.jpg)
Mtunzi: Steve Ndegezy
SEHEMU YA KUMI NA MOJA
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
Angel alidondoka chini nakukohoa mfululizo madam mary alimkimbilia nakumnyanyua wakaondoka.
********_________-----------_______*** mvua ilianza kunyesha kwa Kasi ilikuwa ni mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali,
IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA SIMULIZI
ENDELEA...
ndani ya basi la abiria,wanaonekana abiria wakiwa wamepitiwa na usingizi sababu ya baridi,basi lilienda kwa mwendo wa kawaida,dereva alipata wakati mgumu sababu upepo ulipiga kwa nguvu sana,ikabidi hapaki pembeni kidogo karibu na msitu wa sego,upepo ulipuliza na kufanya hadi basi litikisike,miti mingi ilivunjika nakurushwa mbali.
Baada ya takribani masaa matatu mvua ilipungua nakubaki manyunyu,dereva akawasha basi ili waondoke akapachika gia kisha akaachia krachi nakukanyaga mafuta basi lilitoa tu mungurumo ila halikusogea kumaanisha barabara ilijaa tope,basi likaanza kusogea kidogo kidogo hadi likarudi barabarani,lakini lilianza kuteleza nakuyumba yumba ghafla lilkateleza nakuacha barabara nakuingia ndani ya msitu,liligonga mti mmoja nakuzima,abiria walikuwa wanapiga makelele huku wakihangaika ndani ya basi.Basi lilisimama abiria wakashuka haraka haraka,dereva alilikagua basi nakugundua limeharibika upande wa mbele,aling'ang'ana kuliwasha ila injini ilikaidi kuwaka.
wakati huo huo wale askari pori waliosalia walikuwa wanaendelea kutembea kutafuta njia yakuwatoa ndani ya msitu huo,walilowana kwa kunyeshewa na mvua,walikuwa na hali mbaya sana miili yao ilitetemeka sana lakini hawakukata tamaa,hawakuamini kama wanakimbia vita hakuna aliuyeju kama watakuta hali ni ngumu kiasi hicho.
Walisogea sogea hadi wakafika sehemu fulani nakusikua watu wakiwa wanaongea kwa kulalamika na kulaani kitu fulani,waliingiwa na furaha sana,wakaongeza mwendo hadi wakafika kwenye ile ajali,abiria wote wakawa wanawashangaa wale askari namna walivyochoka nakutetemeka,wale askari nao walishangaa ile basi ilivyogonga mti hakutia neno juu ya huaribifu huo wa misitu walikonyezana kutulia kwanza wafanikiwe kutoka eneo hilo salama ,dereva alifanikiwa kuiwasha aliirudisha nyuma ghafla likazima kabisa,aliamua kupiga simu kwenye kampuni anayoifanyia kazi,mawasiliano yalikuwa ya tabu sana alipanda juu ya basi nakufanikiwa kuongea nakuomba basi lingine lije.
Abiria walisubiria takribani saa zima,ghafla walianza kusikia sauti za vicheko vya ajabu,abiria wote walikimbilia kwenye basi,mara askari mmoja akashikwa miguu nakuvutiwa chini,abiria mwingine alishitukia amefungwa miguu nakamba kisha akavutwa nyuma,abiria wote pamoja na wale askari walijifungia ndani ya basi,wakatulia tuli,wakashitukia kishindo kizito juu ya basi ikachirizika damu kutoka juu nakupita kwenye vioo....
Kelele zilisikika ndani ya basi hilo kila mtu alikuwa na hofu kuu,hatua chache kutoka sehemu lilipo basi linasikika basi jingine la kampuni hiyo likija upande huo huo likuwa lina dereva peke yake.wakati huo huo yule kiumbe hanatokea ndani ya basi hilo bila ya dereva kugundua,anaendesha basi hadi anafika kwenye lile basi lililogonga mti,abiria wanamshukuru Mungu nakushuka ndani ya basi hilo.ghafla yule kiumbe anamuingilia yule dereva,nakubadili akili ya dereva, baada ya abiria wote kuingia ndani ya basi hilo yule dereva analiondoa basi kwa kasi nakuwafanya wale abiria waingiwe na hofu,dereva alizamisha basi ndani ya msitu kwa kasi,
askari pori mmoja akamfata dereva kwa jazba,kwa spidi ya ajabu yule dereva alimrukia yule askari nakuliacha basi likizidi kuingia bondeni, akamgongesha yule askari kwenye chuma,akapoteza maisha hapo hapo,yule kiumbe akamtoka yule dereva kisha akapotea huku akitoa kicheko cha kutisha,dereva alibaki akiwa haamini kama kamtoa mtu uhai,basi lilifika sehemu yenye mseleleko mkali(gentle slope).
Likapinduka nakwenda kujigonga kwenye jiwe,mlipuko mkubwa ukatokea abiria wote pamoja na askari pori wote wakapoteza maisha hapo hapo hakuna aliyepona.
**********************************
Upande wa pili hofu ilizidi kutanda juu ya wanachuo pamoja na maprof walioenda nchini congo kwa ajili ya utafiti,hakuna yoyote aliyejua wana hali gani,hakuna taarifa yoyote juu yao iliyopatikana,uongozi wa chuo ukaamua kutuma timu ya watu kumi kwenda nchini congo kwa ajili ya kwenda kufuatiria nakuleta taarifa,walijianda na kukata tiketi za kusafiria pamoja na pass ya kusafiria,safari ikaanza walitua congo mida ya asubuhi nakwenda moja kwa moja hotelini wakapumzika kesho yake wakaenda kwenye idara inayohusiana na wageni wanaoingia nchini congo,walipewa taarifa ambazo hazikuwalizisha ikabidi waombe msaada utakaowapeleka ndani ya msitu huo,wakapewa askari nakuanza safari ya kuelekea kwenye msitu wa sego.wakiwa ndani ya range rover wanatia timu ndani ya msitu huo.wanashuka sababu gari lao lisingeweza kuingia msituni,wanaingia ndani ya msitu huo,wakiwa wanatembea bila ya kujua kwamba kuna matatizo ndani ya msitu huo,yule kiumbe anatokea juu ya mti mmoja.
-----------------/-------//////------------------\
Angel akiwa na madam Mary pamoja na Prof Moses wanaendelea kutembea bila ya tumaini la kupona,wakati huo Angel anazidi kuzidiwa sababu halikuwa anatokwa na damu nyingi sana mgongoni,wanatembea hatimaye wanafanikiwa kufika kwenye kijiji cha sego,wanapelekwa moja kwa moja hadi kwa mfalme,wanapokelewa kisha angel anapelekwa kwa mtaalamu wao,anawekewa dawa iliyokuwa imepondwa pondwa,kisha wanaletewa chakula wanakula wakati huo Angel alikuwa kapoteza fahamu,yule mganga anaampaka mafuta fulani mwilini mwake anapomshika mkono wake anashituka baada yakuona ule mkufu mkononi mwake angel,
anauchukua kisha anamtizama angel nakumfananisha na malkia ambaye alikwisha fariki,anaamua kutizama nyota yake,baada ya muda kidogo anagundua kwamba angel ndiye binti mfalme aliyesadikika amekufa,habari zinamfikia mfalme kuhusu hule mkufu pamoja na bintiye,akaamua kuja kujionea mwenyewe,alipomtizama angel kweli alifanana na marehemu mke wake anapomgusa, angel anaapata fahamu nakufumbua macho,anapoangalia huku na huko anashituka kujikuta yupo na watu asio wajua,anakurupuka nakupiga kelele za uoga na kutimua mbio,
anazuiriwa na walinzi nakurudishwa ndani,mfalme anamuongelesha angel lakini hawakuelewana, ikabidi aitwe madam Mary aje kumtuliza,angel alipomuona madam Mary akapata matumaini,akaletewa chakula.akala kisha akaelezwa kisa cha kiumbe huyo na chimbuko lake akiwa anatafsiriwa na madam Mary,Angel alikataa kwamba yeye anaundugu nao,ikabidi aonyeshwe na yule mganga,akawasha moto kisha akanuizia maneno haliyoyajua yeye ghafla hule moto ukalipuka nakuwa wa rangi ya blue,badala yakumuonesha angel kilichotokea akiwa mdogo,
hule moto ukatoa ile sauti ambayo angel huwa anaisikia, ikasema waondoke eneo hilo hatari kubwa inakuja kisha ukazimika,kila mtu akabaki ameduwaa hadi mganga naye akawa haelewi,wakiwa bado wanajiuliza angel alijua kitakachotokea akawaambia waondoke lakini walikaidi wakijiamini wakijua yule kiumbe hawezi kufika hapo walipo,angel alimnyakua yule mganga hule mkufu kisha akawaambia madam Mary na Prof Moses wakakikimbia,walinzi wakaanza kuwafukuza mfalme aliwaonya wasimzuru binti yake ila akamatwe nakuletwa kwake akiwa hai,lakini kabla hawajaondoka kijijini hapo wingu zito linatanda angani na upepo mkali kama kimbunga unavamia kijiji hicho nakuharibu vitu,
