BIKRA YANGU (15)

0
Mwandishi: Emmanuel F. Kway

SEHEMU YA KUMI NA TANO
ILIPOISHIA...
Harakati za safari zilianza kuandaliwa wakitafuta boti ndogo ya kukodi iwapeleke mpaka Zanzibar kisha huko siku hiyo hiyo watafute ndege na kuondoka zao.

SASA ENDELEA...
Kwa bahati nzuri jioni hiyo hiyo walifanya mawasiliano na ndege zinazo ondoka jioni ya siku iyo na kuwekewa nafasi baada ya kukata tiketi ya ndege kwa njia ya email, baada ya kupanga mizigo yao waliingia ndani ya boti na boti hiyo kuanza kukata mawimbi.
“una penda nikuzalie mtoto gani Mume wangu”?
“nataka baby boy”
“mi napenda awe wa kike”
“no nataka dume, sitaki msichana”
“mmh basi huyu ni wa kike sasa”
“huyo wa kiume”
Walibishana bishana huku wakiwa wenye furaha sana , walikombatiana na kuanza kunyonyana ndimi zao,

Dakika kadhaa mbele tayari walikua Zanzibar na kushuka kisha bila kupoteza muda walitafuta ndege na kupanda tayari kwa safari. Haikuchukua hata lisaa limoja walikua uwanja wa ndege wa kimataifa mwalimu Nyerere na kushuka ,walipanga siku hiyo watafute hotel kwanza ili waweke mizigo yao kisha baada ya siku mbili waweze kuhamia kwenye nyumba yao mpya ambayo ilikua tayari imeisha kabisa!,.

Hakutaka kufika nyumbani kwao kwanza alitaka kesho yake anyooshe moja kwa moja mpaka Gerezani Segerea ila hakutaka kwenda peke alitaka aende na Mke wake Heather sababu Mama yake alikua ana umwa sana kwaio hakuwahi kumuona hata mara moja ,

Alijua kivyovyote vile mama yake ange kua mwenye furaha ange pewa taarifa za mjukuu wake.

Asubuhi kulivyo kucha waliingia ndani ya gari ya kukodi na safari ya kwenda Segerea kuanza nyuso zao zili tawaliwa na furaha sana , waliowaona wali watamani sana, baada ya dakika chache mbele tayari walikua segerea wakiomba waonane na Josephine Mwasha,.baadae askari magereza walimleta na Enock kutabasamu sana baada ya kumuona Mama yake akiwa na hali ya kuridhisha kiafya, alimpenda sana mama yake

“Mama hakika leo uta furahi sana, nina habari njema za kukwa mbia, kwanza nime kuja na mke wangu huyu hapa, alafu hapo alipo ana mjukuu wako tumboni!.”

Josephine alikaza macho yake kitambo kwa mwana mke aliye kua mbele yake aliye tambulishwa kama mkwe wake, alionekana fika kama alimfahamu alizidi kumkazia macho kama ana kumbuka kitu Fulani cha miaka ya nyuma sana, alizidi kuvuta vuta kumbu kumbu na kuunganisha matukio mbali mbali bila kusema chochote kile, ghafla sura yake ili badilika .

“Nabuuma Heather wewe!, Mwanangu sitaki nikuone na huyu mwana mke kama unanipenda mimi mama yako, kama nili kubeba tumboni miezi tisa, naomba uachane na huyu mwanamke, sio mtu mzuri”

Kauli ile ili mfanya Enock ashindwe kuyaelewa maneno ya mama yake mzazi pengine alidhani amechanganyikiwa sana, alibakia akitoa macho yake huku akimuangalia mke wake ambaye kwa wakati huo alionesha kila aina ya dalili ya hofu kumtanda.

UKIMNYA ulitawala kidogo aliwatazama wana wake wawili mmoja aliye kua pembeni yake na mwingine mama yake mzazi ambaye alionesha chuki za wazi wazi,na maneno aliyo kua akiongea wakati huo ilionekana dhahiri kuwa yana ukweli kabisa ndani yake, kupitia macho ya mama yake aliweza kutambua jambo hilo, sababu aliongea kwa hisia zote.,
“kwanini una sema ivyo mama yangu, huyu ni mke wangu wa ndoa”!
“hata kam……”
“En…ck tumbo nahisi kichomi”

Alilalamika Heather akiwa pembeni yake huku akimshika shati lake na kuanza kulia kwa uchungu kama mwana mke aliye kua ameshikwa na uchungu wa kuzaa,wakati huo alikua na chaguo gumu sana, kumsikilizia mama yake au kumpeleka mke wake hospitali, bado ubongo wake ulizidi kuchanganua mambo mengi sana, alimtazama mama yake kwa kitambo

“Mama naomba nimuwaishe huyu Mke wangu hospitali, alafu nita kuja kuongea nawewe vizuri”
“hakuna cha kuongea Enock, mimi nisha kwambia”

Enock alimbeba mke wake na safari ya kwenda hospitali kuanza pale pale , bado katika akili yake alijaribu kuunga unga mambo mengi sana huku akimtizama Heather ambae kwa wakati huo alikua akipiga kelele nyingi akisingizia kichomi, ukweli ni kwamba hakua ana umwa lolote lile, alikua akizuga ili atoke eneo lile,

“TIIII TIIII TIIII”
MASHINE ya mapigo ya moyo ilizidi kulia mithili ya bomu lililokua lime tegwa na kusubiri kulipuka, juu ya kitanda alilala Catherine ndani ya chumba hiko kilicho fahamika kama ICU cha wagonjwa maututi, kupitia nje waliweza kumuona, hakuna hata mmoja aliye ruhusiwa kuingia ndani ya chumba hiko, ila walipewa nafasi ya kumuangalia kupitia kioo, mama yake mzazi alilia sana , hakua na matumaini tena ya kumuona mwanae akiwa katika hali ya kawaida, alitamani japo aamke ili aweze kusemezana nae machache tu, lakini haikuwa ivyo, ilimbi-di amuombe Mungu baba wa majeshi aliye juu mbiguni ili naye aweze kutenda miujiza, ila vinginevyo uhai wa cate ulikua asilimia mbili pengine.
Walisimama hapo takribani masaa manne wakimuangalia Catherine yeye pamoja na Darlington Shebby, ghafla walimuona binti kaingia huyu walimtambua kuwa alikua rafiki kipenzi wa Catherine aliye itwa Betty alikuja akiwa mwenye wasi wasi mwingi, wote walimvaa na kuanza kumuhoji maswali,
“jamani, hapa hairuhusiwi kufanya kelele, ninge omba mtoke nje ili mfanye hayo mazungumzo yenu”

Alizungumza muuguzi wa kike kisha mama yake Catherine, Darlington shebby na Betty kutoka nje, kila mtu alitaka kujua chanzo mpaka Catherine akakutwa chooni akiwa na mapovu mdomoni,

Betty huku akiwa analia machozi alianza kueleza kila kitu juu ya Enock hakua na haja yoyote ile ya kuficha ukweli sababu alijua kua baadae ukweli unge kua wazi, ilikua ni lazima aweke mambo wazi kwa mama yake ili apatiwe msaada,
“huyo Enock , yupo wapi”?
“mpaka sasa hivi niki mpigia hapokei simu”
“ndo kafanya mwanangu atake kujiua,?”
Mama Catherine aliongea kwa uzuni sana, alimkumbuka marehemu Ramsey ambaye alimpa husia kwamba mwanae asije kudanganywa na wanaume, alivyo kumbuka vile alilia machozi , ndani ya imani aliyo kua amebeba alijua kuwa huko alipo Ramsey amechukizwa sana,

“shoga usipo angalia uta poteza kila kitu, fanya maamuzi mapema”
“sasa nitafanya nini”?
“wewe ikiwezekana hata muuwe tu, ata kuletea kiwingu, ata kuharibia kwa Enock”
“nimuuwe tena”?
“ndio, kama una taka mambo yanyooke”
“sasa nita muuwaje”?
“nita kwambia cha kufanya”

Yalikua ni mazungumzo kati ya Zahara na Heather baada ya kushauriana Zahara aliamua kumshauri amuuwe Mama Enock ikiwezekana huko huko gerezani , akiamini akifanya vile na yeye baadae ata fanikiwa, ushauri ule Heather aliuona bora sana. Kitendo cha kupewa ushauri na rafiki yake kipenzi kili mfurahisha sana, aliona ni bora amuuawe mama Enock kuliko leo hii Enock aje kupewa siri nzito aliyo beba mama Enock kifuani, hayo ndiyo mawazo yaliyo kua yakicheza ndani ya ubongo wa Heather na si vinginevyo, wakiwa nyumbani kwa Zahara Mburahati,.
“alafu mamii, kesho ndo tunahamia kwenye ile nyumba mpya, ni kuuuuubwa hiyo”!
“wewe, hongera Heather jamani”
“nataka kesho nikualike sababu kuna pati kesho hiyo, usikose kuja, kuna pombe za kumwaga bibie”
“mimi tena ntakuja asubuhi na mapema”
“na uje kweli”
“nitakuja bwana”
“sawa acha mimi niende, nimuwahi jamaa, maana siku izi ana wivu, na hiki kiumbe nilicho beba basi, hataki nitoke nje, akijua nime toka ugomvi”
“aya shoga wahi, MAMA KIJACHO”

Heather alitoka huku akiwa mwenye furaha waliagana na rafiki yake ambapo alimsindikiza mpaka nje kisha yeye akaingia ndani ya gari na kuchanja mbuga, kuelekea hotelini alipo panga na Enock,

Watu walizidi kufurika ndani ya nyumba hiyo ya kifahari ambapo ilikua na gorofa yenye rangi nyingi tofauti, hakika Enock alistahili pongezi sana kwa kuporomosha jengo la kifahari vijana kwa wazee wali mpongeza sana kwa kuwa na nyumba nzuri ila yeye shukrani zote alizipeleka kwa mke wake Heather ambae mbele ya macho yake kila siku alimuona Mpya ,alimpenda sana ukizingatia ana kiumbe chake tumboni, watu walizidi kufurika ndani ya nyumba hiyo na magari mengi kupaki ya kifahari sana, kila mtu alistaajabu uzuri wa jumba hilo lili lofananishwa na KASRI anayo ishi mfalme,

Muda wote alimshika Heather mkono wake wa kuume wakitalii na marafiki zake,
“hapa hiii sehemu nime tenga nataka nifuge farasi”

Alizungumza Enock akimwambia rafiki yake Anderson Peter, muda muafaka ulifika na watu kuanza kula na kunywa huku wakikagua nyumba hiyo ndani na nje, ilikua ina kamera za CCTV kila kona na ulinzi wa kutosha kabisa, hakika ilikua ni nyumba ya kuigwa ,

Tafrija ilizidi kuendelea kisha baadae jioni kila mtu kutawanyika sasa,
“nikwambie kitu Enock”!
“niambie mke wangu”
“una jua kuwa hii ni nyumba kubwa sana, na watu wame iona wengi”
“ndio maana nikawaita waione”
“huoni mfano bahati mbaya kesho au kesho kutwa ukifa hapa, mimi na mtoto wako tuta pata shida sana”
“una maana gani”?
“naomba hii nyumba uniandikishe jina langu”
“sasa mbona mapema ivyo umeanza kusema mambo ya vifo, una taka kuniua au?”
“ha ha ha ha ha baby nawewe bwana, kwanini nikuue sasa, mimi nataka ukifa niishi kwa amani, usinifikirie vibaya lakini”

Hayo ndiyo yalikua maongezi yao usiku wa siku hiyo wakiwa kitandani, mara ya kwanza Enock alidhani Heather ana fanya masihala pengine, ila kadri siku zilivyo zidi kwenda ndipo alizidi kuonesha msimamo juu ya kuandikishwa jina lake kwenye hati ya nyumba hiyo kubwa na wakati mwingine akimtishia kuwa ataitoa mimba, ki ukweli Enock alikua katika wakati mgumu sana,
“sasa kwanini uitoe mimba,”?
“si hutaki kunisikiliza mume wangu,, sitaki nije nitange tange baadae”!
“sawa basi subiri leo nika muone mwana sheria, nakuja nae hapa , nikuandikishe jina lako”

Siku hiyo hiyo aliwasha gari na kuondoka zake akielekea kwa mwana sheria wake Mwanguku baada ya kufika ofisini kwake alimueleza kila kitu juu ya mipango ya kumuandika Heather kama mrithi wa nyumba yake mpya.
“Mr, Enock una uhakika na maamuzi unayo taka kuya chukua?”
“ndio , nina uhakika asilimia zote, nataka jina la ile nyumba aandikwe mke wangu”
“sawa mimi sina tatizo, tuta ongozana na mashaidi uweze kusaini kila kitu”
Hayo ndiyo yalikua maongezi ya Mwanasheria huyo na Enock.

“ilo shati shilingi ngapi”?
“elfu thelathini mzee, unataka moja au mengi”?
“nahitaji moja tu”
Ilisikika sauti ya mzee Mwasha ndani ya duka la nguo ila alivyopepesa macho yake juu aliona picha kubwa ya Ramsey akiwa na mwana mke amabye wakati huo alikua akimuuzia nguo pale dukani, hasira za chuki zilianza kujijenga tena upya macho yalimbadilika rangi, alimkumbuka sana Ramsey aliye sababisha yeye aka fungwa , Ramsey huyoo huyo aliye tembea na mke wake, kwa hasira alijikuta anaweka mkono wake kiunoni na kuanza kuitoa bastola yake kwa lengo moja tu kumfyatua Sabrina ambaye alikua ana uza duka hilo la nguo

KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)