KITABU (2)

Zephiline F Ezekiel
0
Jina:
KITABU

SEHEMU YA PILI
ILIPOISHIA...
alipofika aliletewa habari aitangaze kwenye radio...alipoisoma habari ile ilikuwa ni taarifa ya ajali ya roli lililopinduka huko morogoro alafu dereva amekutwa amelala upande wa nje huku maiti yake ikiwa haina kichwa miguu pamoja na mikono.....

IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA SIMULIZI

ENDELEA...
Latifa alistuka akaogopa sana.....akaamua kuwaambia watangazaji wenzake kuhusu kitabu alichotunga chery....miaka kumi na mbili iliyopita(12) kwa sasa matukio na michoro iliyochorwa kwenye kitabu ndio haya yanayojitokeza kwa sasa!!!

watu waliokuwemo kwenye kipindi walistahajabu sana wakawa na shauku ya kutaka kikiona na kukisoma kitabu hicho.....

ilipofika saa kumi za jioni..latiffa alitoka kazini na kurudi nyumbani......akiwa njiani simu yake iliita...alipoitazama aliona mfanyakazi mwenzake aitwae BENJAMINI anampigia...alipoipokea simu hiyo.....benjamini aliomba watoke pamoja kwa ajili ya chakula cha usiku...latifa alikubali akasema"sawa ngoja nifike nyumbani nikabadilishe nguo... nitakujulisha nikiwa tayari....kisha akakata simu....latifa alipofika nyumbani kwake aliingia bafuni kuoga kisha akarudi chumbani kwake....akavaa nguo nyingine tofauti na alizokuwa amevaa kazini...kisha akatoka na kuzipiga hatua za taratibu huku akichezea simu yake.....alipofika barabara kuu..aliamua kumpigia Benjamini amfuate.....kisha akajisogeza kwenye mgahawa uliokuwa pembeni ya barabara akaketi na kuagiza soda....akaanza kunywa huku akimsubiri Benjamini..

**********

baada ya dakika kumi kupita.Benjamini alifika, Latiffa aliweza kumuona Benjamini kwa urahisi kwa sababu alikuwa ameketi jirani kabisa na barabara kuu...akanyanyuka na kulifuata gari la benjamini akafungua mlango na kuingia upande wa ndani...benjamini aliliwasha gari na kuliendesha mpaka SIX PARK HOTEL. walipofika waliagiza chakula na baada ya muda chakula kililetwa wakaanza kula.....benjamini akasema "kunajambo nataka nikwambie lakini naomba ulipokee kwa moyo mkunjufu...kwa sababu ni muda mrefu nimekaa nalo moyoni..lakini leo nimeamua nikwambie..benjamini aliyasema maneno hayo huku akitafuna nyama ya kuku...

kabla hajamaliza kuongea simu yake iliita""sory naomba niongee na simu mara moja...kisha akanyanyuka na kusogea kando kidogo....akaipokea simu ile.....alistuka baada ya kupata taarifa ya msiba wa baba yake pamoja na mama yake wamekutwa wameuwawa kikatiri ndani ya nyumba yao na kukatwa katwa vipande vingi....benjamini alichanganyikiwa akakata simu akarudi haraka mpaka pale mezani alipokuwa amekati akamshika mkono latiffa na kuondokanae...latiffa alishangaa akauliza"" kwani vipi!!!!!kuna tatizo gani sikuelewi""""

benjaminj alibaki kimya hakujibu kitu...ghfla muhudumu aliwafata mpaka kwenye gari akasema"" mbona mnaondoka bila kulipa pesa ya chakula mlichoagiza?????

latiffa akadakia akauliza shilingi ngapi??

yule muhudumu akajibu elfu arobaini..benjamini alitoa pesa kwenye mfuko wa suruali akamlipa yule muhudumu kisha akaliwasha gari na kuliondo kwa kasi...wakati huo latifa alikuwa anamshangaa benjamini...aliliendesha gari mpaka pale alipo mkuta latiffa kisha akamwambia ninamsiba wazazi wangu wameuwawa na mtu asiyejulikana muda mchache uliopita...kisha benjamini akaliendesha gari kwa kasi ya ajabu...macho yalimtoka lattifa...akazipiga hatua za haraka haraka kuelekea nyumbani kwake..alipofika alipitiliza mpaka chimbani..akafungua kabati na kukitoa kitabu cha chery...akafunua kurasa mpaka sehemu ya tatu akasoma ili aone tukio lililotokea je linafanana tukio la kwenye kitabu!!

aliposoma alistuka kusona mchoro wa mauwaji ya kikatili aliposoma ilikuwa hivi"watu wawili mke na mume walivamiwa na kiumbe wa ajabu na kuwauwa kikatiri kisha kiumbe huyi alikatakata vipande vingi maiti hizo na kutokomea kusikojulikana...

latifa alipoendelea kusoma hadithi ilieleza kuwa kijana mkubwa wa wazazi hao waliouwawa alikwenda nyumbani haraka baada ya kupata taarifa hizo..alipofika aliogopa sana kukuta wazaziwake wameuwawa kikatiri....akiwa anatahamaki mara ghafla kiumbe yule alijitokeza na kumuuwa kijana huyo....latifa alistuka akaogopa sana alihisi kuchanganyikiwa alijua wazi kuwa anayefuata kuuwawa ni Benjamini...

akachukua simu na kumpigia benjamini ili asiende nyumbani kwao....simu ya benjamini iliita lakini haikupokelewa.....

*************

upande mwingine alionekana benjamini akiitazama simu yake ikiita lakini alishindwa kuipokea kwa sababu alikuwa amechanganyikiwa na taarifa ya vifo vy wazazi wake..

baada ya muda kidogo alifika akiingia nyumbani kwao akalipaki gari akashuka haraka na kutimua mbio kuingia upande wa ndani.....alipoingia mara ghafla.

kilionekana kichwa cha benjamini kikiruka kutoka shingoni na kudondoka kando....damu nyingi ziliruka benjamini akadondoka chini na kupoteza maisha.

kisha akaonekana yule kiumbe wa kutisha akiwa ametapakaa damu kwenye mkono wake wa kulia kisha akaivuruta maiti ya benjamini na kuilaza kando kando ya maiti ya baba na mama yake..kisha akatoka akalifuata gari la benjamini akaingia upande wa ndani....aliiona simu ikiita akaipokea lakini hakuongea kitu akaikata simu hiyo.. na kuvunjavunja kisha akacheka kwa sauti ya ajabu yenye mngurumo wa kutisha akatoka ndani ya gari hilo na kuzipiga hatua kurudi upande wa ndani alikichukua kichwa cha benjamini pamoja na vile vichwa vya wazazi wa benjamini..........akatoweka kimiujiza..

*****************

Upande mwingine Latifa alionekana kupagawa akazipiga hatua kuelekea upande wa nje....akaanza kutimua mbio mpaka barabara kuu...akasimamisha bodaboda kisha akasema ""nini ni ni nipileke haraka ubungo

river side.....dereva bodaboda aliendesha pikipiki kwa kasi..baada ya dakika kadhaa walifika.....latiffa akashuka haraka kutoka kwenye bodaboda akatimua mbio kuelekea upande wa ndani ya nyumba huku akimuita benjamini.....alipoingia ndani aliogopa kukuta damu nyingi zimetapakaa kuanzia mlangini.....alipoangaza angaza macho alipiga kelele baada ya kuona maiti ya benjamini ikiwa imelazwa kado ya maiti za wazaizi wake....

latifa alitimua mbio kurudi upande wa nje...ghafla aliteleza na kudondoka chini baada ya kukanyaga damu ilioyokuwa imetapakaa kwenye sakafu...akanyanyuka haraka akatimua mbio mpaka nje ya geti akamwambia dereva bodaboda""tuondoke......dereva aliwasha pikipiki wakaondoka.....akiwa njia simu yake ikaita alipoitazama alikuwa anapigiwa simu na mama yake kuwa Meinda ameuwawa namaiti yake kuning'inizwa juu ya nguzo ya umeme....

Meinda alikuwa ni rafiki yake kipenzi aliyekuwa anafanya nae kazi katika kituo cha radio....meinda alikuwa na likizo kwa ajili ya kujifungua....hivyo hakuja kazini kwa kipindi cha miezi mitatu..alikuwa na mimba ya kukaribia kujifungua.....

latifa alizidi kuchanganyikiwa aliogopa sana.....baada ya dakika 40 walifika nyumbani kwa latifa kisha akatoa nyingi alizokuwa ameziweka kwenye sidiria aliyokuwa ameivaa...kutokana alikuwa katika hali ya kuchanganyikiwa hakuzihesabu pesa hizo akampa zote dereva bodaboda....kisha akatimua mbio kuingia ndani kwake.....akachukua kitabu cha chery akakifunua kurasa mpaka sehemu ya nne akasoma muendelezo wa hadithi...aliona mchoro wa mwanamke aliyeuwawa kikatili na kutundikwa juu ya nguzo ya umeme....macho yalimtoka akaendelea kuisoma hadithi.......alistuka kuona kunatukio la mauwaji ya watu wengi wakiwa kwenye basi la kusafirisha abiria......simu yake ikaita alipoitazama alikuwa ni binamu yake wa kike anampigia simu hiyo.......

