TUPEANE (15)

0

JINA: TUPEANE
Mwandishi: Hafidhi J Ikram

SEHEMU YA KUMI NA TANO
Tukiwa bado tunakodoa macho tusijuwe cha kufanya nikaweza kuiyona gari aina ya Jeep ikija pande zile baada kufika ikasimama akashuka baba na vijana kama wanne hivi wote wakiwa ndani ya combati za kijeshi na kuangaza angaza macho tu

SASA ENDELEA...
“hivi hii vua imenyesha huku tu kiwawa mbona kule kivinje na mavuji juwa linawaka kali tu?"
ni maneno ya baba akiuliza hivyo basi kuna dada mmoja akamjibu ya kwamba
“hata sisi wenyewe tuna shangaa hiki kijiji kimejaa mauza uza tu
yani tunaabudu mizimu kwetu ndio kila kitu!!!
“ilo ndio tatizo kubwa baada ya kumtegemea Mwenyezi Mungu nyie mna abudu mizimu pumbavu zenu!!!
baada baba kusema vile wakapanda kwenye gari na kuondoka zao
Figisu akaniambia hivi
“baba hakika ya shetani ana nguvu sana basi siku moja katika pita pita zangu kule mjini nikatokea sehemu moja kuna kanisa kubwa
sema ilikuwa usiku sana nikaweza kusikia mazungumzo kati ya shetani na mchungaji akipewa mashart ya kwamba afanye kila namna namna,
mambo yao yaende sawa yule shetani akatamka

“kwa hiyo nataka kusema kuwa, kuanzia sasa lazima tukaze nguvu zetu ili kuzidisha uasi katika hii dunia naitaji uikamilishe hii kazi haraka iwezekanavyo kusema kweli sauti yake ilikuwa ni kali sana yenye kutisha basi yule mchungaji akaitikia, sawa?”
“Sawa,” kumbe hakuwa mmoja nikajaribu kuchungulia na kuuwona umati mkubwa tu wote wakiwa ndani ya vazi la kaniki nyeusi kichwani wamejifunga vitambaa vya rangi nyekundu huku mkuu wao akiwa amekaa madhabuni akaendelea kusema ya kwamba, “wote.
nataka kuona dunia inachafuka.”“Sawa.”
“nataka kuona binadamu wanaishi kwa wasiwasi, sawa?”
“Sawa.”
“nataka kuona watu hawafanikiwi katika maisha yao,sawa?”
“Sawa.”
“pia, nataka kuona binadamu wanatutegemea sisi kwa kila jambo. Ikitokea tatizo kidogo waende kwa waganga, sawa?”
“Sawa.”
hilo wote itabidi mlisimamie kikamilifu ili mambo yaende tunavyopanga. kwani majira yaliyotajwa yamekaribia sana.”binafsi nilijiuliza mengi sana pasipo kupata jibu ni majira gani hayo yaliyo tajwa na nikitu gani
wanacho kikosa wanaadamu hawa mpaka wanaamua kumtumikia shetani huku wakijivika ngozi ya utumishi wa Mungu ole wao wafike kuzimu
ndio watajuta na kutamani walau wapewe sec moja tu ya kurudi duniani na kutubu dhambi zao
baada
Figisu kusema vile akanyamaza, nikamuuliza hivi
Figisu ni njia gani uliyo tumia kumpasua yule jamaa?"
“vipi kwani unataka nikuonyeshe?"
nikamjibu ndio,"
basi akaenda mbaali kidogo kisha akajistua na kuja kwa speed akazama tumboni mwangu nikahisi anazichezea bandama zangu mara figo
maumivu makali yaka nishika nikajikuta namwita “Figisu!!!figisu!!!
toka bana!!! maumivu yakanizidia na kujikuta nikipoteza fahamu,

nikaja kuzinduka na kujikuta nipo kitandani nikaitaji kujinyanyua lakini nikashindwa maana nilikuwa mzito sana dahaa nikajiuliza kwani nina nini mie mpaka siwezi kunyanyuka kitandani
Figisu nae yuko wapi?"
“naona umerudiwa na fahamu mtukutu ehee!!!
nikamtizama aliye niambia vile ni bibi akaiwa kam beba paka mweusi akaja mpaka pale kitandani na kuniambia ya kwamba muda mwingine acha michezo ya kipumbavu sasa basi umeweza kumuuwa mwanao mwenyewe,
nikastuka na kuuliza “bibi what?
“hakuna cha nati wala chapati ninacho taka kukwambia ni hivi
Figisu hatunae tena duniani,
“bibi unasema?"
“sikia nikwambie mjukuu wangu Hafidhi wakati mnacheza pale mpaka
Figisu kuingia mwilini kwako ni kwamba alishindwa kutoka kwa sababu seri ya mwili wako wewe ni tofauti
na kiumbe chochote kile sasa basi hakuona njia matokeo yake akakosa pumzi na kupoteza maisha
na mpaka mwili wake upo tumboni mwako kwahiyo unacho takiwa kufanya kwa sasa ni kummeza huyu paka aende kuutoa mwili wa marehemu sikuwa na jinsi zaidi ya kufanya hivyo huku mchozi ukinitoka baada ya mwili wa
Figisu kutolewa dahaa akiwa kaungua vibaya sana

Baada mwili wa marehemu
Figisu kutolewa ndani ya mwili wangu ukiwa ume unguwa vibaya sana mpaka hautamaniki kwa mjeraha aliyo yapata
nilikumbuka mengi sana tuliyo yapitia mimi na
Figisu kwenye huzuni na furaha leo hii kwa sababu ya uzembe wangu tu nimemuuwa nikamuuliza bibi
“hivi bibi huwezi kumrudisha tena
Figisu duniani?" akanijibu ya kwamba
“kwa hilo haito wezekana hata kidogo cha umuhimu ujiandae kwa kazi iliyo mbele yako mwanao kashafariki basi,"
“bibi kwa nini unasema Figisu ni mwanangu?"
“khaa! kumbe ulikuwa ufahamu ya kwamba huyu Figisu ni mwanao wa kumzaa kabisa
basi nikwambie ile siku uliyo fanya mapenzi na wale wasichana wa kibinaadamu ndio siku uliyo wabebesha mimba bila wao kujuwa ila taarifa zikafika kuzimu ya kwamba kuna ujio mpya kutoka duniani
siku ya siku ikafika kwa wale mabinti kujifungua kila mmoja kwa wakati wake
akatokwa na damu ya hedhi mibonde mibonde ya damu mpaka mzazi wake akahofia kwa kuona binti yake yupo kwenye majanga ya kupoteza maisha wakati mganga hajafika sisi tukatuma kikundi chetu na kwenda kuwachukuwa watoto wale wakiwa mia mbili kamili,
nikabaki kuduwaa tu na kujiuliza inakuwaje nipate watoto mia mbili kwa mabinti wawili
Bibi akaendelea kusema najuwa unashangaa na kujiuliza umepataje wato mia mbili basi ni
hivi kwa kawaida binaadamu akizaa mtoto mmoja jini au mzimu anazaa watoto mia moja na akifa mtoto mmoja wa kibinaadamu huku wanakufa watoto mia moja wa kijini habari ndio hiyo,

“kwa hiyo bibi watoto wangu mia moja tayari washakufa au?"
“hapana hawajafa aliye kufa ni huyu
Figisu tu basi kingine ninacho itaji kukwambia jitahidi kupambana uitete dunia pamoja na wana damu maana shetani anaitaji kuikamilisha nuru yake kwa kuuteka ulimwengu pambana
maana dunia kwa sasa imejaa imani za kishilikina si kwa wazee vijana wala watoto wote wanapotea
vitu kama hivi vipo sana katika miji iliyo jazana watu
maana
wachawi wanaamini ya kwamba, katika sayari hii kuonekana kwa
vitu visivyoonekana pia vilikuwa
na siku sita mawazo yao katika uumbaji wa Mwenyezi
Mungu, siku ya saba kwa ujinga wao wanazani heti
akapumzika. na hiyo ndiyo sera
ya mchawi mara tu baada ya
kujiunga katika kazi hiyo iliyo laaniwa mpaka siku ya kufa kwake binaadamu
wengi katika
ulimwenguni kote.
Kabla sijaondoka maana kuzimu wana ungojea mwili wa marehemu Figisu
nataka kusema kuwa, kama
kuna shughuli mbalimbali za
binadamu zinazoonekana kwa
macho ya kawaida duniani, pia
kuna shughuli kama hizo hizo
zisizoonekana kwa macho ya kibinaamu ya
kawaida, lakini zinashirikisha
wachawi na na mizimu mashetani yani viumbe vibaya vibaya mambo yao.
Wachawi wana kila kitu, wana
mikutano ya nchi, mikutano ya
kimataifa, ya kanda ya mabara
na pia wana mabenki,
japokuwa kwa macho
tunazungumzia mabenki ya
pesa, wao wana mabenki ya damu, nyama yani ukipata bahati ya kuingia kwenye hizo bank zao mwili uta kusisimka kwa uwoga wa ajabu maana kunatisha
kienyeji.dawa za kienyeji pia
huwa wanakopeshana,
wanalipana na wapo wasiotaka
kulipa ambapo huchukuliwa
adhabu mbalimbali kulingana
na makosa. zipo nchi ambazo
wachawi wake wanafukuzwa
katika uanachama, zipo
zinazoingizwa, wapo wakuu wa
wachawi wa nchi
wanaopinduliwa wengine hata
kuuawa na pia kunakuwa na
uchaguzi mkuu kila baada ya
miaka mitano kuchagua
viongozi wa kichawi wa nchi
husika ambapo wapiga kura
huandikisha majina yao na
kuwa na vitambulisho vya
kupigia kura.
pia kuna wana bendera zao pia
wachawi barani Afrika, Ulaya na
duniani kote. Aidha, kila nchi ina
bendera yake inayoonesha
utambulisho wa kitaifa. mfano,
bendera ya kichawi ya kilwa
ni rangi nyekundu, nyeusi na
kahawia, katikati ina picha ya
mnyama Nipe nikupe ndio mfalme wao
nchi ya nigeria, bendera yake ya
kichawi ina rangi nyekundu bila
mchanganyiko, katikati ina
picha ya mkono mweusi
umeshika kibuyu chenye
shanga.
kuna wachawi wanaofanya
biashara za kimataifa, mfano
kutoa dawa za kienyeji
kilwa kupeleka dodoma kwa
njia za kichawi na kule mchawi
anaweza kununua ngozi za
wanyama akaja kuuza kilwa au
kenya au uganda kwa wachawi
wengine ambao hawana mitaji
mikubwa.
naona muda una yoyoma nikwambie cha mwisho tu

ni kwamba bila shaka umewaona wazazi wako wakija hapa leo na ujio wao unajuwa nini lengo lao ninacho weza kukwambia ni kwamba
Nipe nikupe leo usiku huu ataenda kufukuwa kaburi na kuondoka na mwili wa mdogo wako sasa basi ni wakati wako wa kupambana na kwenda kulilinda lile kaburi usiku huu
maana ule mwili ukitolewa kuna uwezekano mkubwa wa mdogo wako kurudi tena duniani fanya hivyo,"
baada bibi kusema vile akapotea na kuniacha mimi na yule paka mweusi
kama mkaa mimacho inang'aa hiyo nikainua mdomo na kumuuliza “sasa wewe unangojea nini hapa si usepe tu,"
si akanijibu eti “mi siwezi kuondoka hapa nimeambiwa niwe mlinzi ndani ya nyumba hii,
nikacheka sana ha!ha!h!h!
yani wewe ulinde humu ndani kwanza unaitwa nani?"
“naitwa Ningu!!!
“oky Ningu je unaweza kunionyeshea mauwezo yako hata kidogo?"
“ndio naweza boss!
“haya anza kitendo bila kuchelewa akaanza kujibadirisha kila aina ya kiumbe hadi kunguni nikabaki kukodoa macho na kuogopa pale alipo jivika taswira ya
Nipe nikupe maana nikawa narudi nyuma huku nikijiandaa kumtupia kombora nae kwa uboya wake akaanza kunitisha eti “wee kijana unaitaji kupambana nami sasa nakuonya ile nataka kunyoosha mkono tu akawa
Figisu masikini mchozi ukanitoka huku akinipungia mkono mwisho akajirudi na kuwa paka vile vile na kuniambia boss
Hafidhi j ikram time ishafika panda mgongoni twenzetu vitani kwanza nikasita kupanda ila nilipo kumbuka mauwezo yake ya kujibadilisha nikajikuta napanda basi
Ningu akawa mkuubwa aina ya farasi mwenye mbawa na kupaa juu kupitia paa ya nyumba tukatoka nnje
akasema hii leo ndio mwisho wa Nipe nikupe kaka nikaangaza angaza macho na kuweza kupaona makaburini kukiwa na viumbe vikiranda randa
Ningu kama dragon vile akawasha moto kwa kuwatemea viumbe wale nami nikachumpa kutoka juu ya mgongo wa Ningu na kutuwa chini kitendo cha kutua tu upepo mkali ukavuma na miti kutingishika,,

Baada kutua chini basi upepo mkali ukavuma na miti kutingishika maana nilikuwa tayali nisha badirika na kuwa kiumbe mwingine kabisa yani kama mmbwa mwitu vile viumbe tulivyo vikuta pale makaburini vikawa viki jihami kwa kujaribu kutupa makombola yao
yakawa yakinigusa tu yana dunda na kuwarudia wao wenyewe na kujikuta waki tapatapa na kupiga mayowe ya maumivu tu
Ningu nae hakuwa nyuma katika kutoa mashambulizi yake
maana alikuwa hatari sana
kwa kuvi chakaza vile viumbe nikajisemea “ehee hapa nime pata jembe",
yapata takribani masaa mawili hivi tukiwa katika vita kali na wale viumbe wa kila aina maana akifa mmoja wana tokea wawili au wanne sasa ikawa kazi sio kuwa punguza bali kuwa ongeza tu miti inawaka moto katika uwanja wa machafuko usiku ule kumbuka ilikuwa ni vita ya mizimu tu

KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU


TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)