KITABU (3)

Zephiline F Ezekiel
0
Jina:
KITABU

SEHEMU YA TATU
ILIPOISHIA...
alikumbuka alimuachia kitabu lafiki yake kipenzi aitwae latifa...kisha wakakumnatiana na kuagana....

kumbe mwanadada huyo ndiye yule chery aliyepotea miaka kumi na mbili iliyopita...

IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA SIMULIZI

ENDELEA...
pia alikumbuka baada ya kuagana na Latiffa alielekea kwenye kituo cha mabasi.....alipodika aliingia kwenye sehemu ya mapumziko akaketi na kuagiza matunda.....akanza kula matunda huku akilisubiri basi lifike kituoni hapo...

wakati chery anakula alikuwa anawaza juu ya hadithi ya kitabu alichokitunga...huku akijisemea moyoni lazima nikichapishe kitabu hiki...naamini nitapasa pesa nyingi kupitia kitabu hiki.....wakati chery anawaza matukio na michoro ya kwenye kitabu chake...kumbe pembeni yake alikuwepo mwanke mwenye asili ya wingereza...mwanamke huyo alikuwa na uwezo wa ajabu!!! aliweza kuyatambua mawazo nafikra za chery....alivitiwa sana na hadithi hiyo aliweza kuisoma kupitia fikra za chery....kisha akafungua mkoba wake na kutoa biskuti kisha akaanza kula.......baada ya sekunde kadhaa alitoa kipande kimoja cha biskuti na kumpa chery huku akimsihi chery kwa maneno ya ukarimu ale biskuti hiyo....chery aliipokea na kuanza kula....baada ya sekumde kadhaa chery alihisi kizunguzungu huku nguvu zikimuishia......akapoteza fahamu....

mwanamke yule mwenye asili ya wingereza aliita taxi na kumchukua chery akamuingiza ndani ya taxii kisha wakatokomea kusikojulikana......na baada ya miaka kumi na mbili kupita mwanamke huyo alianza kufanya mauwaji ya kikatiri na uenye kutisha kwa kufuata mtiririko wa hadithi ya kitabu cha chery....kumbe muuwaji sio chery ni yule mwanamke mwenye asili ya wingereza

*************

upande mwingine alionekana latiffa akitoka bafuni kisha akanza kuvaa nguo ili aende kazini...alipomaliza alitoka uoande wa nje ma kufunga mlango wa nyumba yake....akazipiga hatua kuelekea kazini.....akiwa njiani kabla hajafika mbali wazo lilimjia kuwa arudi nyumbani akachukue kile kitabu akipeleke polisi akatoe taarifa kuhusu matukio yanayojitokeza yanafanana na matukio pamoja na michoro iliyopo kwenye kitabu hicho....latifa aliamua kurudi akafungua mlango na kuingia moja kwa moja mpaka chumbani kwake akafungua kabati na kukitoa kitabu cha chary....akakiweka ndani ya mkoba wake..lakini alisita akakitoa ili asome tukio linalofuta kwenye sehemu ya tano..akafunua kurasa haraka haraka mpaka sehemu ya tano kisha akaanza kusoma.......ghafla mapigo yake ya moyo yakaanza kwenda mbio...macho yalimtoka akaingiwa na uwoga wa hali ya juu akatimua mbio na kutoka nje huku akikiacha kitabu juu ya kitanda chake...

latifa alitimua mbio huku anapiga simu kule kazini kwake....simu ilipokelewa. latifa akasema"Kimbieni tokeni hapo mtakufa muda si mrefu....

yile mtu aliyepokea simu hiyo alistahajabu akauliza ""latifa umepatwa na nini?? mbona sikuelewi???

""jamani nasema hivi ondokeni hapo haraka mtakufa wote..

mtu yule alikata simu ya latifa akaendelea na shughuri zake....lakini akili yake ilikiwa ikitafakari maneno ya Latiffa..akajisemea moyoni"au latifa kachanganyikiwa!!! aliamua kunyanyuka na kuwafuata watangazaji wenzake akaanza kueleza kile alichoambiwa na Latiffa wafanyakazi wenzake walipuuza wakaanza kucheka...mmoja akaropoka ""kwani nini ni wageni kwa Latiffa huwa anapenda sana utani...yele mtu aliyeeleza taarifa hiyo akaamua kuondoka akaingia kwenye ngazi ya kutumia umeme(lift) na kubonyeza kitufe ili lift ishuke upande wa chini...alipofika chini kabisa alitoka kwenye lift na kuondoka zake.....

kumbe latifa aliposoma kile kitabu cha chery kilionesha jengo kubwa lililokuwa na kuituo cha radio ghorofa ya tano....jengo lile lilifanan na mchoro wa kwenye hadithi ya kitabu cha chery...hadithi ilieleza kuwa kuna kiumbe wa ajabu alivamia jengo hilo na kuuwa watangazaji wote isipo kuwa watangazaji wawili...mtangazaji wakiume na mtangazaji wa kike.....

**************

yule mtu aliyeshuka kutoka kwenye lift kabla hajafika mbali alisikia vioo vikipasuka alipogeuka nyuma aliona vioo vya madirisha ya ghorofa ya tano ndivyo vinavyopasuka kisha akaona watu wanatupwa nje kupitia madirisha hayo....watu hao walidondoka chini na kupasuka vichwa.....mtu yule alikimbia haraka kuelekea kwenye tukio....alipofika aliogopa kuona watangazaji wenzake wote wameuwawa na kupasuka vichwa vyao....watu walikusanyika kushuhudia tukio hilo lakini haikufahamika ni nani aliyefanya tukio hilo.....

************

upande mwingine kule juu ya ghorofaya tano..alionekana yule kiumbe akiwa bado yumo ndani ya kituo hicho cha radio..akaharibu mitambo yote inayohusika kurusha mawimbi ya radio hewani..kisha akatoweka kimiujiza.....

muda mchache polisi walifika eneo la tukio..wakaelekea juu kwenye kituo hicho cha radio...waliweka siraha zao tayari kwa kupambana kisha wakaingia mpaka ndani ya kituo hicho(UCCTV)...walistahakabu kukuta kila kitu kimeharibiwa isipokuwa kamera za ulinzi zilizokuwa zimetegeshwa ndani ya kituo hicho...

polisi mmoja aliifuata kompyuta iliyokuwa inahusika kurekodi mambo yanayoendelea ndani ya kituo hicho......alipotazama matukio yaliyorekodiwa masaa machache yaliyopita..matukio yote yalionekana isipokuwa tangu kiumbe yule alipojitokeza kamera hazikuwa na uwezo wa kurekodi tukio lolote......kipande hicho kilionesha giza..... na baada ya kumaliza kufanya mauwaji pamoja na uharibifu wa vitu vilivyokuwemo humo ndaani..akatoweka na kamera zikaendelea kurekodi kama kawaida hakuonekama muuwaji katika kamera hizo..

yule askari alistahajabu sana akajisemea moyoni""

bila shaka kunajambo lilitokea ambalo sio la kawaida...kisha wakapiga picha kwa ajili ya upelelezi wakaondoka zao..

************

upande mwingine alionekana yule mtangazaji alinusurika kifo...akizipiga hatua za haraka haraka bila kujua ni wapi anakoelekea.....akachukua simu yake na kumpigia Latiffa....

latiffa aliipokea simu hiyo haraka""mtu yule akasema ""umejuaje kuhusu hili jambo kama litatokea???

latifa alidakia na kusema""jamani nakusihi waambie watu wote mtoke humo mdani mkimbiesipofanya hivyo mtakufa....

yule mtu alijibu""muda mchache uliopita wafanyakazi wenzetu wote wameuwawa na kutupwa kutoka ghofani mpaka chini.....kabla hajamaliza kuongea latifa alikata simu......macho ualimtoka jasho likaanza kumtiririka huku ikiambatana na vijampo vya uwoga(bhu bhu)

akatimua mbio kurudi ndani kwake akafunua kitabu cha chery akaendelea kusoma sehemu ya tano ili aone tukio linalofuata........latifa alistahajabu kuona tukio la mauwaji ya kutisha katika shule ya watoto(chekechea) aliogopa sana alipoutazama mchoro uliokuwa umechorwa kwenye hadithi ya kitabu cha chery sehemu ya 5

hakuelewa mchoro ule ulikuwa unafanana na sehemu gani alijaribu kuvuta kumbukumbu huenda alishawahi kuona shule hiyo....Latifa alistuka akazipiga hatua kurudi nyuma kwa uwoga huku amebaki mdomo wazi......

Latiffa akachukua simu yake haraka na kupiga namba za vyombo vya dora....akasita akaacha kupiga simu hiyo akajiuliza moyoni""mmh!! naweza kutoa taarifa hii nikawa matatizoni mungu nisaidie......akakifunika kitabu kile akakirudisha ndani ya kabati.. akatoka nje...akiwa anatembea wazo likamjia kuwa arudi chumbani achukue kitabu kile akipeleke kwenye vyombo vya dora

"" aagh liwalo na liwe....akazipiga hatua akaingia chumbani kwake akafungua kabati akakitoa kile kitabu......akakiweka ndani ya mkoba kisha akatoka upande wa nje.....akazipiga hatua mpaka kwenye barabara kuu...akakodi bodaboda akaenda mpaka kituo cha polisi Ostabey...alipofika alianza kutoa maelezo......maaskari walistahajabu sana....kisha akakitoa kitabu kile na kuwaonesha maaskari hao waliokuwa zamu.....walimcheka kisha wakasema wanakazi nyingi za kufanya hawana muda wa kufatilia jambo la kufikirika ... latiffa alishangazwa na majibu ya maaskari hao....akachukua kitabu na kuondoka zake.......akaenda kwenye mgahawa akaagiza chakula.....wakati anakula alisikia watu waliokuwa wamekaa nyuma yake wakionge jambo lililomfanya ageuze shingo yake awatazame watu wale..... walikuwa wanaonyeshana picha katika simu huku wakionekana kusikitika.....mmoja wapo akasema """sijui ni nani aliyefanya mauwaji haya ya kikatiri...yani hana hata chembe ya huruma... watoto hawa wadogo wanakosa gani!!!! mwingine akadakia ""mmh inasikitisha wameuwawa watoto wote......latiffa aliposikia hivyo alijua wazi kuwa tukio hilo ndio tukii aliloliona kwenye kitabu cha chery.....alisikitika sana machozi yakaanza kumlenga.....akaacha kuendelea kula akaondoka zake......akaenda moja kwa moja mpaka nyumbani kwake.....alipofika akaingia chumbani kwake akakitoa kile kitabu akafunua kusarasa mpaka sehemu ya sita...akaanza kusoma huku uwoga umetanda juu yake....

aliogopa kuona matukio matatu ya mauwaji ya kikatiri...katika sehemu ya sita ya hadithi ya kitabu cha chery.....tukio la kwanza ilikuwa hivi..

walionekana watu zaidi ya kumi wakiwa ndani ya jengo ambalo halijamalizika ujenzi lenye ghorofa saba...watu hao walikuwa mafundi ujenzi.....wakiwa katika shuguri hiyo ya kuendelea kujenga jengo hilo......kuna fundi mmoja alionefkana akitembe kuelekea upande wa juu kabisa ya jengo alipofika aliona kama kunamtu kaketi kamgeuzia upande wa mgongo...mtu huyo alionekana kuwa uchi wa mnyama...na nwele zake zilikuwa nyeupe hata mgozi yake ilikuwa nyeupe(mzungu) alipojaribu kumuuliza ""'unafanya nini huku???? mtu yule aligeuza shingo yake uso wake ulionekana kutisha akanyanyuka na kusimama kama mbwa....yule fundi akaanza kutimuo mbio kwa uwoga.....wakati anakimbia alikuwa amegeuza shingo yake akimtazama kiumbe yule wa kutisha....akajisahau kama yupo juu kabisa ya jengo alikimbia akapitiliza akadondoka kutoka juu ya ghorofa mpaka chini akapasuka kichwa......fundi mmoja alisikia kile kishindo cha nguvu kitu kudondoka kutoka juu...akaacha kuendelea kujenga akzipiga hatua kwenda kutazama ni kitu gani kimedondoka....

alipochungulia upande wa chini alimuona kiumbe yule kaning'inia kwenye ukuta akavutwa kuelekea upande wa chini...fundi huyo alidondoka akapasuka kichwa ubongo ukamwagika.....kiumbe yule akamfuata fundi mwingine aliyekuwa akichanganya simenti na mchanga....akararua kati kwa kati utumbo ukamwagika...kisha akamning'iniza juu ya ukuta kwa kuchomeka shingo ya fundi huyo kwenye nondo iliyokuwa imechomoza kwenye ukuta.....

wale mafundi wengine walistahajabu kuona wanapungua.......fundi mmoja akazipiga hatua kuangaza wenzake wameenda wapi mbiona hawajatoa taarifa!!!!! yule fundi alizipiga hatua huku akiwaita kwa majina...

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

  Ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi Zaidi Naomba Share App kwa Wapenzi wa Simulizi Wapakue(Install) App ya CnZ Media

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)