NILILALA NA MAITI 20 ILI NIOLEWE NA RAIS (9)

Zephiline F Ezekiel
0

SEHEMU YA TISA
ILIPOISHIA...
Hofu! Nilipomaliza kuikatikia tu maiti ya mwisho. Manyunyu yakaanza kudondoka mpaka chini kuashiria mvua inataka kuja.Ngurumo za mianga ya radi zikapenya katika mboni ya macho ya kichawi. Kila mmoja akaanza kutawanyika akikimbia pasipokueleweka.Mvua ikaanza kunyesha. Mvua kubwa ile ya mawe.

IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI

ENDELEA...
Nikainuka namimi kutaka kuondoka lakini nikajihisi miguu mizito kutembea. Nikainua mguu wa kulia ukainuka lakini nyayo zikabaki. Nikainua na wa kushoto napo ukaacha nyayo katika ardhi. Maumivu makali yakanijia mwilini. Nikajikuta eneo lote nikibakia na zile maiti ambazo nilitoka kuzinyonya na kuzilala.Maiti zile zikaanza kuinuka moja baada ya nyingine. Kila zikiinuka zilikuwa zikiweweseka nakuanguka tena uku nyingine zikijikaza mithili ya mazombi. Zililowana sana kiasi cha kuinuka zikiwa na tope tope jepesi. zikaanza kunifuta mpaka karibu zikitaka kuning’ang’ania mwili wangu.

“Niacheni ukoooo!!!”

Nilitoa sauti ya ukali lakini haikusaidia kitu kwani ndio kama nilihamsha na maiti nyingine pale chini. Zikanizunguka nakuniweka kati.Wakanikumbatia kwa wote huku mvua ikiendelea kunitandika mfululizo.Hawakuwa na sauti ya kuongea zaidi ya kutoa sura ya kikatili. Sura ya kumfanya mtu yeyote aweze kuogofya.Wakaanza kunishambulia kwa kunitafuna tafuna. Nikajihisi mwili kunyumbulika kama ilivyokuwa awali. Nikadondoka mpaka chini nakupoteza fahamu.

Adela?”

Nilishtuka nakujikuta nipo chini nimelala katika mazingira ambayo sikuayelewa. Nilikuwa ndani ya maji mengi sana mfano wa bahari. Ilikuwa ni kama dunia nyingine, kila mmoja alikuwa amenizunguka huku sura zao zikioneshwa kuwa na tabasamu la haja!

“Wewe nani?”

Nikauliza kwa ukali kidogo. Nikamuuliza yule dada aliyekuwa ameniita jina langu.

“Naitwa Diana! Nipo paomoja nawe, kwanza hongera!”

Nilijiangalia mara mbili mbili kwanini napewa hongera. Nikawaangalia na wale watu walioonesha kuwa tofauti sana kwani walikuwa wamevaa mavazi mazuri sana tofauti na wachawi wote niliowahi kuwaona. Walikuwa ni wasichana tupu. Shingoni na mikononi mwao kulijawa na dhahabu za kung’aa. Meno yao yalikuwa ya rangi ya silva.Yakimetameta!

“Hongera ya nini?”

Nikang’aka kwa utuli!

“Adela? Umefanikiwa kuwa na vigezo vyote vya kuweza kuolewa na Rais. Na kwa sasa Rais yupo ikulu anakusubiri kufunga ndoa nakuwa rasmi mke wake kuanzia leo kwa muda wa miezi miwili”

“Kweli?”

Sikutaka kabisa kichwa changu kiamini yasemayo na Diana. Nikayafumba macho. Halmashauri yangu ya kichwa ikafanya kazi haraka nakukumbuka kuwa kuna mtu niliambiwa anaitwa Diana ambaye alishawahi kuolewa na Raisi yeye ndiye atakayeniambia kila kitu jinsi ya kufika mpaka kwa Rais. Nilijikuta nikiushukuru moyo kwa uvumilivu ulioonesha nakuniongoza mpaka nilipofika. Zile ndoto zangu za kuolewa na Rais zikawa zimeshakubaliana na akili yangu. Nikainuka nakumkumbatia Diana. Diana akanishika mkono nakuniongoza ndani ya maji kuelekea uko ikulu kwa ajili ya kufunga ndoa.

**** Adela atafanikiwa kufunga Ndoa na Rais? Na ni Rais yupi huyo? Kundi la kichawi la kina Sophy wanajua hilo? Na itakuwaje kama wakijua?

**** Nini hatma ya Adela baada ya misukosuko yote hiyo? Tatizo la umeme linafanya simulizi hii iwe inachelewa kufika muda muafaka. Tuvumiliane kwa hilo ukiona inachelewa kutoka kama ilivyopangwa. Soon Tanesco wataelewa tu!

