sasa wakati wako umefika”

Rais alibaki kimya mithilili ya mtoto mchanga aliyeona kitu kikimzunguka. Alibaki akiwa hajitambui zaidi ya kuendelea kumetameta. Kwa ushupavu niliokuwa nao niliyatoa meno yangu kwa ukali yakaanza kusalimiana na sehemu za siri za Rais. Nikaanza kuitafuna ile mioyo ya watoto wachanga ambayo ilikuwa imepambwa vilivyo katika sehemu zake za siri. Nikaitafuna tafuna kisha nikaimeza. Nikaanza kuitazama mikono. Zamu ya mikono. Nikaanza kuitafuna ile midomo ambayo nayo ilikuwa imezunguka mikono yote. Mdomo wangu wote ukatetwa damu kwa kusalimiana na damu za midomo katika mikono ya Rais. Rais akaishiwa nguvu nakudondoka chini kabisa. Kule kumetameta kukazimika kama Umeme wa tanesco unapozimika usiku. Ule mpango wa mimi kuolewa na Rais ukawa umeyeyuka rasmi.

“Adela? Adela?”

Sophy aliita kwa sauti ya juu na ya ukali. Alikuwa peke yake eneo la pembeni yangu huku akiwa mtupu kabisa.

“Umemfanyaje tena Rais wetu Adela? Kwanini umemuua mungu wetu Adela?”

Kau! Nikanyamaza. Sophy akaanza kunifuata mpaka pale nilipo. Aliponikaribia karibu tu naye nikamgeuza kitoweo. Nikaanza kumtafuna. Nikaanza kuhisi mwili wangu kurudi katika ubinadamu. Nikakamaa mithili ya wale watu wenye ugonjwa wa kifafa. Macho yangu yakawa yakiangaza vikundi mbalimbali vya wachawi wakiwa na viongozi wao wakifurika huku nao wakionesha kuzunguka mwili wa rais pale chini. Wakalia kwa vikwifukwifu. Na huo ndio ukawa mwisho wa utawala wa rais wa wachawi. Bwana Mchungaji nimesimama hapa mbele yako na waumini wote wajue na waeneze habari hizi popote. Huu wote ni Ushuhuda wangu. Mwenye masikio amesikia na hata amesimuliwa.

“Pigeni makofi, Aleluya!!!” Mchungaji Joseph akadakia kisha waumini wote wakaitikia.

“Asante kwa ushuhuda wako uliotoa hapa kanisani. Hakika Mungu amekujalia vitu vingi sana na umepigana kuwaonyesha kuwa unaweza. Kuanzia Leo tutakubatiza na hutoitwa tena Adela bali utaitwa Angelina yaani malaika wa Mungu. Aleluyaaaa!!!”

Waumini karibu wote kanisani wakabaki wakitoa machozi kwa ushuhuda wangu jinsi ulivyokuwa mrefu na wakusikitisha. Kuna waliozimia na wengine kutokuamini na hata wengine kupiga makelele ya mapepo kuonesha bado wanasumbuliwa na wachawi. Yale maziwa yangu ambayo nilikatwa kwa nguvu ya kichawi yalibaki kwa wachawi. Hivyo nilivyokuwa binadamu tena upya nilishangaa kurudi nikiwa na maziwa yangu kamili yote mawili. Nasema namshukuru sana Mwenyezi Mungu hakika wewe ni wa ajabu sana.

Hakika duniani kuna maisha mazuri na yenye kila aina ya kumfurahisha mwanadamu wa sasa ama kumchukiza. Angelina leo hii nimeokoka na nimeshampokea bwana Yesu awe awe mwokozi wa maisha yangu. Nitatembea na Yesu kila mahali nikilitangaza jina lake milele. Hakika kwa Bwana kuna msamaha na leo hii nimesamehewa.

MWISHO

 Ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi Shawishi Wapenzi wa Simulizi Wapakue(Install) App ya CnZ Media

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)