wanakijiji wanatahamaki nakukimbia ovyo ndani ya kile kimbuga anatokea yule kiumbe wa ajabu akiwa kashikilia vichwa vya askari wawili ambao walikuja na kile kikosi kilichotoka tz kwa ajili ya kuja kuangalia kuna nini kimewatokea wanachuo waliokuja kufanya utafiti,kile kiumbe kinavirusha vile vichwa kisha kinamrukia mganga nakumuangusha chini,upepo uliendelea kupiga kwa kwa kasi nakufanya wanakijiji washindwe kukimbia nakubaki wakishikilia miti ili upepo usiwafute,angel na wenzake nao hawakufika mbali wakajishikiliza kwenye mti,yule kiumbe alimtia meno shingoni yule mganga nakumnyonya damu,kisha kikageuka nyuma nakumuona angel,kilitabasamu nakupiga hatua kumfata angel pale alipo.............
Wanatembea huku wanapiga picha kwa simu zao pamoja na camera madhari ya msitu huo wa sego,juu yao anaonekana yule kiumbe akiwa tizama kwa chini bila ya wao kumuona.
Mmoja wao anachukua kipande cha karatasi kilicho chorwa ramani ya msitu huo nakuwaelekeza wenzake sehemu ilipo kambi ya wanaowatafuta.walipokuwa wakiitizama ile ramani,udenda mzito wa damu unadondoka kutoka juu nakuidondokea ile karatasi wanaangaliana Kisha wanainua vichwa vyao juu lakini hawaoni kitu,wanarudi kuiangalia ile ramani wanaikuta imejaa damu,wanabaki wameduwaa.hali hiyo inahashiria hatari kubwa ipo mbele yao,
askari mmoja anaona kitu kinapita kwa Kasi ya ajabu nakupotea,anafuatilia kule halikoona,tena anahisi kitu kinapita nyuma yake kwa Kasi,anapogeuka nyuma anakutana uso kwa uso na yule kiumbe wa ajabu,anapiga yowe huku akimfyatulia risasi yule kiumbe,wenzake wanashituka na kuanza kukimbia kuelekea kule alipoelekea mwenzao,wanapofika wanakuta kiatu tu pamoja na silaha yake mwenyewe hayupo, wote wanajua sasa hali si shwari msituni humo,wanaweka silaha zao tayali kwa kujihami, ghafla kati kati yao yule kiumbe anafumuka kutoka ardhini,wote wanamuona yule kiumbe mubashara kabisa,wanaanza kumfyatulia risasi mfululizo,
Yule kiumbe anazikwepa kwa Kasi ya ajabu,wanajikuta wao kwa wao wanauwana,askari watano wanaanguka chini pamoja na mtu mmoja kutoka tanzania naye anapoteza maisha hapo hapo baada ya kupigwa risasi,wanabaki askari wawili pamoja na watu tisa kwenye kikosi kilichotoka Tz,yule kiumbe anaruka juu na kutua nyuma yao,nakumkaba mtu mwingine kooni,wale askari pori wakamfyatulia risasi tena,kikaingiwa na jazba kilimtoboa tumbo nakumtoa utumbo yule mtu kisha kikafyatuka kama mshale nakuwafikia wale askari,
kiliwafyekelea mbali vichwa vyao vikadondoka chini,kile kikosi kikatawanyikia ndani zaidi ya msitu huo wasijue wapi wanaelekea,kile kiumbe kilihisi hali ya hatari kikaangalia angani kisha kikainama chini nakuvichukua vile vichwa vya wale askari pori,kisha kikabadilika nakuwa upepo mkali,anga lote likatandwa na mawingu mazito pamoja na radi zilizoambatana na ngurumo,upepo huo ukaelekea kule kijijini hukivuta vitu nakuvirusha mbali.
********************************************************************
Upepo ulivuma kwa kasi sana nakuzidi kuongezeka kila dakika,Angel alishikilia mti kwa nguvu ili upepo huo husimvute,yule kiumbe wa ajabu akawa anamfata pale halipo,kilipomfikia kilinyanyua mkono juu ikatokea shoka mkononi mwake,angel mda huo alikuwa kafumba macho sababu ya hule upepo,yule kiumbe alijiandaa kumfyeka Angel,kiliinyanyua ile shoka juu kwa mikono miwili,lakini upepo ulimzidi angel nguvu hatimaye akajikuta anavutwa na hule upepo,yule kiumbe anashusha shoka ili amuangamize anamkosa kosa Angel kinagadhibika nakumfata kwa kasi,
Angel anakwama kwenye mizizi ya mti mkubwa kwa bahati mbaya hule mkufu unadondoka chini angel anajivuta ili hauokote punde si punde yule kiumbe anamfikia nakumshushia shoka Angel anamuona kwa tabu sababu ya vumbi jingi lililosababishwa na hule upepo akajibiringisha pembeni,ile anatoka tu shoka inamkosa kosa na kunasa nguo yake,yule kiumbe anaichomoa chini ile shoka na kutaka kumuua Angel lakini upepo tena unamvuta sababu akujizuia,kile kiumbe kinaamua kuuzuia hule upepo utulie ili afanye kazi yake bila tabu kwani kilijua Adui yake mkubwa ni angel,
mara upepo ukamtii na kutulia tuli,Angel anapoangalia mbele yake anafanikiwa kuuona hule mkufu,lakini yule kiumbe halikuwa karibu yake.akaamua kujitoa sadaka,akasimama nakuufata hule mkufu yule kiumbe naye alimfata Angel kwa kasi,alifanikiwa kuuokota hule mkufu,anapoinuka yule kiumbe anamuwahi nakumpiga na shoka begani inamuingia kisha kile kiumbe kinamvuta kwa nguvu na hile shoka kisha kiinainua mkono wake juu wenye makucha ya kutisha nakumchoma nayo kifuani kwake,Angel anahisi kuishiwa nguvu,
lakini akajikaza nakumvalisha yule kiumbe hule mkufu kwenye pembe zake.kilimnyofoa Angel moyo nakumrusha mbali.ghafla kilihisi kusisimuka hule mkufu huliwaka nakutoa miyonzi mikali iliyokwenda angani kisha zikarudi kwa Kasi nakumuingia yule kiumbe kifuani.kilipiga kelele kali zilifanya msitu mzima utikisike.ardhi ilipasuka na yule kiumbe akatumbukia ndani kisha ikajifunga huo ndio hukawa mwisho wa yule kiumbe.Angel alitoa tabasamu kuashiria amefanikisha kulitatua tatizo na kulipiza kisasi juu ya vifo vya wenzake alizikumbuka taswira za wazazi wake waliomlea pamoja na marafiki zake chozi likamtoka kisha akakata pumzi.
Wanakijiji walioshuhudia walimkimbilia Angel lakini alikuwa ameishafariki,mfalme alilia sana kwa kuipoteza familia yake aliyoangaika kuilinda nakusababisha matatizo hayo kutokea hatimaye yote imeondoka yote alijifungia ndani mwake kisha akajichoma kisu nakufa msiba mkubwa hulikitawala kijiji cha sego.Prof Moses pamoja na madam Mary bao walipatwa na majonzi makubwa kwa kupiteza wanafunzi wao wote walibaki hawajui wafanye nini kile kikosi kilifanikiwa kufika kwenye kijiji hicho nakuwaona Prof Moses na mary waliwachukua nakuondoka kurudi tz angel alizikwa na kijiji hicho kama shujaa wao pamoja na mfalme......
MWISHO
Ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi Zaidi Naomba Share App kwa Wapenzi wa Simulizi Wapakue(Install) App ya CnZ Media