
Mtunzi: Yozz Piano Maya
SEHEMU YA TANO
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
upande mwingine walionekana maaskari wamefika uwanja wa taifa lakini hawakuweza kutoa msaada wowote kwa sababu walikuwa wamechelewa kufika.....
IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA SIMULIZI
ENDELEA...
ilibidi wafanye jitihada za kuondo maiti zilizokuwa zimetapakaa ndani ya kiwanja hicho.....huenda wakakuta kunabaadhi yao bado wapo hai...
wakati huo huo alionekana mkuu wa jeshi kwenye kambi ya akiamuru jeshi lijipange ili kumtatafuta na kumuangamiza kiumbe huyo....
***********
kule nyumbani kwa sebo alistuka akafunga mlango haraka na kurudi upande wa ndani....glafla kiumbe yule alijitokeza upande wa ndani..
ikawa ni mara ya kwanza kwa latifa kumuona kiumbe huyo.....latifa alipotaka kupiga kelele akaona kiumbe yule amemshika sebo na kuzivuta sehemu zake za siri zikang'oka...kisha akamnyanyua juu kuelekea kwenye feni ya juu (pangaboi) iliyokuwa ikizunguka kwa kasi ikachinja shingo ya sebo akapoteza maisha.....
kisha kiumbe yule alizipiga hatua kumfuata latifa.. pale alipokuwa amesimama......
ratifa aliogopa akazipiga hatua kurudi nyuma akajikuta yupo kwenye ukuta hakuna sehemu ya kuendelea kurudi nyuma,kiumbe yule akamsogelea latifa kisha akainua mkono wake ili amuue latifa lakini kabla hajafanya hivyo alionekana kumshangaa latifa , akamtazama latifa shingoni aliona mkufu kumbukumbu ikamjia akakumbukua miaka kumi na tano iliyopitailikua hivii.,
yeye na familia yake walipokua kule serengeti katika mbuga za wanyama kabla hawajaingia kwenda kutalii alikukutana na binti mmoja wa kiafrika,wakati wanazipiga hatua kuingia ndani ya gari ili kuelekea kutazama wanyama alidondosha hati ya kusafiria(International passport ) binti yule wa kiafrika aliokota hati hiyo akapaza sauti akasema"hey is this your passport?"(hii ni hati yako ya kusafiria?) alipogeuka alimuona binti wa kiafrika akiwa amenyosha mkono wake huku akishikilia hati hiyo, aliacha kuingia ndani ya gari na kuamua kukimbia kumfuata binti huyo wa kiafrika pale alipokua amesimama.Yule binti wa kiafrika alimkabidhi passport hiyo, yeye akasema""thanks my friend(asante rafiki) kisha akavua mkufu aliokua kauvaa shingoni mwake na kumkabidhi binti huyo wa kiafrika, alitabasamu kisha akazipiga hatua kurudi kule lilipokuwepo gari
*************
Baada ya kukumbuka hayo aliweza kutambua kuwa huo ndio ule mkufu wake aliemkabidhi yule binti wa kiafrika ,,,akajisemea moyoni"bila shaka huyu ndie yule binti alieokota passport yangu na kunikabidhi .....aliamua kuacha kumdhuru latifa akazipiga hatua kurudi nyuma kisha akarudi nyuma kisha akatoweka kimiujiza.
latifa aliogopa hakuamini kama kiumbe huyo angemuacha hai macho yalimtoka na mapigo yake ya moyo yalikua yakipiga kwa kasi ya ajabu ,akatazama huku na kule alipoona kiumbe huyo ametoweka latifa alikichukua kitabu akatimua mbio akaufuata mlango na kutoka nje alikimbia bila kujua ni wapi anakoelekea.
************
Upande mwingine alionekana chery akiwa ndani ya kile chumba chenye mwanga hafifu wa rangi nyekundu huku machozi yakimtoka na kusema""ee Mungu nisaidie nitoke humu, maisha yangu yakuwa kama mfungwa kosa langu ni nini? chery aliyaongea maneno hayo huku akilia kwa uchungu...alitazama majeraha yaliyokuwa mikononi na miguuni mwake kwenye zile sehemu alizokuwa amefungwa minyororo....
***********
upande mwingine alionekana Latiffa akitimua mbio kuelekea kituo cha polisi ili aombe msaada..
alipofika aliwaelezea polisi kile alichokiona safarii hii walianza kupata wasiwasi kwa sababu nguo za latifa zilionekana kua na damu ,damu hiyo ilimimwagikia baada ya yule kiumbe kumnyanyua sebo na kukielekezea kichwa chake kwenye feni iliyokua inazinguka kwa kasi ikachinja shingo.
Askari mmoja aliekua na cheo aliwaamuru maaskari watatu waongozane na latifa mpaka kwenye nyumba ya sebo , wakatoka nje haraka wakaingia kwenye gari na kuanza safari ya kuelekea kwa sebo ,,wakiwa njiani latifa alikifu.nua kitabu mpaka sehemu ya nane ili aone tukio linalofuata hadithi ilisimulia tukio la mauaji ya kutisha yaliyofanyika kwenye kituo kimoja cha polisi....alionekana kiumbe wa ajabu kuvamia na kuuwa askari wote waliokuwa zamu siku hiyo...latifa alistuka macho yakamtoka..akasema kwa sauti ya juu,"" simamisha gari...
yule askari aliyekuwa akiendesha gari aliamua kupunguza mwendo wa gari hatimae gari likasimama.....latifa akasema""embu waambie askari wote waliopo kituoni waondoke muda huu...watauwawa...
wale maaskari waliokuwemo ndani ya gari walistahajabu walihisi latifa kachanganyikiwa baada ya kushuhudia tukio la mauwaji.....baada ya sekunde kadhaa kupita ilisikika radio call ya kwenye gari ikitoa taarifa kuwa kituo cha polisi cha Temeke usalama wa taifa...kimevamiwa na kiumbe wa ajabu na kuuwa polisi wote waliokuwemo kituoni humo....wale maaskari walistuka wakaanza kumuogopa latifa...wakafungua milango ua gari na kutimua mbio kuelekea kusikojulikana huku wakimuacha latifa ndani ya gari.........latifa alihisi kuchanganyikiwa....akakifunua kitabu haraka ili aone nini kitatokea tena.....alipoanza kusoma hadithi sehemu ya tisa....latifa alipiga kelele.....hadithi ilisimulia mauwaji ya kutisha watu walivamiwa na kiumbe wa ajabu wakiwa hospitali....na kuuwa hakufanikiwa hata mtu mmoja kutoka hai katika hospitali hiyo kubwa
(ya rufaa) latifa akakumbuka kuwa mama yake mzazi ni daktari wa Muhimbili...huenda tukio hilo likafanyika hospital hiyo....
kabla hajamaliza kusoma hadithi hiyo...ghafla simu yake iliita..alipoitazama aliona ni mama yake anampigia.....alipoipokea alisikia sauti za watu wakipiga kelele ghafla simu ikakatwa...
Latifa aliogapa sana akafungua mlango wa gari na kutoka nje..akafungua mlango wa mbele na kuingia uoande wa dereva akaliwasha gari la polisi...akaliondosha kwa kasi mpaka Muhimbili, alipofika aliona watu wakikimbia huku na kule..kila mmoja alioita njia yake....akatoka nje ya gari na kuanza kutimua mbio kuelekea ndani ya hospital..hata walinzi waliokuwa getini walitimua mbio wakalitelekeza geti likiwa wazi...watu walimshangaa latifa kumuina anaingia ndani ya hospitali wakati wenyewe kanakimbia kutoka ndani ya hospitali..ili kuoa maisha yao....latifa alikutana na maiti nyingi....zikiwa hazina vichwa, nyingine zikiwa zimetobolewa tumboni na kutolewa utumbo...latifa aliingiwa na wasiwasi juu ya mama yake...lakini akajipa moyo akazidi kusonga ndani zaidi kunako hospitali hiyo....
kwa mbali aliona kundi la watu wakiwemo manesi na badaktari pamoja na wagonjwa wakitimua mbio....miongoni mwa kunfi hilo alikuwemo mama yake..ghafla kiumbe ye akajitokeza na kuanza kufanya mauwaji ya kikatiri akauwa wote akabakia mama yake latifa pekee akiwa hai...kiumbe yule akaanza kumfuata mama latifa..
mama latifa akaanza kutimua mbio....yule kiumbe alipogeuza shingo yake aliona kunamgonjwa ndani ya wodi..mgonjwa huyo alikuwa anapumua kwa msaada wa mashine maalumu ya hewa safi(oxygen machine) akazipiga hatua kuingia ndani ya wodi hiyo alipomkaribia mgonjwa aliyekuwa amelala kitandani...akamvunja mguu mmoja..mgonjwa yule alihisi maumivu makali sana....kisha kiumbe yule akaunyofoa mguu huo...akamvunja mguu wa pili na kuunyofoa...kisha akazipiga hatua mpaka dirishani akavunja kioo akachukua kipande cha kioo kilichokuwa na ncha kali akarudi mpaka kwenye kitanda alichokuwa amelazwa mgonjwa yule...akanjanyua mkono wake na kumchoma shingoni kwa kutumia kioo hicho kisha akakiacha hapohapo shingoni mgonjwa yule alitapatapa kupigania pumzi kwa sekunde kadhaa akaiaga dunia....
******************
upande mwingine alionekana mama latifa akitimua mbio...huwezi amini pamoja na umri mkubwa aliokuwa nao mama latifa,alikimbia kwa kasi kama binti wa miaka ishirini...ghafla yule kiumbe akajitokeza mbele yake.....akamkamata shingini na kumnyanyua juu..alipotaka kumtoboa tumbo...ikasikika sauti ya latifa""hey muache mama yangu tafadhali nakuimba usimdhuru.!!
kiumbe yule akageuza shingo yake alipomuona latifa akamuachia mama latifa...kisha kiumbe huyo akatoweka kimiujiza.. ....
latifa akakimbia mpaka pale alipokuwa amedondoka mama yake...wakati huoama latifa alikuwa akitokwa na haja ndogo mfululizo....akanyanyua mama yake na kuondoka nae..... wakati huo ukimya ulitawala hospital hiyo..haikusikika sauti ya kitu chochote..hapakuwa na mtu hata mmoja....
walipotoka nje ya hospotal hiyo...latifa alistahajabu kuina maaskari wameizunguka hospital hiyo....huku wameshikilia siraha kuelekea upande walipokuwepo latifa na mama yake.....askari walipogundua kuwa ni binadamu wa kawaida wakashusha siraha zao...kisha wakaingia upande wa ndani ya hospotal ili kumtafuta muiwaji..
***************
mama latifa pamoja na latifa walikwenda moja kwa moja mpaka nyumbani...walipofika latifa akamsimulia mama yake kuhusu hadithi ya kitabu cha chery...mama latifa alistahajabu sana..akaomba asome kitabu hicho alikisoma kuanzia sehemu ya kwanza mpaya sehemu ya nane....alistahajabu kuina matukio yaliyoandikwa ndani ya kitabu ndio yaliyotokea na mengine yanaendelea kutokea.......alipoanza kuisoma sehemu ya tisa macho yalimtoka akaogopa sana hadithi ilielezea mtu mmoja aliyekuwa uwezo wa kipekee mtu huyo anaitwa JABU...
jabu alitengeneza mtego wa kunasa vitu visivyo onekana(invisible) hadithi ilieleza kuwa baada ya kiumbe hiyo wa ajabu kugundua kuwa kuna mtu ambaye ametengeneza mtego ambao ungeweza kumnasa....alichukia sana kiumbe huyo akaamua kumtafuta jabu..
*************
upande mwingine hadithi ilisimulia kuwa siku hiyo jabu aliamua kwenda kufanya majaribio ya mtego huo kwa kuutega angani..kwa hiyo vitu au kitu chochoye ambacho kilikuwa na uhai bila kujionesha mbele za macho ya binadamu basi kitanaswa na kuvutwa upande wa juu kuelekea angani na kuingia ndani ya mtego huo......wakati jabu akiwa njiani kwenda kuutega mtego huo.....
wakati huo huo yule kiumbe alikuwa yupo njiani kuelekea kwa jabu.... jabu akiwa njiani wakakutana uso kwa uso.....jabu alikuwa na uwezo wa kuona viumbe wasionekana kwenye macho ya binadamu wa kawaida.........ghafla kiumbe yule aliruka na kutua juu ya gari la jabu...
Jabu akaliendesha gari kwa kasi,akakanyaga breki..gari likasimama ghafla na kumtusha kiumbe yule mbele akadondoka chini.....kisha jabu akachukua ule mtego na kuuanda harakaharaka...
yule kiumbe alipo ona hivyo akatimua mbio na kutoweka kimiujiza......wakati jabu anatahamaki ghafla kiumbe yule alijitokeza na kumuuwa jabu..
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi Zaidi Naomba Share App kwa Wapenzi wa Simulizi Wapakue(Install) App ya CnZ Media