Mtunzi: Andrew Carlos
SEHEMU YA PILI
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
Huruma kama ya mwanamke aliyetoka kujifungua.Nikatamani sana kuingilia kati kwenda kuwazuia lakini nikaogopa huenda ningefanyiwa kitu kibaya kwa kuharibu mila zao hivyo nikabaki nikiwaangalia huku machozi ya uchungu yakiendelea kunidondoka kwa huruma. Niliendelea kupatwa na hasira kali haswa kwa jinsi mabinti walivyokuwa wakifurahia kwa kupiga makofi.
IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI
ENDELEA...
“Adela? Adela njoo hapa kati?” Mmoja kati ya wale wazee aliniita jina langu la Adela. Sikutaka kuamini kama anayeitwa ni Adela mimi. Niliyageuza macho yangu kuwaangalia wale mabinti huenda mmojawapo anaitwa Adela. Cha kustaajabu kila mmoja alikuwa akinitolea macho mimi kana kwamba anayeitwa ni mimi. Nilijihisi mwili kunitetemeka sambamba na mkojo kunichuruzika huku nikirudi nyuma nyuma nikihema juju. Kwakuwa nilikuwa eneo kama hewani sikuweza kujua wapi pa kutokea na wapi pa kuingilia hivyo nilibaki nikirudi nyuma nyuma nisijue naelekea wapi. “Sitaki niacheni jamani, niacheniii?” Nilijitahidi kutoa sauti lakini haikusaidia kuwanyamazisha wale wazee kwani ndio kwanza waliendelea kunisogelea kwa ukaribu huku lile rundo la mabinti wakiwasindikiza kwa nyuma yao.
Hatua chache nyuma nilishangaa kama nimejikwaa, kwani nilijikuta nikidondoika mpaka chini nakulala kifudifudi kisha viungo vya binadamu vilidondoka kwa kunizunguka. Vipande vipande kuanzia mikono, miguu na viungo vya sehemu za siri za wanaume ambazo vilikuwa vikitoa harufu kali sana. Haraka haraka nilivuta kiungo kimojawapo na kutaka kuwarushia wale wazee waliokuwa wakinifuata mbele yangu. “Weee!! Wee!! Weeee!! Thubuutuuu!!? Mpumbavu kabisa wewe!. Unajua thamani yake hivyo vitu ulivyovishika?” Nilibaki nimeyakodoa macho yangu kwa kustaajabu maneno ya mzee aliokuwa akiniongelesha. Nilijihisi kutetemeka zaidi mwili wangu. Wale wazee wakainama hadi chini nilipokuwepo na kisha wakaanza kuniingiza vidole katika sehemu zangu za siri huku yule mzee mmoja akininyonya papi zangu huku akinimwagia damu nyingi ndani ya mdomo wangu.
Damu damu ambazo bado zilikuwa zimebaki kwenye mdomo wa yule mzee zote kwa kula nyama za yule mtoto zote zikahamia mdomoni kwangu. Aliufanya mdomo wangu atakavyo huku mzee mwingine na yeye akichezea sehemu zangu za siri sambamba na maziwa yangu atakavyo. Niliumia sana moyo wangu. Nilipingana na akili yangu chafu iliyoshinikizwa na nguvu za kichawi kuingia kaburi la mama yangu mpaka kufika huku. nilibaki nalia kwa vikwifukwifu. “Jamila?” Yule mzee aliokuwa akinichezea sehemu zangu za siri aliita kwa sauti ya juu huku akiwaangalia wale mabinti. Hapo hapo halmashauri yangu ya kichwa ikafanya kazi haraka nakugundua kuwa kumbe mmojawapo kati ya wale mabinti anaitwa jamila. Punde huyo jamila alijitokeza. ”Abee baba!” “Nenda kule kwa mama yako kanitafutie lile panga langu” Niliposkia tu panga nikajihisi mapigo ya moyo kukosa ushirikiano. Nikajua hata kama mfu nauliwa tena sasa sijui ndio nitakuwa mfu wa kweli ama mfu wa pili baada ya kufa mara mbili. Mwili wangu ukawa hauwezi kunyanyuka wala kufurukuta zaidi ya kuukabidhi kwa wale wazee waufanye watakavyo.