* Simulizi hii iko katika hatua za kuhamishiwa katika kitabu chake ‘kijarida’ ambacho hutotaka kukiweka chini ukianza kukisoma. Kaa mkao wa kukisoma Tanzania yote kitapatikana.

**** Simulizi hii ni ya kweli na mambo yaliopo ni ya kweli kwa wachawi hakuna hata kimoja kilichobuniwa. Najua lazima kuna baadhi ya wachawi watakuwa wameiona simulizi hii ama kuambiwa na watu. Ni kwamba Adela ameahidi kuwaumbua wachawi wote na njia zao zinazotumika ili watu wa duniani wajue. Kwa pamoja tunaupinga uchawi

“Kwani Diana? Rais mwenyewe sio yule wa duniani?”

“Adela? Unatakiwa uvute subira mpaka tufike tunapokwenda ndio umuone Rais wako. Na hapa ninavyoongea yupo ikulu na maaskari wengi sana wanakusubiria uku wakipiga matarumbeta kwa shangwe.Majigambo! Yaani mimi mwenzako nilifaudu kweli sikutaka hata muda uishe lakini ndio hivyo tena kwa sheria za kichawi ni miezi miwili tu kuishi na rais wetu huyu na siku zako zikiisha ni lazima akukate sehemu zako za siri nakuzibandika kichwani mwake ili asizeeke mapema nakukuacha ukirudi katika kambi yako ulipotoka ya kichawi”

Diana alijiza maneno matamu nakuikuta mwili ukiwa katika shauku zima la kufika uko niendako, nilitamani na mimi niwe na huyo rais toka nilivyoambiwa.sikulijali kabisa swala la kukatwa sehemu za siri na tena na rais anayeheshimika duniani. Nikajipa moyo konde!

”Kwahiyo Diana huyo Rais anayajua mapenzi ennhhh?”

“We weee Adela! Kwa mapenzi kwa rais ndio umefika. Wewe ngoja ukifika utaona mwenyewe. Ndio maana nakwambia nilitamani sana muda uongezwe miezi miwili ni michache jamani kufaidi mapenzi na rais wetu huyu!”

Njia nzima Adela mimi nilikuwa kama nimemwagiwa maji tena yale maji yenye ubarafu ndani yake. nilikuwa mtu wa kusisimka ovyo kila nilivyotajiwa jina la rais. Nilijipa mawazo mengi sana.Mawazo ya kuishi maisha mapya na rais niliokuwa nikitamani sana kuwa naye. Mabinti wale warembo waliokuwa wamevalia nguo za dhahabu na meno yao ya ming’aro bado walikuwa nyuma yetu wakitusindikiza. Njiani tulipishana na wengine tena wengi na wote hakuna hata mmoja aliyetusemesha zaidi ya kuonesha sura za tabasamu. Tabasamu la kunipokea! Tuliendelea na safari ya kupita chini ya maji mengi kwa urefu kidogo bila hata ya kuchoka wala kuogelea. Tulikuwa tukitembea kawaida sana kama tukiwa nchi kavu tu. Mchawi yeyote anauwezo wa kutembea juu ya maji au ndani ya maji pasipo kulowana hata tone. Na yote huwa ni kwa nguvu za kichawi.

“Adela?”

Aliita Diana kwa utuli. Kimya! Akanikagua mwili wangu juu mpaka chini kisha akaninyooshea mkono upande wa pembeni yangu.

“Umepaona paleeee?”

“Ndio kwani kuna nini Diana?”

“Pale wanapopiga matarumbeta ndipo kuna rais ambaye anakusubiri mfunge ndoa. Na wale wapambe wote ni mapolisi na mabodigadi wake. Unachotakiwa ni kunisubiri hapa hapa nikakuletee nguo za harusi upande ule.Nisubiri!”

Aliongea Diana na kuniacha nikiwa na maswali mengi kichwani. Macho yaliendelea kumuangalia Diana lakini akili haikuwa kwake. Nilibaki nikijiuliza moyoni.

“Inamaana ni ndoa ya kichawi au?”

Niliuchukuwa mkono wangu nikapiga kifuani kwa hasira. Upuuzi! Nikageuka nyuma na kutaka kutoroka niondoke zangu. Nguvu za kichawi! Kitendo cha kuinua mguu tu nakugeuza nikashangaa nyao zikibaki chini kama ilivyowahi kunitokea hapo awali. Nikauinua na mguu mwingine nao ivyo ivyo. Nikaanza kuhisi maji yanaingia mwilini mwangu yakiniingilia kutokea chini ya miguu zilipobanduka nyayo. Mwili ukawa mrefu sana na mnene mithili ya mti wa mbuyu. Sikujali! Nikaanza kurudi nyuma nilipotoka. Kadri nilivyoanzisha spidi ndivyo na mikono yangu ilivyokuwa ikituna kwa kujawa na maji mengi.

