BIKRA YANGU (26)

0
Mwandishi: Emmanuel F. Kway

SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA
ILIPOISHIA...
Alifika mpaka nyumbani kwa baba yake na kuegesha gari kisha kubeba mfuko mkubwa uliokua na zawadi ndani yake, alifika na kugonga mlango kisha Baba yake kumfungulia mlango akiwa mwenye furaha sana meno yote nje,“Mamiii”!

SASA ENDELEA...
Mzee Mwasha aliita na kufanya mwanamke aliye kua jikoni atoke na kumtizama Enock akiwa anatabasamu,!

Moyo wa Enock ulimwenda mbio sana, ndani ya akili yake alitafsiri jambo lile ni kama maigizo kwake ,alipigwa na butwaa huku akitetemeka sana alimuona Catherine akimsogelea baba yake kisha kumshika kifua chake,

“Enock my son, huyu unaye muona hapa utamuita Mama, nimekaa muda mrefu sana nikiwa mpweke mwanangu, nimeona huyu binti japo ni mdogo wa makamo yako ila ndiyo chaguo langu, naomba umuheshimu kama unavyoniheshimu mimi,au kama ulivyokua ukimuheshimu marehemu Mama yako”

Maneno aliyokua akiongea Mzee Mwasha hayakuonesha aina yoyote ile ya kuwa na masihala ndani yake, kila aliloliongea alilimaanisha, sababu alikua amemshika kiuno Catherine huku mikono ya Catherine ikiwa ina chezea kifua cha mzee huyo, bila kujua maneno yale yalikua yakimchoma sana Enock ndani ya moyo wake, lakini Catherine alishaligundua hilo,!

“Enock, kuanzia leo utaniita Mama kama alivyo sema baba yako,”

Aliongea Catherine bila utani akiwa mkavu bila kucheka na kumtizama Enock machoni huku mkono wake mmoja ukiwa juu ya kifua cha Mwasha kisha kumbusu mdomoni..

Mambo yanayo tokea mbele yake siku hiyo hakuyaamini, maneno yaliyo tamkwa na baba yake yalimchoma ndani kabisa ya mtima wake, mwanamke huyu aliye simama mbele yake, aliye mpenda kutoka moyoni mwake, ambaye alishawahi kuwa mpenzi wake siku za nyuma sasa ana mahusiano ya kimapenzi na baba yake mzazi,bado alikuwa amepatwa na ngekewa akiwa tizama watu waliokuwa mbele yake kimahaba tena wakinyonyana midomo yao, alitizama chini kwa aibu na kutoelewa ni nini akifanye, akili yake ilicheza kama umeme na kujua yale ni malipizo kutoka kwa Catherine na wala sio vinginevyo,

“Nashukuru kukufahamu Mama!”

Ilibidi aitikie ili baba yake asihisi chochote kitu, ilikua ni lazima afanye mambo taratibu ili kurudisha mapenzi kwa msichana huyu Catherine ambaye alikua chaguo la moyo wake, lakini sasa hivi baba yake alimwambia amuite Mama,haikuwa kazi rahisi hata kidogo !

Catherine alimtizama Enock machoni na kumuona jinsi gani alivyokua anaweweseka, alijua ni lazima atakua ameumia moyoni, kwake yeye swala lile lilikua ushindi tosha na kufurahi moyoni mwake bila kujua kuwa anafanya mambo ya hatari,

Mzee Mwasha hakuelewa nini kinaendelea kati ya Enock na Catherine hata kidogo aliwaacha na kupanda ngazi na wawili hao wakiwa wanaangaliana.

“stop acting crazy, what are you doing Catherine?(acha uchizi,sasa una fanya nini)?, unadhani nitaumia wala siumii I don’t care(sijali)”

“kwani una taka nini Enock, nieshimu mimi mama yako.”

“ishia hapo hapo koma, wewe ni mpenzi wangu tena bado nakupenda”

“umechelewa sasa Enock, sahau yaliyo pita ndo ukweli huo, na baba yako anataka kunioa”

Walizungumza kwa sauti za chini chini sana kama waliopanga kuiba kitu, pale pale mzee Mwasha alitokea huku akitabasamu kwa furaha na wote kumgeukia na kumwangalia sababu ilionesha alikua na jambo ambalo alitaka kuongea.

“Enock mimi na mama yako tutaenda Brazil, wiki tatu zijazo nimeongea na Benja Ngowi, sasa nilikua naomba usisamie kila kitu hapa nyumbani”

Hakujua yale aliyoyaongea yalizidi kuukoroga ubongo wa Enock na kumfanya azidi kuchanganyikiwa akili yake.

“Samahani Mr. mkeo kwa bahati mbaya ujauzito aliokua ameubeba umeharibika kutokana na kupata mishtuko mingi tofauti,

ivyo ilipelekea ukuta wa uzazi kupasuka kabla ya siku zake. Ina bidi tulisafishe tumbo lake mapema, pole sana”

Maneno hayo yalichomoka kutoka kinywani mwa Dokta huyo kama mishale ya moto na kupenya ndani ya moyo wa kway, alikua ameketi huku machozi yakimlenga lenga alimtizama daktari Yule na kuvuta kiti kwa nyuma bila kuongea chochote, alitembea mpaka wodi alilolazwa Julia na kukaa pembeni ya kiti huku akimtizama mke wake kipenzi kwa macho yaliyo jaa huruma.

“unaweza kuwatambua watu waliokuchukua ukiwa ona sura zao”?

“tumuachie Mungu tu Mume wangu, tutapata mtoto mwingine, nashukuru Mungu nipo Bien,hayo ya pembeni tumuachie yeye Muweza wa yote”!

Aliongea Julia akiwa juu ya kitanda hiko ndani ya hospitali ya wilaya ya Tanga mjini, licha ya kuongea maneno hayo lakini Kway hakutaka kukubaliana na hilo, bado alikua na kinyongo dhidi ya watu wabaya waliofanya unyama kwa mke wake mpaka kupelekea ujauzito wake kuharibika kabisa,

alisimama na kumuendea mtoto wake Natu kisha kumbeba mikononi mwake hakika aliipenda sana familia yake na kuhakikisha kuwa atailinda mpaka siku ya mwisho atakapo fukiwa mavumbini.

Kadri siku zilivyo zidi kwenda ndipo hali ya julia ilizidi kuwa sawa, madaktari walisha msafisha tumbo lake na kurudi katika hali ya kawaida,waliruhusiwa na kuanza safari ya kurejea jijini Dar es salaam,

Kway alionesha mapendo yote kwa mkewe sababu kipindi hiko ndipo alipo hitaji faraja pekee kutoka kwa mumewe na ivyo ndivyo alivyo fanya na upendo kuongezeka mara dufu,siku zilienda sasa na mke wake kurudi katika hali ya kawaida akiendelea na majukumu yake ya biashara,

Siku moja kway akiwa ofisini kwake alipigiwa simu na Sabrina kuwa ana hitaji kuongea nae, ni mazungumzo ya muhimu sana, hakukua na haja ya kipingamizi, alifika mpaka ofisini kwake kariakoo TRANSCONTINENTAL PUBLISHERS na kukaribishwa mpaka ndani kisha kuketi mbele ya kiti kilicho kua cha wageni.

“nambie Sabrina una mpya gani leo”?

“Kway, sizioni siku zangu nilienda hospitali jana kupima nikakutwa nina ujauzito”

“sasa mimi sina kipingamizi chochote kile, ina kubidi ukae na huyo baba wa mtoto muongee, mambo mengine sio mpaka uniambie mimi Sabrina,ni wakati wako wa kutafuta maisha yako,Ramsey Alisha fariki tayari hakuna jinsi nyingine ya kufanya mimi sioni kama una kosa hapo”!

“kway huja nielewa kitu kimoja,”!

“kitu gani tena”?

“nina wasi wasi mkubwa sana kuwa hii mimba ni yako, siku ile tulivyo lala wote nilikua katika siku mbaya za kushika mimba”

Kway aliya toa macho yake akimtizama Sabrina aliyekua mbele yake, jasho jembamba lilianza kumtoka japo kulikua kuna kiyoyozi ndani ya ofisi hiyo,

“embu acha mambo ya masihala masihala bwana, mimba hiyo ina ingia ingiaje siku moja?, alafu kumbuka mimi ni mume wa mtu, nina familia”

“kwani mimba ina ingia siku ngapi,usijifanye mtoto Kway, nimekuja hapa ili tujue tuna fanya nini, nina uhakika hii ni yako sijawahi lala na mwanaume yoyote kwa kipindi kirefu zaidi ya wewe”

Maneno aliyokua akiongea Sabrina hayakuwa na utani ndani yake kabisa, Kway alionesha kuchanganyikiwa sana hakutaka jambo la kuzaa nje ya ndoa yake litokee. Alijilaumu sana kufanya tendo la ndoa na mwanamke huyo alizilaumu sana pombe, aliamini kua endapo angekua sawa siku iyo asinge kubali, alibaki akimtizama Sabrina machoni.

“nita mueleza nini mke wangu Julia, kwanini usiitoe?”

“sitaki kupata dhambi kway, siwezi kuitoa,tutafute njia nyingine hapo lakini sio ya kuua, ni dhambi kubwa.”

“sasa umekuja hapa kufanya nini?, umekuja kuniambia kuwa una mimba au umekuja kutaka kujua tuna fanya nini”?

“vyote vyote”

“ujue usiichanganye akili yangu, hapa ilipo ina mambo chungu mzima!”

