SEHEMU YA KUMI NA TATU
Nikajikuta nabadirika na kuwa kiumbe cha ajabu sana hata
yule mtoto akanihofia maana sikuwa mimi tena nikamzoa yule jamaa na kummeza kabisa ndugu msomaji ombea iwe story kwako au iwe kama unacheki muvi tu maana hali ikawa tete katika jiji la dar es salaam
SASA ENDELEA...
Watu wakabaki kukimbizana kila mmoja akiitaji kuiyokoa nafsi yake nikawa nafinya kila ninae mpata na kummeza roho ya kinyama iliyo niteka
nikasababisha maafa makubwa kabisa
police wakafika
kuja kupambana nami
nikawa nawapulizia upepo tu na kujikuta wakirushwa huku na kule pamoja na magari yao kikosi cha fanya fujo uwone
nao wakafika cheki upumbavu wao sijui walijuwa mimaji yao ya washa washa au mabomu ya machozi yata nituliza kumbe wamenia jeshi likaitwa na kuanza kunivurumishia makombora nikawa nayarudisha kwao
damu ikazidi kumwagika huku kila maeneo miili ya watu ikiwa imetapakaa nikiwa katika kuangamiza watu wasio kuwa na hatia gafla mbele yangu akatokea mdogo
wangu
Hafidhi j ikram na huku akilia nikabaki kumtizama tu akaniambia “kaka nakuhitaji uje viwanja vya jangwani akapotea kitendo cha yeye kupotea na mimi nikapotea nikatokea jangwani ndio ni mdogo wangu sasa swali la kujiuliza amekujaje huku
wakati yupo kifungoni katika gereza linalo milikiwa
na Nipe nikupe
hakutaka kupoteza muda alipo niona tu akasema ya kwamba
“kaka nilikutegemea sana ya kwamba utafanya haraka kuniokoa katika kifungo cha mateso huko nilipo nateseka sana mpaka natamani kufa kaka kumbuka damu nzito kuliko maji inakuwaje husikii wala kujali jinsi ndugu yako ninavyo umia umepewa kazi ya kuja kupambana na
Nipe nikupe matokeo yake umemkimbia kule kilwa umekuja huku kucheza na wanaadamu kwa taarifa tu kaka yangu
Nipe nikupe anajisifia usiku na mchana kuwa yeye noma hakuna anae muweza
kama kweli
kaka unanipenda
basi rudi kilwa ukamuangamize huyo fisadi
Nipe nikupe kazidi kuwapoteza watu kila uchwao,
kusema kweli maneno ya mdogo wangu yali nichoma sana hakutaka kusubili nitasema nini zaidi ya yeye kuondoka zake nikapiga mahesabu na kuapa usiku huu huu nitavamia kilwa nikajigeuza mtu wa kawaida tu na kuanza kukata mitaa ya jangwani nikaja kutokea kwenye jengo la clabu ya yanga nikakodi bajaji na kumuomba dereva anipeleke kinondoni mkwajuni tukiwa njiani yule dereva akaanza kusema “duhuu yani siamini, nikamuuliza huamini nini kaka?"
“kwani wewe hujasikia kilicho tokea leo k/koo?"
“hapana sijasikia
“kweli ndugu yangu umechelewa ukisikia mwisho wa dunia ndio huu basi uamini tu ndio huu maana kilicho tokea leo ni balaa sijui jini au shetani kashuka toka mbinguni kaja kuwaonyesha wanaadamu ya kwamba wao si chochote si lolote marofa tu akawasha moto viafande na vibastora vyao vya kitoto mbona walisanda hicho kiumbe hakishikiki yani
kikafanya umafia
wa kinyama kisha akapotea,
"ehee ikawaje baada kupotea?"
“inavyo semekana kuna kitoto cha ajabu wamekinasa maeneo yale kina minjino mireefu mpaka sasa sijui wame kipeleka wapi?"
nikastuka kusikia kuna kitoto cha ajabu eti wamekinasa maeneo yale nikajuwa bila shaka atakuwa yule mtoto niliye kutana nae kwenye daladala mpaka sasa sikuweza kufahamu katokea wapi zaidi ya kufahamu ni mzimu mwenzangu ila yeye hana nguvu kiviile kama mimi, basi tukafika kinondoni nikashuka
nikamlipa dereva na
kwenda zangu nyumbani
kwa wazazi maana nime waacha tokea jana usiku
baada kufika maeneo yale nikajivika kivuli nisiweze kuonekana
nikaingia ndani nikakuta kuna furaha ya ajabu baina ya mama na baba wanacheza cheza na kukimbizana huku na kule
mara wapo jikoni mara sebreni,
baba akauliza swali
“kwahiyo mke wangu shart la
kwanza nishalifanya nimerudi kazini leo hii je hilo shart lingine unataka litendeke lini?"
