BODY SPRAY: HANDSOME BOY (1)

Zephiline F Ezekiel
0

SEHEMU YA KWANZA
Baada ya kumaliza chuo pale TIA kozi ya accountancy upatikatikana wa kazi ulikuwa mgumu mimi na rafiki yangu Richard philipo tulijitahidi kuzunguka maofisi mengi hapa town na kutuma application nje ya dar ili kutafuta kazi lakini wapi, tukienda mabenki mara wanataka uzoefu, mara kujuana, mara kahela kidogo/takrima na wakati mwingne hata tulithubutu kukatishwa tamaa na maneja waajiri wengi waliotwambia "toeni chochote kitu ili mpate kazi kama hamtaki muwe na mareferees napo kama hamna bora msipoteze muda mjini rudini shamba mkalime" roho iliniuma lakini nitafanyaje kusoma nimesoma kwa shda na wakati wa kujilipa ndo huu mpaka sasa mambo hayaendi sawa. Nakumbuka hiyo siku tulikuwa tumetoka kuomba kazi benki ya AZANIA sasa hapo tumeshazunguka sana yule secretary akatwambia tuache nakala ya vyeti vyetu na CV kisha watatupigia simu kama tutaitajika lakini sasa nafasi zinatakiwa 15 tunacompete/shndania watu 209 hapo utagundua nafasi yetu ni finyu sana kupata nafasi.

"oya dickson haya maisha mpaka lini kaka? Hapa hatujui tutapata kazi mbele ya watu wale 209 dah sijui itakuaje?"

"sikiliza nikwambie richie mwanaume upaswi kukata tamaa ni kupambna mwanzo mwisho upaswi kurudi nyuma hapa unapaswa kuwa baba wa baadae familia yako unapaswa kuiandaa leo nae mama richard anakutegemea na wadogo zako rajabu na rahma wanataka kusoma, we have 2 struggle man"

Tulikuwa tunabadilishana mawazo mimi na best yangu richard tukiwa tumeketi ndani ya uwanja wa karume tukitafakari safari ya toka saa moja asubuhi na tulipokunywa chai na mandazi matatu matatu ya kukopa kwa mama vickie mpaka saa tisa hatukuweka kitu tumboni.

"sikiliza nikwambie dick maisha haya ni kuthubutu we unaonaje tukajiajiri wenyewe kuliko kutegemea kuajiri, me nina shamba langu mbezi kibanda cha mkaa tuweza kulitumia lile kupata mkopo benki"

"dah yani aki ya mungu nyie wachaga mna akili ya biashara aisee hapo nimekukubali, lakini kaka ni biashara gani sasa tuianzisha?"

"me naona duka ya cosmetics/vipodozi linalipa hasa tukiliweka hapa city centre"

IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA SIMULIZI

ENDELEA...
Biashara ilikolea sana na wateja wetu wengi walikuwa ni wakina dada, wamama na wanaume sio wengi na vitu vilivyokuwa vinanunuliwa kwa wengi ni body spray za 13000, 30000 na 80000, pia lotion za remon na aloe vera na perfume. Mimi nilikuwa na uhakika wa kuondoka na 50000 kwa siku sasa hapo pombe situmii wala sigara.

Ndani ya mwaka mmoja tulifanikiwa kulipa mkopo wa mil.80 tukawa tunadaiwa mil.20 hapo tuliona tusilipe wote tukafungua saloon ya kike mtaa wa bamaga sinza pale mimi mwenyewe nilijifunza kusuka mitindo yote na pia tuliwaajiri wasichana watatu wa kusaidia pale. Kwahiyo ofisi ya town alibaki richie mimi nikawa kwenye ofisi mpya ya bamaga mwendo wa kupiga kazi hakuna kulala basi ndani ya miezi mitatu nikajijengea jina pale sinza yote kwenda hadi tegeta kuja ubungo na maharusi wengi wakawa wanakuja pale kwangu kupambwa.

Jioni ya jumapili tulikutana na richie kujadili maendleo ya biashara zetu na kufikiria kulipa pesa iliyobaki then tukope tena tukachukue mzigo dubai.

"hivi richie unamkumbuka sister jane mganga nae alimaliza pale TIA mbele yetu{akaitikia} yule si alienda dubai tunaweza kumtumia yeye kuagiza bidhaa badala ya kwenda sisi wenyewe"

"dah kaka wazo zuri sema ngoja nitafute email yake tujue tutafanya vipi biashara"

****

Ule mzigo wa dubai ulikuja kipindi hicho richie bado alikuwa dubai me nilibaki kuangalia biashara, katika ule mzigo sister jane alinipa zawadi ya body spray chupa2 na lotion yake pamoja na mafuta yake ya kweli.

Ilikuwa ni jumatatu siku ya kazi hapo nilipigiwa simu na wateja wangu kuna kama vichwa vinne vinanisubiri ilibidi nipitie dukani town kwanza ndo niende sinza. Kwa mara ya kwanza natumia body spry ile kwakweli ilikuwa na harufu nzuri sijawai kuona muda wote ikanifanya nijinuse. Sasa kila nilipokuwa napita kila mtu aligeuza shngo yake. Wakati naingia pale saløøn wadada wote walitahamaki baada ya kusikia ile harufu upendo ndo aliropoka..

"hapna jamani nimeshndwa kuvumilia jamani dick unanukia vizuri na ulivyo mtanashati na dimpoz nahisi wifi anafaidi"

"eeh bora umesema wewe wangu jamani dick wewe ni mwanaume mzuri jamani hizo dimpoz zako kwa hakika hapana umebarikiwa we mkaka" aliongea mama nuru aliyekuja nimsuke.

"nyie jamani acheni ujinga kusifia bwana za watu wengne mmeolewa mna miji yenu lakini bado vinawasha" aliongeza aisha abasi huyo binti wa kisambaa

"jamani huu ni muda wa kazi hayo mengne baadae rehema naomba niletee vifaa vyote nianze kazi" niliamua kumaliza yale malumbano na kazi ilianza mara moja na mdada wanamuita anna bernad yeye anakaa mbezi juu lakini cha ajabu hawa wanawake sijui wapoje huko mbezi kuna saloon nyingi lakini kaja hapa kwa "dick hair beauty&saloon" haya ndo mambo ya kike ila mimi ninachojari mkwanja hayo mengne hayanihusu. Unajua tena mambo ya saloon maneno ndo jadi yake hapo ni umbea hakuna. Upendo akaanzisha tena.

"ila jamani twende mbele turudi nyuma hiyo body spray ya dick me nimeipenda samahani dick nipe namba yako ya simu"

"tse tse tse tse yamekuwa hayo ya kuomba namba za simu halloo kula nile mie machuzi utoe weye " walicheka wote kicheko cha kinafki. Cha ajabu nilipomtajia namba yangu wote walinyanyua simu zao na kuandika.

"haya upendo nataja, ni 0716082149 na nyingine 0684979066"

"nyooo yamewashuka chuuu! Kumbe kuanza kazi mmengoja mimi niombe nyie muandike mna bahati waone" nae upendo aliwatolea uvivu

***

Nilirejea home/ghetto na kujiegesha kwenye sofa mpaka usingizi uliponichukua na kuasha cd ya fally ipupa live in dar ikiendelea kugonga kwenye home theater yangu. Bwana bwana kumbe Amina yule mtoto wa mama mwenye nyumba aliingia ghetto kwangu akajipakaa lotion yangu, mafuta ya nywele na mwisho ndo akaniamsha eti kuniomba body spray yangu.

"dickson! Dick! Dickson! Dick"

"Mmh! Mmh! Mmh! Naaam! Naam!"

"samahani dick naomba nijipulizie body spray yako tafadhari nataka niende kwenye send off ya lilian?"

"chukua tu usijari"

"asante, ila kaka dick mbona upo besy sana unafanya kazi wapi?" mtoto huyu ana maswali.

"mimi nimejiari mwenyewe nina saloon sinza bamaga na tuna duka la vipodozi hapo town tu"

"hongera sana na sisi tukimaliza masomo mtuajiri, vipi una mpenzi? Kwani sijawai hata siku moja ukija nae hapa?"

"hahahaha mtoto huna maswali wewe mpenzi sina kwa sasa labda kwa siku za usoni"

"wow! Lakini samahani kwa hili unajua dicksön wewe ni mzuri napenda mwili wako hasa ninapokutana na wewe unakwenda gym, urefu wako hasa hasa hizo dimpoz zako unanichanganya kabisa"

Nilijukuta nimebaki kimya kwani sikuamini yale maneno yote yalikuwa yanatoka kinywani mwa msichana mdog vile wa kidto cha tano tu. Aliniaga anatoka ila atarejea baadae kuangalia movie nikajiuliza huyu mtoto nimeanza anzaje mazoea nae? Na wakati sikuwa nataka mazoea na mtu kwenye ile nyuma lakini chanzo ni #bodyspray kutoka dubai ndo inapelekea haya yote. Wakati anatoka tu mara simu ya upendo ikaingia akawa ananiuliza nipo wapi anitoe hofa mmh mwenzangu ktk maisha yangu sipendi vitu vya kudandia visije vikanitokea puani. Nilimdanganya kesho yake itakuwa poa ila kwa leo nina hangover. Nikiwa ndani nikasikia ubishani mkubwa kati ya amina na mama swaumu.

"we mtoto unaenda wapi yani usione mkaka mzuri unataka awe wako"

"mama tuheshiane usitake tuvunjiane heshma naomba niache kama nilivyo kwani kutmbw natmbw mie au wewe? Fyoo kubwa zima una soni wala aya"

Amina akaingia ndani na sinia lenye chakula akiwa amevaa dela lake alilochomekea kwenye nguo ya ndani. "karibu msosi kaka dick" aliongea amina huku ananinawisha na kufunua sahani ewaa ilikuwa ni biliani. Mara umeme nao chaaaaaap! Mambo gani tena!

"umeme wa tz bwana hata hautabiriki ona sasa" nilinung'unika nikajua leo nalala bila feni na lile joto pale ndani imekula kwangu.

"usijari ngoja nikakufatie taa ya chemli" aliongea amina huku ananyanyuka

"hapana usiende nina taa inayotumia solar power hiyo hata ukiwa unaitaji kujisomea uje kuifata"

"nashukuru sana kaka dick kwa kunijari kula basi au?"

"haha au nini sasa mbona we mgomvi?

"unataka ulishwe na my wizo, leo hayupo naomba nimrithi kidogo kama itawezekana"

"haaa bwana mbna nilikwambia sina au unanichora?"

"haya bwana ila amini tayari umeshampata"

"khe nani tena huyo?

"Hata sijui we fikiria tu"

Kwa kauli ile ikanifanya niamini kuwa mtoto ananikubali me si mtu mzima. Niliendlea kula mpaka nikamaliza huku tunapiga stori akarudisha vyombo fasta hata dk3 nyingi huyo hapo kafungua mlango.

"kwani kaka dick mwanamke unayetaka kuoa unapenda awe na sifa gani? Na uwe umempita miaka mingapi"

"napenda mwenye kunipenda mimi na ndugu zangu, aniheshmu, anijari asitende na hasa napenda nimpite miaka mi3"

"kwani wewe una miaka mingapi?

"mimi nina miaka 22 wew je"

"wow kumbe nina sifa za kuwa mke wa dicksön edward ha ha ha"

Tulipiga story pale mpaka muda ukawa umesonga sana sasa nashndwa kumwambia nenda kalale yeye akawa anaendlea kupiga story mimi nikapitiwa na usingizi kwani niilikuwa mchovu sana. Kutahamaki najikuta natikiswa na mkono.

"we kaka unafanya nini na Amina mdogo wangu? Ebu angalia saa ngapi sasa hv"

Niliangalia saa ilikuwa ni saa 6

usiku, kumuangalia amina amelala huku ameniegemezea miguu yake dela lake limepanda mpaka kifuani na kuifanya ikulu yake ijichore vizuri kwenye nguo ya ndani aliyovaa.

"nimekuuliza dickson, ndo maana siku hz ananukia vizuri hapa nyumbani umeamua kumpa hadi body spray"

"hapana dada aliniazima kwa muda ila mbona hunaonekana una jazba?

"ndio nina jazba we si unajifanya mjanja unatembea na mdogo wangu ngoja nikamwambie mama"

"hapana sada, we unamjua mama yako alivyo mkorofi kweli nakwambia toka moyoni ule ukweli wangu wote sijamgusa amina"

"anha bado unabisha nisubiri hapo" aliongea kwa vitisho huku akawa kama anataka kuondoka.

"amina ni kama mdogo wangu, na isitoshe sikumfanyia chochote yule ni mwanafunzi kesi ile jamani niambie unataka nini basi?"

"nataka kama ulichompa amina"

"khee makubwa nilichompa nini body spray au?"

"usifunge mlango nakuja sasa hv ngoja nimpeleke amina kulala"

Sada alimuamsha mdogo wake na amina akawa ananiaga vibaya mpaka nikawa nakasirika kuwa dada yake atanielewa vibaya.

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

  Ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi Zaidi Naomba Share App kwa Wapenzi wa Simulizi Wapakue(Install) App ya CnZ Media

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)