Notifications
  • MY DIARY (39)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA TISATULIPOISHIA...Nilikuwa na furaha sana huku nikiamini kuwa ndoto zangu za kuja kuwa mtu maarufu zinaweza kufanikiwa hata kabla ya kuyapata yale madini. Sikutaka mbwembwe niliamua kuikopi na kuipesti hiyo stori kama ilivyo na kuifowadi kwa Mark.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Baada ya kama lisaa hivi Mark alipiga na kuniuliza kama kweli ilikuwa nai mimi nimetunga hiyo…
  • MY DIARY (38)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA NANETULIPOISHIA...Usiku nilishituka usingizini baada ya mbu kuning’aata na kunisumbua sana. Niliwachukia sana hao mbu kwa sababu walinikatisha ndoto yangu ambayo nilikuwa nikiota.Ndoto ilikuwa ikielezea jinsi harusi yangu na Mark itakavyokuwa. Ndoto ilikuwa tamu sana maana ilinipa taswira ya picha halisi ya maisha yangu ya mbeleni.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nilishusha neti…
  • MY DIARY (37)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA SABATULIPOISHIA...Hapo alitulia tulii kama mtu aliyeaamia dunia ingine. Kimoyo moyo nikawa najisemeha kama amehamia dunia ingine na kuanza kuwaza ujinga sahuri yake mimi nipo kazini bwana acha nitafute hela. Ndio ni lazima nifanye kazi kwa utaalamu na utundu wa hali ya juu ili waendelee kusimuliana huko mjini ili niendelee kupata hela.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Wewe…
  • MY DIARY (36)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA SITATULIPOISHIA...Sasa wewe fikiria mimi niliyeletewa zawadi sikujua ni zawadi gani lakini yeye tayari alishafungua na kuchungulia na kujua nini kilifungwa huko ndani.Basi nikaendelea kumuhudumia yule mama huku na yeye akiniambia kuwa itabidi nikimmaliza hizo zawadi tusifungue hapo hapo na waniimbie wimbo wa happybirthday.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Tuliendelea na stori mbili…
  • MY DIARY (35)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA TANOTULIPOISHIA...Tatu niliambiwa kuwa ndugu zake na wazazi wake walihusika kwenye mipango hiyo hivyo walibariki kabisa huyo binti kuniacha mimi mumewe wa ndoa na kuamua mtoto wao aolewe upya. Nne ni kwamba huyo mzungu amewaamishia wazazi wake mjini na amewajengea nyumba ya kifahari.Kwa hiyo mimi ninavyowapigiana simu na kuwajulia hali kumbe wenzangu huwa wananichora tu.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (34)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA NANETULIPOISHIA...Hapo nikakumbuka kuwa zile zana zangu za kazi nilikuwa nazo ni vile vifaaa vya kupimia ukimwi ambavyo huwa navitumia kabla ya kukutana na mwanaume yeyote nisiyemfahamu. Nikaamua kumkubalia huku nikiamini kuwa hiyo ndo kinga yangu pekee iliyobaki kama mwanaume huyo atataka kuzini na mimi usiku huo.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Basi tuliondoka na kwenda sehemu…
  • MY DIARY (33)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA TATUTULIPOISHIA...Nilikuwa nachanganya staili za kijamaika na hizi za kwetu, sikuacha pia zile za Nigeria hapo nikapata vitu vyangu vya tofauti kabisa. Basi baada ya kujihakikishia kuwa nipofiti kwa mastahili yangu hayo nilisubiri siku ya shindano ifike nikafanye yangu. Siku ya shindano ilifika na mimi nilikuwa miongoni mwa washiriki walioingia tatu bora.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (32)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA MBILITULIPOISHIA...Lakini kuchepuka kwangu na kuingia mgombani haikumaanisha kuwa sheria ingeniacha hivi hivi.Ilifika mahali ikabidi nizime gari na kutulia tulii kusikilizia nini kitafuata.Tayari nilikuwa nimezungukwa na mapolisi ambao walikuwa wakinifuatilia kwa kutumia pikipiki.Kwa bahati nzuri dereva wa lile gari na yeye alishafika hapo na alishawaambia polisi kuwa mimi naugua ukichaa na nilifufuka kutoka mochwari.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA…
  • MY DIARY (31)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA MOJATULIPOISHIA...“marehemu pia alinieleza kuwa ana miliki duka la vitu vya urembo wa kike ambalo pia Leah analisimamia ila hilo apewe mdogo wake Marry ambaye yupo hapa. Mama mdogo huyo mara baada ya kuyasema hayo alikaa zake chini. Baba mdogo ambaye hakurizika na maelezo hayo alisimama na kusema “kwa hiyo kama marehemu alijua kuwa atakufa hivi karibuni kwani nini hakufuata taratibu za kisheria za kuandika wosia na kurithisha mali.IKIWA UNASOMA…
  • MY DIARY (30)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINITULIPOISHIA...Baada ya hapo Nnilimwomba mama mdogo ajikaze na kuwatarifu ndugu wengine habari hizo za msiba.Tulisaidiana hivyo hivyo maana sio siri kila mmoja alikuwa na uchungu sana kutokana na mazingira ya kifo hicho. Habari zilizidi kusambaa kwa kasi na majirani walianza kukusanyika hapo kwa mama mdogo.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Msiba ni msiba tu na ukitaka kujua binadamu…