mama akamtizama baba akiwa aamini kile akisikiacho,
nikafahamu nisipo fanya kitu hapa mambo yanaweza kualibika sasa hivi nikaenda kumuingia mama ndani ya mwili wake akatamka “vizuri sana mume wangu
naitaji hili zoezi lifanyike kesho hasubuhi,
“sawa mke wangu hakuna neno tutatoka hapa leo hii usiku tukiwa na Jeep ya jeshi nitachukua vijana wangu
kazaa na kwenda kuifanya kazi hiyo,
“sawa mume wangu wakakumbatiana na kuanza kutekenyana mi nikatoka na kuitaji kuiyandaa safari ya kurudi kilwa nikapanga kabra sijaondoka nifanye ishu ya kwenda kumtoa yule mtoto mikononi mwa mapolice nikacheki kwenye kiganja cha mkono wangu na kuona jinsi alivyo jikunyata mpaka anatia uruma dahaa
nikamwita “wee figisu!!!figisu!!!
akayatoa macho pima,!
Nikamwita “wee figisu!!!figisu!!!
akayatoa macho pima huku akishangaa shangaa kwa kugeuka ni wapi sauti hii inatokea,
nikabaki kucheka tu,
mida hiyo mpaka usiku kama saa mbili hivi wazazi bado wapo ndani wakilicheza sebene tu
nikaitaji kujiandaa kwa safari nikaizunguka kwanza nyumba na kuikagua kama iko salama au vipi nikanyoosha mkono wa kushoto juu nikajikuta naenda angani nikapaa moja kwa moja mpaka gereza la ukonga sikuta shida kufahamu
ya kwamba figisu kaifaziwa sero ipi nikam beba na kusepa nae nikamkumbuka yule konda ili nisiweze kumuacha kwenye mateso bila shaka atakuwa kajifunza kitu nikaenda hadi kituo cha police msimbazi na kuingia kwenye sero aliyo
fungiwa
nikamkuta kalala nikamshika kwa kumuamsha akastuka
sana akabaki kufikicha macho asiamini kile akionacho mbele yake
nikamuuliza
“je unanikumbuka?"
akatikisa
kichwa kuashilia ya kwamba hanikumbuki, nikamshika begani huku nikitabasamu na kumfahamisha ya kwamba “mimi ni mmoja kati ya abilia walio panda daladala uliyo kuwa ukisanya wewe ukafika muda wa wewe kukusanya nauli na ulipo
fika kwangu mimi sikuwa na pesa nilivyo jaribu kukwambia brother sina pesa ukanitukana kwa kuniita mimi ni mtoto wa malaya na kusema unaenda nyuma kudai nauli ukirudi kwangu uikute pesa yako
nilicho fanya mimi ni kuzibeba pesa zote
basi hii itakuwa fundisho kwako sio kila umuonae ni binaadamu wa kawaida
wengine ni mizimu sasa basi mimi naondoka
ila kesho hasubuhi atakuja mkeo na mwanao kukuangali
na boss wako ataitaji kukufunga
cha kukusaidia mpatie hii mkeo kuna kitu nikampatia konda yule
akawa anaogopa kupokea
maana katika maisha harisi kuongea na mzimu si jambo la kawaida “pokeaaa!!! kwa sauti ya ukali nikamwambia hivyo
huku mikono ikimtetemeka akaipokea baada kuona tayali
kashaipokea
nami sikuwa na cha ziada tena zaidi ya kusepa tu
kama msaada nishampa nikatoka zangu nnje ya kituo kile na kumkuta figisu amekaa akinisubilia
nina mengi maswali juu yake niweze kufahamu wapi
ametokea familia yake ipo wapi?"
kwa jinsi anavyo tia huruma nikajikuta namwambia “sina haja ya kujua wala kufahamu matatizo yako kuanzia leo nakuahidi nitakulinda
mimi ndio baba yako au kaka yako napenda uwe na furaha,
Figisu akatabasamu na kumwambia twenzetu,
safari ikaanza kwa kukata mawingu usiku ule usiku wenye kila dhoruba uko angani tuliweza kuyaona
mengi tu wachawi wakiwa katika kupiga misele yao huku vibwengo wakipiga rada kwenye uso huu wa dunia,
safari yetu ilikuwa ni ndefu sana ila yenye furaha njia nzima tukawa tukipiga
story za hapa na pale mpaka tukaingia kilwa kivinje yapata majira ya saa nane usiku tukatua hapo maana
tulikuta timbwili timbwili si laki toto baina ya wachawi na waganga wa mji huo ilikuwa ni vita tupu nikamshika kichwa Figisu na kumpa full mauwezo sasa ngoma inogire,
tukawa tumeshika mijeredi ya moto
na kuanza kuwachapa nayo basi wakawa wanapiga makelele huku wasiweze kuona wanaazibiwa na
nani Figisu kwa kutaka sifa anawachapa mijeredi ya matakoni baada kuona hali
imezidi kuwa tete kwao
wakaanza kukimbizana
waganga wakashukuru kwa kuweza kupata msaada
maana walikuwa
washazidiwa tukafika Kiwawa na kumuonyeshea Figisu nyumba ambayo nilikuwa naishi tukaingia ndani na kupakuta pako vile vile kama nilivyo paacha,
hakuna aliye weza kushangaa au kujiuliza baada kuniona mimi nikiwa nimerudi pale wakati mimi nahisabia tokea niondoke hapa kwenda town
ni siku ya pili sasa kumbe
wenzangu wanajuwa miezi miwili maana Azizi aliniambia “kamanda tokea uondoke kwenda town miezi miwili sasa ndugu,
nikataka kum bishia sio miezi miwili ni siku mbili nikasita kufanya hivyo tusije tukaanza kubishana bure,
nikamcheki
Figisu akiwa anacheza na watoto wa pale kijijini
kuna maneno
nikayatamka
kumwambia figisu
japo kimoyo moyo hata
Azizi aliyoko mbele yangu hakusikia wakati
Figisu yuko atua akasikia
na kuitia sawa mkuu
nilimwambia ya kwamba
Figisu mwanangu cheza nao vizuri hao watoto usiwaogopeshe kwa hali yeyote ile,
Azizi
akaendelea kuniambia ya kwamba
“hivi kaka unamkumbuka yule msichana ambaye kuna siku
tulikuwa tumekaa pale kijiweni akaja na kukuomba ukamtwishe gogo?"
“ndio namkumbuka,
“basi yule demu
juzi tu kaenda mjini kitendo cha kurudi tu jana leo hii amekutwa kitandani amekauka,
“ame kauka ndio nini ndugu?"
“yani amekufa!!!
nikastuka kusikia vile na kumuuliza
“msiba upo wapi kwa sasa?"
“upo nyumbani kwao, nikamshika mkono na kumuomba twende tukatoka haraka haraka mpaka nyumbani kwao yule na kukuta kina mama wakilia nikaenda kukaa kwenye jamvi mimi na Azizi tukawa tukiona pilika pilika za watu wengine kuzimia baada kuzidiwa kwa uchungu wa kifo cha yule binti sikumbuki hata jina lake
Azizi akaniambia ya kwamba inavyo semekana binti amevunja mira za kijiji kwahiyo nipe nikupe kashafanya yake
katika kutupa tupa macho yangu nikaweza
kumuona yule binti akiwa kapiga magoti afu mbele yake kuna kiumbe anakiomba msamaha kucheki vizuri kile kiumbe ni Nipe nikupe nikaitaji kwenda kuwasha moto ila nikajiuliza nitaanzaje anzaje kufanya hivyo kwakuwa Azizi pekee ndio yupo karibu yangu akiongea na mimi nilicho fanya ni kumshika mshipa wa fahamu haraka sana
akaniegemea na kuanza kukoroma kwa usingizi nikamlaza kwenye jamvi kisha nikaenda hadi pale yule msichana alipokuwa kapiga magoti nikamnyanyua
Nipe nikupe akastuka kwa kitendo kile nilicho kifanya nikaanza kumchimba biti sasa
“wewe ni kiumbe mdogo sana katika uso huu wa dunia ila una jina kubwa sana kila kiumbe kina kutaja wewe
Nipe nikupe sasa basi
hilo jina lako ni kama sisimizi kwangu nakufinya tu nimeondoka kwenda mjini juzi ukaanza kujisifu nimekukimbia wewe kwa kipi hasa ulicho nacho mpaka nikukimbie
sasa nimekuja kuwasha moto naanza na kumrudisha huyu binti duniani tena mbele ya macho yako,!!!
“Ha!ha!ha!ha! ni kicheko cha kifedhur alicho kitoa nipe nikupe na kusema “Kijana acha kujidanganya huwezi kupambana na mimi hata kidogo hao walio kutuma jiulize kwa nini hawakuja wenyewe kuifanya hiyo kazi walijaribu wakashindwa umesema mimi ni sawa na sisimizi ndio sikatai ila wewe ni kiroboto tu huwezi kufanya chochote juu yangu kama unaweza basi nakualika leo usiku saa nane katika uwanja wa shule tuonyeshane kazi!!!"
KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU