
Mtunzi: Ally Mbetu 'Dr Ambe'
SEHEMU YA KUMI NA MBILI
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
“Dada alivyoonza nikaogopa nikajua mtoto wa kike naweza kukimbia na kufuri mkononi. Kila dakika zilivyokuwa zikizidi kukatika ndivyo alivyokuwa akipoteza uwezo wake. Yaani hatua za mwisho ilibidi niwe mpiga debe, konda na dereva mwenyewe.”
IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA SIMULIZI
ENDELEA...
“Mmh! Sasa kipi kilichomfanya akununulie gari?”
“Dada wakati ana nguvu nilichokifanya hawezi kusahau hata alipochoka kama dume la bata niliendelea kumpa machejo ya kinyozi wa kipara.”
“Mdogo wangu kwa maneno, kinyozi wa kipara ndiyo machejo gani tena?”
“Dada si unajua mtu anayenyolewa kipara hatakiwi kijitikisa, akijitikisa amekatwa?”
“Ndiyo, ehe?”
“Basi, baada ya kuchoka nilimuweka mkao wa mtu anayenyolewa kipara, mtoto wa kike nikageuka kinyozi kwa kukwangua kila kilichopo kichwani na kuwa mwepesiiii.”
“Hongera mdogo wangu, sasa itakuwaje? Mmoja unampiga chini?”
“Mmh! Jamaa amekataa nisiachane na ndugu yake, eti niendelee naye penzi letu liwe la siri.”
“Mmh! Haya, kwa hiyo kadi ya gari amekupa?”
“Kila kitu dada, gari mali yangu.”
****
Kama kawaida Shuku jioni alimfuata mpenzi wake na Jeep, alipofika aliisimamisha sehemu yao ya kawaida na kupiga honi. Lily aliyekuwa amejilaza chumbani alinyanyuka na kuchukulia nje.
Alipoliona Jeep alifurahi na kujua MJ amekuja, kutokana na tamaa alijikuta mapenzi yote kayaamishia kwa MJ.
“Dada jamaa amekuja.”
“Nani?
“MJ.”
“Mbona hajakujulisha?”
“Labda kanifanyia surprise, machejo ya yana lazima angenitafuta.”
“Naona ukimpa mara tatu atakununulia ndege.”
“Wacha nimuwahi baba asije kasirika.”
Lily alisema huku akitoka nje na kwenda mbio kumlaki mpenzi wake. Alipokaribia Shuku alitoka kwenye gari na kumfanya Lily ashtuke.
“Ha! Ni wewe?”
“Ndiyo mpenzi nimeamua kubadili gani?”
“Mmh! Karibu.”
“Asante, vipi mbona kama hujajiandaa.”
“Naumwa.”
“Nini tena mpenzi ingia kwenye gari twende hospitali.”
“Nimeisha kwenda.”
“Pole sana mpenzi,” Shuku alisema huku akivuta pochi na kuhesabu wekundu ishirini na kumpa.
“Zitakusaidia kununua matunda.”
“Asante.”
Lily aliona kama Shuku anacheza lakini alizipokea na kuagana naye. Alirudi ndani ya Shuku alirudi zake nyumbani na hamu zake. Lily alipofika ndani dada yake alimuuliza.
“Vipi mbona shemu kaondoka leo hamtoki?”
“Si kaja yule mchovu nikamdanganya naumwa si kajiiiikakamuuua na kutoa vilaki viwili eti ninunue matunda.”
“Mmh! Mbona makubwa laki mbili tu ununue matunda?”
“Umeona nyingi?”
“Tena sana, kwa hiyo umeanza kumchoka?”
“Dada siwezi kutumikia mabwana wawili tena wa nyumba moja, lazima niachane na Shuku.”
“Lily..Lily mdogo wangu usiache mbachao kwa msala upitao. Kwanza hiyo mali ya nani?”
“Sijajua kila mtu ukimuuliza anasema ya wote.”
“Sasa nataka kukuambia huenda mali ni ya Shuku, siku zote mwenye fedha huwa mgumu kuliko mtumiaje asiyejua uchungu wa fedha. Kuwa makini unaweza kumuacha Shuku kumbe ndiye tajiri na huyo MJ mpambe mshika pembe tu.”
“Mmh! Kweli eeh!”
“Tumia akili, heri uende nao wote kwa siri ili Shuku asijue, hujiulizi kwa nini MJ amesema usipokwenda anavyotaka atakupiga chini unafikiri ni kwa nini?”
“Hata sijui.”
“Basi anaongopa kuharibu kwa ndugu yake ambaye ndiye mwenye mali.”
“Mmh! Dada sasa nimepata picha mali ni za Shuku.”
Lily alikubali kuendeleza penzi la siri huku akiendelea na Shuku kama kawaida.
****
Penzi la siri la MJ na Lily liliendelea bila Shuku kugundua kilichokuwa kikiendelea huku Lily akizidi kuchanganyikiwa na ofa za MJ zilikuwa tofauti na Shuku ambaye kila siku alitoa ahadi zisizo timia.
