TUPEANE (18)

0

JINA: TUPEANE
Mwandishi: Hafidhi J Ikram

SEHEMU YA KUMI NA NANE
“Hilo lisikupe shida hata kidogo mama
awe mzimu au zombie yule bado ni mtoto wetu tu
hiki kijiji kina wachawi na ndio walio mchukuwa mwanetu kwa kumfanya msukure kwa bahati nzuri hakukatwa ulimi sie tukajuwa kafa na kwenda kuuzika mgomba dadeki"

SASA ENDELEA...
“Walio fanya kitendo hiko sio wachawi wala nini hayo ni mambo ya
Nipe nikupe tu, baada kusikia jina la
Nipe nikupe basi mwili uka nisisimka kwa uoga maana hiki kiumbe nakikumbuka vizuri nikazidi kusikiliza hasa bibi alivyo sema

mnajuwa yapata miaka miwili sasa tokea mwanenu Hafidhi j ikram afariki kama kumzika tushamzika na keshaoza huyu aliye kuja hapa sio yeye ni mzimu tu, kwa sauti yenye hasira na jazba baba akatamka
“wee mama heshima ni kitu cha bure yule ni mwanangu mimi na wala sio mzimu kwanza yuko wapi?"
mama akamjibu “ame toka kwenda mazoezini, “oky andaa mizigo turudi zetu mjini maana mama yako kashaanza kuleta mambo sio tusije kuonana wabaya bure au ndio mchawi mwenyewe nini?"
“wee mwana koma mchawi mzazi wako aliye kuzaa sio mimi pumbavu wee!!!
basi baba kwa hasira akamkunja bibi kwa kumkaba kiukweli hakuna aliye weza kumnasua bibi kwenye mikono ile ya kicommando nikaja haraka kufanya jambo japo sina ubavu nika shangaa namtoa mikono yake kama vile katoto kadogo
baba akaniambie kuanzia leo tambua ya kwamba bibi yako si mtu mzuri kwako ame kuweka ndondocha takribani miaka miwili sasa shika begi turudi zetu mjini hakuna kukanyaga tena katika kijiji hiki,

kauli ile ya baba ilikuwa so lias basi tukajiandaa haraka haraka na kuondoka kwenda stendi sikuweza kushangaa tena kwa kuona watu wakiulizana kila nilipo pita pale kijijini kutokana na kusikia yale
mazungumzo kati ya baba na bibi kumbe mimi ni mfu niliye kwisha kufa kitambo tu,
nilivyo fikilia ni jana tu kumbe ishapita miaka miwili sasa tokea nitokomee porini mawazo yaka nizidi nikiwa ndani ya bus mpaka usingizi ukanipitia na kujiona niko sehemu na kile
kiumbe kinacho dai ni kaka yangu akinipa mafunzo jinsi ya kupambana na watu wabaya mwisho akaniambia kupitia mimi tunaweza kumuangamiza
Nipe nikupe, nikaweza kuongea nae mambo mengi sana na kuniambia bila yeye mimi nisinge kuwa hai tena maana kafanya kazi nzito ya kupambana na
Nipe nikupe mwisho akasepa na kwenda kusiko julikana ila kupitia mimi ata patikana tu,

nikaja kustuka tushafika mbagala basi tukapanda DCM inayo kwenda mwenge kwakuwa ina pitia maeneo ya kinondoni nikaweza kushuhudia jinsi nyumba zilivyo bomoka bomoka maeneo ya jangwani mpaka mkwajuni huku mabondeni
“baba mbona nyumba ziko hivi maeneo haya?"
“dahaa mwanangu wee acha tu serikar hiyo!!!
serikar ime fanyaje tena?" ndio walio bomoa hizo nyumba, “kisa nini hasa mpaka wana bomoa nyumba za wananchi?" “inavyo semekana wapo maeneo ya hatari zaidi yani kuna uwezekano mkubwa wa kusombwa na maji pindi mto utakapo furika maji yani mafuriko,
“ahaa kumbe lakini si wame watafutia maeneo salama zaidi na kuwalipa gharama zao?"
“kusema kweli sijajuwa bado ila nilivyo sikia kuna baazi ya wananchi walilipwa na kupewa viwanja huko mwagwe pande cha ajabu baazi yao wakauza viwanja walivyo pewa na kurudi tena maeneo yale yale waliyo ambiwa wahame, “duhuu kumbe Kuna watu hamnazo kabisa ehee!!!
“ndio hivyo mwanangu ujinga wa watu wachache ina sababisha wengine wasilipwe kitu maana serikar ina hisi mambo ni yale yale,
“sasa kwahiyo nyumba yetu hivi ipo?"
mama akabaki kucheka tu na kusema “yani siamini mwanangu umekuwa na maswali kwa kuongea kama kagreta vile tokea tukiwa ndani ya daladala mpaka tunashuka maswali tu,
“unajuwa nini mama, “eheee niambie
“kipindi naondoka huku kila kitu kilikuwa shwali ila nimerudi mambo yapo hovyo hovyo kwahiyo lazima nimuulize baba anipe majibu,
“haya karibu nyumbani, ni mama huku akifungua geti la nyumba yetu
“mama hivi picha za marehemu kaka yangu unazo au?"
“mmh Hafidhi wewe unataka picha za mtukutu za nini?"
“nazitaka tu nimuone kaka yangu haya angalia ile kwanza ya ukutani naenda ndani kukuletea albaam yake,
kitendo cha kuinua kichwa changu na kuitizama ile picha nikastuka maana ni yule yule pindi ninapo lala hunijia ndotoni cha ajabu sijui maruwe ruwe au vipi nikaona kwenye picha ananicheka mimi kisha akatoka na kuja kunishika nikapiga zinga la ukeleleee
“mamaweeeeeeeee!!!

Zile kelele zimkafanya baba na mama watoke mbio kuja sebureni na kuuliza kunani tena, nikakosa jibu zaidi ya kukodoa macho tu kama vile fundi saa aliye poteza nati basi baba akanishika na kuniambia nikae chini kwanya kisha akasema “mama Hafidhi bila shaka mtoto atakuwa katika mazingira magumu sana tu sasa cha umuhimu kesho tuki jaaliwa uzima wa hafya baada kutoka swalati ljumaa tumpeleke kwa shekhe mirongo akapate daawa nahisi matatizo yote yatakwisha haya, “sawa mume wangu mi sina neno maana hali ya mtoto ndio kama uionavyo, “baba!!! “naamu mwanangu, “hivi kumbe mimi nimekufa?" lile swali liliwastua sana na kushindwa kujibu huku midomo ikiwacheza nikauliza tena kwa ukali zaidi, “naomba mnijibu je mimi nilikufa!!!?
“hapana mwanangu haukufa bali ulipotea tu katika mazingira ya utata, “baba niambie ukweli usi nifiche kitu chochote, “Hafidhi mwanangu ukweli gani unao utaka wewe?"
“mama naomba uondoke hapa niache mimi na baba tu! basi mama akanitupia ile albaam na kuondoka zake chumbani tukiwa tume baki wanaume watupu baba hakuwa na budi zaidi ya kunipa full story mwanzo mwisho nikabaki kuduwaa tu mpaka baba alipo maliza ile story kifua changu kikawa kimeloa chapa kwa machozi na kuhisi presha ina panda presha inashuka nikakumbatina na baba kumbe mama nae hakwenda ndani zaidi ya kusimama mlangoni tu akaja kujiunga nasi basi nikaenda kuoga nikala na kwenda kulala usiku huo hata kaka alipo nijia sikuweza kuogopa tena nikapiga nae story za hapa na pale akanichukua hadi coco beach na kuzidi kunipa mafunzo ya kupambana na kila kiumbe binafsi alikuwa ni mkali wa mapigo ya kila aina taikondo karate king boxer shaollin n.k nilijifunza mengi usiku huo hasubuhi kulipo kucha nipo kitandani basi nina maumivu kila maeneo kutokana na tizi la jana usiku nikaenda kupiga mswaki nikanywa chai “Assalam alaykum ya ibnaiya, ikiwa na maana ewe mwanangu basi nikaitikia “waaleykum ssalam yaa Abiiii basi nikatoka zangu nnje kwenda maskani kwa washkaji kufika tu kila aliye niona akatoka nduki mpaka kufikia wengine kujikwaa na kudondoka vibaya sana nikawa nishatambua kinacho wakimbiza nini nikaenda kukaa kwenye benchi huku nikishika tamaa nikastuka baada kuguswa begani kucheki ni kaka kwanza nika tabasamu kwa kuweza kumuona live tena hasubuhi ile juwa lina waka basi akawa amekaa kwenye benchi kwa mbele yangu na kusema
“popote ulipo nami nipo, nikatabasamu na kumuuliza “una maanisha nini kusema hivyo?"
akajibu ya kwamba “mpaka sasa kuzimu tuna msaka
Nipe nikupe hatujui yuko wapi ila kupitia wewe atajitokeza tu maana wewe ndio adui yake mkuu, “hivi kaka kwa nini usiende nyumbani ukajionesha kwa wazazi tukaishi pamoja? kusema kweli ile kauli ikamfanya kaka acheke sana
“hahahaha! kipindi yeye anacheka nika shangaa washikaji wa kitaa wanarudi kuja kukaa pale maskani huku wakinipa tano mimi na kaka basi kijiwe kikanoga zaidi baada kaka kutupa story ya Chanduka,
“yani kwa kifupi huyu Chanduka baada kutupwa kutoka ndani ya meri na kujikuta anatua ndani ya bahari tena kwenye kina kirefu balaa aka jitahidi sana kupiga mbizi asijuwe wapi ana kwenda gafla akahisi kuna kitu kina kuja kwa kasi ya kimbunga kucheki kwa mbaali si akauona upanga kumbe ni papa Chanduka akadata na kujuwa huu ndio mwisho wake wakati yule papa ana mkalibia kwa kitendo cha kustua akatokea zinga la joka na kumpiga kikumbo yule papa kisha akammeza Chanduka na kusepa nae wakati yote yana fanyika yeye alikuwa kashapoteza fahamu zamani tu akaja kustuka yupo misiwani ame zungukwa na watu wa ajabu ajabu akabebwa mpaka kijiji cha wale viumbe yani wanawake wa tupu hakuna mwanaume hata mmoja yani ajabu hii,
wakati kaka anaendeleza story nikamuona mama akija pale kijiweni kwa kitendo cha haraka kaka kuna kitu akakifanya nikajuwa bila shaka asiweze kuonekana na mama
na kweli alipo fika kila mmoja aka muamkia na kuniambia “Hafidhi mwanangu baba yako ana kwita, nikanyanyuka kwenda kusikiliza wito huku nikimuacha kaka pale anaendelea kuwapa story washikaji
basi nikamkuta baba amesha jiandaa kwa kupiga kanzu yenye kung'aa na barakashia yake kwakuwa nilikuwa tayari nishaoga nikavaa tu mavazi ya kuendea msikitini tukatoka zetu nilipo pita pale mskani jamaa yangu mmoja anae kwenda kwa jina la Yasini akaja mbio na kuniuliza “vipi ndio masjid au?
nikamjibu ndio kama vipi twenzetu basi aka muamkia baba safari ikasonga kwenda masjid mtambani siku hiyo nilijisikia furaha sana kwa kuingia ndani ya nyumba ya ibada hasa shekhe kwenye khotuba yake alipo kuwa aki zungumzia kuhusu asiri ya majini maana ali nikuna sana embu tumsikilize shekhe alicho kisema

Assalam alaykum warahmatu llah wabarakatur ndugu zangu waislama napenda kuwahusia pamoja na kuihusia nafsi ya juu ya kumcha Allah (s.w.t) leo katika khutuba yetu tata zungumzi kuhusu majini
majini ni viumbe ambao wameumbwa
kwa moto na walikuwa wakiishi
duniani kabla ya binadamu miaka
milioni nyingi iliyopita.
viumbe hawa wana tabia kubwa mbili;
yaani ya kibinadamu kwa maana
wanakuwa wanafanya mapenzi,
wanazaa na wanakufa.
tabia nyingine ni ya Kimalaika
ambayo ni kwamba wana uwezo wa
kujigeuza katika umbo lolote
wanalotaka na vile
vile wanaruka na kwenda
wanakotaka au kupita wanakotaka
bila kutumia chombo chochote.
taifa la Majini limegawanyika
katika makabila milioni Sabini na
mbili (72,000,000) na wana uwezo wa
kujifunza lugha yeyote wanaoitaka.
idadi ya majini ni kila binadamu
mmoja kuna majini 300 na wanaishi
katika majumba yetu, kwenye Miti,
majangwani, Kwenye mapango na
sehemu zenye misitu mikubwa.
majini wako katika aina Mbili (2);
maruhani na mashetani.
maruhani ni majini wema ambao
wanamtii Mwenyezi Mungu na
wanawasaidia binadamu katika
mambo mengi.
mashetani ni majini waovu ambao ni
wakorofi na wanawaletea watu
madhara na matatizo mara kwa mara.baba wa majini anaitwa Jann
ambaye kimaumbile yeye ana tofauti
ndogo na wenzie kwamba yeye
ameumbwa kwa ulimi wa Moto.
pamoja na mambo mengi
wanayoyafanya majini na
kujihusisha na binadamu, majini
vilevile wanafanya kazi za malaika
hasa zile za mambo ya kupeleka
habari na kuwalinda binadamu,
mambo ya doria za angani. Kazi hizi siyo zao lakini kwa vile wanapenda
kuiga mambo basi huiga hata kazi ambazo siyo zao.majini na binadamu wana sifa zinazofanana kwani wote wana akili na wote watahesabiwa siku ya hukumu
na watazawadiwa kwa mema yao na maovu yao, wote wanakula na kuzaa.

KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU


TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)