HAA! KUMBE TAMU (3)

Zephiline F Ezekiel
0
Mtunzi: Frank Masai

SEHEMU YA TATU
ILIPOISHIA...
Mabusu hayo yaliendelea kumwagika kutoka katika kinywa cha Longino.na sasa yakawa yanaenda sambamba na mikono ya Longino kuingia ndani ya sketi ya Mercy. Sketi ambayo haikuwa imembana kama kimini bali ilikuwa imejiachia kama sketi za shule ya msingi.

IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA SIMULIZI

ENDELEA...
Hali hiyo ya sketi, ilimpa urahisi Longino kuyatabaruku mapaja ya Mercy kwa kuyapapasa na kuyashika shika kwa utaratibu kama achaguaye nyanya au embe.

Mikono mikakamavu ya Longino iliendelea kutalii kwenye mapaja ya moto ya Mercy na wakati huo Mercy alikuwa hajiwezi kutokana na yale mabusu aliyokuwa anapigwa sehemu mbalimbali.

Mercy akawa macho legevu na pumzi zikizidi kupishana bila kutoa nafasi ya kusubiri pumzi nyingine kutoka. Ungemuona, ungehisi labda anakata roho au ana kifafa.

Bado mkakati kabambe wa mikono ya Longino uliendelea kujipa raha taratibu kwenye mapaja ya Mercy huku sura zao wote wawili zîkionesha zipo katika hisia za mbali mno katika dunia hii.

Longino aliendeleza safari aliyoianza na safari hiyo ambayo ilitawaliwa na mikono, ilitaka kwenda hadi kushika lastiki ya chupi ya mwanadada yule kwa lengo la kuivua lakini hali hiyo ilipingwa vikali na Mercy.

Hakupinga kwa kuwa alikuwa hajatoa jibu kuwa kakubali, bali alipinga kwa sababu ilikuwa ni zaidi ya mapema kuvuliwa chupi na mwanakaka yule ambaye alibahatika sana kumchezea mwanadada yule kirahisi kuliko hata ilivyotegemewa.

"Hapana Long. Hatuwezi kufanya leo kwani bado mapema sana kukimbilia haya mambo. Hunijui sikujui, kwa nini kwanza tusijuane hasa katika afya na tabia?."Mercy alitoa ushauri baada ya Longino kukasirika kunyimwa mchezo.

"Mercy. Usione kama nimekutaka mapema sana kufanya mapenzi na wewe. Lakini nipo katika hamu mwenzako, na sifanyi kwa ajili ya kujiridhisha nafsi yangu bali kwa sababu nakuhitaji. Nakuhitaji sasa, na nitakuhitaji daima.Nitakuoa wewe Mercy na si mwingine."Mwanaume alijitetea kwa hisia kali.

Lakini kwa bàhati mbaya Mercy alikuwa bado hajamwamini. Juzi tu, alikuwa anamtaka rafiki yake, leo hii anasema ànampenda na ànamuhitaji. Hiyo haikumuingia akilini Mercy na àlimwona Longino kama mchezeaji tu.

"Long nakupenda sana tena sana. Naomba ufahamu hilo. Nitakupa chochote utakacho katika mwili kwa sasa kasoro ngono tu! Magonjwa na mimba Long. Unanijua? Unazijua tabia zangu? Hamu ya kufanya ngono isikupeleke kaburini. Tuchukue muda wetu kwa àjili ya kujuana kwanza.

Usidhani labda mi sina hamu. Nina hamu na wewe hata tufanye hadi asubuhi, lakini haiwezekani Long. Nahitaji kukujua japo kiafya,tabia tutarekebishana tu. Naomba unielewe."Longino alikuwa kimya wakati dada yule akionesha kuwa hakufika kidato cha tano bure, elimu yake anaweza kuitumia ipasavyo hata kwenye ushauri.

"Sawa Mercy. Nimekuelewa na samahani kwa nilichotaka kufanya. Nisamehe mpenzi wangu."Longino alimwomba msamaha dada yule na bila hiyana Mercy alielewa maneno hayo ya msamaha.

Walikuwa kama tayari wameshafanya kile kitendo, kwani baada ya kupeana misamaha, kila mmoja àlijirekebisha kimavazi na kuanza kuongea mambo mengine ambayo yalijenga zaidi mahusiano waliyoyaanzisha siku ile.

"Saa nane natakiwa kurudi kambini. Tutaonana baada ya wiki mbili kwa kuwa tutaenda kucheza na mechi huko Tunduma." Longino alimwambia maneno hayo Mercy na kuifanya hali ya furaha ya kimwana yule ipotee ghafla kama vumbi linapokutana na maji.

"Sasa mbona hukuniambia?."Mercy aliuliza kiunyonge.

