BIKRA YANGU (25)

0
Mwandishi: Emmanuel F. Kway

SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO
ILIPOISHIA...
Zahara na Catherine walijikuta wakiita kwa pamoja jina hilo, Mzee Mwasha alishindwa kuelewa na kubaki kuwatizama wote wawili na kushindwa kuelewa mwanae amemjuaje mwana mke huyo na kumuita jina jingine ambalo yeye hakulizoea.
SASA ENDELEA...
Ndani ya moyo wa Catherine alijikuta akiumia sana baada ya kumuona Enock akiwa katika hali ile, machozi yalianza kumlenga lenga lakini hakujua kwanini, hakuamini kuwa mtu waliye mfuata alikua niyeye na kufanya ukimnya utawale ndani ya kituo hiko,kila mtu akishindwa kuelewa nini kinaendelea….


Mbele yake alisimama mzee wa makamo mrefu kiasi mwenye mvi chache sana aliyeitwa Mwasha, pembeni yake alisimama Enock akiwa hana shati anavuja damu,wote walikua wakimtizama yeye ambaye alikua akitetemeka, aliunganisha matukio tofauti yaliyopita juu ya watu hao wawili waliokua mbele yake na kujiona wenda amefumaniwa,alijaribu kuvuta kumbu kumbu za nyuma na Enock wakiwa kitandani,alimtizama mzee Mwasha na kukumbuka matukio tofauti waliyo yafanya awali, ilionekana kabisa ndani ya akili yake kuna mengi alikua akiyafikiria juu ya watu hao wawili waliokua mbele yake wamesimama wame duwaa wakimtizama yeye!.

“Dad, ahsante kwa kunitoa”

Enock aliongea na kumsogelea baba yake mzazi aliye kua mbele yake, moyo wa Catherine ulizidi kulipuka na kumdunda, baada ya kujua kuwa Enock na David ni mtu na baba yake, alijiona ni mtu mwenye dhambi sana kuwa changanya , licha ya hayo yote lakini hakujilaumu sana sababu yeye binafsi hakuelewa, lakini pia aliona ni kama wana mchezea mchezo m-baya,

“huyu ni my last and first born wangu, nafikiri mnajuana kama sikosei,”

Aliongea Mzee Mwasha huku akimtizama Catherine machoni ambae wakati huo alikua akitetemeka kwa hofu nyingi sana.

“Nani!.. Enock huyu anaitwa…..”

“asante kwa kumfahamu naomba niende nina haraka kweli,Suzi utanikuta hostel”

Kumbukumbu za kusalitiwa na Enock zilianza kujijenga ndani ya kichwa chake na kufanya kama filamu, mwanaume aliyemfanya atake kukata uhai wake sasa yupo mbele yake, alishusha ngazi za kituoni hapo na kutafuta bajaji haraka haraka na kuanza safari ya kurudi posta CBE hostel huku machozi yakimlengalenga, kuwachangaya mtu na baba yake alijiona mwanamke mwenye dhambi, pengine aliuona mwili wake hauna thamani. kutokana na mawazo mengi kuwaza kichwani mwake, ndani ya dakika chache alikua teyari kesha fika posta na kumlipa dereva Yule kisha kushuka kama chizi akitembea haraka haraka, alivyo fika tu alijitupa kitandani chali akiwa mwenye mawazo sana juu ya mambo yaliyo tokea muda mfupi ulio pita kituo cha polisi!,

Betty rafiki yake kipenzi alikuja na kumuona rafiki yake alivyokua na mawazo mengi, ilibidi amuulize nini kilicho tokea, bila kufikiria chochote ilibidi Catherine aanze kumueleza kila kitu tangu alivyo kua kituoni na kilicho mfanya awaze, badala ya Betty kusikitika alianza kucheka na kubaki akimshangaa na kutoelewa kilicho kua kiki mchekesha rafiki yake huyo.

“cate unajua nini, natamani mimi ninge kua wewe”

“kwanini una sema ivyo”?

“ninge kua mimi hapo ninge mkubali mzee David ili nimkomoe Yule mwanaharamu mpuuzi, ninge mfanya aniite MAMA, yaani mimi nakushauri ufanye ivyo Catherine, iyo ndo habari ya mjini, mwana ume akikuzingua wewe tembea na baba yake ili akuite Mama, ili akupe heshima, tena na Yule Faisal nayeye simuelewi, nitatembea na baba yake”

“huoni itakua hatari, alafu sasa mbele ita kuaje”?

“mambo mengine utajua mbele kwa mbele”

Betty alizidi kumsisitiza rafiki yake huyo ili aweze kumkubali Mwasha na wamkomoe Enock, mawazo ya rafiki yake sasa aliyaona bora, aliona ni sahihi kufanya vile ili amkomoe Enock aliona kufanya vile atamuumiza sana, japo hakua na uhakika kama jambo alilotaka kwenda kulifanya litafanya kazi, ila wakati mwingine aliona ni bora kufanya vile, potelea mbali alitabasamu na kugonganisha mikono yake na Betty na kucheka kwa pamoja kumaanisha kuwa amekubaliana nae.!

Ugomvi ulizidi kuendelea maradufu ndani ya nyumba ya wanandoa hawa Heather na Enock,walikua ni maadui wakubwa sana ndani ya nyumba yao kama paka na panya! japo waliishi pamoja lakini hakukuwa na maelewano hata kidogo,ilibidi kikao kidogo kiitwe cha familia ambacho kiliwashirikisha wazazi wa pande zote mbili mchana huo wa saa nane na nusu.

Mzee Mpelembe na mke wake walitoka mkoani Morogoro kijiji cha Matombo siku hiyo hiyo na kufika nyumbani kwa mkwe wao Enock baada ya kusikia ugomvi mkubwa sana uliosababisha mpaka watoto wao wapelekane polisi, kama watu wazima ilibidi wakae chini waya zungumze ili wajue nini tatizo, !
Anderson peter na Zahara washenga wao, nao walikuwepo ndani ya nyumba kubwa ya Enock,wakisikiliza kesi hiyo!

“wazazi wangu wa pande zote mbili , nime amua kuwaita hapa, ili mjue kwanini nafanya ivyo,kabla sijaongea mimi naomba Heather mwenyewe aongee kila kitu kilichotokea na akiri makosa yake”

Aliongea Enock akiwa ameibana mikono yake yote miwili huku akiwa ameiweka kwenye kidevu chake akiiongea taratibu kwa upole sana..

Heather aliye kua pembeni yake na tumbo kubwa teyari alisimama na kuanza kulia kwa uchungu wote na kufanya kila mtu amuonee huruma mwanamke huyu mjamzito mwenye tumbo kubwa, kila mtu alimuangalia kwa macho yaliyo jaa simanzi!.

“Enock amenikosea sana, amenikosea sana! Nime mvumilia mengi sana kama mke, ameni….tesa sa…na nampenda sana mume wangu, tangu siku ya harusi yetu hapo mwa,,anzo tuliishi vizuri, ila baada ya kurudi huku sikuwa namuelewa amekuwa mlevi, ana kuja na wana wake ndani,ananipiga kama mbwa kila siku, mimi kama mke nilimvumilia sana ,akaona haitoshi akaamua kutembea na rafiki yangu kipenzi Zahara huyu hapo, inauma sana walikua wakilala hapa kisha kuniacha mimi seblen nang’atwa na mbu,nilivumilia yote hayo kama mwanamke, sikutaka kumwambia mtu kuogopa kuiweka ndoa yangu mashakani, alafu na kitu kingine kinachoniuma zaidi wananisingizia mimi ni mshirikina na wamenikuta kwa mganga nikifanya nae mapenzi!, alivyo rudi nyumbani siku iyo asubuhi, nilivyo muuliza akaanza kunipiga sana mpaka nika poteza fahamu,….”

Maneno aliyokua akiongea Heather kwa mtu yoyote Yule ambaye aliyemuona aliona ni mwana mke anaye onewa sana na ange muonea huruma sana, mama yake aliyeitwa Chiku alidondosha chozi alijua ni jinsi gani mwanae alikua akipata mateso ndani ya ndoa yake, bila kujua ulikua ni uwongo mtupu,
Mzee Mpelembe tayari alishapandwa na jazba na kumkata jicho kali Enock ambaye kwa wakati huo alikua ameachama midomo yake wazi na kushangazwa na maneno yale kutoka kwa Heather

Ukimnya wa hali ya juu ulitokea ndani ya seble ile huku kwa mbali kilio cha kwikwi kusikika kutoka kwa Heather, kila mtu alimuonea huruma Heather aliye kua akiongea huku akibubujikwa na machozi mengi yaliyofanya mashavu yake yalowe na kuchuruzika mpaka kifuani! .

“wewe mwana haramu, umelazimishwa kumuoa huyu eee, wewe mwana izaya usiyekuwa na haya wala aibu, shwetani mkubwa,,leo hii tunaondoka na mwenetu hajaua sawa”!

Aliropoka mama mzazi wa Heather huku akiongea na kutema chembe chembe za mate mithili ya mvua.

“jamani naomba upunguze jazba Mama,hatujaja kubomoa hapa, tumekuja kujenga, Enock mwanangu usiongee chochote mimi namjua Heather miaka mingi sana, naamini anayosema hapo sina uhakika sana kama anayoongea yana uwongo, sijui lakini, naomba umuombe msamaha ili yaishe,nyie ni wana ndoa hii ni mitihani ya ndoa,Enock wewe ni mwanangu upo peke yako,tabia za marekani usilete hapa Afrika, naomba uombe msamaha sasa hivi, mbele ya wazazi wake”

Maneno hayo aliongea Mzee Mwasha akiwa amesimama.

Enock aliya bana meno yake kwa hasira bado katika akili yake alikua anajishauri ni nini akifanye alimtizama Heather kwa hasira na kuonesha kuna kila aina ya dalili kuwa ni lazima angefanya fujo.

“broo sikia, kubali yaishe, usifanye kitu chochote cha kijinga, jifanye fala tu utaharibu”

Alizungumza mshenga wake Anderson peter kwa sauti ya chini sana huku akiwa ameushika mkono wa Enock uliokua umekunja ngumi huku ukiwa na jasho jingi la hasira na kumfanya atetemeke

“bora niharibu wajue moja nimeharibu kaka kuliko kukaa kimnya underson, this is bullshit, anaongea uwongo huyu!”

“haifai haifai,kama una nisikiliza mimi usifanye ivyo Enock, ona hawa wazee wote wapo hapa, watakupa laana uta muaibisha dingi yako, mwanaume wa kweli mwanzo hujifanya fala, ila baadae huonekana mjanja”

Enock bado alikua na hasira wote walimtizama yeye alipo, wakisubiri aombe msamaha kwa aliyo yafanya, ilimbidi tu asikilize ushauri wa rafiki yake na kusimama, taratibu alisimama na kuongea akiomba msamaha japo kua moyoni aliumia sana kuomba msamaha kwa kitu ambacho hakuwahi kukifanya kamwe!

Aliwaomba msamaha wote waliomzunguka kisha kumfuata Heather na kumkombatia ila ndani ya moyo wake alikua bado ana hasira nae kama simba aliye jeruhiwa na mkuki.

“Enock siwezi kukusamehe, mpaka unihaidi kuwa utakaa mbali na huyu mwanamke shetani hapa, nihaidi mbele ya watu wote hutorudia kutembea nae,”

Alipayuka Heather na kujitoa mikononi mwa Enock huku akizidi kulia kwa sauti kama mtu aliyeonewa sana.

Enock alimtizama Heather na kupepesa macho yake kwa kila mmoja aliyekua ndani mule na kushusha pumzi ndefu sana ya kuchoka alijutia sana kukiri kosa lake mbele ya kadamnasi, sasa aliona ni wakati wa Heather kumpelekesha sana.

Ilimbidi tu Enock akubali yote mbele ya jopo lile la wazee na kufanya roho ya Heather kutulia.

Mawasiliano kati ya Mwasha na Catherine yalizidi kuendelea kila siku na kupamba moto mwisho wa siku mzee huyo kufanikiwa kuwa nae kimapenzi, alijiona mshindi sana na ndani ya moyo wake alitaka kufunga nae ndoa hakujali umri wala chochote kile, jambo la kufunga ndoa na Catherine lilikua ndani ya akili yake , lakini hakuona ni jambo la busara kufanya vile bila kumtambulisha mtoto wake Enock kwa mwanamke huyo ambaye atamuita mama baada ya mama yake mzazi Josephine kufariki dunia.

Tayari walikua ndani ya nyumba kubwa ya mzee Mwasha wakimsubiri Enock, ndani ya akili ya Catherine alijua ujio wa Enock siku hiyo asubuhi na mapema akiwa amevalia kimini chake na kufanya kalio lake litokee kwa nyuma na kuchonga kimlima kilichosambaa na kutengeneza hips kwa pembeni, na mapaja yake laini kuonekana, ili mfanya azidi kuwa na mvuto sana,

Enock tayari alikua njiani akiwa na kihoro sana cha kumuona Mama yake mpya, alifurahi sana na kuamini kuwa baba yake atarudi kuwa mwanaume mwenye furaha sana, aliendesha gari huku mara kadhaa akimpigia baba yake akimwambia kuwa yupo karibu kufika, pembeni yake alibeba zawadi kubwa sana ya kuwakabidhi baba na mama yake huyo mpya na hakua na roho ya kinyongo kuhusu hilo,

Bila kujua kuwa upande wa pili, mwana mke huyo ni Catherine mwanamke anayempenda kutoka moyoni mwake,mwanamke ambaye aliye mtoa bikira yake,

Alifika mpaka nyumbani kwa baba yake na kuegesha gari kisha kubeba mfuko mkubwa uliokua na zawadi ndani yake, alifika na kugonga mlango kisha Baba yake kumfungulia mlango akiwa mwenye furaha sana meno yote nje,“Mamiii”!

KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)