TOROJO BAMIA (22)

Zephiline F Ezekiel
0

SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI
ILIPOISHIA...
Mwanaume hakutaka kulemba tena, siku zote mtoto hatishiwi ubwabwa ndicho chakula anachokipenda. Chombo kikarudishwa kwenye maji na kupiga kasia mtindo mmoja mpaka walipojikuta wakiangukiana baada ya kila mmoja miguu kupoteza uwezo wa kusimama kwa muda mrefu.

IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA SIMULIZI

ENDELEA...
Kwa vile ulikuwa mpambano wa kushtukiza, baada ya kuoga walirudi ndani na kupanda kitandani kujipumzusha na kujikuta wakipitiwa usingizi mzito.

Wa kwanza kuamka alikuwa Lily, bado hakuamini kama kweli Shuku ameoa, ili kupata uhakika alianza kupekua kwenye kabati iliyokuwa wazi.

Alichambua kwenye nguo labda atakuta nguo za kike, lakini hakuona kitu. Alichukua albam na kuangalia picha na kushangaa kukuta picha zake na Shuku za zamani wala hakukuwa na picha za mwanamke mwingine pia kulikuwa na picha alizopiga Shuku akiwa shamba alipokuwa akienda kukusanya mazao.

Baada ya kufanya upekuzi wake uliochukua chini ya dakika kumi bila kuona alichokikusudia. Alijikuta akijiuliza huyo mwanamke aliyemuoa Shuku yupo wapi na mbona hakuna picha wala nguo zake na kwa nini picha zake iwepo kwenye albam ya Shuku na si ya huyu mwanamke wake.

Alijikuta akikosa jibu la moja kwa moja, kuwepo kwa picha zake ilionesha Shuku bado ana mapenzi na yeye lakini mbona kamwambia ameishaoa? Alijikuta akichanganyikiwa na kushindwa kuelewa hatima yake kwa Shuku.

Alijiuliza akiamka atamwambia nini ikiwa tayari amemtamkia ameoa. Alirudi kitandani na kukaa pembeni ya Shuku aliyekuwa bado amepitiwa na usingizi baada ya shambulizi ya kushtukiza lililomchosha sana.

Lily alianza kulia kilio cha sauti ya chini iliyomshtua Shuku kwenye usingizi.

Aliposhtuka na kumukuta Lily amekaa kitandani akilia, aliuliza.

“Lily unalia nini?”

“Najua nitakufa Shuku.”

“Utakufa! Kivipi?”

“Utaniua wewe Shuku.”

“Mimi nikuue wewe! Kivipi?”

“Hunipendi.”

“Mimi na wewe nani hampendi mwenzake?”

“Wewe Shuku, kwa nini kila mara unapenda kunidanganya?”

“Kukudanganya kivipi?”

“Shuku huna mwanamke.”

“Nani kakwambia?”

“Shuku nimekufuatilia muda mrefu ndiyo maana hata wewe kukubali kufanya mapenzi na mimi ulijua huna mtu.”

“Hiyo siyo sababu.”

“Shuku kweli huna mwanamke, nakuapia hapa sitoki tena, mi ndo nimefika,” Lily alisema huku akijilaza juu ya Shuku ambaye hakupata nafasi ya kuzungumza kitu.

Mtoto wa kike akaanza utundu uliomfanya Shuku asisimke kwa vile alikuwa na ugwadu wa muda mrefu, chombo hakukichelewa kukolea moto.

Mtanange wa bafuni japokuwa palichimbika bila jembe lakini ilikuwa kama kupasha moto mwili. Mchezo ulihamia kwenye uwanja wa vita wa sita kwa sita.

Lily alimkalia juu Shuku na kuanza kufanya utundu uliomdanya aliruke kama kalalia siafu.

Alijiteremsha kuufuata mdomo wa Shuku ambao aliupata na kuifanya igandane,

Shuku naye alitii amri kwani sumu ya hamu ilikuwa imemtawala mwili mzima naye alipitisha mkono shingoni kwa Lily na kumvutia kwake na kuanza kubadilishana mate.

Kwa umbile na uwezo wa Lily ulimfanya Shuku asahau maudhi yote ya zamani ya mpenzi wake. Lily alimpindua Shuku na yeye kuwa chini na kuikutanisha miguu yake mgongoni kwa Shuku kama mtoto wa nyani.

Kama kawaida Lily alikanyaga mpira na kumfanya Shuku autafute kwa muda kwa muda mfupi. Hakuchelewa kuupata alipoupata naye akajibu mashambulizi kwa pasi fupifupi zilizomfanya Lily alalamike.

“Jamani Shuku mpenzi wangu siyo hivyoo au hufurahii kuwa na mimi.”

