SEHEMU YA KUMI NA TATU
ILIPOISHIA...
“Enock”!
Alinong’ona Anderson Peter mpambe wake kwa sauti ya chini baada ya kumuona Enock kaduwaa, hakika hata yeye alibaki akistaajabu na kutoelewa nini kili fanya hali ile itokee, Zahara nayeye moyo ulimwenda mbio sana, vile vile moyo wa Heather ulizidi kudunda kwa kasi tena kwa dakika moja ulidunda mara mia tano,
SASA ENDELEA...
“ndio nime kubali awe mke wangu wa maisha. kwenye shida na raha, tabu na mateso, mpaka pale kifo kitakapo tutenganisha”!
Maneno hayo yalitoka kinywani mwa Enock Mwasha akiwa anamvika pete ya ndoa Heather na kufanya kelele nyingi na picha kupigwa za mnato,ndani ya kanisa hilo la st,joseph, hakuna kilichosikika zaidi ya tarumbeta, furaha ili tanda isipokua kwa Catherine ambaye alikua akilia tu muda wote, kushuhudia kitendo kile ilikua ni sawa na mtu kuingia ndani ya mtima wake na kuuchoma mkuki wenye moto, hakuwa na sababu ya kuendelea kukaa na kuchomwa mtima wake ndani ya kanisa, alisimama huku akilia sana na kutoka nje, watu waligeuza shingo zao na kumsindikiza kwa macho na kutoelewa nini kina endelea ndani ya moyo wa binti huyo,
“Catherine Catherine, nisubiri”!
“betty niache, betty niache nakwambia!”
Ili mbidi rafiki yake amkimbilie na kumfuata kwa nyuma alimuonea sana huruma rafiki yake ,
“nawewe nakuchukia sana, nakuchukia betty, kwanini mimi lakini, kwanini umea mua kuniingiza kwenye mapenzi tena, mi nilijua mapema Enock alitaka….”
Alishindwa kumalizia kuongea kilicho fuata hapo kili kua ni kilio kisichokuwa na mwisho, bajaji ili tafutwa na wote kuanza kurudi hostel, ndani ya bajaji hakuacha kulia huku akijilaumu sana na kutaja jina Enock mara nyingi, maumivu aliyo sikia ndani ya moyo haya kuweza kuelezeka kabisa aliya jua Mungu peke yake, mapenzi kweli yalimuumiza sana , moyo wake alimkabidhi Enock na kumwachia mwili wake , amtoe bikra yake , bora ange mfumania kuliko kushuhudia Harusi kabisa, kwake aliona ni kitendo cha kinyama pengine dharau alijiona hana thamani nje ya uso wa dunia, alimchukia sana Betty ,
Baada ya kufika hostel alijitupa kitandani huku akilia sana , juhudi za kumbembeleza ziligonga mwamba na kushindikana kabisa, mawazo ya kutoweka duniani yalianza kujijenga ndani ya ubongo wake, hakuona sababu ya kuishi tena, hapo hapo shetani alimuingia na akili moja kumjia kujiua tu, na si vinginevyo,
Alifuta machozi yake na kutabasamu ili Betty asielewe lolote lile,
“naenda duka la madawa hapo narudi”
“hapana nitaenda na wewe, una enda kufanya nini?”
“usijali Betty nipo sawa, kichwa kina niuma tu!”
“kweli mamii”?
“ndio kweli, nakuja sasa hivi”
Alimfuata Betty na kumkombatia sababu alijua fika anachoenda kuki fanya aliamini kabisa hatorudi tena , , alikua ni kama anamuaga alitabasamu na kufikicha macho yake na kutoka nje, laiti kama Betty ange jua ndani ya mawazo ya rafiki yakekipenzi asinge thubutu hata kumruhusu aende peke yake, moja kwa moja ali vuka bara bara na kuelekea upande wa pili , na kufika ndani ya duka la madawa,
“nipe cloroqin kumi na vidonge vya panadol thelathini”
“ivyo vote vya nini”?
“nime agizwa vya kufanyia practical chuoni”
“okay sawa”
Dada Yule alipokea pesa na kumfungia vidonge vile,
Baaada ya kuchukua aliviweka ndani ya mkoba wake na kutoka kabisa eneo la chuo alitafuta dala dala la Ubungo na kuingia, ndani ya kichwa chake alikua na mawazo tele mawazo mengi, alimkumbuka sana mama yake siku chache alivyo mfokea na kumuita Malaya baada ya kutoka kituoni, ila hakuelewa ni jinsi gani ata kavyo kua endapo ata sikia ametoweka duniani, leo hii anaenda kujiua kisa mapenzi, hakika aliweza kuamini kuwa mapenzi yana ua kabisa, aliwahi kusikia stori tu au kuona filamu mbali mbali akajua ni maigizo ,ila dakika hio alijua mambo hayo yapo kabisa,
“konda nishushe MORROCO”
Baada ya kutoa kauli iyo aliteremka na kutafuta moja ya baa na kuagiza bia ili amezee zile dawa,
“nipe na konyagi”!
Kabla ya kufanya kitendo kile alimuomba Mungu amsamee sababu alijua kabisa katika maandiko yana kataza kujiua , ilikua ni dhambi kubwa sana, ila hakua na chaguo lingine kwa wakati huo,
Alichukua chupa ya konyagi na kuvishika vidonge viile na moja kwa moja kuelekea chooni akiamini huko hakuna mtu yoyote atakae muona, aliingia chooni na kuji fungia mlango,.
“acha nife tu, sioni haja ya kuishi duniani”
Alifungua chupa ile ya konyagi na kupiga fundo kubwa huku akiya fumba macho kwa uchungu wa pombe kali ile,
Alifungua vidonge vile na kuviweka mdomoni na kufanya mdomo ujae kweli alidhamiria kufa kabisa!, alichukua chupa ya konyagi na kushushia yote mdomoni na kutupa chupa ile chini, haikupita hata sekunde saba tayari tumbo lilianza kumkata kama viwembe.
“shosti naomba usini sahau”
“aah wapi wala usijali, siwezi kuku tupa subiri mambo yakae sawa!”
Zahara aliimnong’oneza Heather wakiwa angani juu ya helikopta ambapo safari ya kuelekea bandarini ilianza baada ya kutoka kanisani , kweli sherehe hiyo iliandaliwa vilivyo , ili gharimu sio chini ya dolla elfu ishirini za kimarekani . huku wapambe wengine wakiwa kwenye magari wanaelekea bandari kila mtu akiwa na kadi ya kiingilio ndani ya boti hiyo kubwa ambapo harusi iyo ili pangwa ifanyike ndani ya moja ya boti za BAKHRESA , dakika chache baadae rubani wa helikopta hiyo aliishusha helikopta hiyo taratibu juu ya maegesho maalumu ya helikopta, na Enock kushuka akiwa na mke wake sasa Heather,
Ki ukweli Heather hakuwahi kuota hata kufikiria kama ata kujakuwa na maisha ya kifahari kama hayo, zahara vile vile muda wote alikua akikenua meno yake sababu yeye vile vile alitoa ushamba kwa kupanda helikopta.
“this way please(huku tafadhali)”
Aliongea captain wa meli hiyo huku akiwaongoza ndani bwana na bibi harusi,
Hakua na habari kuwa upande wa pili wa shilingi Catherine ana hangaika kuutoa uhai wake kwa sababu yake , dawa ya wakyokyo kweli ili fanya kazi kwa asilimia zote, na kuichukua akili yake nzima nzima , baada ya dakika chache wageni waalikwa wakiwemo ndugu jamaa na marafiki wa pande zote mbili walianza kuingia ndani ya boti hiyo, kisha boti hiyo ilianza safari yake na kuondoka huku Yule Yule Mc KAPILIMA akizidi kuchangamsha tafrija hiyo iliyo kua ya kipekee kabisa,
Nahodha Yule aliye kua akiendesha boti hiyo alikua na kazi moja tu kuizungusha boti hiyo baharini na hio ndiyo ili kua kazi yake huku harusi ndani ya meli hiyo kuendelea.
Watu walikunywa na kusaza na kuacha vinywaji, kweli harusi hiyo ili kua yakuzungumziwa ,
Saa sita ilivyo fika walistaajabu sana baada ya kuchungulia na kuona ndege ndogo ambazo zenye uwezo wa kutembea kwenye maji, ikiwa ipo nje tayari,
“Enock mume wangu nakupenda sana”!
“hata mimi nakupenda sana Heather wangu”
Kili cho fuata hapo yalikua ni mabusu ya midomoni. Na wageni kuanza kupiga makofi na hapo hapo picha za mnato kupigwa.
“fungate nataka twende visiwa vya chake chake, ndege ina tusubiri hapo nje”
Alizungumza Enock huku akimbeba Heather, .
“bwana na bibi harusi sasa wana enda kupumzika jamani, Dj tupo mambo sasa, sisi tuna endelea kuburudika humu humu”
Waliagana na ndugu na kuanza kutoka nje, waliingia ndani ya ndege ndogo na kuanza safari ya kuondoka huku ndege hiyo iki tembea kwenye maji kisha kupaa angani..
