SEHEMU YA KUMI NA MBILI
ILIPOISHIA...
Ilikua ni sauti ya kike, iliyotokea katika kipaza sauti iki tangaza kwa lugha nyingi tofauti ili kiila mtu aweze kuelewa, tayari ilikua ni saa nne za asubuhi ,SASA ENDELEA...
Mawasiliano ya marubani yalizidi kutolewa huku ndege hiyo ikijiandaa kushuka yalitangulia matairi kutoka nje na sasa kugusa ardhi ya Tanzania, ilivyotua iliyumba kidogo kisha kukaa sawa, ilitembea kwa kasi sana huku taratibbu ikipunguza mwendo na mwishowe kusimama kabisa,
Magari maalumu yalifika hapo na kuweka ngazi milangoni na taratibu abiria kuanza kushuka akiwemo Kway na familia yake.
“niliacha bastola yangu,na magazine tatu”
“ nipatie kadi”
“hii hapa”
Kway Aalifika chumba maalumu alipoacha silaha yake na baadae alipewa karatasi aweke sahihi na kupewa bastola yake, aliiweka vizuri kiunoni kwa nyuma na kuifunika na shati ili isiweze kuonekana na kutaka nje ya chumba hiko!,
“Dad njaa ina uma!”
“usijali utakula kwa Anti yako, atakuja sasa hivi Nattu mwanangu!”
Moja kwa moja walitoka nje na kumkuta tayari Loyda kesha fika ana wasubiri kwa kuwa alikua ana jua ujio wao, ivyo aliwahi mapema sana, alifurahii sana kuwaona na wote kukombatiana kwa furaha sana.
Na kuanza kuongozana mpaka kwenye maegesho ya magari waliweka mizigo yao ndani ya gari na safari kuanza. !
“ poleni na safari,, ume fanana na mwanao , lakini sura kachukua kwa mama yake, ndo wa kwanza huyu?”
Alivunja ukimnya Loydah
“aah nime choka kweli asante. Ndiyo ndo wa kwanza huyu,ana itwa Natttu ,”
“ hongera sana, naona una taka kuongeza mwingine, kana miaka mingapi”?
“ana miaka sita, “
“kazuri”!.vipi za Malaysia”?
“ovyo tuu, nili pata na matatizo makubwa balaa, bila Mungu ninge kua nisha kufa”
“nini tena”?
“una jua kuwa nili hamia sehemu moja ina itwa kuala Lumpur, nilikua nafanya kazi shirika Fulani ivi la ki swizz, , siku iyo natoka bank, kuchukua pesa nilipe lipe madeni, kumbe kuna majambazi walikua waki ni fuata nyuma mimi sijui, sasa nime paki gari ili nipige simu, ponea yangu ili kua kuvuta kiti nilale, ile nime binua kiti nyuma risasi ika pita mbele yangu, ilikua ipite kichwani, sija kaa sawa, kama umeme hawa hapa, waka nitoa ndani ya gari, walinipiga kishenzi, wakachukua na ile gari ya kampuni”
“pole sana ndo mitihani ya Mungu, tushukuru tu upo hai, sasa ukachukua hatua zozote”?
“kwanza nili changanyikiwa na ndo hiyo siku mke wangu ana jifungua Nattu, ili kua nitoke hapo niende hospitali kumuona, sasa wa-swizi wale hawa kunielewa , wana taka gari yao, madeni yale bado sijalipa, ukisikia mtu kawa chizi usi mcheke wengine wana kuwa hawa jarogwa, nili changanyikiwa, nadaiwa hospitali Dollah mia saba”
“Mungu wangu enhe”!
“nili uza kila kitu, nikaanza na moja, wale jamaa waka ni fukuza kazi, nili teseka acha tu, ange kua mwanamke mwingine angesha nikimbia kabisa, ndo maana hua namuheshimu sana huyu mwana mke, kanivumilia mengi mno!”
Walipiga stori za hapa na pale wakiwa wenye furaha sana baadae kidogo gari liliegeshwa nyumbani kwa Loydah, kwa kuwa walikua wana jua ujio wake chakula kilia ndaliwa na wote kujumuika mezani na kuanza kula kwa pamoja.
“alafu nani huyu, huyu, mke wa marehemu Ramsey yupo”?
“yupo ndio Sabrina, nilikua nae hapa wiki iliyo pita, nili mwambia kuwa una kuja leo,”
“ina bidi nika muone kesho”
Waliendelea kula chakula hiko huku wakipiga stori za hapa na pale.
Catherine aliendelea kusota bado mahabusu hakuna mtu aliye kuja kumuona zaidi ya rafiki yake kipenzi Betty, jambo lile walili fanya siri sana hakutaka kumshirikisha mama yake, alielewa kabisa kuwa kumwambia mama yake ange mpiga sana, siku ya tatu sasa , bado hakutaka kuamini kuwa Enock ame mtupa alidhani anaota ndoto ndefu sana ya kutisha, ila mambo yaliyo kua yanaendelea yalikua yana ukweli ndani yake,
Mbu wakubwa wa maabusu walizidi kunyonya damu yake na kumfanya apate vipele pele vingi kutokana na ngozi yake kuwa laini, alimlaumu sana Rafiki yake kwa kitendo cha kumsha wishi aweze kumkubalia Enock,
Kila alipo jaribu kumuombea Rafiki yake huyo dhamana alizuiliwa hii ni kutokana na Heather kutoa pesa nyingi ili asitoke na ikiwezekana kesi ile ipelekwe mahakamani na afunguliwe kesi nyingine hata ya kuuua aka sote huko Gerezani hayo ndiyo aliyokua akiwaza Heather ndani ya ubongo wake ..
Akili ya Enock sasa ili sha badilika kabisa hakuwa ana msikiliza hata mama yake tena, mapenzi yote aliya hamishia kwa Heather jumla jumla, dawa ya Wakyoyo ili fanya kazi kwa asilimia zote, nyumba yake iliyo kua Mbezi ilikua bado vitu kidogo tu iweze kuisha na waweze kuhamia na baadae ndoa ifungwe,
Alipelekeshwa sana na Heather aweze kumalizia hiyo nyumba kubwa yenye kila kitu ndani, akili ya Heather ilikua ni moja tu baada ya nyumba ile kuisha katika hati ile jina lake liwepo nayeye awe mmiliki wa ile nyumba,
“fanicha ina bidi niagize china, kontena nzima, kuanzia makochi, t,v choo kile cha yakuza, nataka hii nyumba iwe ya kisasa sana, hata rafiki zangu wakija wajue hapa ana ishi Enock”
“sawa baby, mimi sina taizo”
“baada ya hii nyumba kuisha, tuta funga harusi bab kubwa, just wait,”
Maneno hayo alizungumza Enock baada ya kuzunguka na kuikagua nyumba yake hiyo iliyokua na eneo kubwa sana ilikua ni gorafa tatu kwenda juu yenye swimming pool nje. Ilikua ni ya kisasa sana, wakati wote Heather udenda uli mtoka sana akiwa kama mmiliki wa nyumba hiyo baadae, huku nyuma alikua na rafiki yake zahara akimshawishi afanye jambo hilo, mambo sasa kwake yalikua yaki sesereka kama kunywa maji, hakuacha kumshukuru mganga wake kalumanzila .
Juhudi za kumtafuta Catherine chuoni zilishindikana, walimuulizia chuoni hapo Sabrina na Kway lakini hawa kupata majibu ya kuwa ridhisha kabisa,
“huyu mtoto keshaanza umalaya, ata kuwa wapi?”
“huwezi jua, mambo ya chuo haya, ina wezekana akawa discussion”!
“discussion gani hiyo, wenzake wana sema hawa jamuona siku ya nne hii”
BADO walizidi kumsaka kila chumba mwishowe waka elekezwa chumba ana cholala, hawa kusita kwenda walinyoosha na kwenda humo,
Wali mkuta rafiki yake Betty kachoka akiwa na mawazo na kuumulizia, majibu waliyo pewa yaliwa fanya wabaki midomo wazi na kustaajabu!,
“yupo kituoni ameenda kumuona nani?”
“haja enda kumuona mtu, kasingiziwa kesi, na ninavyo kwambia hapa kesho anaenda mahakamani kusomewa mashtaka,”
“kafanya nini tena huyu mtoto”?
“wamemsingizia kaiba dhahabu, wana sema sijui aliiba mali nyingi kwenye duka la muhindi, mambo kibao mengi mengi tu”
“yupo kituo gani”?
“msimbazi”
“tuongozane”
Haraka haraka walirudi ndani ya gari na safari ya kwenda msimbazi kituo cha polisi kuanza , baada ya kufika hapo wana kuta mambo tofauti kabisa, walinyimwa kabisa kumuona Catherine na kutoa mgomo wa dhamana.
“kwani aliua”?
Alihoji Kway
“hapana, ila ana kesi nyingi sana”
“sasa m-me kataa kutoa dhamana, hata kumuona?, naomba nionane na mkuu wako”
“bwana eeh, embu nendeni nje, nime sema hivi, hamuwezi kumuona na pia msipo angalia na ninyi mtaingia ndani kusaidia mahakama”
“nisikilize kijana, hizo jezi zisiku fanye utupige mikwara sawa, usinitishie umeelewa, usinitishie kabisaa!, naona huni fahamu sawa sawa. Sasa subiri uone,”!
Kway alitoka nje kidogo na pale pale kutoa simu mfukoni alienda kwenye majina na kutafuta jina RPC Mkumbo na kuipiga simu ile, hakusita kueleza kila kitu kili cho mkuta
“ongea na hii simu”
“wewe mpuuzi nini, niongee na nani sitaki kuongea na wajinga wako, toka bwana.”
Alizidi kuropoka polisi huyo bila kujua simu ile ipo hewani na mkuu wa jeshi la polisi akimsikia kwa kila kitu alichokua akiongea,
“kuanzia leo hauna kazi, vua hayo magwanda sitaki kukuona kazini, na huyo binti naomba apewe dhamana sasa hivi, na maelezo ya kutosha kuwa alifanya kosa gani mpaka asipewe dhamana!”
“lakini mkuu. Usi…”
“nime maliza”!
Sauti hiyo ilisikika vizuri baada ya kuwekwa loudspika na kupenya kwenye ngoma za masikio ya polisi Yule aliitambua sana sauti ile ilikua ya RPC Mkumbo.
Watu walizidi kufurika ndani ya kanisa la st Joseph lillilo kua posta siku hiyo ya jumamosi tarehe saba mwezi wa tisa, saa nne na dakika tatu, wengine walikua nje wakitaka kushuhudia harusi hiyo ya kifahari ambayo hata ilitangazwa katika vyombo vya habari, na magazetini pia, matajiri wali furika na kujaza kanisa hilo ila cha kushangaza mpaka dakika hiyo bado bwana wala bibi harusi hawakuonekana, na kufanya watu wengi kuingiwa na hofu sana mioyoni mwao,
ilishaanza kusikika minong’ono ya chini kwa chini kuwa hakuna harusi tena.
“tuku tuku tu ku tuku tuku”
Zilikua ni kelele za helikopta na kufanya upepo mwingi upulize na kufanya vumbi jingi kuruka, baadhi walichungulia, helikopta hiyo ilitua nje ya kanisa la St, joseph na watu hawa kuamini kabisa kumuona Enock akiwa ndani ya suti nyeupe akishuka na mpambe wake baada ya helikopta hiyo kutua, huku pembeni alikuwepo Heather ndani ya shera kubwa sana na la gharama llikua kubwa mno,
Hakika walipendeza sana na kuwa kivutio kwa watu walioshuhudia.
“hii ni balaa, sijawahi ona harusi kama, kuna watu wana pesa”
“kweli kaka, hii ni balaa, hapa kanisani tu sipati picha ukumbi uta kua wapi,”.
Ilikua ni minong’ono ya chini chini.
Hakika jambo lile halikuwahi kutokea Tanzania illikua harusi ya kifahari na funiko kabisa, walishuka taratibu na kuelekea mbele ya madhabau taratibu sana huku waumini wakisimama na kuwa pigia makofi, hakika walipendeza kupindukia,
Muda wote Catherine alilia kwa uchungu ndani ya kanisa nayeye pia hakutaka kupitwa hakutaka kuamini kuwa Enock mwana ume anaye mpenda kwa dhati kutoka moyoni ana funga ndoa, alilia sana na watu kumshangaa,
Mchungaji alisoma neno kisha baadae pete zika letwa pale mbele yao tayari kwa kuvalishana ili wafunge pingu za maisha, Muda wote Heather alikuwa mwenye furaha sana hasa alivyo mfika pete Enock na kufanya kelele nyingi sana., nyuma yake alikua ame simama mpambe wake Zahara
Ila ilipo fika zamu ya Enock kupewa pete macho yake yalitua machoni mwa Catherine ambaye alikua akilia sana mpaka akawa mwekundu pengine kujilaumu kwa nini alikuja kanisani hapo.
“Mr.ENOCK ume kubali bibi Heather Nabuuma awe mke wako katika shida na raha, tabu na mateso”?
Mchungaji Edward alirudia tena mara ya tatu lakini Enock alibaki kimnya muda wote bila kusema lolote na kumfanya Heather aingiwe na wasi wasi..
“Enock”!
Alinong’ona Anderson Peter mpambe wake kwa sauti ya chini baada ya kumuona Enock kaduwaa, hakika hata yeye alibaki akistaajabu na kutoelewa nini kili fanya hali ile itokee, Zahara nayeye moyo ulimwenda mbio sana, vile vile moyo wa Heather ulizidi kudunda kwa kasi tena kwa dakika moja ulidunda mara mia tano,
KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA