KITABU (6)

Zephiline F Ezekiel
0
Jina:
KITABU

SEHEMU YA SITA
ILIPOISHIA...
yule kiumbe alipo ona hivyo akatimua mbio na kutoweka kimiujiza......wakati jabu anatahamaki ghafla kiumbe yule alijitokeza na kumuuwa jabu..

IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA SIMULIZI

ENDELEA...
mama latifa alistuka akakifunika kitabu hicho wazo likamjia kuwa kuna mjomba wake aliyekuwa anaishi bukoba.....alikuwa ni fundi wa kutengeneza miatambo mbalimbali kwa kubuni yeye mwenuewe....akachukua simu yake na kumpigia mjomba wake....wakati huo latifa alikuwa akimshangaa mama yake...alijiuliza mama yake anampigia nani simu!!je kaona nini kwenye hadithi ya kitabu cha chery???

simu ikapokelewa...kisha mama latifa akauliza hata bila kumsalimia mjomba wake""upo wapi ???

mjomba akajibu,"nipo bukoboba najiandaa kuufanyia majaribio mtambo wangu mpya ambao unauwezo wa kunasa vitu vilivyo na uhai visivyoonekana....mama latifa akasema kwa sauti kubwa"" usiende mjomba utakufa...mjomba wake akacheka na kusema "kwa nini unasema hivyo mpwa wangu???

mama latifa akajibu kunakiumbe anayeuwa watu kikatiri atakuangamiza,nakusihi usiende......ghafla simu ikakata....

****************

upande mwingine alionekana mjomba wake mama latifa...akiuingiza mtambo ule ndani ya gari lake na kuianza safari ya kwenda kuufanyia majaribio......alipofika eneo aliloona kuwa ameona litafaa kwa kuutega ule mtego..alishuka kutoka ndani ya gari nakuushusha mtambo ule.....akachimba shimo refu kiasi kisha akauweka mtego ule ndani ya lile shimo.....akauwasha...ikatokea mionzi iliyoelekea upande wa juu (angani) mionzi hiyo haikuonekana kirahisi mpaka uwe na lenzi maalumu ya kuweza kuiona mionzi ile.....kisha akafukia shimo lile..... mionzi hiyo alisambaa angani kwote.....alipohakikisha ameutega vyema mtego huo akaingia ndani ya gari na kurudi nyumbani kwake...

akiwa njiani akatoa rimoti maalumu ya kuuruhusu mtambo huo ili ufanye kazi...kabla hajabonyeza kitufe kwenye rimoti hiyo.....ghafla kiumbe yule akajitokeza na kutua juu ya gari lake.....akatoboa upande wa juu na kunyofoa kutoka ndani ya gari na kumrusha upande wa nje.akadondoka na kuvunjika kiuno...kiumbe yule akamfuta ili amuuwe...kumbe alipodondoka rimoti ikamponyoka na kudondokea kando yake.....alipogeuza shingo yake..aliiona rimoti ile akajivuta akaichukua rimoti ile..

kiumbe yule akamrukia na kumtoboa tumbo...

wakati anapigania kuivuta pumzi ya mwisho akabonyeza kitufe cha rimoti hiyo....ule mtambo ukaanza kufanya kazi muda huohuo...

wakati huohuo alionekana chery akiwa ndani ya chumba kile chenye mwamga hafifu wenye rangi nyekundu...chery alinyanyuka akachukua shoka lililokuwa kando kando juu ya meza iliyokuwa na zana za kutisha....akaanza kukata minyororo ile...akafanikiwa kukata minyororo iliyokuwa imefungwa miguuni mwake....lakini alikuwa amechoka sana kwa sababu alitumia nguvu nyingi sana mpaka kuweza kukata minyororo hiyo. akawa amedondoka chini na kupoteza fahamu.....

************

upande mwingine alioneka latifa na mama yake...

mama latifa aliipiga simu ya mjomba wake lakini iliita tu bila kupokelewa.......

latifa akakichukua kitabu haraka akafunua mpaka sehemu ya tisa akasoma hadithi.....alipofunua ukurasa wa sehemu ya kumi latifa alipiga kelele..

hadithi ilielezea mauwaji ya kikatiri aliyofanyiwa binti mmoja aliyekuwa amefungwa ndani ya chumba....alipotazama mchoro wa picha iliyokuwa imechorwa ndani ya kitabu ilionesha binti huyo amefungwa minyororo alifanikiwa kuikata minyororo hiyo alipotaka kutoka ili akimbie kiumbe yule alijitokeza huku ameshikilia mashine maalumu ya kukatia vyuma (grender mchine)

kisha akaiwasha na kuzipiga hatua kumfuata binti huyo aliyekata minyororo na kujaribu kutoroka....

alipomkaribia akataka kumkata mara ghafla ule mtego wa mjomba wake mama latifa ukaanza kufanya kazi ukamnasa kiumbe yule na kumvuta mpaka kwenye lile shimo ambalo aliufukia ule mtambo uliotoa mionzi kuelekea juu ya anga..

kiumbe yule akadondoka kando ya shimo hilo....na kisha akazungukwa na mionzi akawa yupo kati kati...hakuwa na ujanja tena....

******************

upande mwingine alionekana chery akijaribu kujinasua kutoka kwenye minyororo aliyokuwa amefungwa mikononi...hatimae alifanikiwa lakini alipata maumivu makali sana...kwa sababu kipindi anavuta mikono yake,kuanzia juu ya viganja vyake ngozi ilitoka utadhani mtu anavua groves..kwa sababu minyiroro ilikuwa imekazwa vyema..

alipiga kelele kwa maumivu makali aliyoyapata..akanyanyuka na kuanza kutimua mbio kutoka ndani ya chumba kile...alipotoka alistahajabu sana nyumba hiyo ilikuwa kubwa sana ilikuwa na vyumba vingi, akapagawa hakujua ni mlango upi wa kutokea upande wa nje. ..

ndani ya jumba hilo palikuwa na giza...ilionekana miale ya jua iliyochomoza na kupenya ndani kupitia baadhi ya matundu madogo madogo...

chery alizidi kuogopa wasiwasi ukatawala juu yake

akawa anazipiga hatua kwa kubahatisha njia..akasikia sauti ya kitu kikidondoka...akakimbia na kuingia nda ya chumba kimojawapo...akajificha nyuma ya mlango..alisimama kama sanamu...macho yalimtoka kwa hofu...akajiziba mdomo.....alisimama hapo kwa dakika kadhaa lakini hakuona dalili yoyote ya mtu kuja kwenye chumba hicho..akatoka kwa kunyatia akachungulia.....lakini hakuweza kuona kitu chochote kwa sababu giza lilitanda ndani ya jumba hilo...alipokuuwa anatoka akagusa swichi pasioo yeye kujua ghafla taa zikawaka.....akastuka alipogeuza shingi yake nyuma....akapiga kelele..baada ya kuona viungo vya binadamu...

vichwa,,,mikono...viganja...miguu..vidole..masikio..

nyeti za wanaume,,,,utumbo wa binadamu...

chery aliogopa sana akatimua mbio kutoka ndani ya chumba kile.....akawa anakimbia kuutafuta mlango wa kutokea upande wa nje...alikutana na viungo vya binadamu kila kona ya jumba hilo....katika chumba kimoja aliona kuna compyuta ikiwa inawaka...akaamua kuingia ndani ya chumba hicho huku akitembea hatua za tahadhari....alipoifikia kompyuta hiyo akapekua mafaili yaliyokuwa mdani ya kompyuta hiyo..akaona kunafail lina video zilizorekodiwa....alipoziangalia aliona kuna video ambayo ilimuonesha yeye alivyokuwa akiingiza mdani ya chumba hicho na kufungwa minyororo...pia akaona video nyingi za mauwaji ya kutisha aliyo yasababisha kiumbe yule.. chery aliogopa sana akaendelea kupekua mafaili mengine....akaiona ramani ya jengo hilo ikionesha milango ya kutokea upande wa nje..akaisoma kwa makini ramani hiyo..akawa ameinakili kwenye ubongo wake....kisha akachukua shoka lililokuwa ndani ya chumba hicho..na kutoka ndani ya chumba hicho......