Wakiwa bado wanamsubiri |Jamila.Yule mzee aliokuwa akininyonya mdomo wangu akaendelea tena kuniyonya mpaka mdomo wake ukabadilika rangi nakuwa nyekundu si nyekundu na hata bluu si bluu. “Hili hapa baba!” Sauti ya Jamila nikaisikia kwa mbali kama ikikabdihi hilo panga aliokuwa ametumwa. Macho yangu yakawa hodari kwa kuangalia ni panga kweli au la!. “Mhh!! ama kweli?” Nilibaki nausemea moyo baada ya kuona mfupa mkubwa sana ukiwa umekaa mithili ya panga Jamila akimkabidhi baba yake. “Adela?” “Abee baba!” “Unawaona wenzako wote hao waliokuzunguka hapa?” “Ndio nawaona” “Embu jaribu kuwaangalia vifuani mwao?” Nilianza kuyatoa macho yangu kwa kuaangaza wale mabinti waliokuwa wamenizunguka. Japokuwa walikuwa uchi wa mnyama. Niliweza kugundua kuwa hawakuwa na maziwa vifuani mwao. “Nimewaona tayari” “Umegundua tofauti yao na yako ipi?” “Hapana baba sijagundua chochote” Ilinibidi kuwaongopea kwa makusudi ili niepukane na kukatwa kwani nilijua wazi wanataka kunitoa maziwa yangu nifanane na hawa mabinti.
Yule mzee alichukuwa lile panga na kuanza kunikata nalo ziwa moja baada ya jingine. Sikuwa na nguvu ya aina yeyote tena na wala sikusikia maumivu zaidi ya kuhisi kama natekenywa. Ni dhahiri kuwa lile panga lilikuwa na dawa zao za kuweza kumpumbaza mtu anapokatwa asisikie maumivu yeyote. Alipomaliza kunitoa maziwa yangu yote mawili akawarushia wale mabinti wakaanza kugombania kwa kuyala bila kujali limbi la damu zake. Nilitamani sana kutoa sauti kwa ukali ya kuwatukana lakini nilishindwa. Tayari nilikuwa kama nimefanyiwa dawa za kutokutoa sauti kwa kipindi. Nilibaki kuwa kama mtu aliyefungwa mdomo kwa kutokuwa na uwezo wa kutoa sauti. ”Adela, sasa umekamilika mwanetu, inuka?” Nilidhani utani kuwa nisingeweza kuinuka. Nilishangaa nguvu za ajabu zikinirudia na kuweza kuinuka kutoka pale chini.
Maswali mengi yalibaki kichwani mwangu ikiwa ni pamoja na kuyatoa maziwa yangu, pili sijaona damu zozote wala maumivu ya aina yeyote na tatu nilishangaa kuishiwa nguvu zote na baada ya kukatwa nilipata nguvu ya kuinuka. “Sasa waweza kwenda pale ukakutane na kiongozi wako uanze kazi leo leo,sawa Adela?” “Sawa baba!” Niliondoka kiunyonge huku nikijihisi kama aibu kubwa imenitawala Adela mimi. Kwa mwendo wa taratibu huku nisielewe mazingira ya chini yapoje poje kwani hayakuwa na vumbi wala ardhi yaani yalikuwa ni kama angani tu. Ndani ya muda mchache nikawa tayari nimeshafika kama nilivyoelekezwa na wale wazee walionitoa maziwa yangu na kuwapa wale mabinti wagawane kwa kuyatafuna. “Adela mwanangu umekuja?” Aliongea yule mama wa kwanza kabisa. yule alioniambia kuwa ni kiongozi wao na atanipangia kazi ya kulala na maiti ishirini. “Ndio mama” “Umependeza mwanangu! Hivyo ndivyo mabinti wakike wanavyoishi huku kwetu. Si umeniona hata mimi sima maziwa? Yaani huku hayana kazi maana kama mimba hatupati, watoto wanaliwa na wazee na hawaruhusiwi kuishi sasa miziwa niwe nayo inafanya kazi gani?”
Nilijiangalia mara mbili mbili kifuani mwangu kwa hasira ya hali ya juu. Yale maziwa madogo dogo na ya kumvutia kila mwanaume sasa yakawa hayapo tena katika kifua changu. Yametolewa na wale wazee wachawi wenzangu. Niliumia sana lakini kwa kuwa tayari nilishakubaliana na nguvu ya kiuchawi ilinibidi yatolewe. “Adela?” “Abee mama!” “Kuanzia sasa usiniite mama, mimi siyo mama yako sawa? Mbona mimi sikuiti mwanangu nakuita Adela? Nataka uniite Sophia ama sophy, tumeelewana Adela?” “Ndio maama nimekuelewa” “Haya sogea karibu yangu hapa nilipo kisha nikumbatie kwa nguvu” Aliongea yule Sophy kwa sauti ya ukali akinisisitizia kwa mkazo. Nilitahamaki maneno yake ya ukali lakini nilijikuta naingiwa na moyo wa subira. Moyo wa kuvumilia yote nionayo na nisikiayo. Mwili wangu bado ulikuwa haujakamilika kabisa kwa uchawi kwani nilianza kuhisi woga woga ukininyemelea kila muda niliokuwa nikiongea na Sophy. Hata aliponisihi nimsogelee na kumkumbatia bado nilikuwa nikimuogopa.
“Hivi unanisikia Adela ninachokuambia? Au unataka nikurudishe kule kwa wazee ulipokuwepo wakakuchezee tena mwili wako?” “Hapana mama, anhh nisamehe!!. Hapana Sophy!” Kwa uoga uliochanganyikana na aibu kwa mbali ilinibidi nimsogelee na kisha nichukue mikono yangu na kupitisha mabegani mwake kwa lengo la kumkumbatia kama alivyohitaji. *Baridi kali lilikuwa likiendelea kuusumbua mwili wangu. Kiza kinene kiliyashinda macho yangu angavu.Macho yenye nguvu ya kuangaza popote sasa yakawa hafifu. Hafifu kwa kutoweza kuona vizuri mbele wala nyuma.Nikajikuta nikiwa juu ya mti mkubwa sana. Mti aina ya mbuyu uliopukutika majani yake na kuwa mkavu. Nafsi yangu iliuliza moyo lakini akili ilibaki kutokujua na kukataa kuujibu moyo juu ya kinachoendelea.Sauti za ndege aina ya popo na bundi ndizo zilienea zaidi. Mwili wangu haukuwa mwili wa kawaida tena kutokana na kujikuta nimezungushiwa shanga na hirizi karibu mwili mzima na mikononi nikiwa nimefungwa vitambaa vyekundu.Pembeni yangu alikuwepo Sophy akiwa amebebelea ungo mkubwa uliokuwa umejaa vibuyu,vidole vya watoto,masikio ya watu wazima pamoja na mikia. Sikuelewa vizuri ilikuwa ni mikia ya mnyama gani kutokana na mikia kuwa mirefu sana. Sophy alionesha kufurahi jambo huku akinitazama usoni mwangu. “Adela sasa kazi yetu inaanza rasmi sasa hivi.
Na hapa nilipo nipo kwa ajili ya kukuonesha tu utakavyokuwa unafanya na siku nyingine utakuwa unakuja peke yako mpaka utakapomaliza zoezi la kulala na maiti zote ishirini, umenielewa Adela?”“Nimekuelewa Sophy”Nilijibu kwa kujiamini kana kwamba tayari ni mchawi aliyekamilika.Baada ya hapo Sophy akachukuwa Mikia miwili na mmoja wapo akanikabidhi kisha akaniamuru ule mkia niwe nauchovya kwenye kibuyu kuna nguvu zetu za kutulinda tusionekane na wala tusikamatwe na mtu yeyote na hata tukikutana na mchawi ambaye hayupo katika himaya yetu asiweze kutudhuru. Nilifanya hivyo pamoja na Sophy naye alikuwa akifanya hivyo hivyo huku tukishuka kwa kuteleza chini ya mbuyu taratibu, na tulipofika chini kabisa nilishangaa kukutana na makaburi mengi yakiwa yamejipanga.“Adela?”“Abee Sophy?”“Haya ni makaburi ya Mwananyamala, na kwa kuanza chukua hiki kibuyu kitakuwa kinakuongoza.
Unapita mstari huu wa makaburi uku ukiyapandia juu yake mpaka kule mwisho na ukijiona mzito unashindwa kwenda mbele ujue hilo ni kaburi la mwanaume ambaye amezikwa leo leo. Haya tuanze mimi nipo nyuma yako taratibu”Nilijikuta nauvaa moyo wa kijasiri na wakiuchawi. Woga uliniyeyuka ghafla na kuvaa ngozi ya kichawi tena yule mchawi aliyekubuhu kwa uchawi. Nilianza kupiga hatua huku nikifuata mstari wa makaburi kwa kuyakanyaga juu yake. Nilifanya hivyo kwa zaidi ya makaburi sita lakini nilipolikaribia kaburi la saba nilishangaa mwili wangu kama kutetemeshwa. Ganzi! Ndio ganzi mithili ya shoti ya umeme ilikuwa imeninyuka katika miguu yangu vilivyo. Nilitetemeka nakutaka kuanguka mpaka chini.“Adela? Nini tena unafanya? ““Sophy nashindwa kutembea, nashindwa nivute?”
“Hivi unajua kuwa ilo sio kaburi unalotakiwa kulichimba leo. Na kaburi hilo uliokanyaga ni la zamani sana. Na ukionea miguu inatetemeshwa ujue hilo kaburi litakuwa la mchungaji ama kiongozi wa kanisa au msikiti. Na mara nyingi huwa inatutokea tukiwa katika mawindo yetu haya. Sasa si unaona na maua kabisa yanaonekana yamewekwa leo. Watakuwa walikuja kulisafisha na kuliombea mchana au asubuhi”“Ndio”“Lazima utakuta waliweka maji yao ya Baraka sambamba na kuliombea lakini usijali Adela, dawa zetu zina nguvu zaidi yao twende.”
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi Shawishi Wapenzi wa Simulizi Wapakue(Install) App ya CnZ Media