"Ndio nakwambia hivyo totoo."Longino alijibu huku akishika nywele ndefu za mwadada yule.

"Basi mi nataka."Mercy maneno yalimtoka kwa kudeka huku akimsogelea Longino ili amchezee na mwisho wangonoke.

"Wataka nini sasa?."Longino aliuliza huku akitabasamu kwa kituko anachotaka kukifanya Mercy.

"Nataka hiyo."Swali likajibiwa na Mercy huku akioneshea sehemu ya zipu katika suruali ya Longino.

"Hapana totoo. Ujue mimi niliingiwa na shetani la tamaa za mwili tu. Ila kama ningefanya na wewe, leo mazoezini ningekoma.

Leo Jumatatu tunapigaga mazoezi magumu sana kufidia siku zote tulizokaa nyumbani. Na pia, tujenge uaminifu kwanza ndio tuingie huko. Michepuko mingi sana kwa sasa, si rahisi mimi kukuamini wewe wala wewe kuniamini mimi.Tuaminiane kwanza. Mwili wako upo, na wangu ùpo. Kama ukifa àu nikifa,hayo ni ya MUNGU, ila kwa sasa, ningependa tufahamiane afya zetu, kama ulivyotaka."Longino aliongea hadi akamfanya Mercy atabasamu kwa kuona sasa kapata mtu muelewa.

"Nakupenda Longino. Sina cha kukwambia zaidi ya hicho." Mercy alimkumbatia Longino huku akitamka maneno hayo.

"Nakupenda pia Mercy. Utakuwa kama Mussa kwa wana wa Islael. Umekuja kuukomboa moyo wangu toka katika fukwe za mateso ya mapenzi. Nitakupenda daima."Sauti yenye maneno matamu ilipenya vyema kwenye masikio ya Mercy na kumfanya Mercy ahisi kama yupo peponi karibu na Malaika.

*****

Siku hiyo nzuri kwa wapenzi wale ikaishia kwa kwenda kumchukua Jesca shuleni alipokuwa anasoma na kurudi naye kwa furaha huku Mercy akiwa mstari wa mbele kumpenda mtoto yule kwani alifahamu umuhimu wa kuuteka moyo wa Longino kwa kupitia pendo atakalompa mdogo wake.

Baada ya kukaa wote kwa muda, hatimaye ulifika ule muda wa Longino wa kurudi kambini. Muda ambao ndio kapangiwa na kocha wa timu ile ya chunya.

Bila hiyana alimuaga mdogo wake ambaye alikuwa katika majonzi kiasi kwa kuachwa na kaka yake kipenzi, lakini hakuwa na jinsi kwani kaka alienda kutimiza ndoto zake.

Kwa upande wa Mercy, yeye alimsindikiza hadi kituo kidogo cha kupandia magari yaendayo Wilayani. Walipofika huko, walibusiana kidogo na Longino alipanda gari huku akimwachia maneno machache ya “Nakupenda sana Mercy”, naye Mercy alijibu kwa aibu kuwa anampenda pia na hapo Longino alifunga kioo cha gari ile ndogo huku nje akimuacha Mercy akiondoka kurudi yalipo makazi yao.

*******

Longino alipokuwa katika gari ile ambayo ilishaanza safari ya kumpeleka ilipokuwa kambi yao, alianza kumfikiria Mercy uzuri wake. Akayakumbuka yale mapaja yake laini kama manyoya ya sufi, akaenda mbali zaidi akakumbuka jinsi alivyobaniwa kumvua nguo ya ndani binti yule. Hapo akatabasamu kidogo na kujiona kuwa alitaka kufanya jambo la kipumbavu sana.

Mawazo hayakuishia hapo, mara ya kuruka na kuanza kumuwaza Subira. Subira yule yule aliyemtupia vito vya shaba usoni. Subira mwenye mapozi kama anahela za kununulia hata kuku, kumbe hana chochote zaidi ya kumsubiri baba yake ajikune tako ili atoe wallet na yeye ndio apewe shilingi kadhaa za kwenda kununulia makochokocho ya kujipambia uso na mwili wake.

Eti ndiye aliyemtupia Longino vito usoni huku akivinadi kwa kebehi kuwa ni mabati. Hata kama ni mabati kweli, lakini ni zawadi. Tena zawadi ilitolewa fedha ili kununuliwa, sasa kwa nini aweke dharau zake kwenye kitu ambacho kimetolewa fedha? Au anajua labda Longino aliokota au alimuomba dada fulani mwenye navyo ndio akaletewa yeye. Wote hatujui, na itabaki kuwa siri yake. Siri iliyojazwa maswali kati yako msomaji na Longino muhusika.