********************

upande mwingine alionekana latifa akiendelea kukisoma kitabu kile......alisikitika sana wazo likamjia akajisemea moyoni," huyo binti aliyekuwa amefungwa minyororo ni nani!!! nina wasiwasi yawezekana ni chery......kisha akatazama mchoro wa jengo hilo....akaanza kuvita kumbukumbu jengo hilo kaliona wapi!!!!........akastuka kisha akanyanyuka na kuanza kutimua mbio....mama latifa alistahajabu..akajiuliza je latifa kaona nini ndani ya kitabu hicho??? wasiwasi ukaanza kumuingia...na yeye akaanza kutimua mbio.alihisi huenda kiumbe yele anakuja..

latifa alitimua mbio akakodi taxi impeleke Bagamoyo......alipofika aliliona lile jengo lililofanana na mchoro uliokuwemo ndani ya kitabu cha chery.....akaingia ndani ya jumba hilo ili aone kama kweli chery yumo humo ndani kama hadithi inavyoeleza......aaliingia lakini hofu kubwa ilitanda juu yake kwa sababu jumba hilo lilionekana kutisha...alizidi kusonga ndani zaidi..huku akiita kwa sauti ya chini chini ""chery...chery........

alimtafuta kwa masaa mengi kiasi hatimae akafanikiwa kumuona chery..latifa alilia kwa furaha ya kumuona rafiki yake kipenzi aliyepotezana nae miaka kumi na mbili iliyopita...wakakumbatiana kwa furaha...kisha latifa akamuinesha chery kile kitabu chake....huku akifunua kurasa mpaka sehemu ya kumi....ghafla latifa akaogopa akamwambia chery.."mama yangu anauwawa muda mchache ujao...tuondoke ndani ya jumba hili tafdhali...

wakaanza kutimua mbio kuekekea kwenye mlango wa kutokea upande wa nje..

*****************

upande mwingine alionekana yule kiumbe akihangaika kujinasua katika mtego ule.....aliangaika sana lakini alishindwa kadri masaa yalovyozidi kusonga..mtego huo ulizidi kumuathiri kiumbe huyo ile mionzi ilikuwa ikimchoma akawa anapata maumivu makali sana...akaanza kupiga kelele zilizotoa mngurumo mkubwa sana....alifanya jitihada hatimae akafanikiwa kujinasua kutoka kwenye mtegi huo akafukua lile shima na kuutoa mtambi ule uliokuwa ukitoa mionzi kuekekea angani...kisha akauharibu kwa kukata nyaya za mtambi huo...

akawa huru....akatoweka kimiujiza na kujitokeza upande wa nje wa jumba lile walilokuwemo Latifa na Chery........ghafla walisikia sauti ya mlango ukifungwa...kisha taa zikazimika ghafla pakawa na giza nene..

yule kiumbe akazipiga hatua kuelekea kwenye kile chumba alichomfungia chery...ghafla kaanza kubadilika kutoka katika umbile la kutisha na kua katika umbile la binadamu, ni yule mwanamke wa kizungu mwenye asili ya wingereza, alistaajabu mwili wake kubadilika bila yeye mwenyewe kutaka ,lakini hakujali akaangaza angaza macho ndani ya chumba kile lakini hakumuona chery.....alikasirika sana akageuza shingo yake na kuangaza macho yake huku na kule akatazama kwa hisia ili abaini ni wapi chery alipo....lakini hakuweza kutambua wala kugundua.....alipotaka kujibadilisha ili awe kwenye lile umbile la kutisha...alishindwa......akajaribu kwa mara nyingi lakini alishindwa...

kumbe kipindi aliponaswa na ule mtego wa mjomba wake mama monica.... mionzi iliyochomoza kutoka kwenye mtego huo ulimchoma na nguvu zake zikawa zinapungua taratibu kadri masaa yalivyozidi kusonga... alipo ona ameshindwa kujibadilisha akapiga kelele kwa sauti ya juu iliyojaa hasira na chuki ndani yake....akatoka ndani ya chumba hicho akaelekea kwenye chumba kilichokuwepo upande mwingine..

akaingia ndani ya chumba hicho lilionekana sanduku la kuhifadhia maiti ya binadamu likiwa juu ya meza kubwa....akazipiga hatua kulifuata sanduku lile.....

****************

akalifungua kwa nguvu..ghafla walitoka wadudu wa kila aina kutokea ndani ya sanduku hilo..

mende..ng'e..tandu..mijusi..na wadudu wengi watambaao.....akafunua naironi lililokuwemo ndani ya jeneza hilo...alilotoa naironi hilo...zikaonekana zana za kutisha zikiambatana na nyundo misumari mikubwa na yenye unene waa milimita kumi na sita..

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

  Ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi Zaidi Naomba Share App kwa Wapenzi wa Simulizi Wapakue(Install) App ya CnZ Media

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)