BIKRA YANGU (27)

0
Mwandishi: Emmanuel F. Kway

SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA
ILIPOISHIA...
Sauti nzito ilisikika kutokea nje ya mzee Mwasha akiwa anagonga mlango wa chooni ndani ya ndege hiyo na kuwafanya waanze kuogopa.
SASA ENDELEA...
“kwanini uliniua, kwanini umeukatisha uhai wangu?”

“toka, toka unataka nini?,”

“basi namimi lazima nikuue kabla hujataka kufanya mambo mabaya kwa mwanangu, unataka kumuuwa na mwanangu ili uuze hii nyumba hutoweza, mimi ndiye mama yake, nitailinda hii nyumba.. ha! Ha! Ha! Ha! Ha!ha!ha!”

ilikua ni sauti ya Mama Enock akiwa na shuka jeupe mwili mzima akimkimbiza Heather usiku usiku huku akiwa na tumbo lake kubwa baada ya kufika mbele alidondoka kama mzigo, alivyoangalia nyuma hakumuona tena mama Enock aliyekua akimkimbiza!,aliinuka na kuanza kutembea tena ila mbele alikutana na mama huyo ambaye alifanya njama za kumuua lakini leo hii akiwa anasumbuliwa sana,

Heather alizidi kukimbia kama mwenda wazimu akiomba msaada barabarani lakini kila mtu alimpita wakimuona wenda ni kichaa au mwehu.

“uwii mama Enock anataka kuniuaa, jamani nisaidieni, anataka kuniua jamani, jamani naomba msaada wenu”

Alikua amesimama barabarani akipunga mkono ila magari yote yalimpita na kumuacha pale alipo.
“ha ha h ha ha ha ha ha “

Sauti ya Mama Enock ilizidi kusikika ikicheka huku ikijirudia rudia kama sauti yenye mwangwi ilikua ni picha ya kutisha sana kwake. Kumuona mtu aliye kufa tena, alikimbia mbio mbio mpaka nyumbani kwa Zahara usiku huo huo bila kuogopa kiza hilo totoro, na kugonga mlango alivyofika tu nje, japo kua hakua na uhakika kama atapata msaada kwa rafiki yake huyo ambaye walishagombana sana kisa Enock!

“shosti nakimbizwa”

“na nani”?

“Mama Enock, naomba niingie kwanza ndani, huyo anakuja huyo anakujaaaa uwiiiiii”

Alizidi kuogopa Heather na kumsukumiza Zahara ambaye alikua keshaanza kuogopa sana sababu usiku ulikua ni mnene

“huyo Mama Enock yuko wapi si kesha kufa tayari”?

“ndio, ila ila leo kanitokea nilikua nje pale ya nyumba sa..sa”..

Upepo wa ghafla mithili ya kimbunga ulianza kupuliza na kurusha vitu vilivyokua ndani seblen hapo na kumtupa Heather pembeni na kumpigiza ukutani ulimchukua tena na kumtupa chini,na kumfanya aanze kuvuja damu mwilini mwake, Zahara kuona vile alifungua mlango na kutafuta njia yake sababu aliona mambo ya ajabu sana.

Josephine au Mama Enock akiwa anavuja damu mdomoni alimsogelea Heather huku akiwa mwenye hasira sana, alimfuata kohoni na kuanza kumkaba Heather.

“Mamaaaaaaaaaaaaa”

Alikurupuka kitandani kutoka katika njozi ya kutisha aliruka mpaka kwenye switch na kuiwasha taa, alivyojishika kichwa chake alihisi maumivu makali sana na kuzidi kutetemeka kwa hofu, ndani ya jumba hilo alikua peke yake, Mume wake Enock alimuaga amesafiri kikazi bila kujua kuwa alikua safari moja na Catherine,

Hakupata tena usingizi alikaa kitandani kitako mpaka kuna kucha kisha kumpigia Simu Fredy Kiluswa ambaye alikua akihitaji kununua nyumba hiyo,

aliona ni bora auze nyumba ya Enock nayeye apotelee mitini ili hata kukosa wakose wote kabisa, hiko ndiko kilichokua kikicheza ndani ya akili yake

Mzee Fredy kiluswa teyari alikua akitembezwa ndani na nje ya nyumba hiyo kubwa sana na Heather.
“una uza hii nyumba milioni mia tano”?!

“ndio milioni mia tano”

“Mbona pesa ndogo sana ukilinganisha na nyumba yenyewe,”?

“nina matatizo, mume wangu alifariki ghafla. Alafu alikua anadaiwa bank, hapa nina watoto wanne wana nitegemea, si unajua ni mama wa nyumbani sina kazi, matatizo ndo yana nifanya niuze nyumba, pia kuna magari kama unataka nayo nayauza vile vile!”