Mkono wa kushoto ukatuna sana maji ukapasuka nyang’anyang’a chini. Ukagawanyika vipande vipande. Sikutaa kuzubaa nikaendelea na safari ya kutoroka tena, nikashangaa mkono wa pili nao ukipasua vipande vipande nakuanguka mpaka chini.Mikono yangu yote ikiwa haipo. Nikabaki nikiongozwa kwa miguu pekee pasipo mikono. Kila hatua nilivyokuwa nikizidisha kupiga ndivyo na miguu nayo ilikuwa ikinivimba. Nikahisi nayo ikijaa maji nakutanuka kuwa mikubwa sana mithili ya mnyama tembo. Nguvu ya kukimbia sikuwa nayo tena, nikabaki natembea.Tena nikitembea ule mwendo mdogo wa mnyama ‘tembo’.

“Adela? Adelaaaaaaaaa??”

Nikasikia sauti ya Diana ikiniita kwa mbaali sana. Nikainama chini nakumuona Diana mdogo kama sisimizi. Nikasogeza sikio langu kumsikiliza. Akapanda na kulishikilia sikio langu. Nikainuka naye akiwa kaning’inia kwenye sikio langu la upande wa kushoto.

“Adela, nini tena unataka kufanya?. Hili ni zaidi ya eneo la kichawi na kamwe usijaribu kutoroka kabisa!. Rais amekasirika sana baada ya kuona unataka kumkimbia. Na hajaamini kama kweli umeshalala na maiti ishirini. Hakuamini tena na akikasirika zaidi utarudi tena duniani ukachomwe moto na watu wa duniani wasiotupenda tuwe wachawi.”

Maneno ya Diana yaliuchoma sana moyo wangu. Diana akajishikiza karibu na pua yangu nakuteremka mpaka kwenye lipsi ya mdomo wangu uku akipishana na machozi yaliokuwa yakianza kunibubujika. Akatumia mikono yake kuutanua mdomo wangu. Akadumbukiza dawa ndani yake. Dawa yenye nguvu za kichawi.Akatoka mpaka nje nakudondoka chini. Ile dawa ikanifanya nijisikie kizungu zungu kwa muda nikiweweseka. Nikadondosha limwili langu mpaka chini nakuanza kunywea nakurudi katika mwili wangu ulivyo kuwa. Nikawa mdogo

“Adela?”

“Ndio Diana”

Sikuamini kama ndani ya ule muda mfupi nilikuwa nimerudia katika ile hali yangu ya Adela yule wa zamani. Viungo vyangu vyote vilikuwa vimeshajikusanya nakuwa Adela mpya aliokamilika viungo vyote. Diana akanikabidhi nguo nzuri na za kung’aa. Nikazivaa kisha akanipa saa na pete inayong’aaa vyote vikanipendeza sana.

“Tanua mdomo Adela?”

Nikatanua, Diana akaniweka meno ya bandia. Yale meno yenye mng’aro wa silva.Nikametameta! Diana akanishika mkono nakuongoza tena tulipokuwa mwanzo pale ambapo niliona umati wa watu kwa mbali ukisherekea kwa matarumbeta. Ambapo Diana aliniambia kuwa rais ananisubiri tufunge ndoa. Mikononi walinipa nishike kichwa cha binadamu tena cha mtoto mdogo ikiwa ni ishara kama ua. Gauni langu lilikuwa lakumetea meta sana hali iliyofanya kule kumetatmeta kushindane na mwanga wa maji. Hatimaye baada ya hatua kadha tukawa tumeshafika eneo ambalo rais alikuwa akinisubiria kwa hamu.

“Adela, rais huyo hapo anakuja kukuchukuwa mpokee na mpige busu uondoke naye!”

Aliongea Diana kwa kunong’ona kupitia sikioni mwangu. Macho kodo! Sikutaka kuhamini.

“Jesus!”

Hakuwa rais yule wa duniani niliyemdhania bali alikuwa ni rais wa wachawi. Mwili wake mkubwa na weusi uliopitiliza mithili ya dikteta yule wa zamani wa Uganda ‘Idd Amin’. Minyamanyama ya mwili wake ikanifanya kuogofya sana. Mwili wake ulikuwa umezungukwa na vichwa vya watoto wachanga zaidi ya thelathini tena vikitoa machozi kwa kulia kwa uchungu. Macho yake yalikuwa na rangi tofauti tofauti. Yalikuwa yakibadilika kama taa za disco kila alipokuwa akinisogelea. Kichwani hakuwa na nywele hata moja zaidi ya kuwa na manundu manundu na aliponikaribia karibu zaidi ndipo nikagundua kuwa kichwani kuna sehemu za siri za wanawake wengi zimeganyanyika gawanyika.

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

 Ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi Shawishi Wapenzi wa Simulizi Wapakue(Install) App ya CnZ Media

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)