“Nitamuonesha. Nitamuonesha kuwa dharau kwa mwanaume ni sumu kali ambayo hakupaswa kuionesha bali kukaa nayo moyoni.” Longino alijiwazia huku akigeukia upande wa kioo na kuanza kuangalia mandhari ya Jiji la Mbeya lakini mawazo hayakuwa katika mandhari hayo bali Subira.

“Sijui nitalipa lini hiki alichonifanyia, ila nitalipa tu! Nitamuonesha kuwa uzuri wa simu siyo muonekano wake bali programu zilizowekwa ndani yake. Anajidai mzuri sana, sasa kikomo cha hayo yote kimekwisha. Pozi zote zitamshuka tu! Hatujui wanaume, hajui kuwa hata farasi akichoka goti huangukia, na hata maji ya yakizidi ubaridi sana hayaitwi tena maji, bali barafu. Nitamuonesha hayo yote, ila Mercy nitampenda daima japo huyu mbwa bado yupo moyoni kwa sasa.” Longino na mawazo yake ya kisununu yaliendelea kumtawala hadi akajikuta akipitiwa na usingizi.

******

BAADA YA WIKI MOJA.

Nyumbani anapoishi Longino kulikuwa kunafaraja mpya kwa familia ile. Mercy alikuwa kila mara hakosi kwenda nyumba ile na kuwasabahi mama mkwe pamoja na wifi yake Jesca.

Kwa muda mchache tu! Mercy alikuwa kipenzi kikubwa cha familia ile. Ilifikia kipindi alikuwa hawezi kulala bila kwenda kuiona familia ya akina Longino. Ukweli ni kwamba , pale penye upele palipata mkunaji hasa. Na Mercy ndiye alikuwa mkunaji, alikuna kipele hata kile kidogo na kukisababishia kiwe kikubwa.

Hapa nina maana kwamba, kipele kidogo ni imani ya Mama wa Longino ambayo ilikuwa moyoni mwake juu ya Mercy.Mama Longino hakuamini kama kuna mapenzi ya kweli katika mahusiano ya sasa. Alijua mwanaye anaenda kuumizwa na yule mwanamke hasa ukizingatia Longino aliishia kidato cha nne na Mercy alikuwa anaelekea kidato cha sita.

Mercy aligundua hilo, kile kipele kidogo akakikuna vizuri na kuwa kikubwa. Yaani ile imani ndogo ya mama yule, akaitanua na kuwa kubwa. Akaonesha kuwa anajali, akawa mstari wa mbele kuisaidia familia ile kwa kazi ndogo ndogo, na kilichompa pointi zaidi, ni kumjali Jesca. Jicho ambalo familia ile ilikuwa kama mbogo pale itakapoliona lina tatizo. Mercy akawa karibu kabisa na Jesca, naye Jesca akafurahia uwepo wa Mercy. Hapo moyo wa Mama Longino ukatua mzigo wa kumfikiria vibaya mtoto yule wa kike.

Mercy akapewa kibali ambacho hakikuwa cha moja kwa moja, lakini ni kibali ambacho alipewa kwa kuwa alionesha kujali. Ni hatua ndogo sana aliyoipiga lakini ilikuwa ni hatua kubwa kuliko zote katika maisha yake.

Hatua kama ile ni wanawake wengi wanashindwa kuipiga kutokana na kujiwaza wao zaidi kuliko yule aliyefanikisha kumleta mtu yule wampendaye. Wanawake wengi wanadhani kumpata mwanaume ndio kumaliza kila kitu, hata wakikohoa dume litakurupuka lilipo na kuuliza kwa nini umekohoa.

Lakini wanasahau kuwa yule mwanaume ana familia. Yapaswa kuijali familia hiyo ili mwanaume aseme wewe ndiye unanifaa. Kama usipoijali familia ya mpenzi wako, sidhani kama utamjali na mwanaume kwani wewe utakuwa unamsumbua tu kuhusu familia yako. Mara mama anaumwa, mara baba anataka msuri, mara dada kafanyiwa oparesheni, na mengine kama hayo ambayo inafikia kipindi mwanaume anachoka na kuanza kujutia uamuzi wa kukuchukua. Hatua hiyo Mercy alijaribu kuipiga kabla hata hajaingia ndani zaidi ya familia ile. Heshima na utii alionesha kwa familia ile,sidhani kama kuna mwanamke wa kileo angefanya vile.

****

Kwa upande wa Subira, yeye aliringa kwa kuwa wazazi wake walikuwa wana kitu cha kumpa. Si wazazi pekee, hata kaka yake aliyekuwa analangua vitu kutoka Dar es Salaam, alikuwa anamlinda dada yake na kumfanya aonekane ni dada wa kileo.

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

  Ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi Zaidi Naomba Share App kwa Wapenzi wa Simulizi Wapakue(Install) App ya CnZ Media

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)