
Mtunzi: Alexis Wamilazo
SEHEMU YA SITA
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
Hivyo mzee huyo akamsimamisha Marongo kwa upole ikiwa wakati huo wameshapishana kama hatua mbili. Marongo akiwa na hofu alisimama. "Habari yako kijana" mzee huyo alimsabahi Marongo. Hivyo Marongo nae akiwa bado na wasiwasi ..
IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA SIMULIZI
ENDELEA...
akaitikia kisha akamwongeza na heshima yake. "Malakhabaa..kijana samahani nimetoka kijijini leo nikija kumwona mwanangu ambae jina lake anaitwa Adnani, sasa kwa sababu muda mrefu sana sijaja huku! Kiukweli mazingara yamebadilika yamenipotea kichwani.. sana kwahiyo nahitaji msaada wako kwa usiku huu ili kesho asubuhi nimtafute" alisema Mzee huyo alionekana kula chumvi nyingi. "Daah mzee umenisimamisha nikijuwa unajambo la maana kumbe ushenzi tu.. achana na mimi hapa mjini bwana na nyinyi ndio wachawi" Marongo alimjibu hivyo kwa hasira mzee huyo.. kisha akaondoka zake. Cha ajabu baada Marongo kuondoka zake,huyo mzee aliyeomba msaada kwa Marongo...alicheka saana kisha akasema "naam mimi ndio Baluguza" kwisha kusema hayo mzee huyo ambae anaitwa Baluguza alichuchumaa chini kisha akapotea.. akaibukia kule alikotupwa Mele akiwa hana faham...napia ikumbukwe kuwa Baluguza ndio yule mganga aliempa Mele sumu ya kumuua kazula baada Mele kwenda kwa mganga huyo kutafuta dawa ya kumpatia mtoto baada kuishi na Kazula kwa muda mrefu bila kupata mtoto.
Hivyo wakati Baluguza akiibukia kule alikotupwa Mele...upande wa pili nako Marongo alifika nyumbani kwake..moja kwa moja akaingia mpaka chumbani kwake...na alipowasha taa ili alale na kesho afanye mpango wa kutoroka...mala ghafla kitandani aliona mwili ukiwa umelazwa huku umevishwa sanda..na pembeni ya mwili huo palikuwa na jeneza ambalo lilionekana kuchakazwa na damu.
Ikiwa kwingineko napo..mzee Baluguza alifanya uganga wake akawa amemrejeshea faham Mele...ambapo Baluguza aliweza kumtuliza Mele kwa kumtowa woga...kweli Mele akatulia ingawa sio kiviile kama inavyotakiwa...na mwishowe Mzee Baluguza akamwambia Mele hivi "kumbuka ulikosea masherti na ndio maana ukamuua mumeo " Mele hakujibu kitu zaidi aliishia Kulia usiku ule. "Huna haja ya kulia. .amini mumeo bado yupo ila kuna kitu inabidi ukifanye na ndipo utafanikisha kumrejesha mumeo duniani " Wakati Mele akilia kwa uchungu mzee Baluguza aliongeza kwa kusema hivyo...Mele alishtuka na papo hapo faham ikamjia vizuri ..kwanza akahoji nipo wapi hapa? Mzee Baluguza alicheka kisha akamshika kichwa Mele kitendo ambacho kilirudisha kumbukumbu nyuma...na hivyo Mele akakumbuka kuwa kabla ya kufika hapo alipigwa vibaya na mume wake.
Baada kukumbuka hayo,Mele alishusha pumzi kisha akahoji "Ni kweli unaweza kumrejesha Kazula wangu duniani? Alihoji Mele kwa masikitiko "ndio ila mpaka ufanye jambo fulani" mzee Baluguza alijibu.
"Jambo gani hilo! Kabla mzee Baluguza hajamwambia Mele jambo hilo analotakiwa kufanya..Alicheka kwanza kisha akasema..
Mzee Baluguza alicheka kwanza,kisha akasema.
"katika mwili wa marehem mume,wako kuna hurizi kaivaa...hirizi hiyo endapo ukiipata na kisha kuniletea..amini unaweza kumrudisha duniani Kazula " Alisema mzee Baluguza akimwambia Mele. "Hirizi? kwa hiyo nitaipataje hurizi hiyo" Mele akionekana kuwa na mshangao Alihoji hivyo..
"Hahahaaa Mele kuipata hirizi hiyo...lazima umfuate kazula kuzimu je,uko tayali? Kiukweli lilikuwa swali gumu sana kwa Mele kuweza kujibu kwa haraka. Hivyo alishusha pumzi huku akijishauli mwenyewe akilini mwake, kitendo ambacho kiliweza kuchukuwa muda kutoa jibu. "Binti inaama huna haja ya kumrejesha mumeo duniani? Maana naona hukubaliani na masharti hayo ya kuelekea kuzimu " aliongeza kwa kusema hivyo mzee Baluguza huku akimtazama Mele ambae nae aliinamisha uso wake chini kwa kuhisi haibu.
"Hapana babu,kumbuka mimi ndio niliekufuata ili unipatie dawa ya kuweza kutupa mtoto..lakini kama unavyodai kwamba kukosea masharti kwangu ndio kulisababisha kifo cha mume wangu..kwahiyo naomba unipe muda nikajifikilie" Mele alijibu kwa upole "Hahahaaaa binti unampenda mumeo? " Baluguza alimuuliza Mele ."ndio bado nampenda na bado najutia maamuzi yangu" "Ok kama bado unampenda..jambo ni moja tu lakifanya...hahahaha mfuate kuzimu ukachukue hirizi aliyoivaa kisha niletee mimi mganga kati ya waganga kuwahi tokea balani Africa na Dunia kiujumla" Mzee Baluguza aliongea hivyo kwa sauti ya chini chini mfano wa mtu anaemnong'oneza mwenzie.
Kiukweli Mele aliendelea kujishauli kuelekea kuzimu..amabapo alienda mbali zaidi kwa kukumbuka maisha anayo ishi na Marongo...akakumbuka na maisha aliyo kuwa akiishi na Kazula enzi za uhai wake..akaona heri ya Kazula licha ya kuishi kwa taklibani miaka miwili bila kupata mtoto ila Bado kwa kiasi fulani amani ilikuwepo ambapo tafuti na Marongo ambae muda huo alikuwa amempiga mpaka kuzimia. "Babu nipo tayali " Mele akajitaidi kujibu ingawa usoni mwake bado alionekana kuwa na hofu. Hivyo mzee Baluguza baada kusikia jibu hilo la Mele,kwa hakika alicheka sana. Na mwishowe akamwambia hivi "sikiliza binti...yaani wewe bonge la shujaa unafaa sana maana unaroho ya chuma cha pua " alisema mzee Baluguza huku akiachia tabasam. Lakini licha ya mzee Baluguza kutabasam ila Mele hakuweza kutasam kwani akili yake ilikuwa mbali mno akifikiia safari hiyo ya kuelekea kuzimu kwa lengo la kufuata hirizi je, nitafanikiwa? Ndilo swali liloweza kumuumiza akili Mele.
Baada ya Mele na mzee Baluguza kukubalia hayo,hatimae mzee Baluguza alimwamlisha Mele asimame. Mele akasimama. Mzee Baluguza akamshika mkono Mele kisha akamwambia Mele afumbe macho. Punde si punde mzee Baluguza akarudia kumwambia Mele kuwa afumbue macho yake ambapo Mele alifumbuka akajikuta kafika nyumbani kwake."haya upo nyumbani kwako binti..na kabla hujaingia ndani,napenda nikwambie kuwa safari ya kuelekea kuzimu itakuwa siku ya ijumaa..kwa sababu ijumaa kutakuwa na sherehe huko kuzimu hivyo siku ya alhamisi usiku nitakuja ili nikufunde mambo kadhaa ya kutakiwa kufanya kabla hujaenda na baada kufika huko kuzimu! Sawa binti "
"Sawa nimekuelewa" Mele aliitikia kwa huku akiwa bado hajiamini.
"Ok unaweza kuingia ndani"
"Ndani? Hapana babu siwezi mala hii ataniua kabisa huyu mwanaume" kiukweli licha ya kurudishwa nyumbani baada kutupwa na Marongo ambae alimpiga hadi kuzimia,Mele bado aliogopa kuingia ndani akimhofia Marongo kumpiga kwa mala nyingine. Hivyo mzee Baluguza baada kuona Mele anaogopa kuingia ndani..ghafla alipotea pale nje akaibukia chumbani ambapo alimkuta Marongo kalala usingizi mzito. Hivyo kwa kutumia mkono wake,mzee Baluguza alimgusa Marongo kichwani...wakati huohuo Marongo akaota ndoto nzuuri akifurahia maisha na Mele ...ndoto ambayo ilikomea baada kutoka kwenye starehe ghafla Mele akawa amegongwa na gari huku akiwa na ujauzito. Hivyo hiyo ndoto ilimkurupusha Marongo kutoka usingizini huku akimwita Mele "Meleeeeee "
Marongo alishtuka akatoka usingizini ..akatazama kitandani hakumwona Mele..muda huo huo akakumbuka kuwa alimpiga na kisha kumtupa mbali kabisa na nyumbani kwake akihofia kuwa amumuua. "Mele..Mele. ..Mele " Marongo alimtaja Mele moyoni akijutia kwa kitendo kile alicho kifanya...na punde machozi yalimtoka huku huku akishuka kitandani ili aelekee kule alipo mtupa ili ahakikushe kama kweli Mele kafa au alizimia tu.
"Mungu wangu nisaidie ili nimkute akiwa hai " alijisemea Marongo huku akifunga mifungo vya shati ili aelekee kule alipomtupa Mele.
Na wakati Marongo akipanga suala hilo la kumfuata Mele, upande wa pili nako nje...mzee Baluguza alimwambia Mele "tayali nimesha mvuruga,na muda huu anataka kukufuata kule alikokutupa,,kwahiyo basi wewe kaa hapa ili akifungua mlango tu akuone. ..kamwe hawezi kukupiga tena" kwisha kusema hayo,mzee Baluguza alitoweka..ikabaki sauti nzito ikimsisitiza Mele kuwa siku ya ijumaa ni safari ya kuelekea kuzimu... Na wakati sauti hiyo ilipokuwa ikimuhimiza Mele kuhusu suala la kwenda kuzimu, ghafla Marongo akafungua mlango ambapo alishtuka kumuona Mele,hima Marongo akamkumbatia na kisha kumwambia "nisamehe mke wangu.. zile zilikuwa hasira tu"
"Usijali nimesha kusamehe " Mele alimjibu Marongo, lakini akili mwake alikuwa akijisemea" Marongo siri ya furaha yako hii ya madakika,naijuwa ...hivyo msimamo wangu utabaki kuwa pale pale...nipo tayali kuelekea kuzimu kuifuata furaha yangu niliyo ipoteza pasipo kujuwa"
Mele alizidi kuweka nia pale pale..nia ya kuelekea kuzimu kufuata hirizi ili ampe mzee Baluguza, nae mzee huyo ambae ni mganga wa kienyeji..aweze kumrejesha Duniani Kazula.
Hivyo siku zilisonga amani kidogo ikionekana kutawala malangoni kwa Mele..na hatimae ikafika siku ya alakhamisi..ambapo usiku wa siku hiyo,alitokea mzee Baluguza chumbani kwa Mele akawa amewakuta Mele na mume wake wakiwa wamesinzia fofofo. Mzee Baluguza akiwa ameshika kibuyu kidogo mkononi mwake...kibuyu ambacho ndani kilikuwa na dawa..alichovya kidole chake cha Kati ndani ya kibuyu kile alichokuwa ameshika,kisha akampaka usoni Marongo kitendo kilicho mfanya Marongo kuendelea kusinzia pasipo kutikisika. Mzee baluguza alicheka kwanza baada kufanya kitendo kile kisha akamwita Mele
"Binti...Binti...Bintiiiii" Aliita mzee Baluguza,sauti hiyo Mele aliisikia kwa mbaaali ambapo aliweza kushtuka na kugundua kuwa sauti ile ilikuwa ya mzee Baluguza, Mele aliyafikinya macho yake ili apate kuona vizuri kwa Maana alikuwa ametoka usingizini. Kweli hatimae macho yaliona vizuri...akaweza kumuona mzee Baluguza akiwa amesimama kwenye kona ya chumba,huku akiwa amevaa nguo nyeusi..na usoni akiwa amejichora alama mbali mbali watumiazo waganga wa kienyeji. "Hahahahaaa...Binti simama na kisha nifuate " Alisema mzee Baluguza kwa sauti ambayo ilisikika ikijirudia mala mbali mbali.
Hivyo Mele akionekana kuwa na hofu kubwa moyoni mwake,alijifunga khanga yake moja vizuri kwa mwili wake kisha akazipiga hatua kumfuata mzee Baluguza pale kwenye kona ya chumba...na mala baada Mele kumfikia mzee Baluguza, punde si punde walitoweka mle chumbani,wakaibukia kwenye makaburi ya mji. Mele aliogopa sana lakini mzee Baluguza alimtuliza akimwambia "usihofu ondoa shaka kabisa sawa binti?...." Alisema mzee Baluguza huku wakiwa tayali wamesimama juu ya kaburi. Lakini licha ya mzee Baluguza kumwondoa hofu Mele kwa kumwambia hivyo,ila baado Mele alionekana kuogopa...kitendo ambacho kilimfanya mzee Baluguza kumhoji "Kabla hatujaendelea...unaonekana huna ujasiri wa kwenda kusimu je, utaenda au huendi? Alihoji mzee Baluguza kwa sauti iliyo ambatana na hasira.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi Zaidi Naomba Share App kwa Wapenzi wa Simulizi Wapakue(Install) App ya CnZ Media