TUPEANE (19)

0

JINA: TUPEANE
Mwandishi: Hafidhi J Ikram

SEHEMU YA KUMI NA TISA
Kazi hizi siyo zao lakini kwa vile wanapenda
kuiga mambo basi huiga hata kazi ambazo siyo zao.majini na binadamu wana sifa zinazofanana kwani wote wana akili na wote watahesabiwa siku ya hukumu
na watazawadiwa kwa mema yao na maovu yao, wote wanakula na kuzaa.

SASA ENDELEA...
Kama ilivyo, kuna wataalamu wa
Kijini wenye fani sawa na wataalamu wa kibinadamu wenye kufanya kazi zinazofanana.tofauti kubwa iliyopo kati ya majini na binadamu ni kwamba; majini
hawana maumbile maalum na wana
uwezo wa kujibadilisha katika
maumbile mbalimbali ingawa wengi
wa majini wapo katika maumbile ya paka, nyoka na ndege.
binadamu wao wana umbile maalum ambalo halibadiliki.
majini wana uwezo wa kuwaingia binadamu wakati binadamu hawana uwezo wa kuwaona majini isipokuwa
kwa ufundi maalum.
namna majini wanavyowaingia
binadamu iko katika njia tatu njia ya kwanza : ni kama remote control; hii inamfanya
yule aliyedhibitiwa kuweza
kuelewa au kuwa na fahamu zake
lakini anakuwa hawezi yeye
mwenyewe kuudhibiti mwili wake
na anasema yale anayotaka yule
Jini njia ya Pili jini humwingia
binadamu ndani ya utosi na
kuingia katika mfumo wa damu.
hii inamfanya yule binadamu
kupoteza fahamu na anakuwa
haelewi kabisa kinacho endelea na anafanya yote anayotaka yule
jini njia ya tatu ni ile ya jini kukaa nyuma ya binadamu. njia
hii humfanya yule binadamu anakuwa hapotezi fahamu ila anakuwa hawezi kufanya lolote
na mwili wake.
{mospagebreak}
majini vilevile wana uwezo wa
Kusafiri kwa kasi ya upepo bila
kutumia chombo chochote; binadamu
hana uwezo huo isipokuwa kwa
msaada wa majini hiyo ni kusema kwamba mambo yote
yanayofanywa na wachawi na wanga
hayawezekani isipokuwa kwa msaada wa kijini.
jambo la muhimu ni kwamba pamoja
na uwezo mkubwa walionao majini,
wanadamu wana uwezo wa
kumtawala na kumdhibiti Jini na vivyo hivyo majini nao wanaweza
kumtawala na kumdhibiti binadamu wote kwa kutumia utaalamu maalum.
wako majini wa kila dini na kila
Kabila, na kuna watu wanaofuga
majini kwa kujikinga, na kwa
kuboresha kazi zao au kujipatia
utajiri. pia kuna watu wanaofunga
ndoa na majini kwa kutumia
utaalamu au kwa hiari za majini
hao.wabaya wa majini ni mashetani
ambao wengi hawana Dini na ndio
wanaoharibu mimba za wazazi na kufanya mapenzi na watu usingizini
bila hiari zao.
kuepuka usichafuliwe kimapenzi,kabla ya kulala mtangulize Mwenyezi mungu
kusema kweli hotuba ilikuwa ndefu sana mpaka nikapitiwa na usingizi nikaja kustushwa
time ya kuswali baada
kuswali kama
baba alivyo sema tukaenda kwa shekhe mirongo basi nikasomewa duwa na kupewa daawa yapata saa kumi na
moja hivi
nikiwa nyumbani
kaka akaja hadi
chumbani
kwangu na kuniambia “kwanza kabisa nimekuja na habari njema ndugu yangu,
“habari zipi hizo kaka!!!
“ni kuhusu
Nipe nikupe, baada kumsikia kaka akimtaja kiumbe huyu nikaogopa, akanishika begani na kusema “kwa sasa hutakiwi kuwa muoga kwa chochote kile wewe ni zaidi ya fighting power ni high speed kwa kuupima tu uwezo wako tu embu nifate baada kusema vile akatoka nnje basi nikamfata kwa kutaka kuujuwa uwezo gani nilio nao safari yetu ikaishia kawe beach basi akaniambia ninyooshe mkono huku nikiwa navuta hisia ya kwamba nawasha moto nikafanya hivyo kitu kama kombora hivi kikatoka kwenye mkono wangu na kujikuta naulipua mtumbwi wa wavuvi flani hivi uka tawanywa vipande vipande nikatoka mbio kwenda kwenye maji cha ajabu natembea juu ya maji kama
vile niko
nchi kavu “khaa kumbe hii inakuwa kweli mi nilijuwa ni ekti tu katika ile muvi ya jann dushman pale aaman koil alipo kuwa akiikimbiza boti kwa miguu tu yani watu walio niona wakabaki kustaajabu sana na kutoa cm zao kuchukuwa video au picha kuna upepo kaka akautoa na kufanya zi camera zao zisiweze kuchukua chochote kile
basi nikatoka mbio nikikimbia juu ya bahari na kujiona kunzia sasa mimi ni noma tena balaa zaidi “nazani umeona mwenyewe kwa jinsi ulivyo ila hapo ni cha mtoto tu una mengi makubwa embu angalia hapa,!
akanionyesha kiganja chake cha mkono nikaweza kuona viumbe vya ajabu vyenye kutisha wakiwa wame kizunguka kiumbe kimoja kikuubwa hivi anaongea kwa hasira vibaya mno,

“hii dunia ni yetu sisi binaadamu hana nafasi ya kutawala sayari hii mshenzi mmoja tu aliye tumwa kutoka kuzimu kaja
kuuwaribu utawala
wangu wote sikuwai kushindwa na sitoshindwa kamwe mpaka niikamate hii dunia katika mikono yangu mimi ndio
Nipe nikupeeeeeeeee,,,!!!!!
hasira zikanishika na kujikuta naupiga mkono wa kaka kwa nguvu nikizani nampiga Nipe nikupe nikastuka hata yeye hakuamini maana mkono wake ukakatika basi akayumba yumba huku damu zikimtoka kwa wingi sana nikaita “kakaaaa!!!

Nikaita “kakaa!!!
cha ajabu akaniambia “please mdogo wangu usinisogeree kwa hiki ulicho ktenda kinatosha, gafla akapotea mbele ya upeo wa macho yangu nikabaki kuita tu “kaka!!! nisamehe sikukusudia kufanya hivyo ni hasira za kumuona adui yangu
Nipe nikupe sikuweza kupata majibu yeyote mchozi ukanidondoka ajabu kila tone linalo dondoka kwenye maji ni damu “khaa ina maana nalia machozi ya damu au?"
nikajaribu kuyakinga niweze kuya tizama ni machozi ya kawaida tu ila yakidondoka kwenye maji ni damu nikabaki kushangaa tu
nikarudi nyumbani nikiwa mnyonge sana hofu ikazidi kunitanda katika moyo wangu nikiwa sijui mustakabali mzima wa maisha yangu usiku na mchana nikawa namngojea kaka iwapo nitaweza kumuona lakini haikuwa hivyo hatimae mwaka mmoja na nusu ukatimia taratiibu nikianza kusahau maswahibu yote yaliyo nikumba basi siku moja nikiwa nyumbani
naandika story flani hivi nikasikia sauti ya binti akiita “barafu!!! wenyewe barafu!!!
ile sauti haikuwa ngeni masikoni mwangu nikajiuliza hii sauti nimewai kuisikia wapi au masikio yangu tu ni kweli nyumbani tunauza juice barafu na ice cream na kazi ya kuhudumia wateja anaifanya house girl anaye kwenda kwa jina la Nasra ni msichana aliye kuja na mama kutoka Zanzibar
ila siku hiyo nikajikuta nanyanyuka kwenda kumcheki huyo mteja kufika sebureni nikapokelewa na sauti nzito ya sauti kutoka kwenye sabufa huku Nasra akiwa anayakata mauno kwa kuzungusha kwa kucheza
mziki wa mwambao nikaenda kuizima radio kwanza huku yeye akidondosha zinga la msonyo “nyoko zao tanesco kwa kunikatia raha zangu kumbe hakujuwa kama mimi ndie niliye zima kwa kuwa aliipa radio mgongo hata mie nilipo fika hapo hakugundua baada kugeuka na kugundua sio tanesco akabaki kuona aibu tu
“hivi Nasra ushaanza kuwa chizi sio!
“mmh hapana boss nilikuwa naondoa mawazo tu!!!
“kwahiyo kuondoa mawazo mpaka ufungulie mziki sauti mpaka mwisho sio?"
“akashindwa kujibu na kubaki kujiinamia chini tu kusema kweli sinaga mazoea na huyu binti tokea ameleta miezi sita iliyo pita nahisi ata yeye alijiuliza mimi binaadamu wa aina gani nikamwambia “kuna mteja nnje huko anaita muda wote anataka barafu wewe husikii embu nenda kamtizame huko,'
“nisamehe boss akatoka mbio kwenda nnje akarudi na kusema “boss mteja mwenyewe hayupo!
“kwa sababu ya ujinga wako huo mtu anaita wee mpaka anachoka bwana afu kitu kingine usiniite boss niite Hafidhi j ikram, “sawa boss
“nyoko zako husikii au?"
nikaingia ghetto kwangu kuendelea kuandika story ya Chanduka wakati naishika tu laptop yangu ile sauti ikaita tena “barafu!!! wenyewe barafu!!!
basi nikatoka nnje haraka sana nikastuka kwa kile nilicho kiona mbele ya upeo wa macho yangu dahaa

ni Mwajuma japo alikuwa katika sura ya kutisha na kuogopesha maana jicho lake moja lilikuwa lina ning'inia huku moyo wake ukiwa nnje unadunda kwa speed ulimi nao umekatwa yani kwa binaadamu wa kawaida unaweza kupata stroke ukafa kabisa akawa anajitahidi kutamka kitu hawezi sasa kama hawezi kutamka kitu nani kaita barafu tena sauti yake ni Mwajuma gafla akaibuka adui wa maisha yangu tena kwa kicheko ni
Nipe nikupe “ha!ha!ha!ha! kijana naona unaweza kushangaa kwa nini nimekuja hapa mchana huu kweupe kwa sababu najiamini hakuna chochote kitakacho weza kuniangamiza mimi

kingine nakuonea huruma katika vita hii umebaki peke yako yule boya sijui kaka yako ameshakufa kitambo tu watu tushalia vilio vya kinafki tukazika na kula ubwabwa kwa maharage!!! ile kauli ya Nipe nikupe kusema kaka yangu kafa ikanifanya niwe na hasira mpaka wingu gafla likaanza kutanda nikasema “nyamaza nyau mdogo wee usizani utaweza kushinda vita hii kama kaka yangu aliweza kukushinda mpaka ukaikimbia kilwa utawezaje kupambana nami niliye kabiziwa nguvu za maelfu ya watu,

“ha!ha!ha!ha! kijana nimependa kwa jinsi unavyo jiamini ila tambua ya kwamba dunia siku si nyingi itakuwa mikononi mwangu na dalili moja wapo wafuasi wataongezeka kwenye mitandao ya kijamii kutwa kucha watashinda huko watasahau neno la Mungu vitabu vitakatifu kwao wataviona kama vile kushika mavi au kaa la moto unywaji wa pombe utaongezeka zinaa itakuwa halali huku watoto wa nnje ya ndoa wakijaza dunia!!!
“nikapaza sauti kwa kumwambia “nyamazaa!!! hizo ni ndoto za mchana tu endelea kuota

hakuna kitu kama hiko embu naomba nikuulize kitu wewe si ndie uliye kuwa ukitoa hukumu ya kifo
kwa kila binaadamu anaye fanya
mapenzi nnje ya ndoa si wewe au?"
“kijana achana na mambo ya kizamani wewe hii ni karne mpya unamuona huyu binti nazani bila shaka unamkumbuka sasa basi tulimtuma mwanao aende kuichukuwa ile kacha na yeye bila kufahamu kama atamuangamiza mama yake akaenda kuichukuwa ndipo tukapata nafasi ya kumchukuwa mtu wetu tuliye kuwa tukimuwinda kwa muda mrefu sana sasa kazi iliyo bakia mbele yetu ni kuha kikisha tunakushika wewe tukurudishe jera maana ulitoroshwa,
“ha!ha!ha! Nipe nikupe tambua ya kwamba mimi sio tena yule mlio nitesa kipindi cha nyuma kama kaka yangu alikushinda kwa kukupiga mpaka kukukamata mimi nitakufuna kabisa poteaaa!!! nikatoa sauti ya ukelele iliyo unguruma kama vile radi nikanyoosha mkono na kutema cheche za moto
Nipe nikupe akapotea na Mwajuma
nikaingia ndani na kumkuta Nasra kalala kwenye sofa tena yuko fofofo nikamshika na Kumu wamsha “wee Nasra!!!
basi akakurupuka kutoka usingizini na kuuliza kwa tahamaki “nini boss?"
nikamshika shavu lake lainii na kumfinya huku nikimwambia “mimi sio boss niite Hafidhi mbona husikii wee mtoto! “ahaa boss unaniumiza bwana!!!
“kudadeki zako nikamuachia sijui bahati mbaya au tuseme nini" nikajikuta mkono wangu unatua moja kwa moja kwenye titi lake la kushoto sijui niligandishwa na super grou au vipi nikashindwa kuutoa na kuishia kulipapasa mtoto huyu mwenye sifa ya kipakee

Tokea siku ya kwanza anaajiliwa kuja kufanya kazi za ndani miezi sita iliyo pita sikuwai kumsaminisha au kumtamani kwa chochote kile hii ni kutokana kutokuwa na hisia na wanawake kabisa toke yanitokee majanga kule kilwa kiwawa nikatokea kuwaogopa wanawake kabisa ila sasa nimenasa gafla kama short ya umeme kwa kitoto kutoka zenji

KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU


TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)