TOROJO BAMIA (14)

Zephiline F Ezekiel
0

SEHEMU YA KUMI NA NNE
ILIPOISHIA...
“Eti anaomba msamaha.”

“Nimefurahi kusikia umemsamehe mdogo wangu ukitaka kula na kipofu usimshike mkono.”

IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA SIMULIZI

ENDELEA...
“Lakini dada nimemsamehe kwa ajili yako kitendo alichonitenda kiliniumiza sana.”

“Kikuumize vipi wakati kuna wasichana wenzako nawatumika bure lakini wewe una gari na nyumba inakuja.”

“Eti anataka leo tuonane.”

“Kwa hiyo?”

“Aah! Mi siendi, Shuku anaweza kunitafuta itakuwaje nami sitaki kumuudhi tena?”

“Kwani mlikubaliana leo muonane?’

“Tumeagana tu, anaweza kunitafuta ili kuona niliyomuomba msamaha nayatekeleza.”

“Sasa fanya hivi mkubalie MJ, Shuku akikupigia mwambie mi mgonjwa.”

“Jamani akija na kunikosa itakuwaje?”

“Fanya hivi mwambie MJ akupitie saa mbili ili tujue kama Shuku atakutafuta tujue tufanye nini.”

“Ngoja basi nimpigie kumujua tukutane wapi.”

“Mpigie.”

Baada ya kupiga simu ilipokewa upande wa pili.

“Haloo.”

“Haloo.”

“Niambie mpenzi?”

“Kwa hiyo?”

“Nakusikiliza wewe.”

“Leo wapi?”

“Pa jana.”

“Saa ngapi?”

“Saa mbili usiku.”

“Utanifuata?”

“Noo bebi njoo tu na usafiri wako.”

“Poa.”

Baada ya kukata simu alimgeukia dada yake.

“Amesema kama jana.”

“Nenda mdogo wangu kijua ndicho hiki ndo wakati wa kuuanika.”

“Nimekuelewa dada, naomba tu Shuku asinitafute.”

Kwa vile alikuwa amechoka baada ya kuoga Lily alipanda kitandani kulala.

****

Majira ya saa mbili usiku kama kawaida Lily alipaki gari lake maeneo ya Sea Cliff hoteli. Alimpigia simu MJ na kumueleza kila kitu alikwisha lipia alimueleza akachukue ufunguo mapokezi ili atangulie chumbani.

Lily alifanya kama alivyoelekezwa kwa kuchukua funguo na kuingia chumbani kumsubiri MJ kwa kuagiziwa kila kitu alichokitaka kutumia usiku ule kilikuwa kimelipiwa.

Akiwa amejilaza kitandani huku akipata wine, alifikiria jinsi atakavyompelekesha MJ ili apate kitu kingine cha thamani. Alijikuta akikaa muda mrefu bila MJ kutokea, kitu kilichomshtua sana. Alipopiga simu ya MJ haikuwa hewani aliendelea kumsubiri. Muda nao ulikatika alijikuta akikaa zaidi ya saa nne bila kuonekana.

Hasira zilimpanda kuamua kuondoka, wazo la kurudi nyumbani hakuliafiki aliamua kwenda kwa Shuku ili akamalize hasira zake. Kama kawaida alimkuta Shuku amejilaza kwake.

“Vipi mbona ghafla?” Shuku alishtuka kumuona Lily muda ule.

“Nimekukumbuka mpenzi wangu.” Lily alizunga

“Karibu.”

“Asante, Shuku nakupenda nimelala usingizi umekataa kabisa nikaona noje nilale na wewe mpenzi wangu.”

“Mmh! Haya.”

“Mbona unaguna mpenzi?”

“Nimefurahi kuona upendo umerudi.”

“Vipi shemu yupo?”

“Alikuwepo, ooh! Kweli ametoka si unamjua mtu wa totoz alikuwa na mtu wake kamsindikiza.”

“Ametoka saa ngapi?”

“Sasa hivi, nina imani hata dakika kumi hazijapita ungewahi ungemkuta.”

“Mmh!”

“Vipi mbona unaguna?”

“Ndugu yako ataukwaa anapenda sana wanawake.”

“Ndiyo hobi yake, unafikiri na mimi ningekuwa kama yeye ningeteseka hivi.”

“Jamani usiseme hivyo, mbona mi yamekwisha mpenzi wangu.”

“Mmh! Sawa, ila ikijichanganya nami naanza kazi ya kuoa usiku kuacha asubuhi.”

“Usifanye hivyo mpenzi wangu, Shuku nakupenda sana.”

“Haya mama karibu.”

Waliingia chumbani huku Lily akizidi kufura kwa hasira kutokana na kitendo cha MJ kumpaki hotelini kumbe ana wanawake wake. Moyoni aliapa kumshikisha adabu MJ kwa kitendo alichomtenda.

Alipokuwa akivua nguo ili aende bafuni simu yake iliita, alipoitazama alikuwa MJ aliikata huku ajifyonza. Kitendo kile kilimshtua Shuku na kuhoji.

“Vipi mbona hivyo?”

“Si huyu dada nimemwambia nimekuja kwako ananipigia.”

“Si umpokelee unajua amepiga kwa sababu gani?”

“Achana naye mi ndiye ninaye mjua ni msumbufu.”

“Mmh! Haya mi simo.”

Baada ya muda ujumbe uliingia aliufungua na kuusoma:

“Bebi upo wapi? Mi nimeishafika.”

Kauli ile ilimuudhi sana Lily na kuona kumbe alitangulizwa hotelini ili alishwe makombo. Kwa hasira aliizima simu kabisa na kuuapia moyo wake kesho kumfanyia vimbwanga ili ajue naye ana thamani mbele ya mwanaume yeyote.

Walikwenda bafuni kuoga na kurudi kitandani, moyoni Lily aliuapia moyo wake kumpa Shuku penzi zito litakalo mchanganya na kuiomba ndoa ili kuepukana na MJ aliyekuwa akimnyanyasa kimapenzi tofauti na Shuku. Walipofika kitandani baada ya maandalizi mchezo ulianza huku Lily akifungua kitabu cha dazeni burudani zenye utamu usoisha hamu kwa kujituma huku akilalamika muda wote kama anaonewa kitu kilichokuwa kigeni kwa Shuku na kumfanya apagawe zaidi.

“Shu..shu..ku.”

“Mmh!”

“Jamani niitikie basi mpenzi.”

“Bebi unanirusha stimu maana leo umekuja na machejo mapya yaani mimi mwenyewe hoi raha mwanzo mwisho.”

“Niitikie basi..Shu..shu..ku.”

“Mmh!”

“Jamani mbona hivyo hutaki kuitikia mpenzi wangu?” Lily alilalamika kwa sauti ya kumung’unya sukari guru.

“Bebi nikiitikia mtamu atadondoka.”

“Shuku muongo utamu upo juu au chini?”

“Kote kote mpenzi mdomoni kumezidi huwezi kuimba huku unatafuna karanga mpenzi.”

“Niitikie basi usikie nataka kukwambia nini?”

“Haya niite.”

“Shu..shu...aaah.. gari limenaelekea bondeni nidake mpenzi wangu naanguka peke yangu,” Lily alipiga kelele baada ya kwenda markiti bila kutalajia.

Shuku aliwacha atatalike kama kakalia msafara wa siafu, baada ya kutulia aliendelea na safari huku akipata muda wa kumuuliza Lily.

“Mpenzi.”

“Abee.”

“Vipi?”

“Safi.”

“Mbona uniiti tena?”

“Nani alikuwa akikuita?”

“Si wewe.”

“Mimi nimekuita?”

“Ndiyo”

“Muongo! Nimekuita ili iweje?”

“Mmh! Basi.”

Shuku aliendelea kupiga kasia kutoka maji mafupi kuyafuata maji marefu ambayo yalikifanya chombo kianze kuyumba kwa mawimbi kwa kwenda juu na kushuka chini.Kila safari iliyokuwa ikiendelea na ufundi wa Shuku kupiga kasia Lily alikuwa akizidi kukolea ghafla tui lilikolea nazi na kuanza kutatalika tena.

“Shu..shuku mpenzi wangu.”

“Mmh!”

”Shuku niitikie mpenzi wangu nikwambie kitu.”

“Niambie.”

“Nitakwambiaje bila kuitikia.”

“Niite basi.”

“Shuuuku.”

“Naam.”

“U.u.na..nipenda?”

“Ndiyo.”

“Muongo.”

“Kweli nakupenda Lily.”

“Mbona unioi?”

"Nitakuoa mpenzi wangu.”

“Lini?”

“Bebi unazimaliza raha zangu,”

“kwa vipi?”

“Stimu zinapanda unazitibua Lily.”

“Ni..ni..sa..sa..me..me..meeeee....li,lingine tena jamani Shuku yaani leo hata sijui mpenzi wangu.”

Lily alitetemeka kama mgonjwa mwenye degedege na kutulia akiwa amekwenda markiti kwa mara ya pili mfurulizo huku mwanaume kwake mambo baaado kabisa. Mpaka mwanaume anakanyaga yai la kuku na kulipasua mtoto wa kike shughuli ilimkuta na kujikuta akifunua mdomo bila kutoa maneno kama samaki anayekunywa maji.

Kwa vile wote walikuwa wamechoka walipitiwa na usingizi mpaka siku ya pili Lily aliporudi nyumbani kwao. Wakati anatoka alikutana na MJ akitoka chumbani kwake alimkata jicho kisha alibinua midomo na kufyonza kisha alielekea nje kitu kile kilimshtua Shuku na kujiuliza kuna kitu gani kati ya mpenzi wake na MJ.

Wazo lake la haraka lilikuwa labda MJ alimtongoza Lily na kumtolea nje lakini hakutaka mawazo yake kuyaelekeza huko moja kwa moja aliamua kulifuatilia kwa siri.

Walipofika nje waliagana na Lily kurudi nyumbani kwao, njia nzima Lily alijikuta akizidi kumchukia MJ na kuapa moyoni kumkomesha kwa vitendo alichomtendea cha kumwita na kumwacha hotelini kumbe alikuwa na mwanamke mwingine.

Alipofika nyumbani alioneka mtu aliyekosa furaha japo penzi la Shuku lilikuwa mwana ukome. Dada yake alikuwa wa kwanza kuigundua hali ile japokuwa alijitahidi kuificha.

“Vipi mdogo wangu kulikoni?”

“Kawaida tu dada.”

“Hapana haupo vizuri umetibuana tena na shemu nini?”

“Yaani bora tungetibuana kuliko anachoendelea kunifanyia.”

“Kipi tena?”

“Si cha kuita hotelini asitokee na kunifanya kama sina pa kulala.”

“Sasa kama alikuita hotelini asitokee kwa nini usirudi nyumbani kulala. Nawe unapenda mtu hatokei unalala mpaka muda huu.”

“Dada si yamejirudia yaleyale ya Shuku kuokoa jahazi, tena sasa hivi sijui Shuku anajua natembea na MJ yaani penzi analonipa toka nivunje ungo sijawahi kupewa leo nilichanganyikiwa. Yaani kama ndiyo nimo ndani ya ndoa lazima nidai taraka ili ikalifaidi.”

“Mmh! Usiniambie.”

“Dada Shuku anayajua mapenzi anajua apige wapi kumsambalatisha mwanamke.”

“Wacha weee!”

“Nilipanga kumpagawisha lakini nimepagawa mimi.”

“Mmh! Usiniambie.”

“Dada Shuku anayajua mapenzi anajua apige wapi kumsambalatisha mwanamke.”

“Wacha weee!”

“Nilipanga kumpagawisha lakini nimepagawa mimi.”

“Jamani mdogo wangu natamani nami nirudi umri wako nikutane wa wanaume kama Shuku.”

“We ulie umekula kwako endelea na shemeji.”

“Lakini hata shemeji yako anajitajidi akinishika mwenyewe naipata.”

“Dada mi nimeamua kuachana na MJ bora mapenzi yangu yote niliyarudishe kwa Shuku.”

“Ni kweli uamuzi wako ni mzuri, nina imani MJ humuelewi lakini ikimjua hawezi kukusumbua.”

“Dada nina moyo gani wa kuniacha hotelini mara mbili niendelee kuwa naye?”

“Sikiliza mdogo wangu mjini jua kula na kipofu, MJ mchukulie kama sehemu ya kukuingizia fedha ila penzi unalipata kwa Shuku.”

“Sawa dada lakini lazima nami nimkomeshe.”

“Mdogo wangu mwanaume hakomolewi kwa vile tupo wanawake wengi.”

“Kama angejua hilo kwa nini amenifuata akijua mimi ni mpenzi wa ndugu yake. Ukiona ona hivyo kipo kilichomvutia kwangu na kuamua kunifuata.”

“Mmh!”

“Dada usigune yaani anayonifanyie MJ si ya kumtetea.”

Wakiwa katikati ya mazungumzo simu iliingia alipoangalia alikuta ni MJ. Aliiangalia bila kuipokea kitu kilichomfanya dada yake amuulize.

“Vipi MJ nini?”

“Umejuaje?”

“Pokea.”

“Ataniambia nini?”

“Msikilize mdogo wangu, mpaka mtu anapiga ana la kusema.”

“Siwezi kumsikiliza kwa leo labda kesho sitaki kusikia sauti yake wala kuiona sura yake.”

“Haya, lakini usitumie hasira, heri Shuku angekuwa anatoa fedha ulikuwa na haki ya kuachana naye.”

“Tena nimekumbuka narudi huko huko,” Lily alisema huku akinyanyuka.

“Kuna nini?” dada yake alishtuka.

“Nikirudi nitakupa jibu.”

Lily alikwenda kuoga na kubadili nguo kisha aliingia kwenye gari na kurudi kwa Shuku akiwa na lake moyoni mwake.

Nguo alivaa nguo za usiku ziluacha mwili wake sehemu kubwa nje zilikuwa za kuvaa usiku lakini alivaa mchana kwa vile alikuwa anaendesha gari. Moyoni aliapa kumtesa MJ kama akimkuta naye aumie kwa kumuona si mali kitu kumtelekeza hotelini mara mbili.

Alipaki gari kwenye maegesho na kuingia ndani, sebuleni aliwakuta MJ na swahiba wake Shuku wakipiga stori aliwasabahi kwa furaha ya uongo kwani moyoni alimchukua sana MJ.

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

  Ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi Zaidi Naomba Share App kwa Wapenzi wa Simulizi Wapakue(Install) App ya CnZ Media

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)