******************

Latifa akaipokea....waliposalimiana binamu yake alisema""nipo safarini nakuja dar es salaam naomba uje unipokee ubungo ghafl mtandao ukakata kwa sababu walikiwa porini....latifa akapiga ile namba ya binamu yake simu ilimjibu

samahani mteja unayempigia hapatikani...latifa akaangua kiliona kusema""ee Mungu wy me??

akakifunika kitabu na kukirudisha kabatini haraka akajitupa kitandani huku akilia kwa uchungu wa kuwapoteza marafiki wawili kwa wakati mmoja...mbaya zaidi tukio linalofuata ni mauwaji yatakayofanyika ndani ya basi la abiria...latifa alizidi kulia kwa sauti alijua binamu yake arauwawa muda mchache ujao....ghafla SMS iliingia kwenye simu yake upande wa WhatsApp akapuuzia kuifungua baada ya kuona ni SMS za kwenye magroup ya WhatsApp...akanyanyuka akaingia bafuni kuoga alipotoka bafuni aliweka neti kisha akapanda kitandani baada ya dakika kadhaa alijikuta machozi yakimtoka akashindwa kujizuia akaanza kulia kwa sauti ya chini. akanyanyuka na kwenda sebuleni akawasha Runinga(Tv)na kuanza kuangalia....lakini fikra na mawazo yake yalikuwa hayapo kwenye Runinga(Tv) akaamua kuizima na kurudi chumbani...

*********

akafanya maombi kwa kumuabudu mungu amlinde usiku wa leo..alipomaliza alijilaza na kuanza kuutafuta usingizi lakini alishindwa kulala alikuwa akitafakari juu ua mauwaji ya mfululizo yanayojitokeza...alibaki macho kwa masaa machache kisha akachukua simu yake ili atazame picha za benjamini na Mainda enzi za uhai wao....baada ya kumaliza kutazama picha hizo walizopiga pamoja akaingia upande wa whatsApp na kufungua SMS za kwenye Group.....

Latifa aliangua kilio baada ya kusoma SMS ile...kisha aliona picha za mauwaji ya kutisha katika basi hilo lililopata ajali.....inasemeka kuna kiumbe wa ajabu alijitokeza katikati ya barabara na kusababisha ajali hiyo mbaya kisha akalifuata gari na kuanza kumtoa nje abiria mmoja moja na kuwanyofua vichwa ka kuvivuta kwa kutumia mikono yake yenye nguvu za ajabu....kisha akatoweka....

latifa hakuweza kupata usingizi alilia sana mpaka pakakucha....akanyanyuka kitandani na kuelekea bafuni kuoga....

***********

upande mwingine alionekana mwana dada mmoja akiwa amefungiwa katika chumba chenye mwanga hafifu wenye rangi nyekundu huku mikino na miguu yake imefungwa kwa minyororo....mwanadada hiyo alionekana kudhohofika sana...ngozi yake ilionekana kuwa na vidonda kwenye sehemu alizokuwa amefungwa minyororo......macho yake yalionekana kuregea kama mtu mwenye njaa kali sana......alipojaribu kunyanyuka alionekena kutokuwa na nguvu za kisimama....akajivuruta mpaka kwenye kona ya chumba hicho akajilaza sakafuni....kumbukumbu ilianza kumjia alikumbuka tukio lililomtokea miaka kumi na mbili iliyopita.....ilikuwa hivi...

siku hiyo chery alionekana akimuaga Latifa latifa baada ya kuhitimu masomo ya elimu ya juu kwenye chuo alichokuwa akisoma.....alikumbuka alimuachia kitabu lafiki yake kipenzi aitwae latifa...kisha wakakumnatiana na kuagana....

kumbe mwanadada huyo ndiye yule chery aliyepotea miaka kumi na mbili iliyopita...

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

  Ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi Zaidi Naomba Share App kwa Wapenzi wa Simulizi Wapakue(Install) App ya CnZ Media

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)