“nakuchanganya vipi sasa,mimi ndo ivyo Kway,”

Aliongea Sabrina kwa kujiamini sana,

Mzee Mwasha tayari Alisha fika uwanja wa ndege huku pembeni yake akiwemo Catherine pamoja na Betty rafiki yake kipenzi wakisubiri shirika la ndege la Fly emirates ili waanze safari yao, kushoto kwake alisimama mzee wa makamo mwenye mvi chache aliye fahamika kwa jina Benjamin Ngowi,
alikua ni tajiri aliyekua na maduka mengi sana hapo kariakoo alikua na kampuni ya kutengeneza viatu iliyoitwa NGOWI LEATHER GOODS ,hakuna asiye mfahamu mzee huyu wa kichaga aliye kua pia na maduka MWIKA,ROMBO MKUU mpaka kibororoni na machame pia lakini kuiona elfu kumi yake ilikua ni kazi kubwa alikua mbahili mno!, alikua ni tajiri na ndiye huyo pia alikua mwenyeji wa huko nchi ya Brazil,.

“kama nilivyokwambia Dear, huyu ni rafiki yangu nili soma nae Marangu lakini baadae akaenda nje ya nchi ni rafiki yangu sana, yeye ndiye aliye nifundisha biashara”
“asante kwa kukufahamu”!

Aliitikia Catherine huku akimpa mkono mzee huyo, Mr, Mwasha nia ya kumpeleka Catherine Brazil ilikua ni moja tu kufanya nae mapenzi katika nchi hiyo kwa mara ya kwanza, alikua na furaha sana moyoni mwake,catherine na Betty wazazi wao walijua wapo chuoni wakijisomea kumbe walikua na safari ya kwenda nchini Brazil, tena kwa mara ya kwanza kupanda ndege alikua na hamu sana, alikua amependeza mno siku hiyo huku mara nyingi akiwa ana tabasamu na kufanya uzuri wake uonekane mara mia machoni mwa watu.

“Dad”

Sauti hiyo ilisikika na kufanya Mr, Mwasha ageuke, alimuona Enock akiwa na begi dogo amelishika mkononi huku pembeni yake akiwa na marafiki zake watatu wakiwa na mabegi, walionekana kabisa ni watu walio taka kusafiri pia.,

“samahani siku kwambia, namimi nili kata tiketi ya kuelekea Brazil, ili nikafurahi nanyi, hawa ni marafiki zangu, nafikiri tupo safari moja.”

Aliongea Enock huku akimtizama Catherine kwa macho ya kuibia.

“ni vizuri mwanangu , tena umefanya jambo la maana sana”

Aliongea Mwasha huku akiwa na furaha bila kujua ndani ya kichwa cha Enock nini anawaza, kipaza sauti kilisikika kuwa ndege ya Fly emirates ipo tayari ivyo abiria wapande, Enock aliburuza mabegi yake akiwa amevaa kaptula yake nyeupe na kuweka miwani yake nyeusi vizuri machoni,waliingia mpaka ndani na kugonga mihuli passpot zao kisha kuingia ndani ya chumba cha wasafiri kwa ajili ya ukaguzi wa mwisho,baada ya hapo tayari walikua wana panda ngazi za ndege hiyo kubwa ambayo baada ya masaa machache ingetua DOHA na kubadilishiwa ndege nyingine,

Enock muda wote alikua akimuwaza Catherine sababu bado alimpenda sana, kipaza sauti kiliwaomba wafunge mikanda sababu ndege inaanza kuondoka,

“Catherine embu tupige selfie hapa moja tupo kwenye pipa, niweke DP”

“umeanza sasa Betty”

“inahusu, watajuaje kuwa nimepanda ndege”

Betty alianza kupiga picha nyingi nyingi na kuweka kwenye mtandao wa watsap akiwatumia marafiki zake.

Taratibu ndege ilianza kutembea kisha kuchanganya mwendokasi na baadae kunyanyuka ikipaa angani, baada ya ndege kuwa hewani Catherine alisimama na kuelekea chooni, Enock alimuona na kumtizama baba yake kama anamuona nayeye kumfuata Catherine kwa nyuma alivyoingia chooni nayeye aliingia.

“Enock una taka kufanya nini”?

“hujui au”

“embu niachie, nitapiga kelele, unataka kunibaka”

“piga tu”!

Enock alimkamata Catherine kiuno chake kwa mikono miwili na kuanza kumlazimisha kumyonya mdomo wake, na kufanya ubishi uanze kutokea, bado Catherine alikuwa mbishi kukubaliana na kitendo anachotaka kufanya Enock.

“Catherine, nakupenda sana, sipo tayari kukuona unatembea na baba yangu labda nikiwa nime kufa,”

“wewe si una mke?”

“I don’t care, una jua kilicho tokea”?

“sitaki kujua”

Enock alimkamata Catherine vizuri na kupeleka mdomo wake taratibu mdomoni mwa Catherine.
“baby”!

Sauti nzito ilisikika kutokea nje ya mzee Mwasha akiwa anagonga mlango wa chooni ndani ya ndege hiyo na kuwafanya waanze kuogopa.

KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)