SEHEMU YA KUMI NA SABA
ILIPOISHIA...
Alimganda sana akimshika shati kutokana na kelele nyingi za kutisha, katika hali ya kushangaza Darlington Shebby alimvuta karibu kisha kuzidi kumvuta tena mpaka mdomoni kwake na kuanza kumnyonya mdomo, Catherine hakua na ujanja tena hapo alijikuta ana kubali na wote kuanza kulambana midomo ndani ya jumba la sinema.SASA ENDELEA...
Siku hiyo kichwa kilimuuma sana Enock akiwa ofisini kwake juu ya meza yake, aliwaza sana kwa muda mrefu, arobaini ya mama yake ilisha fanyika tayari, ili mbidi tu asahau japo ilikua vigumu sana kwake,
Ilimbidi akubaliane na hali halisi kuwa hakukua na jinsi tena ya kufanya mama yake kesha toweka tayari, alitafuta dawa na kumeza lakini haikusaidia kwa lolote lile, hakua na chaguo lingine zaidi ya kuondoka ofisini kimnya kimnya na kuingia ndani ya gari ili arudi nyumbani kwake kupumzika ,
Alifika na kuacha gari nje kisha yeye kuingia ndani kimnya kimnya, kwa mbali sana alihisi sauti zina bishana aliweza kuzitambua sauti izo alikua ni Heather mke wake na mwingine aliiitambua sauti ile ilikua ya Zahara .
“Malaya wewe, nilikuamini sana kumbe nyoka tu! una fikiri hapa duniani kuna siri, Rafiki mnafki wewe, umelala na mume wangu Enock, unadhani nisinge jua, hapa mjini nitanyimwa pesa lakini sio maneno”
“usini tukane Malaya mwenyewe usiye jiamini mpaka ukaenda kwa wagamga wa kienyeji kufata dawa, ukaona haitoshi ukaamua kuuwa”
“hata kama lakini haikuhusu , na ndo ivyo hapa Enock apindui uta ishia ivyo ivyo”
Maneno yale yote yalitiririka vizuri na kupita juu ya pina za masikio kisha kuingia mpaka ndani ya ngoma za masikio ya Enock akiwa nje dirishani ameganda kama barafu la shilingi ishirini ,alifikicha macho yake na kuchungulia ndani ili ahakikishe kama ni kweli au ni sauti a mizimu, bado waliendelea kutukanana huku Zahara akizidi kutoa siri za rafiki yake huyo bila kujua walikua wanasikiwa kwa kila kitu.
Picha ya Catherine sasa ilianza kumrudia alijiona mtu mwenye tofauti sana, moyo ulimuuma aliikumbuka siku ya kanisani na kuona sura ya Catherine ikiwa ime jaa machozi, aliikumbuka siku alipotoa kauli kuwa Catherine afungwe polisi,
Bila kusema chochote pale pale aligeuza na kuliendea gari lake akitaka kwenda sehemu moja tu CBE chuo alichokua ana soma Catherine ili aweze kumuomba msamaha, hakuelewa kuwa leo hii yeye ndiye aliye msababishia mwanamke .
huyo atake kujiua, kweli alikiri sasa moyoni alimpenda kwa dhati lakini hakuelewa kua kama juhudi za kumrudisha tena mikononi mwake zingezaa matunda,
Moja kwa moja alinyoosha mpaka posta na kuegesha gari pembeni, ya chuo hiko cha CBE.,
“Samahani namuulizia Catherine Ramsey, yupo”?
“hapana, mwezi huu ume pita hajawahi kuonekana hapa chuoni”
“Betty, Betty , Betty “??
“Betty yupi. Betty Lizzy baby drama?”!
“ndo huyo nafikiri”
“huyo yupo hostel kwao”
Enock alikimbia mbio mbio na kupanda ngazi mbili mbili za hostel hiyo na moja kwa moja kugonga mlango, kwa bahati nzuri alimkuta Betty .
Lakini alifukuzwa kama mbwa, aliji tahidi kumbe-mbeleza na mwishowe kuambiwa sehemu anayo ishi Catherine moja kwa moja alirudi ndani ya gari lake na kuelekea Bunju alipoelekezwa kwa kina Catherine,
Dakika chache baadae alikua ameegesha gari upande wa pili wa geti la rangi nyeusi na kutokua na uhakika kama ndiyo pale,
Aliliona gari aina ya Virgo ya silver inapaki pembeni ya geti hilo jeusi na kijana mmoja wa makamo kushuka kisha baadae kutoka nje akiwa na catherine wakiwa wenye furaha moyo ulimuuma zaidi na kushindwa kuvumilia hasa alivyowaona wana nyonyana midomo yao kimahaba, hakukuwa na haja ya kuulizia nini kina endelea,ilionesha dhairi kuwa wawili wale aliowaona pale walikua ni wapenzi tena wenye mapenzi ya dhati sana, alishindwa kujizuia, wivu ulikua ume mkaa juu ya koromeo lake na kifua kikipanda juu kwa hasira, alifungua mlango wa gari na kuvuka bara bara upande wa pili.
Katika moyo wake hakutaka kumkosa mwana mke huyo tena.
“Catherine”!
Aliita jina hilo na kufanya Catherine ageuke nyuma na kusitisha zoezi la kuingia ndani ya gari..
Alivyo geuka alionana na sura ya mwana ume ambaye alifanya maisha yake yaende ndivyo sivyo, mwana ume ambaye aliye fanya atake kujiua ,mwana ume ambae aliye mtoa bikira yake kisha kumtelekeza na kumuacha solemba, mwana ume huyo huyo sasa alifunga ndoa kanisani na leo ni mume wa mtu,
leo hii ameji tokeza mbele yake, picha mbali mbali za matukio tofauti zilizidi kujiseti ndani ya akili yake huku kumbu kumbu nyingi tofauti zikipita ndani ya ubongo wake na kupenya ndani kabisa ya moyo wake, mwili uli mbadilika rangi ukiwa mwekundu na kuanza kutetemeka kwa hasira sana, midomo ili mcheza na kuji kuta akilia kwa kwikwi pale pale, laiti kama ange kua na bastola mkononi asinge jiuliza mara mbili mbili, ange mfyatua tena ya ubongo ili amuuwe,
“Catherine najua una hasira na mimi, ila naomba usahau yaliyo pita, nakupenda Catherine , tugange yajayo”!
Aliongea peke yake huku Catherine akibaki akimwangalia alivyotaka kumjibu alishindwa sababu alihisi kama kuna kitu kimemkaa kooni kutokana na hasira nyingi kumkaa ndani ya koromeo lake na kusababisha kifua chake kushuka na kupanda juu kwa jazba.
“a…cha..na na m..imi, acha…ana na mimi Toka sitaki kukuona, umeni sababishia matatizo katika maisha y..ngu,, toka Enock”!
Darlington shebby akiwa ndani ya gari alikua ametulia tuli sana, akiwaangalia wawili wale hakua na la kuongea zaidi ya kushuka kwenye gari na kumshika mkono Catherine kisha kumuingiza ndani ya gari,
Kitendo kile hakikumpendeza Enock.
“we una mshika huyu demu una mjua”?
Aliuliza Enock akiwa amemsogelea karibu Shebby akionesha hasira za wazi wazi.
“kwani wewe una mjua”?
“muulize, mimi ni nani”!
“Catherine mpenzi wangu, una mjua huyu”?
“simjui.”!
“ume m-sikia”!
Jibu la Catherine lili kata maini ya Enock na kupata jazba sana. ndani ya moyo wa Shebby alichukulia ule ni ushindi sana, alifurahi sana ila alivyo taka kugeuka na kuondoka alishikwa begani na Enock , alivyogeuka alihisi maumivu makali juu ya pua baada ya kupokea ngumi kali iliyotua yenye uzito, hakukaa sawa alipokea nyingine ya mdomo na kusukumizwa chini pale pale , aliteleza kidogo na kudondoka Puuh!,Kama mzigo kwenye mfereji.
“sipendi dharau mimi, sija wahi kudharauliwa maishani mwangu, nimekaa ulaya miaka mingi sana, wana nijua kule, nime fanya umafia wote .. magenge yote ya kihuni yana nijua kule, mpumbavu wewe,son of a bitch!”
Aliongea Enock akiwa mwenye jazba amesimama , Catherine alishuka ndani ya gari na mbio mbio kumuendea Shebby aliyekua chini kwenye mtaro ameshika pua zake huku damu zikiwa zina mvuja, alimuinua bila kusema chochote na kuingia nae ndani ya gari.
“sikia catherine nikwambie kitu, mimi ndiye nime kutoa bikra yako, najua utarudi tu”
“kwaio ,, bikra ndo nini?, na uliyo fanya hapa sitokusamehe daima, bora nife kuliko kutembea nawewe tena, yaani sahau kabisa toa katika akili yako.. umenielewa Enock”!
“sawa tutaona, mimi na huyo nani zaidi”!
“una maana gani”?
“uta jua tu”
Enock alitembea akiwa na hasira na kuliendea gari lake upande wa pili na kuligeuza kwa mwendo wa kasi kisha kulisimamisha upande wa dereva ambao alikua Darlington Shebby ana hangaika kuwasha gari, ilionekana kabisa ngumi zile zilimuingia vizuri sana!.
“na unisikilize vizuri,huyo demu uta niachia la sivyo natangaza vita nawewe, mpaka naingia kaburini!”
Aliongea Enock na kioo cha gari lake kupanda juu kisha gari kuserereka mbio likiacha vumbi na moshi mwingi pia nyuma yake.
“ UNA SEMA IME KUAJE”?
“wenzangu wote wame kufa”!
“ongea kama mwana ume ongea kwa sauti na utoe maelezo yatakayo niingia akilini mwangu, sio una ongea ongea kwa sauti za chumbani, una nitongoza au”?
“ndo ivyo bosi, tulivyo fika pale hatu kumkuta kuna bwana mdogo mmoja aka tuambia kuwa yupo nyumba ya mbele hivyo alituambia tuingie kwenye gari twende, baada ya hapo akatoa bastola yake, akaanza kurusha risasi”
“uzembe huo, mpaka mtu ana toa bastola , wote wame kufa”?
“ndio nina uhakika huo, sababu alikua analenga saiti za kichwani”
“hadi mpwa wangu Sangusangu amemuuwa”?
“ndio bosi”
Yalikua ni mazungumzo ya mzee wa mwasha na mmoja wa majambazi ndani ya gari, ambaye alitumwa kwenda kumteka Sabrina ili amuuwe, kweli alidhamiria kuteketeza uzao wa Wa Ramsey familia yake yote ndipo atakapo ishi .
kwa amani kabisa, uso wake ulizidi kujikunja kwa hasira sana na kufanya macho yake yawe mekundu, kumbu kumbu mbali mbali za mke wake enzi zao wakiwa wenye furaha zilipita kichwani mwake sasa na kufanya kama historia,alimpenda sana mke wake, hilo alikiri ila alivyo kufa na ndipo alipo zidi kupata hasira, alijua ni mtu mmoja tu ndiye aliye fanya ivyo Ramsey.
Kitendo cha kuuliwa kwa ndugu yake pia ambaye alikua ni mmoja wa majambazi kili mfanya azidi kuingiwa na hasira sana .
“huyo aliye wapiga bastola ni nani”?
“ata kua sijui mume wake, ila namfahamu kama sija kosea”
“kivipi”?
“ni mwandishi wa vitabu ana itwa Eymer Kway, ndio nisha mkumbuka, sura yake haiwezi nitoka, ni mtu maarufu kidogo”
“una jua ana poishi”?
“nita pajua”
“nife mimi afe yeye, lazima ajute, nataka nimuuwe mwenyewe kwa mikono yangu, kaingia kwenye vita isiyo muhusu”
Alisema Mwasha akiwa mwenye macho mekundu, kulikua kuna kila dalili ya kisasi ndani ya maneno yake sababu aliongea huku akiwa amejawa na hasira nyingi sana
“tafuta anapoishi leo hii hii kabla jua halija zama, kesho uende na vijana wengine,Nita mpigia Mhaiki awape silaha!”
“sawa bosi”
“anza sasa hivi shuka kwenye gari yangu”
Mwasha kweli alidhamiria kuua hakuona tena haja ya kuishi kitu alicho kipenda hakikuwa tena duniani, ivyo aliona sawa tu kulipiza kisasi, hakuelewa amfanye nini kway endapo ata mtia mikononi mwake leo hii, alichukua bastola yake na kuikagua vizuri kisha kuiweka vizuri kiunoni na kuchanja mbunga.
Walikua wamegandana midomo yao wakinyonyana ndimi kama njiwa au makinda ya ndege huku wakishikana shikana maeneo mbali mbali ya miili yao, kila mtu alikua akihema mihemo ya juu juu sana kwa mwenzake juu kochi kubwa la seblen, baada ya kutoka kuangalia sinema, kilicho fuata hapo ni kubebana msobe msobe huku njiani wakiendelea kubigana mabusu moto moto,
Tayari wali fika chumbani na Catherine kutupwa kitandani na Darlington Shebby kisha yeye taratibu kuvua shati lake jeupe na kuuvuta mkanda wa suruali na kuutupilia mbali, hisia zao zilikua mbali sana zilikua katika sayari nyingine ya huba,
Catherine akiwa kitandani aliridhia kabisa hakua na sababu ya kuendelea kukaa na maumivu ya Enock moyoni alijua ile ndiyo itakua njia sahihi ya kumsahau, Alisha aamua tayari kumpenda Darlington shebby na kuamua kumpa mwili wake kama zawadi ya kuokoa maisha yake, alijiona mwanamke mwenye furaha
pengine kuliko wote ulimwenguni , alishaya sahau mambo yote aliyo tendewa kipindi cha nyuma, ili mpasa tu asonge mbele, na maisha yazidi kuendelea.,
KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA