NYOKA WA KUTUMWA (10)

Zephiline F Ezekiel
0

SEHEMU YA KUMI
ILIPOISHIA...
MFALME: Lazima usinielewe kwa kuwa ukweli umejulikana, sasa nataka uniambie yule Nyoka ulieniambia anaitwa Ruka wa nani. { Mfalme aliongea kwa hasira }

KAMA SIMULIZI HII UNASOMEA NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI KUPATA VIPANDE VYOTE KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈

ENDELEA NAYO...
Sube alikataa na kusema amfahamu mwenye yule nyoka lakini mfalme aliendelea kum’bana na mwishoe sube akakosa kitu cha kujitetea na kubaki akiwa ameinamisha kichwa chni kuashiria kukubali lile kosa, Mfalme alisikitika sana alipoona jambo lile ndipo akaanza kumuonya.

MFALME: Sube nilikuamini sana na sikufikiria kama wewe ungekuwa muhusika wa jambo hili nimekufanya uwe mshauri wangu na ukanishauri mambo mazuri kumbe ulikuwa ukiniuma huku unapoliza, kwanini uliamua kufanya hivi nimeumia sana nilipofahamu ukweli huu. ujio wangu kwako nimekuja kukupa onyo mzuie huyo yoka wako, na usirudie tena kufanya jambo hili maana sitakusamehe tena bali hukumu ya kifo itakuwa juu yako kama nilivyofanya kwa wenzako waliosababisha matatizo hapa kijijini.

Aliposema hivyo akawachukua walinzi wake na kuondoka nao bila kuaga huku akiwa na hasira, kitendo kile kilimshangaza sana bibi sube na kujiuliza nini kimetokea, haraka akakimbilia sehemu aliyokuwa mume wake na kumkuta akiwa amesimama huku ameinamisha kichwa chini kama mtu alieonewa, ndipo akaona bora amuulize kilichotoekea.

BIBI SUBE: Meme wangu kwani kimetoke nini mbona mfalme ametoka kwa hasira vile.

Sube hakujibu kitu na kuendelea kuinamisha kichwa chake chini, jambo ambalo lilizidi kumchanganya bibi sube.

BIBI SUBE: Mume wangu kwani si ninakuuliza au aunisikii, kimetokea nini kati yako na mtukufu mfalme.

Sube aliopna mke wake ameng’ang’ania jambo hilo ndipo akamjibu huku misuri ya kichwa ikiwa imemsimama kutokana na kuchukia yale maneno ya mfalme.

MZEE SUBE: Mfalme amegundua ukweli kuhusu Yoka nahisi kuna mtu amemwambia.

Bibi sube alishtuka kupita kiasi na kuishiwa nguvu ya kusimama

BIBI SUBE: Eeeeeeeee !! Mume wangu mfalme amejua kweli ?. Sasa itakuaje jamani si kufa huku mume wangu.

aliposema hivyo Sube akajibu huku akiwa na jaziba kama mtu aliefumania ugoni au kuona mtoto wake akipigwa na jirani.

MZEE SUBE: Hafi mtu eti anasema amenisamehe ila nisirudie tena, chamoto watakiona sitajificha tena na nitafanya juu chini mpaka mfalme na yeye nimuangushe madarakani, na huyo alieenda kumwambia nikimgundua lazima arudi kuwa mavumbi, sipendi mtu aingile mambo yangu.

BIBI SUBE: Hapana mume wangu kama tumesamehewa tuachane na mambo haya tutakufa.

MZEE SUBE: Siogopi kufa na leo Mfalme ama zake ama zangu.

BIBI SUBE: Kwahiyo unataka kumfanya nini.

MZEE SUBE: Subilia utaona ikifka usiku.

Sube akatoka na kwenda kusikojulika na kumuacha mke wake bado akiwa amekaa pale pale chini, Bibi sube alisikitika sana na kujirahumu kwanini alikubali wafanye jambo lile lakini alikuwa ameshachelewa kuwaza jambo hilo. Mfalme alipofika nyumbani kwake kama kawaida mawazo yaliendelea kumtawala huku ajirahumu kwanini alimuamini mzee sube haraka vile mpaka inapelekea anashindwa kufanya hukumu inayo mstahiri. alijirahumu kwanini alikuwa akifanya mambo bila kuomba ushauri kwa wazee wengine na kusababisha kuondoa viongozi waaminifu na kumuweka mzee sube.