Mabadiliko ya Lily alimshtua Shuku kutokana na kuwa na dharula kila wakati tofauti na siku za nyuma kitu kilichompa wasiwasi. Aliamini aliyemnunulia lile gari ndiye aliyekuwa akimchanganya na kumfanya amuone si lolote si chochote.
Alitamani naye kuonesha makeke yake lakini alikwama kutokana na MJ kumueleza matumizi makubwa kwake yasizidi milioni mbili.
Hali ili ilimnyima uhuru na kujiona kama anacheza makida kwenye penzi lake na msichana mrembo kama Lily. Aliamua kwenda naye hivyohivyo lakini akiamini penzi lao lilikuwa limekalia kuti kavu kudondoka asingeshangaa.
Alipanga kumpiga chini baada ya kumpa penzi zito ili popote atakapokwenda ajue jamaa hana fedha lakini mapenzi anayajua. Siku aliyompigia simu Lily wakutane ndiyo ilikuwa siku ya kuonana na MJ. Aliendelea na danadana zake.
“Haloo bebi vipi leo?”
“Mmh! Leo mama kaja.”
“Sasa akija tatizo nini?”
“Sasa nitaondoka vipi na mama kaja jioni hii.”
“Bebi mbona sikuelewi.”
“Unielewi kivipi?”
“Yaani si Lily niliyemzoea, najua siku hizi unipendi.”
“Nakupenda sana wasiwasi wako tu.”
“Hapana Lily hunipendi mapenzi yetu yamekuwa kama umeme wa mgao kama hunipendi si uniambie nijue moja,” Shuku alilalamika.
“Nakupenda Shuku.”
“Si kweli najua sasa hivi una mwanaume mwingine.”
“Shuku unalalamika sana au ndo unataka kuniacha kwa kusingizia nina mwanaume mwingine?” Lily alilia wivu wa uongo.
“Si kukuacha bali sasa hivi penzi limekuwa shubiri.”
“Niamini mpenzi wangu nakupenda sana, Shuku si muda mrefu nitarudi katika hali yangu ya kawaida. Naomba univumilie mpenzi wangu.”
“Yaani hali hii ikizidi nitashindwa mimi.”
“Basi kesho nitakuja ili kukufuta machozi, hakuna mwanaume chini ya jua ninaye mpenda kama wewe hujui tu,” Lily alimpaka Shuku mafuta kwa mgongo wa chupa.
“Mmh! Sawa nimekuelewa mpenzi wangu punguza kunitesa.”
“Nikuahidi sitakuumiza tena nakupenda Shuku wangu kesho nitakuja kweli.”
Shuku aliamini kabisa Lily hakuwa na mapenzi na yeye bali alijali kitu na baada ya kununuliwa gari la kifahari mapenzi yote aliyahamishia kwa mtu aliyemnunulia gari. Moyoni bado alijiapia kufanya mapenzi ya mwisho na kumpiga chini na yeye kuishi maisha ya rafiki yake MJ ya kubadili wanawake kwa vile hakuna wa kumuumiza zaidi heat and run.
***
Usiku wa siku ile Lily alikutana na mpenzi wake MJ Sea Cliff hotel. Walichukua chumba kama ilivyo kawaida na kusaluana nguo huku Lily akipanga kujituma zaidi baada ya kupewa ahadi ya nyumba moyoni aliapa siku ile ndiyo siku ya kununuliwa nyumba.
Wakati tui linakaribia kukolea nazi na Lily kulegea kama ute wa yai kusubiri hukumu kutoka kwa Mj, simu ya MJ iliita alipoangalia ilikuwa ya demu wake mtoto wa waziri aliyekuwa nje ya nchi. Alinyanyuka na kwenda kuongelea pembeni kwa sauti ya chini:
“Bebii.”
“Bebii upo wapi?”
“Nimetoka kidogo, vipi upo wapi?”
“Ndo nakaribia kwako.”
“Umekuja lini?”
“Ndo nimetua na ndege na breki ya kwanza kwako, kesho ndo natinga home. Nimewadanganya nitatua kesho kutwa nitakaa kwako siku mbili, nina hamu ile mbaya mpenzi wangu.”
“Mmh!” MJ aliguna na kujiuliza lazima aonane na yule binti ambaye alidanganya familia yake kwa ajili yake alijua akimkimbia ataharibu kila kitu.
“Bebii mbona unaguna au hutaki nije kwako, basi nalala hotel kwa siku bili kesho ndo nakwenda home ila ilewa nisipokuona leo nitaumia vibaya. Si unajua nilitaka nikufanyie surprise.”
“Hapana bebi lazima tutaonana japo nipo mbali kidogo.”
“Basi utanikuta kwako.”
“Hakuna tatizo bebi wangu ngoja nimpigie mtu akufungulie nyumba.”
“Hakuna tatizo ndo maana nakupenda MJ wa ukwe..ehe.”
“Umeona eeeh, poa nakuja,” MJ alikata simu na kurudi kitandani Lily alipokuwa akimsubiri ili apate nyumba usiku ule kama alivyopata gari. Japo alikuwa ameahidiwa nyumba aliamini kupitia utamu wa nyonga yake mpaka kunakucha wangetoka na kwenda moja kwa moja kwenye nyumba.
Akiwa anajiandaa kumpokea MJ kwa mahaba motomoto alishangaa mwenzake kukaa kitako na kuinama mikono kichwani.
“Bebii vipi, kuna nini?”
“Kuna tatizo lazima niondoke.”
“Tatizo gani tena bebeiii?”
“Nitakueleza kesho lakini lazima niondoke.”
“Utarudi?”
“Sina uhakika sana.”
“Basi nipe kidogo mpenzi nipo kwenye hali mbaya,” Lily alilalamika kwani alikuwa amejiandaa vilivyo.
“Hapana bebii lazima niondoke.”
“Sawa nimekubali uondoke, lakini si unajua ushazipandisha nani wa kuzishusha mpenzi, nipo katika hali mbaya basi nipe hata moja la mguu wa jini.”
“Sorry mpenzi, unavyonichelewesha ndivyo unavyozidi kunifanya nisirudi kabisa.”
“Kwani unakwenda wapi?”
“Bebii si lazima kila kitu changu ukijue,” MJ alisema huku akichukua nguo zake na kuvaa. Baada ya kuvaa alimfuata Lily na kumbusu.
“Mmmwa bebi baadaye.”
MJ baada ya kumbusu alichomoa nyekundu kumi na tano na kumtupia.
“Bebi kama nisiporudi utaweka mafuta kwenye gari lako, baii.”
Lily alishindwa kumuaga kwani moyo ulikufa ganzi baada kushindwa kutimiza malengo yake. MJ hakugeuka nyuma alitoka kumuwahi demu wake mtoto wa waziri. Alimpigia simu Shuku ampokee.
****
Muda ulizidi kukatika bila MJ kutokea saa ya ukutani ilimuonesha Lily ni saa tisa za usiku akiwa macho kumsubiri. Wazo la kwenda kwa Shuku alikuwa nalo lakini alikuwa na wasiwasi wa MJ kurudi na kumkosa.
Aliamua kukomaa mpaka asubuhi huku sumu ya mahanjamu ikiwa juu bila mshushaji kutokea. Kwa tamaa ya nyumba alijikuta akisubiri mpaka saa mbili asubuhi ndipo alipoamini MJ harudi hata simu yake haikuwa hewani.
Kwa hasira aliamua kwenda kwa Shuku ili kumkata kiu hasa alivyoufahamu uwezo wa Shuku wanapopotezana muda mrefu siku wakikutana huchimbika bila jembe. Aliwasha gari lake mpaka nyumbani kwa Shuku.
Muda alipofika alikuta bado amelala baada ya kumpigia simu alimfungulia na kuingia ndani. Alipofika alijifanya amemmisi sana Shuku na kumpiga mabusu mfurulizo.
“Vipi mbona asubuhi?”
“Kwani kuna ubaya mtu kuja asubuhi kwa mpenzi wake?”
“Hiyo iliishapita.”
“Kivipi tena bebii?”
“Ndio maana nakushangaa toka upate gari umekuwa matawi ya juu.”
Kauli ile ilimtisha sana Lily na kuona kama dhamira yake haiwezi kutimia na kuondoka na hamu zake.
“Mpenzi si nilikueleza nina matatizo jamani.”
“Matatizo kwa vile umenunuliwa gari unasahau nina uwezo wa kununua magari kama hayo kama elfu moja kwa siku moja,” Shuku alijitapa.
“Si ungeninunulia mpenzi?”
“Kwa hiyo kazi yako kuhongwa siyo?”
“Basi mpenzi, lakini nilikueleza gari hili nililikataa, lakini aliyeniletea alisema nichukue. Lakini anajua kabisa nipo na wewe na sipo tayari kurudiana naye nakupenda sana Shuku,” Lily alisema huku akimchezea chuchu na kumfanya Shuku askari ashtuke kambini na kusimama imara kutoa kipigo kitakatifu kwa adui. Lily alimvutia ndani na kumtupa kitandani na kusaula nguo chache za Shuku na yeye kuzitupa za kwake pembeni. Kutokana na kushika alikuwa kama mbwa kwa chatu.
Shuku moyoni alijiapia atakachokifanya lazima Lily amkumbuke miaka mia moja itakayo kuja kwa kuamini amezidiwa uwezo hivyo alitakiwa kutumia nguvu alizipewa na Mungu ili kumfanya Lily akitoka pale awe amechanganyikiwa.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi Zaidi Naomba Share App kwa Wapenzi wa Simulizi Wapakue(Install) App ya CnZ Media