Maongezi yalizidi kuendelea na mwisho wa siku walifika tamati na Heather akisubiri malipo ya nyumba ile ili akimbie mbali sana.

“akija Enock atajuta shenzi mkubwa, mimi ndio mtoto wa mjini, yeye si kaishi marekani, sasa mimi ni mtoto wa kigogo mburahati, kafua dafu, ataonja joto la jiwe”!

Aliongea Heather mwenyewe baada ya kuagana na Fredy Kiluswa kisha yeye kuingia ndani na kupanga nguo zake kwa ajili ya kuondoka zake endapo dili lake likikaa sawa, kumiliki milioni mia tano kwake ilikua kama ndoto.

“DAD THAT MAN, DAD THAT MAN!”

“una tatizo gani Natu,”?

“Dad that Man”

Aliongea Natu akiwa anachagua viatu na nguo ndani ya GAME mlimani city baada ya kumuona Mwanaume mmoja pembeni yake akiwa anachagua chagua vitu,alijificha nyuma ya baba yake Kway na kuonekana akiwa mwenye hofu sana, alimchukua mwanae kisha kumbeba upande wa kulia na mkono mmoja.

“Dad that Man, Dad he is the one, Dad that MAN!”

Bado Natu aliendelea kusisitiza huku akisonta kidole kwa mwanaume aliye kua mita chache mbele yao, Kway alimuangalia mtu huyo huku akimkazia macho na kumuona kama aliyekua na wasiwasi baada ya kugonganishana nae macho, kweli hata yeye alimkumbuka alikua ni koplo Mwita, ambaye kipindi cha nyuma ndiye alikua ana msaidia kutafuta familia yake,ilionekana kabisa mtoto mdogo NATU alikua akikumbuka kitu kibaya sana sababu alificha sura yake na kuanza kulia, kupitia macho ya mtoto wake aligundua kuna kitu ndani yake,lakini hakujua ni kitu gani.

Alivyoangalia tena upande alipokua amesimama koplo Mwita hakumuona tena na ndo hapo alipoanza kumtafuta ndani ya supa maket hiyo akiangaza huku na kule.

“oyaaa Ngesa kale katoto nimekaona, ndio ndio , Yule uliye mteka na mtoto wake, kanijua nielewe basi, isha kua soo kubwa, ndio nakusikiliza. Ndio ndio, enhee, nisikilize fala wewe, yupo na baba yake nadhani, . Kale katoto inabidi tu tukaue sababu ndiye peke yake aliona sura yangu.fanya ivyo sasa, mimi nitaseti mipango subiri. Okay poa poa”.

Aliongea Koplo Mwita kisha kuingia ndani ya gari na kuchapa mwendo, Alisha gundua teyari mtoto mdogo Yule aliikumbuka sura yake,

ivyo ilikua ni lazima afanye jambo ili apoteze ushahidi huo ambao unge muweka jela kwa kosa kubwa sana. Ivyo ilibidi afanye mambo taratibu sana kama kamanda wa polisi kwake swala lile lilikua dogo sana.

Kwa mbali aliona gari la koplo Mwita likiishia getini na kumshusha Natu chini ambae alikosa raha kabisa kumbu kumbu za mama yake akiteswa na kupigwa tumboni zilianza tena kujijenga kichwani mwake na kuanza kulia tena kama mtoto aliyeachishwa kunyonya maziwa ya mama yake.

ilikua ni picha mbaya sana kwake, picha ya koplo Mwita haikuweza kumtoka ndani ya kichwa chake, na ndiye huyo aliye mpiga ukofi mtoto huyo na kuzimia.

“Natu una nini mwanangu”?

“Da….d am scared. Please take me home..nirudishe nyumbani namtaka Mama”

“hutaki tena nguo?”

“chitaki nirudishe nyumbani Dad sasa hivi!”

“nawewe msumbufu kama mama yako”

Ilibidi tu Kway ambebe mwanae na kuingia nae ndani ya gari lakini bado alimuhoji mwanae maswali ni kitu gani kilicho mfanya aanze kulia peke yake, Natu hakua na jibu la kumpa zaidi ya kulia kwa kwikwi.

Walifika nyumbani na kumkuta Mke wake julia ana andaa chakula cha mchana ambapo baada ya hapo, alitokea Loyda na ugeni kuongezeka walionekana kuwa wenye furaha sana siku hiyo wakila mezani na kufurahi mno.

“Kway yaani umefanana na mwanao kila kitu, atakuja kuwa mtundu kama wewe, yaani kweli mkeo hakucheza faulo”

Alizungumza Loyda huku akimtizama Natu ambaye alikua akilishwa na Mama yake ugali.!

“wee acheze faulo hapa pangetosha unadhani!, angekula mtu vikombe vitasa vichwa mpaka kieleweke”
“ha ha ha ha una vituko wewe”

“Dad nini maana ya kucheza Faulo”?

NATU aliuliza na kufanya watu wote mezani wacheke sababu hawakutegemea kama angeuliza swali hilo.

“kucheza faulo mwanangu maana yake ni ku … kuu…”

Kabla ya kumalizia sentensi mlango uligongwa kisha baadae watu waliovalia mavazi ya kipolisi kuingia na nyuma yake alisimama mwanamke mmoja mnene kiasi akiwa analia sana.

“Mama ndiye huyu”?

Mmoja wa maaskari aliuliza

“ndio ndio ndi..o yeye”

Mama Yule alimtizama Kway na kuitikia, hakuna mtu aliye jua nini kinachoendelea kila mtu aliacha kula na kumtazama mwana mke Yule,

Julia alimdaka mwanae na kumshika vizuri mikononi mwake, ukimnya ulitawala sauti iliyosikika hapo ilikua ni ya mama huyo aliyekua akilia kwa uchungu kama aliye fiwa na mume wake.

“ndi..o ndi..o huyu alimbaka mto..to wangu alimtishia na Bastola yak…e. Nash….dwa kuelezea”

Mama huyo aliongea kwa uchungu sana, Kway hakuelewa kinachoendelea kilicho fuata hapo maaskari wale walimfuata na kumvuta kwa nguvu na kumuweka ukutani kisha kuanza kumsachi baadae walichomoa bastola yake iliyokua kiunoni na kumfunga pingu kwa nyuma.

“wewe una jifanya mbakaji sio, sasa utaenda kuonesha ulijari wako mbele huko.una jua kesi ya kubaka wewe?”

Kitendo kile kilifanyika ndani ya Sekunde mbili na kumfanya kila aliye ndani akae kimnya,

“niachieni kwanza sielewi mnaongelea nini,?,

nime mbaka nani, mbona mnanifunga pingu kama jambazi, hiyo ni sheria ga….”

Pale pale Kway alipigwa na kitako cha bunduki mdomoni na damu nyingi kama mchuzi kuanza kumvuja kwenye lips zake, walimsukumiza ndani ya defender haraka haraka na gari kutoa vumbi nyingi, na kumuacha mke wake akilia ndani ya moyo wake, kila mtu alikua amepigwa na butwaa!

“BABY subiri kidogo”

“muda wote huo are you okay”?

“nipo sawa usijali honey”

Alijibu Catherine huku Enock akiwa kimnya sana ndani choo kile kwenye ndege, baada ya hapo walitoka na kila mtu kufika kwenye kiti chake na kukaa!,

Ndege hiyo kubwa ilizidi kutoboa mawingu angani, walifika DOHA na kubadili ndege ambayo ilianza safari nyingine kuelekea Brazil,usiku kucha ndege ilikua angani, baadae ilisikika sauti kuwa wafunge mikanda sababu ndege iyo inaenda kutua kiwanja cha mji wa Brasilia asubuhi hiyo,. hapo ndipo Mwasha na wengine walitakiwa kushuka, baada ya ndege kutua, walianza kushuka taratibu ngazi,
walitoka nje,ulikua ni mji mzuri sana hali ya hewa ilikua tulivu mno, magorofa marefu sana kwenda juu, na kumfanya Catherine astaajabu. Betty kazi yake ilikua ni kujipiga selfie tu muda wote na kuwarushia marafiki zake watsap, na kuziweka instagram, baada tu ya kuweka vocha.

“wapi hiyo mama”?

“nipo Brazil, Nasra”

“mmmh mmmh, Brazil tena”?

“ndio Brazil, Brazil nipo huku na mdosi mmoja ana pesa huyo balaa, we kaa tu Zanzibar ule karafuu mimi nakula maisha”

“sasa mmeenda kufanya nini?”

“kula bata”

Betty alikua akichat baada ya kufika nje ya uwanja wa ndege na kusubiri kita kacho fuata,

hawakuamini baada ya kuona LIMO mbili nyeusi na nyeupe zikiwa zime fika mbele yao,zilikua gari ndefu aina ya benz zenye milango nane ambazo mara nyingi hutembelewa na maraisi au MATAIKUNI wenye pesa zao,. LIMO zili simama mbele yao kisha mwanaume mmoja wa kibrazili aliye bana nywele zake kwa nyuma aliyejitambulisha kwa jina la Franco, aliwapokea mizigo yao na kuiweka ndani ya boneti la nyuma.

“welcome to brazil(karibuni Brazil)”

“thank you”(nashukuru)

Enock na wenzake waliingia kwenye Limo ya nyuma huku baba yake, Betty,Catherine na Ngowi waliingia kwenye Limo ya rangi nyeupe kisha safari hiyo kuanza, ambapo dereva huyo alionekana kabisa alijua ujio wa ugeni huo,

KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)