Masaa yalienda hatimae usiku ukafika, Sube na mke wake wakajiaanda vizuri kufanya kazi yao kisha wakaenda nyumbani kwa mfalme kwa nija ya kichawi, na kumkuta akiwa amelala fofofo pamoja na mke wake, Ndipo wawili wale wakaanza kuimba na kucheza zile nyimbo zao za kichawi huku wakizunguka kitanda cha wawili wale. Mda huo Yoka na yeye alikuwa akizini kuuma watu kwa kasi maana Sube aliamua kufanya ubaya zaidi kwa wanakijiji wote. Walipomaliza kucheza Sube akachukua unga na kumlisha mfalme huku akisema maneno ikiwa kama kunuia kile anachomlisha.

MZEE SUBE: Wewe mfalme ninapokulisha unga huu ninataka usiwe na kauli yoyote kwangu na kila nitakachokisema mimi ukakikubali mara moja. Na endapo utaenda kinyume kifo kiwe juu yako.

Bibi sube akachukua maji yaliyokuwa kwenye kibuyu na kumnywesha mfalme, kisha wakatoeka na kutokea nymbani kwao huku wakiwa na furaha kutokana na kufanikiwa jambo lao. Ndipo Sube akaanza kumueleza mke wake vitu gani anatakiwa yeye afanye ikifika kesho yake ili ile dawa ikamilike asilimia zote.

MZEE SUBE: Mke wangu mpaka sasa hivi kazi tulioifanya imefikia asilimia Hamsini kwahiyo bado hamsini zingine ili kazi yote ikamilike kabisa.

BIBI SUBE: Kwanini umesema hivyo.

MZEE SUBE: Hii dawa itakamilika kesho asubuhi inabidi mimi nikamuamushe mfalme kabla ajaamka yeye mwenyewe au kuamshwa na mtu mwingne yeyote na endapo nitafanikiwa kufanya hivyo dawa itakuwa tumeifanikisha kwa asilimia zote..

Bibi sube hakua na chakuongea zaidi ya kumuomba mume wake awe makini atakapoenda huko kwa mfalme, wawili wale wakala. Mfalme akiwa kwenye usingizi alianza kuota ndoto.

Alikuwa yeye pamoja na mzee sube wakiwa wanatembe huku na kule katika kijiji chao huku mzee sube akiwa amebeba ule unga wenye rangi nyeupe na nyekundu na begani mwake alikuwa amembeba yule nyoka anaeitwa YOKA.Wakati wapo katikati ya safari ghafla mzee sube akaanza kurefuka na kuwa mkubwa, hapo hapo mfalme akabadirika na kuwa kama mtoto wa miaka minne au mtano, ndipo Sube akaanza kumcheka na kuongea maneno ya kumdharau.

MZEE SUBE: Hahahaha nahisi jeuri yako imefika mwisho. Siku zote siwezi kuongozwa na mtoto mdogo kama wewe na utakuwa ukifuata kila nitakachokuambia mimi.

Kisha akachukua ule unga na kumlisha,,,,,,, ghafla mfalme akashtuka kutoka usingizini na kukaa kitako huku akiitafakari ile ndoto. Mda mchache mbele mke na yeye akaamka na kumkuta mfalme akiwa amekaa akamuuliza tatizo, mfalme bila kuficha akamwambia nini ameota, mke alisikitika sana na kumwambia itakuwa mizimu imeamua kukuonyesha ubaya wa mzee sube kwahiyo kazi kwake kumuhukumu au kumsamehe kama alivyosema yeye mwenyewe. Maneno ya mke wake yalimgusa na kumfanya abadili ule uamuzi wake, akatoka nje na kuchukua walinzi kadhaa na kwenda nao mpaka nyumbani kwa mzee sube, mda huo ilikuwa yapata majira ya saa kumi na moja alfajiri.