Kili cho fuata hapo yalikua ni mabusu ya midomoni. Na wageni kuanza kupiga makofi na hapo hapo picha za mnato kupigwa..
“fungate nataka twende visiwa vya chake chake, ndege ina tusubiri hapo nje”
Alizungumza Enock huku akimbeba Heather, .
“bwana na bibi harusi sasa wana enda kupumzika jamani, Dj tupo mambo sasa, sisi tuna endelea kuburudika humu humu”
Waliagana na ndugu na kuanza kutoka nje, waliingia ndani ya ndege ndogo na kuanza safari ya kuondoka huku ndege hiyo iki tembea kwenye maji kisha kupaa angani
SONGA NAYO.
“chagua gari sasa, mi naona unge chukua lile pale,”
“ipe, ile ya mudogo”?
“ndio ile vitz ita kufaa”
“una bazimu wewe, nataka gari ya kabambi kama ya kaka Bozii au chanci,”
“uwiii mama Natu, una taka Range”?
“ndio”
“Mama, uta nisamehe mimi sina uwezo, yaani hapa nime jikamua kishenzi! sababu hapo ume beba mtoto wangu tumboni, kama una taka Range mimi bado sina uwezo”
“duru sana wewe, una bazimu, kichwa yako haiko sawa haiko bien,”
“nakununulia hii gari kama hutaki nita tumia mimi huku wewe uki subiri hiyo Range nikiokota pochi ya mzungu, . lakini sherii mimi sina makuta sasa hivi, nikisha pata utaendesha Range na hata ndege nita kununulia”
Yalikua ni mazungumzo baina ya Kway na mke wake huyo ambaye alionekana ni muogeaji sana kupita hata mumewe lakini Alisha mzoea sasa yote aliona ni sawa kwake, aliamini pia ni mimba ndiyo ina mpelekesha, walifanya malipo na kulipia gari lile kiasi cha shilingi milioni saba kisha wakaondoka zao.
“sista jaqlin embu nisubiri ndani ya gari naenda kukojoa hapo baa,”
“usichelewe sasa”
“dakika sifuri”
Kijana huyo alishuka ndani ya gari ila alivyo fika maeneo ya msalani maeneo ya baa iliyo kua morroco aliona kundi la watu likiwa lime tengeneza duara hakutaka kupitwa alipangua pangua watu kisha akafika nayeye ili achungulie,
“jamani ana kufa huyu, tuta futeni gari sasa hivi awaishwe hospitali ,”
Ilisikika sauti ya mwana ume mmoja akiwa na wasi wasi sana aliye kua chini pale alikua ni mwana mke ambaye dakika chache ana enda kukata kauli sababu alikua akihema kwa shida huku povu likianza kumtoka puani, alikua ni catherine baada ya kuingia chooni bila kutoka ivyo waliamua kuvunja mlango na kumtoa nje, juhudi za kutafuta gari ziligonga mwamba kulikua kuna kila dalili ya Catherine kupoteza maisha kama angecheleweshwa kupatiwa matibabu ya haraka.
Alipatiwa maziwa lakini hakutaka kufungua mdomo wake kunywa, alidhamiria kufa japo alihisi maumivu makali tumboni.
“ina maana hakuna mwenye usafiri hapa”?
“mimi hapa ninao”
Kijana Yule aliitikia
“ume paki wapi gari yako”?
“ile pale Vigo ya silver”
“tusaidianeni basi tumpeleke hospitalini huyu dada”
Wote walisaidiana kum-beba Catherine ambae wakati huo alikua ameshika tumbo lake akiwa anatafuta pumzi kila mtu alimuonea huruma hawa kuelewa nini chanzo hawakuelewa nyuma yake kuna mtu aliyefanya mpaka yeye atake kuutoa uhai wake kabisa, walimuingiza ndani ya gari na baadhi ya watu kumshukuru sana kwa utu alioufanya.
“kaka ubarikiwe sana, una itwa nani”?
“naitwa Darlington Shebby!”
“yaani wakitokea watu kama nyie wenye roho nzuri ndani ya hii nchi, shemeji mambo”!
“huyu ni kama dada yangu ana itwa Jaqlin Lucian,sio shemeji yako”
Gari lile aina ya Virgo lilizidi kuchanja mbunga kilicho tokea hapo ni ukimnya sababu ya kasi aliyokua akitumia Darlington Shebby kuya pita magari mengine huku akiwa amewasha taa za mbele zote kuashiria kuwa ana dharura na haraka pia,
KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA