NYOKA WA KUTUMWA (9)

Zephiline F Ezekiel
0

SEHEMU YA TISA
ILIPOISHIA...
Mfalme kwa kuwa hakutaka mzee sube ajulikane akaona bora amdanganye mke wake japokuwa hakupenda kufanya hivyo.

KAMA SIMULIZI HII UNASOMEA NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI KUPATA VIPANDE VYOTE KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈

ENDELEA NAYO...
MFALME: Hapana hatujafanikiwa maana hatukuona kitu chochote kwahiyo sijui kama wanamsingizia au laa.

Mfalme aliongea huku akiwa na wasiwasi na kumfanya mke wake ahisi kitu Fulani.

MKE: Mh! Ila kutokana na unavyoongea naoka kama sio kweli unavyonimbia .

MFALME: Kwanini unasema hivyo mke.

MKE: Nakuona jinsi unavyoongea una wasiwasi sana .

MFALME: Hapana mbona nipo kawaida, na wala sijakudanganya.

MKE: Sawa ila naomba uniambie kwanini tangu umerudi umekuwa mtu wa mawazo wala hauna furaha kuna kitu gani kimekukwaza huko utokako.

Mfalme baada ya kuulizwa vile, akamtazama mke wake na kuamua kumwambia ukweli wa kile kilichotokea.

MFALME: Mke wangu kwanza naomba unisamehe kwa kutokukuambia kweli kuhusu kule nitokako. Ila jambo ambalo walikuja kilisema wale vijina kuhusu mzee sube ni kwel kabisa tena nimeshuhudia kwa macho yangu mwenyewe, na nimegundua kitu kumbe mzee Sube ndie mwenye yule nyoka.

Mke wa mfalme alishangaa sana kusikia vile maana na yeye alitokea kumuamini mzee sube kama alivyokuwa akiaminiwa na mume wake.

MKE: Eeeeeee ! Mume wangu kwahiyo unataka kuniambia kumwamini kote kule kumbe ni mbaya kias hiko. Sasa baada ya kuona hivyo umechukua huamuzi gani.

MFALME: hapa kichwa chote kinawaka moto maana hata sijui cha kufanya kwa mzee yule. Alafu kitu kingine, jambo hili nataka iwe siri yangu mimi na wewe tu maana watu wengene wakisikia wanaweza kudhania kuwa mimi na mzee sube tulikuwa tunashilikiana kufanya jambo hili kutokana na kuwa karibu nae.

MKE: wewe unataka iwe siri wakati wale vijana na wao wamemuona huyu mzee sube.

MFALME: Hapana hawakumuona walikuwa wamelala.

MKE: Sawa ila mume wangu mzee sube inabidi ahukumiwe kama watu wengine wanavyofanya kitu kibaya hapa kijijni kwetu.

MFALME: sawa ila kabla sijafanya hivyo ninataka nimuite ili nimuonye endapo atarudia au ataendelea kufanya vile nitamuhukumu.

MKE: Mh! mume wangu bado unataka kumtetea mzee sube ila basi kwa kuwa wewe ndio mfalme fanya utakalo.

Waliendelea kuongelea jambo lile na mwishoe wakaachana nalo huku mke akimshangaa mfalme kwanini amekuwa akimtetea Sube kiasi kile. Kwa upande wa wale vijana walishtuka sana baada ya kuamku maana hawakutegemea kuona mfalme ameondoka mahara pale bila kuongea na wao, hofu ilitawala kwao, kila mmoja alimuuliza mwenzake nini ameona ule usiku lakini hakuna jibu liliopatikana maana wote walikuwa wamelala fofofo. Wote kwa pamoja wakaanza kupanga mipango jinsi gani wafanye ili mfalme asiwape adhabu ya kifo maana walikuwa awajui, nini mfalme ameona mwishowe wakapanga kwenda kumuomba msamaha endapo atakataa basi watakuwa tayari kupokea adhabu hiyo.

Wakiwa wanaendelea kuongea ghafla wakasikia mlango wa ile nyumba ukigongwa kuashiria kuna mtu anataka kuingia humo, mapigo ya mioyo yao yakaanza kwenda mbio maana walihisi wamekuja kuchukuliwa na askari wa mfalme ili wakapewe adhabu yao. Japokuwa walikuwa wanaogopa lakini hawakuwa na jinsi mmoja wao akanyanyuka kwenda kufungua mlango na kukutana na kijana mwenzao anaeshughulika kule kwa mfalme, haraka akaingia ndani. Akasalimiana na wenzake kisha akaanza kuwaeleza nini kimempeleka mahara pale.

KIJANA: Nimeagizwa na mtukufu mfalme nije kuwapa taarifa anawahitaji majira ya mchana mfike nyumbani kwake.

Taarifa ile ilizidi kuwatisha na kujua kuwa mda wao wa kuishi hapa duniani umefika tamani, Yule mtoa taarifa alipomaliza akaondoka zake na kuwaacha wenzake wakiwa wamejiinamia. Waliendelea kukaa mle ndani kila mmoja akiwa na mawazo yake na hatimae mda walioambiwa waende kwa mfalme ukawadia, wakatoka kwenye ile nyumba na kuanza safiri ya kuelekea huko, Kwa kuwa ni vija walitembea kwa mwendo wa kijeshi { haraka } mda mfupi mbele wakafanikiwa kufika huko, na kamkuta mfalme akiwa amekaa pamoja na mke wake, wakawasalimia na kusubilia kuambiwa walichoitiwa, ndipo mfale akaanza kuongea.

MFALME: Nimewaita hapa ninataka mniambie nani kati yenu ameona kitu kwa mzee sube, maana nyie mlisema yeye ndie msababishaji wa mambo yote.

Wale vijana baada ya kuulizwa vile, walijikuta viungo vya miili yao vikifa nguvu na kulegea maana moja kwa moja wakagundua kuwa mfalme na yeye hakubahatika kuona kitu chochote kwa Sube, kumbe Mfalme aliwauliza vile kama kuwatega ili aone kama kuna ambae alikuwa ameona kile alichokiona yeye kwa mzee sube. Wale vijana walikaa kimya na kuinamisha vichwa vyao chini kuashiria hakuna kitu walichokiona, Mfalme alipoona vile akaona bora awaambie ukweli kile alichokuwa amekioa yeye japokuwa alihitaji afanye siri.

MFALME: Najua hakuna hata mmoja ambae ameona kitu kwa kuwa mlilala, ila mimi nilifanikiwa kuona kila kitu kwa mzee sube na sasa naamini yale maneno ambayo nyie muliniambia.

Vijana hawakuamini kile walichokisikia haraka waliinua vichwa vyao na kumtazama mfalme huku furaha ikitawara nafsini mwao na kufukuza huzuni, walipongezana kwa kazi mzuri walioifanya lakini mwisho wakahitaji kufahamu nini mfalme atafanya kwa mzee sube.

KIJANA 1: Tunashukuru sana mtukufu mfalme kama umeliona jambo hili maana sisi tulikuwa na wasiwasi tulidhani na wewe haukuona kitu chochote. Ila tunahitaji kujua kitu gani umepanga kumfanyia mzee Sube.

Baada ya kuulizwa vile akaa kimya kwa sababu yeye hakutaka kufanya kama wao walivyokuwa wakidhania atafanya kwa yule mzee, lakini mwisho akaona bora awaambie ukweli jinsi yeye alivyopanga kufanya kwa Sube. Lakini mda huo Sube na mke wake walikuwa awajui chochote kuwa tayari wamefahamika wao ndio wabaya wa kile kijiji bali waliendelea kufanya shughuli yao ya kutibu watu walioumwa na yule nyoka.

MFALME: Mimi sina lengo la kumpa adhabu mzee sube kwa kuwa hii ni mara yake ya kwanza kokosea hapa kijijni. Kwahyo nataka nimuite ili nimuonye na endapo ataendelea kufanya hivi hapo nitampa adhabu.

Jibu la mfalme liliwashangaza sana wale vijana maana wao walijua kama mfalme ameshajua ukweli kilichobaki ni hukumu kwa mzee sube. Lakini vijana hawakukata tama wakaendelea kumuuliza maswali kutokana na uamuzi aliouchukua.

KIJANA 2: Lakini mfalme sheria ya hiki kijiji chetu inasema mtu akifanya jambo la kuhatarisha maisha ya wenzake kwa makusudi anatakiwa kupewa hukumu ya kifo mbele ya wanakijiji. Sasa inakuaje mzee sube unataka kumuonya na wakati yeye inatakiwa ahukumiwe kifo.

MFALME: Ni kwel kijina unachosema ila kwa hili ninaomba mnisamehe maana siwezi kumuhukumu haraka hivi kwa kuwa kwa sasa najua ana mambo mengi hapa kijijini pia amekua akitoa mawazo na ushauri mzuri kwangu jinsi ya kuongoza hiki kijiji. Kwahiyo endapo nitachukua uamuzi wa kumuua nitakuwa nimempoteza mtu muhimu kwangu.

Jibu la mfalme liliwaacha vijana mdomo wazi na kuhisi kitu Fulani kutoka kwake, maana kosa alilolifanya sube hakutakiwa kutetewa na mtu yoyote yule. Kwa kuwa mfalme ameshaamua kufanya hivyo wale vijana ikabidi wakubari kuwa wapole japokuwa waliumia kupita kiasi. Lakini kabla awajaondoka kijana mwingine akauliza swali.

KIJANA 2: Mtukufu mfalme hivi mtu muhimu anaweza kufanya jambo baya na hatari kama hili, hivi unajua nia ya yeye kufanya hivi, inakuaje kama alikuwa anahitaji kukuangamiza wewe. { Kijana aliongea hivyo ili kumjengea chuki mfalme lakini mfalme hakujali }

MFALME: Hayo unayoniuliza ni sahihi ila jua kuwa na yule ni binadamu kuna siku anakuwa anapitiwa na shetani na kujikuta akifanya vitu kama vile. Kwahiyo ni wajibu wetu kumrudisha mzee sube kutoka kwa shetani.

Maneno ya mfalme yalimchukiza sana mke wake pamoja na wale vijana, ndipo mke akadakia na kuanza kuongea maneno ya kumshangaa kwanini anafanya vile.

MKE: Hivi mume wangu kwani huyo mzee sube amekufanyia kitu gani kizuri mpaka umtete kiasi hiko kama washauri si utampata wingine mbona wazee wamejaa hapa Mbaka. Mara ngapi umewahukumu watu ambao ilikuwa ni mara yao ya kwanza kukosea au ndio unataka kubadilisha sheria. Ila kumbuka ulimuhukumu mke wako uliempenda sana pamoja na mkwe wako kwa kosa ambalo lilikuwa la kwanza wao kulifanya hapa kijijini au wale hawakuwa na umuhimu kwako na kwa hiki kijiji. Amka mume wangu huyu mtu unaemtetea leo ni zaidi ya Shetani kwa hiki kitendo alichokifanya kwetu sisi pamoja na hiki kijiji chetu cha mbaka.

Baada ya kusemaa vile kwa asira akaainuka na kuingia ndani na kuwaacha wale vijana wakiendelea kusubilia, Japokuwa maneno ya mke yalikuwa makali lakini hayakuweza kubadilisha msimamo wa mfalme, jambo ambalo lilizidi kuwachukiza wale vijana. walipomaliza kuongea wakaruhusiwa warudi majumbani kwao huku wakiwa wamepewa onyo endapo baya lolote litamkuta mzee Sube hukumu itakuwa juu yao, vijana wakaondoka huku wakisononeka.

Baada ya kupita dakika kadhaa Mfalme akachukua walinzi wawili na kwenda nao nyumbani kwa sube na kumkuta akitengeneza dawa, sube akafurahi sana alipoona ametembelewa na Mfalme akamkaribisha vizuri kama sio yeye anaefanya mabaya, akaenda ndani kumuita mke wake, mda huo alikuwa ajui lolote bali alijua mfalme ameenda kumtembelea tu. Wakasalimiana nae ndipo Mfalme akamuomba Sube wasoge pembeni ili waonge kidogo, bila uwoga sube akasogea na kumuacha mke wake akiwa pamoja na wale walinzi, ndipo maongezi yakaanza.

MFALME: Mzee sube nimekuja hapa kwa ajili ya jambo moja ambalo limenisikitsha sana baada ya kufahamu ukweli wake.

Sube alipooambiwa vile hakuogopa maana alijua hilo jambo litakuwa linamuhusu mzee Bugu kwa kuwa yeye ndie alizaniwa kufanya mambo mabaya.

MZEE SUBE: mmmmh !!!. Jambo gani hilo mtukufu mfalme. { Aliuliza bila uwoga }

Sube alipouliza hivyo, Mfalme akaa kimya kwa huku akimtazama na kujiuliza wapi aanze kumwambia, mwishoe akaamua kuongea

MFALME: Kuhusu nyoka anaesumbua hapa kijijni.

MZEE SUBE: Ehe niambie umegundua ukweli gani kuhusu huyo nyoka. { alijifanya kuongea kwa mshangao mkubwa }

MFALME: Sube usijifanye kushangaa wakati wewe ndie muhusika wa jambo hili.

Mlipuko mkubwa mithiri ya bomu la nyukilia ulitokea kwenye moyo wa Mzee sube na kuanza kutetemeka maana hakutegemea kusikia kile alichoambiwa na mfalme, lakini akajitahidi kujikaza na kuendelea kuongea.

MZEE SUBE: Sijakuelewa mtukufu mfalme.

MFALME: Lazima usinielewe kwa kuwa ukweli umejulikana, sasa nataka uniambie yule Nyoka ulieniambia anaitwa Ruka wa nani. { Mfalme aliongea kwa hasira }

USIKOSE SEHEMU IJAYO

Ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi Share App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)