Walipofika nyumbani kwa mzee sube ndipo mfalme akafungua mlango na kuingia ndani bila hata hodi na kukuta wawili wale wakiwa bado wamelala. Akaamuru wale walinzi wawachukue,,,, Sube na mke wake walishtuka kuona mfalme amekuja kuwakamata maana hawakutegemea kabisa kutokea jambo hilo. Bila kuchelewa walinzi wakafanya kama walivyoambiwa wakawachukua na kuwapeleka mpaka mbele ya nyumba ya mfalme ambako huko ndiko utolewa hukumu. Kijana mmoja akaenda kupiga ngoma ya dharula ili wanakijiji wasogee sehemu ile washuhudie hukumu itakayo tolewa kwa mzee sube na mke wake.

Watu wengi walijiuliza kitu gani kimetokea mpaka ikapigwa ile ngoma maana wengi wao walikuwa awajui nini kinaendelea pale kijijni. Kutokana na shahuku waliokuwa nayo haraka walitoka majumbani kwao na kuwasili nyumbani kwa mfalme na kukuta wawili wale wakiwa wamefungwa kwenye mti uliopo sehemu hiyo. Watu wengi walishangaa kuona sube na mke wake wapo sehemu ile pia wale wazee na wao walishangaa na kujiuliza nini sube amefanya mpaka afikie hatua ile wakati alikuwa mtu wa karibu na mfalme. Lakini maswali ya watu wote waliofika sehemu ile yalijibuwa baada ya Mfalme kueleza kosa la watu wale.

MFALME: Jamani nimewaita hapa kwa ajili ya kuona hukumu ya watu hawa kwa kosa la kutengeneza nyoka ambae ameleta madhara makubwa sana hapa kijijini kwetu na kusababisha vifo vya wenzetu wengi.

Maneno ya mfalme yalisababisha kutokea kimya kisichokuwa cha kawaida kutokana na watu wote kubaki vinywa wazi, kutokana na kuto amini kile walichokisia, mara minong’ono ya chinichini ikaanza ndipo mfalme akaendelea kuongea.

MFALME: Siku zote tumekuwa tukikataza watu kufanya mambo kama waliofanya wawili hawa na hukumu kali tumekuwa tukitoa kila anapopatikana mkosa lakini bado watu wanajifanya awaelewi wanaendelea kufanya mbambo yao, kwahiyo kutokana na kosa walilolifanya wanaukumiwa kifo kwa kupigwa mawe mpaka mwisho wa uhai wao.

Mfalme aliposema vile baadhi ya watu walipiga makofi na kushangilia jambo lile lakini wengine waliwaonea huruma na kutamani wangewasamehe, lakini kwa kuwa hukumu ilikuwa tayari imetoka basi hakukua na jinsi. mfalme akaendelea kuongea.

MFALME: Ila kabla ya yote napenda kutoa shukrani kwa vijana wa hiki kijiji kwa kazi yao kubwa walioifanya mpaka tukafanikiwa kumpata msaliti na hadui kwetu, na kuanzia sasa wale vijana wote walioshiriki kutika kumpata mbaya wetu watukuwa askari wangu. Ila kuna kitu nimejifunza sio kila anaekuchekea ni mwema kwao bali mda mwingine anasubilia ugeuze kisogo ili atoe makucha yake, nilimuamini sana huyu mzee na alikuwa akinipa ushauri mzuri kumbe huyo huyo ndie adui kwangu na kwa wanaichi wangu. ….. kwahiyo kuanzia sasa hukumu itolewe kwa watu hawa.

Ndipo wakaja baadhi ya askari wakiwa wamebeba mawe na kuweka mbele yao, walipomaliza kazi hiyo ndipo waanza kuwarushia. Wakati wanafanya vile, ghafla kwenye kichaka akichoishi Yoka kikaanza kuwaka moto na kutekete Yoka akiwemo ndani yake. Wale askari wakaendelea kuwapiga huku umati wa watu wakishuhudia jambo lile mpaka wawili wale walipokata roho, wakachukuliwa na kwenda kutupwa msituni kuwa chakula cha wanyama na wadudu waishio huko……. Na Huo ndio ukawa mwisho wa Sube, mke wake pamoja na Yoka, kuanzia hapo kijiji kikarudi kuwa na amani kama dhamani na wawili wale wakabaki kuwa kama stori hapo kijijini.

USIKOSE SEHEMU IJAYO

Ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi Share App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)