“Nafurahia mpenzi wangu.”

“Sasa mbona unanibania nipe raha zangu nilimezikosa muda mrefu.”

Mtoto wa kike alilipandisha jicho pumzi zilimtoka kwa shida chini nyonga ilifanya kazi kama nyoka anavyosafiri kwenye majani.

Aliamini hakuna njia nyingine ya kujirudisha kwa Shuku ni kumpa penzi shatashata lisilochanganywa na maji. Shuku aliyekuwa kama mbwa kwa chatu anapokutana na Lily naye aliyeuanza mchezo kwa kusuasua alirudi mchezoni.

Alianza kutandaza soka safi huku akitawala sehemu ya kiungo na kumfanya Lily autafute muda wote. Baada ya Lily kupata kipigo cha pweza alijikuta akitoa siri ya MJ.

Shuku alimchanganya Lily na mtindo wa Punzu magulu remix. Alijikuta akihama katika dunia aliyoizoea na kujikuta akitokwa na maneno kama mvua.

“Shuuuukuuu aashiii, unajuaaa, Shuku unajuaaa. Shuku niliota kutu kupakwa shombo na MJ leo chuma kimapata msasa safishaaa mpenziii.”

Lily alilalama huku akiiachia nyonga izungumze na Shuku naye alikuwa amemisi maini ya Lily kwa muda mrefu mwiko ulifanya kazi ya kuyageuza kwa mahiri mkubwa. Alijigeuzia atakavyo, mpaka wanakwenda mapumziko Lily alikuwa ndwembwendembwe.

Baada ya mpambano wa kukata na shoka Lily aliangua kilio kilichomshtua Shuku.

“Lily unalia nini?”

“Kwa nini ulinidanganya?”

“Kukudanganya kivipi?”

“Kwa nini hukuniambia ukweli mwanzo wa penzi letu?”

“Nilijua nitakukosa, Lily nilikuwa nakupenda sana.”

“Kwa hiyo sasa hivi unipendi?”

“Narudi mimi na wewe nani hampendi mwenzake?”

“Wewe.”

“Nani aliyemsaliti mwenzake?”

“Wewe.”

“Kwa nini?”

“Hakuniambia ukweli kitu kilichosababisha niyaamini maneno ya MJ.”

“Kwa nini ulimuamini?”

“Mitego niliyokutega ndiyo iliyokunasa, kwa hiyo yote aliyoniambia niliyaamini. Ona raha hizi nilizipoteza Shuku nazidi kukulaumu kunidanganya.”

“Sasa kama uliyaamini tatizo nini?”

“Nimegundua MJ si mkweli mgombanishi kupitia fedha zake. Shuku yote umesababisha wewe,” Lily aliendelea kumlaumu Shuku.

“Lakini uli...”

“Shuku usiseme lolote kila siku nitakulaumu wewe.”

“Basi yamekwisha.”

“Shuku unanipenda?”

“Zaidi ya kukupenda.”

“Naomba usinidanganye ili nami nidumu kwenye penzi lako. Mimi si mpenda fedha kama unavyodhani bali naogopa kudanganywa.”

“Nimekuelewa mpenzi wangu.”

“Kama umenielewa nipe haki yangu.”

Shuku hakuwa na hiyana kwani hata yeye aliumia kuachwa na Lily mwanamke ambaye kwake ndiye aliyekuwa chaguo la moyo wake. Kazi ikawa bandika bandua kila mmoja alitaka kuonyesha anajua mapenzi mpaka raha ikageuka karaha na kuamua kupumzika wakiwa hoi.

***

Penzi lilirudi kwa kasi huku Lily akimganda Shuku kama luba ili kuhakikisha hampotezi. Baada ya muda Lily aliuza nyumba na kuhamia kwa Shuku kujipanga na ndoa yao. Kila kitu kilikwenda kama kilivyopangwa. Siku ilipofika ilifungwa harusi ya kifahari huku MJ akichangia kwa kiasi kikubwa na siku ya harusi aliitumia kuomba msamaha kwa maharusi.

Shuku hakuwa na hiyana na rafiki yake alimsamehe huku akimpa onyo akimfuata tena mkewe atamteremsha mshipa. MJ alimwambia rafiki yake kuwa kuoa kwake kumpa fundisho kubwa hivyo naye aliamua kumtafuta mwanamke mmoja na kufunga naye ndoa kuanza maisha mapya.

Mpaka sasa hivi maisha yanakwenda Shuku na Lily wana mtoto mmoja na mke wa MJ anakula maembe mabichi na mate yanamjaa mdomoni.

MWISHO

  Ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi Zaidi Naomba Share App kwa Wapenzi wa Simulizi Wapakue(Install) App ya CnZ Media

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)