
Mtunzi: Alexis Wamilazo
SEHEMU YA TANO
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
Kiukweli Marongo alishtuka sana kwa woga aliusogelea mwili wa Mele kisha akaugusa Sehem ulipo moyo akakuta mapigo ya moyo yakiwa yamesimama..daah Marongo alitaharuki ghafla kijasho chembamba kilianza kumtoka wakati huo huo akimnyanyua na kisha kumtwaa begani..
IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA SIMULIZI
ENDELEA...
moja Kwa moja akampeleka chumbani.
Baada Marongo kumfikisha chumbani mke wake ambae tayali alikuwa amepoteza faham..hara haraka akatoka ndani akazipiga hatua kwenda kwa jirani yake kuomba msaada wa usafiri,na kwakuwa jirani yake huyo alikuwa na gari ndogo ya kutembelea hivyo ikawarahisi sana kwa bwana Marongo kusaidiwa.
Ndani ya hospital Mele akafikishwa vipimo vilifanyika ikiwa wakati huo huo faham zilikuwa zimemrudia Mele ambapo neno la kwanza kuongea ilikuwa ni"Nisamehe Kazula" alisema hivyo huku akionekana kuwa na wasiwasi lakini Doctor alimtuliza wakati huo akiendelea kumfanyia vipimo vingine ambavyo vinahusu mambo ya uzazi na mengine kadha wa kadha.
Baada ya masaa mawili kila kitu kilikuwa tayali..na katika vipimo vyote alivyopemwa Mele,jibu moja tu ndio lililoweza kumshtua Marongo baada mke wake kugundulika kuwa hana uwezo wa kuzaa. Kwa hakika Marongo alifadhahika sana moyoni mwake akakumbuka kuwa Mele alishawahi kunasa mimba sasa iweje leo hii aambiwe kuwa Mele tasa?
"No sikubali " Alisema Marongo kwa hasira kali huku akiwa amejiinamia chini.
Sikubali ndilo neno aliloweza kusema Marongo baada kupewa report ya doctor ambayo ilionyesha kuwa Mele tasa. ..yaani hatoweza kuzaa. Kiukweli Marongo alionekana kuchanganyikiwa mno ambapo alinyanyuka kutoka mapokezi kisha akatoka nje ya hospital, huku akiwa na kuwaza ni jinsi gani mke wake ataweza kumpatia mtoto. Wakati huo akiwaza hayo..Marongo alishusha pumzi kwa kasi na mwishowe akaano njia pekee ni kuachana na Mele pindi atakapo pona kwani aliona atamshawishi kwenda pasipo stahili mwishowe ajikute akisababisha madhala kama yaliyomkuta kazula..."siwezi kupanda mmea usio zaa " Alisema Marongo.
kweli baada siku kadhaa Mele kupata ahueni,ghafla mambo yakaanza kubadilika. Mele akaona wazi kabisa kuwa Marongo wa zamani sio wa sasa kwani ilifikia hatua Marongo akawa anamjibu mkewe kivyovyote anavyo jisikia. Hali ambayo ilimfanya Mele kukosa amani, na hivyo akawa anajutia mamuzi yake ya haraka ..mamuzi ambayo yaliyomuondoa duniani kijana Kazula baada kupewa chakula chenye sumu na mke wake ambae ndio Mele alie kimbilia kwa mganga wa kienyeji kutafuta dawa ya kupata mtoto baada kuona miaka ikisonga wao bila kupata mtoto. Hakika Mele alilia sana huku akimtaja Kazula kila mala..wakati huo Mele akilia, alikumbuka maneno fulani aliyowahi kuambiwa na mume wake siku za nyuma baada kutofautia kauli
"Kamwe sitoweza kuishi na mwanamke asie zaa " Ni maneno hayo ambayo yalikuwa yakijirudia kichwani kwa Mele huku akibubujikwa na machozi. Kiukweli Mele aliumia sana moyoni mwake akawaza ataishi vipi endapo akiachwa na Marongo. Lakini wakati akiwa katika dimbwi zito la mawazo,mala ghafla alimuona mume wake kwa mbali akirejea kutoka kazini. Hiyo tayali ilikuwa saa kuminambili jioni. Kiukweli macho ya Mele hayakuamini baada kumwona mumewe akirejea nyumbani huku akiwa amelewa, Mele alistaajabu sana kwani haikuwa kawaida yake Marongo kulewa pombe na istoshe zaidi bwana Marongo alikuwa akitoa matusi mabaya kwa mke wake..lakini kwa kuwa Mele alikuwa hana kimbilio . hivyo alikaa kimya licha ya Marongo kumtukana sana huku akikazia saula la kumtimua mele nyumbani kwake.
Naam baada kufoka kwa muda mrefu hatimae Marongo alitulia kitandani ambapo punde si punde akapitiwa na usingizi..na hivyo Mele akawa amepata unafuu ingawa alifaham fika kuwa yeye sio mali ya Marongo tena baada kugundulika kuwa hazai. "Nitafanya nini mimi? Mele alijiuliza wakati huo tayali giza limeshatanda. Na kabla hajapata ghafla alisikia mtu akitembea sebleni. Mele alishtuka mwili ukaanza kumsisimka na punde si punde mume wake nae alishtuka kutoka usingizini hivyo akadai apelekewe maji bafuni ili aoge...
kiukweli licha ya Mele kusikia vishindo vya mtu akitembea sebleni cha ajabu alipiga moyo konde hakutaka hata kumwambia mume wake...na hivyo alishuka kitandani kisha akazipiga hatua kuelekea sebleni ,na wakati anafungua mlango wa chumbani ili aingie sebleni..alishtuka baada kumwona mtu alievaa sanda akiishia kwenye kona ya seble. Mele alipiga kelele lakini alipewa jibu moja tu na mumewe "acha kuleta uchizi wako hapa..peleka maji nikajimwagie tasa wewe nitakubomoa sasa hivi ebo" Alisema hivyo Marongo kwa sauti ya ukali..Mele aliumia sana chozi lilimtoka ila alijikaza kisabuni kisha akampelekea mume wake maji bafuni kama alivyo ambiwa.
"Kukaribia maji mume wangu yapo tayali" Alisema Mele baada kurejea ndani na kumkalibisha Marongo maji..na Kwa chuki aliyokuwa nayo Marongo kamwe hakuweza kuitikia ile karibu,bali zaidi alichukuwa taulo yake akajifunga kwa kiuno kisha akazipiga hatua kuelekea bafuni kuoga. Dakika zisozidi kumi zilikamilika Marongo akiwa bafuni kuoga,na mala baada kumaliza alitoka ambapo alipokuwa akirejea ndani,ghafla alitokewa na mtu nyuma yake..mtu huyo alikuwa kifua wazi huku macho ya huyo mtu yalionekana kuwa mekundu mfano wa mtu aliekula pilipili vilevile mtu huyo alikuwa na kucha ndefu na nywere ndefu pia..yani kimsingi mtu huyo alionekana kutisha " Kaka kaka kaka" yule mtu alimwita Marongo kwa sauti ya kunong'ona.
Marongo nae baada kuisikia hiyo sauti,alishtuka hima akageuka nyuma..cha kushangaza hakumuona huyo mtu aliyekuwa akimwita ...hivyo Marongo akaamua kukazana ili aingie ndani lakini kabla hajaukalibia mlango wa kuingilia ndani...ghafla akageuka nyuma kwa mala ya pili ambapo alitaharuki baada kuona jopo la wafu wakimfuata na katika wafu wale alikuwemo Kazula. .kwa hakika Marongo aliogopa sana hima akatimua mbio kuusogelea mlango punde akaukalibia lakini mlango ulikuwa umefungwa...hivyo Marongo akapasa sauti kwa ukali akimwambia Mele afungue mlango ikiwa wakati huo Mele nae alikuwa kaketi kitandani akiyatafakali maisha ambayo anaishi na mume wake ambae alionekana kubadilika kwa asilimia kubwa tangu agundulike kuwa tasa...hivyo hata sauti ya kuitwa na mumewe kamwe hakuweza kuisikia kwani wale wafu waliifanya sauti ya Marongo isambae mahala popote.
Hofu na woga ulimjaa Marongo akiwaogopa wale wafu waliokuwa wakizipiga hatua kumfuata..hivyo Marongo aliendelea kupiga kelele za kumwita mkewe Mele ambae nae alikuwa yupo chumbani kaketi kitandani akiyatafakali maisha anayo ishi na mume wake ambae ndio Marongo, kwani tangu bwana huyo agundue kuwa Mele tasa..upendo wa dhati ulipungua hadi kufikia hatua Marongo kumtolea maneno mabaya Mele. Na hivyo Mele akajikuta akikosa amani. Na wakati Mele akiwa bado yupo katika dimbwi la mawazo, upande wa pili nako Marongo aliendelea kupiga kelele akimwita mkewe aje kumfungulia mlango,,lakini sasa kutokana na wale wafu waliokuwa wakimfuata Marongo kuzuia sauti isiweze kupasa mahala popote,
hatimae Mele hakuweza kuisikia ile sauti Kwani laiti angelisikia,hima angemfungulia mlango mumewe ili ajiokoe dhidi ya wale wafu waliokuwa wakizipiga hatua kumfuata. "Mele nifungulie mlango mumeo nakufa! Mele nifungulie mlango mumeo nakufa!" Alisema hivyo Marongo huku akipiga mayowe,ila bado mayowe hayo hayakuweza kusaidia. Naam punde si punde wafu tayali wakawa wamemkalibia Marongo ,na katika wale wafu alijitokeza mfu mmoja ambae ni Kazula. Kazula alijitokeza akionekna kachakaa kila sehem ya mwili wake...huku kucha na nywere zake zikiwa ndefu,na mdomoni alikuwa akitokwa damu. Hakika Marongo aliogopa sana baada kumwona Kazula, haraka sana alirudi nyuma..lakini kutokana na kuisogelea nyumba jirani zaidi..hivyo akashindwa kurudi nyuma sana,hali iliyomfanya marehem Kazula kumsogelea zaidi. "Marongo Marongo unanikumbuka? " Kazula akiongea kwa taabu saana,alimhoji hivyo Marongo...lakini kwa sababu ya woga aliokuwa nao Marongo. .kiukweli alishindwa kujibu na zaidi aliishia kuhema kwa kasi huku akimwomba msamaha Kazula. Kazula nae baada kumeona Marongo
akiomba msamaha,aligeuza shingo yake akiwataza wafu wenzake.. na hapo Kazula akawa amekutana na uso wa mfu mmoja alieonekana mzee kuliko wote...mfu huyo alionyesha ishara fulani. Ishara ambayo Kazula alitambua kuwa muda wa kuendelea kutembea duniani umekwisha. Kiukweli kazula baada kugundua hilo aliinamisha uso wake chini ...akionekana kukerwa..ila hakuwa na budi. Zaidi alisema "Bado nipo hai popote mlipo nipo lazima nilipe kisasi " kwisha kusema hayo Kazula pamoja na jopo la wafu wenzake walipotea.
Hakika Marongo alibaki ameduwaa alicho kiona asiamini kama kweli ama ndoto. "Kazula! kazula! " Alijisema Marongo huku akijifunga taulo yake sawa..kwani kutokana na woga aliokuwa nao..taulo yake ilimdondoka. Hivyo wakati Marongo akijifunga sawa taulo yake kwa kiuno chake,upande wa pili nako. .. ghafla Mele akatoka kwenye dimbwi la mawazo,ambapo alishtuka baada kutomuona mume wake chumbani..hivyo Mele akiinuka kutoka kitandani..alisikika akijusemea "mungu wangu..kakutwa na nini mume wangu tangu muda ule hadi sasa hajarudi" alisema Mele huku akiusogelea mlango,na punde akafungua ambapo alikutana na kipigo kizito kutoka kwa mumewe..kipigo ambacho Marongo alikuwa akikitoa huku akimtukana matusi mabaya "unataka kumwambia kuwa hujanisikia nilipokuita? Mbona unadharau sana malaya mkubwa wewe.. hakika wewe mchawi sana na ndio maana umemuua Kazula pumbafu" Alisema Marongo kwa sauti kali akimfokea Mele huku akiendelea kumpiga. Maskini Mele alilia sana akiomba msamaha..ila Marongo hakujali msamaha wa Mele hivyo aliendelea kumpiga hadi Mele akapoteza faham.
Hali ile ya Mele kuzimia, ilimshtua bwana Marongo kwani alijuwa kuwa tayali kauwa. Hivyo ili kukwepa jela kwa kuhusishwa na mauaji,Marongo aliamua kumbeba Mele na kisha kwenda kumtupa mbali kabisa na nyumbani anakoishi...kisha akarudi nyumbani kwake huku akijutia ndani ya nafsi yake juu ya unyama alioutenda.. aliogoapa sana kiukweli Marongo .
Lakini wakati marongo akirejea nyumbani kwake baada kumaliza shughuli yake ya kuutupa mwili wa mkewe Mele , ghafla njiani alikutana na mzee mkongwe mno. .mzee huyo mkononi alikuwa ameshika kifurushi kidogo na kibuyu kilicho zungushiwa shanga. Hivyo mzee huyo akamsimamisha Marongo kwa upole ikiwa wakati huo wameshapishana kama hatua mbili. Marongo akiwa na hofu alisimama. "Habari yako kijana" mzee huyo alimsabahi Marongo. Hivyo Marongo nae akiwa bado na wasiwasi ..
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi Zaidi Naomba Share App kwa Wapenzi wa Simulizi Wapakue(Install) App ya CnZ Media