BIKRA YANGU (30)

Mwandishi: Emmanuel F. Kway

SEHEMU YA THELATHINI
ILIPOISHIA...
Catherine aliita huku akitizama chini baada ya kumuona nyoka mkubwa akitambaa aina ya
Python mwenye mabaka mabaka meusi akija mbio usawa wao,
SASA ENDELEA...
“hapa kuna mawili kway utoe milioni kumi kesi ifutwe au tuendelee na kesi”?

“nashindwa kuelewa Sabrina, lazima nitoke humu ndani, japo niudhurue msiba wa mwanangu”

“sasa ina kubidi ufanye ivyo mimi nita toa millioni tatu,nime kupigania sana, hii kesi yako ilikua unaenda jela, nime muomba sana Yule mama anataka hiyo pesa niliyokutajia”

“niende vipi jela wakati sio kitu cha kweli”?

“hapo mimi sijui sasa,”

“poa nitatoa, kamwambie nipo tayari”

Yalikua ni mazungumzo kati ya Sabrina na Kway huku akiwa ndani ya nondo amechoka kabisa, mawazo na mateso vilishatafuna mwili wake wote na kubadilika kabisa na kumfanya hata ngozi yake iote ukurutu, kutokana na kutooga siku kadhaa zilizo pita,

Baada ya kupata pesa zile ilibidi tu kway aachiwe huru hii ni kutokana na Mwita kumaliza ushahidi baada ya kuagiza vijana wake wamuuwe mtoto wake Kway aliyeitwa Natu,

Shukrani alizozitoa kwa Sabrina hazikuweza kuelezeka kwa maneno, alifika kwake na kumkuta mke wake bado akilia sana huku akitaja jina Natu, haikuwa kazi rahisi kumtuliza mwanamke huyu ambaye ilionekana aliguswa sana na kufiwa na mtoto wake, kilicho muuma zaidi ni jinsi alivyo uwawa kwa kukatwa mapanga na kufanya kiwili wili wala kichwa kisi onekane, waliweza kuutambua mkono tu.

Kway alisogea na kujumuika na mke wake huku wakilia kwa uchungu,majirani ndugu na jamaa hawakuwa mbali, walikusanyika nyumnbani kwa Kway kimara kwa msuguli na kuzidi kumfariji kwa yaliyo mtokea,

kila mtu alimuonea huruma mwanaume huyo ambaye walitafsiri huo ulikua ni kama mkosi kwake.

“Kway jikaze kaka, ni mitihani ya Mwenyezi Mungu, wewe ni mwana ume, usilie usilie,”

Alikua ni rafiki yake kipenzi aliyeitwa Chesta mkurugenzi wa kampuni za Mamodo jijini Arusha, baada ya kupokea taarifa hiyo aliruka mara moja na ndege na kufika Dar es salaam ili kumfariji rafiki yake huyo,

licha ya ivyo nayeye pia alijikuta akitoa leso na kujipangusa machozi yaliyokua yakimtoka, huku Kway alikua akilia mke wake Julia sasa alishazimia mara nne kila akiamka alikua akizimia tu na kuzidi kulia,watoto wawili sasa Alisha wapoteza mmoja aliyekua tumboni na mwingine Natu, wamama kwa wasichana walikua pembeni yake wakimpepea na kanga zao,hakika msiba wa mtoto huyo Natu ulimgusa kila mtu sababu bado alikua mdogo mwenye ndoto nyingi hapo baadae.

Jeneza lililetwa lakini hawakuweza kuuwaga mwili wake sababu haukupatikana, safari ilianza siku iyo saa tisa mchana na costa mbili kutafutwa na safari ya kwenda mkoani Kilimanjaro kuanza,

kesho yake asubuhi walifika Moshi kijijini Mwika na tararibu za mazishi kuanza huku wakimpumzisha mtoto mdogo Natu kwenye shamba la Kway ambalo lilikua na migomba na kahawa nyingi.!

“oyaa Ngesa, usimuuwe huyo mtoto”
“una wazimu nini”?

“kuna dili nataka nikupe”

“acha wazimu huyu mtoto lazima tumuuwe, Mwita ndo katoa hilo agizo”

“nisikilize Ngesa,nisikilize mimi, Mwita hatokusaidia kitu, kuna dili la pesa ndefu sana,haka katoto kazuri, kuna jamaa anaitwa Don Mullosi Jah Gwan. mtu wa jamaica, ananunua watoto wa kike wadogo kwa pesa ndefu alafu anaenda kuwachezesha muvi chafu”

“una ongea utumbo wewe,Joel”

“aya shauri yako”

Gari ilizidi kwenda kasi huku nyuma ya siti akiwa Natu amelala baada tu ya kuchomwa sindano ya usingizi ili alale hakuelewa kinachoendelea,

Joel alimtizama NATU siti za nyuma na kuvalisha bastola yake kiwamba kinachozuia sauti za bastola zisitoke bila Ngesa kujua, baada ya kufanya ivyo aliiweka vizuri kiunoni,

Walisha fika Mto msimbazi usiku huo wa saa saba, na kumtoa Natu nje kwa nia moja tu wamuuwe, ilakatika kitendo cha ghafla Joel alitoa bastola yake na kumfyatuaya kichwa pale pale Ngesa,alichokua anakiwaza kichwani kwa wakati huo ni kutengeneza ela nyingi kupitia Taikuni Mulosi ambaye alikua ni raia wa Jamaica anaye fahamika kwa kuwa na madanguro ya wanawake machangudoa nchi mbali mbali za Afrika Mashariki,japo alijifunika na mwavuli wa biashara ya kusafirisha mafuta ya kupikia na unga pia, hakuweza kugundulika kabisa kirahisi.

Joel alifanya haraka haraka na kumtupa Ngesa kwenye maji ya mto msimbazi kisha kuondoka na Natu, aliiivua saa ya mtoto huyo, kishaa baada ya siku chache alinunua maiti ya mtoto iliyo kua haina ndugu kisha kuivalisha saa ile na kuikataka taka, baada ya hapo aliivalisha saa ya Natu na kufika posta na kuitupa pembezoni kabisa ya bahari,

Kila alilolifanya alifanya kwa akili nyingi kupindukia,

Tayari alianza kufanya mazungumzo na Mullosi ambaye alimtupia picha ya Nattu kwenye mtandao., na kuanza kupatana bei na kufikia dolla elfu tatu zilikua ni pesa nyingi sana kwake yeye kwa kazi ndogo kama hiyo, hakuelewa kuwa wazazi wa mtoto huyo walikua wakilia machozi wakidhani amekufa tayari,

“kesho nita kuja kumchukua uwanja wa jommo Kenyatta Kenya tukutane pale, fanya ivyo”!
Upande wa pili wa simu kutoka kwa Mullosi ulisikika kisha simu kukatwa.

Bado wivu wa mapenzi ulizidi kumfanya Enock apiganie penzi la mwanamke Catherine ilikua ni lazima arudishe penzi lake kutoka kwa mwanamke huyo aliye kiri kuwa ni mrembo sana,
moyo wake uliruhusu kuinua kinywa chake na kutamka ukweli wa mambo, ili baba yake ajue, kuliko yeye kubaki na maumivu ya ndani kwa ndani,

Baba yake akiwa mwenye jazba amesogea karibu yao kitendo cha kumuona Enock kumlazimisha kumpiga busu catherine kilimuuma sana na kujenga picha mbaya tofauti ndani ya mtima wake.

“Enock… nini unafanya, unavuta bangi siku izi?, au umelewa”?

“Dad sija lewa wala sijavuta bangi, nataka kukwambia ukweli”

Aliongea Enock huku akimuachilia Catherine taratibu na kumfuata baba yake mzazi kwa nia moja tu amwambie ukweli wa mambo na kupasua jipu., Mkojo kwa mbali ulianza kumbana Catherine na kuanza kuogopa sana kwa kitendo anachotaka kukifanya mwanaume huyu Enock aliyekua kiburi asiye ogopa kitu…

Mwanamke Heather alizidi kuteseka sana siku zake za kujifungua zilisha fika na sasa kuanza kusikia uchungu tumboni mwake ni baada tu ya kupata ahueni, ndugu zake walisha fika hospitalini hapo kumuona ili wajue anaendeleaje, kila mtu aliyemtizama alimuonea huruma jinsi alivyochoka na kuchakaa kabisa, mawazo na mateso aliyo kua akiyapata yalisha kula mwili wake wote na kubakisha macho na kichwa peke yake,

Hii ilitokana na kutokewa na mama Enock kila wakati, alitamani kufungua kinywa chake ili azungumze kile kilicho mfanya ateseke lakini hakuweza hata kidogo , kufungua kinywa chake ilikua ni sawa na kujitia kitanzi au kwenda jela kufungwa kifungo cha maisha, ili m-bidi akae kimnya atulie na maumivu yake.!

Kitanda chenye magurudumu kilikuja mbele yake nayeye kuwekwa juu yake na safari ya kuelekea leba kuanza huku akiwa na maumivu mengi tumboni,licha ya yote hayo alikua ni mwenye furaha sana siku hiyo baada tu ya kuambiwa anaenda kujifungua mtoto,

“jikaze shangazi jikaze, kuwa mwanamke jasiri”

Alizungumza shangazi yake aliyeitwa Rehema akizidi kumpa moyo Heather, kwao waliona ni ushindi sana,

Kitanda kilifika mpaka mlangoni na madaktari bingwa kuingia haraka haraka ndani ili kuweza kumzalisha mwanamke huyo Heather,

“Pushhhh”!

“push, bana pumzi zako”

Muuguzi wa kike alizungumza huku akiwa amekinga mikono yake kati kati ya miguu ya Heather akisubiri mtoto atoke tumboni,jasho jingi sana na uchungu ambao haukuweza kuelezeka ulimkuta Heather, lakini alijikaza kisabuni, alibana pumzi zake na kujikamua kama aliyekua anatoa haja kubwa huku jasho jingi likimtoka mwilini mwake,

alihisi kitu kigumu kina toka kati kati ya mapaja yake , ilikua kidogo manesi wakimbie, kila mtu alishtuka ndani ya chumba hiko na hofu kuzidi kuwa tanda,mmoja wa manesi alidondoka chini na kupoteza fahamu zake pale pale baada tu ya kuona kiumbe cha ajabu kikitoka tumboni mwa Heather, kilitangulia kichwa chenye nywele nyingi sana huku kikiwa kina mikono mirefu na kucha ndefu sana, kila mtu alistaajabu kabisa,

Heather alikua amechoka kimnya ana tabasamu kwa mbali sana kwa kujifungua salama, alijipongeza moyoni mwake, hakuelewa kuwa kuna muuguzi amezimia chini na kuona kiumbe cha ajabu,

“ng”aaa ng”aaaa”

Mtoto huyo alianza kulia kwa sauti kubwa sana, hakika unge bahatika kumuona mtoto huyo hata wewe ungedondoka chini na kuzimia kama sio kukimbia,

Kilikua ni kitu cha ajabu chenye kuweka historia hapo hospitalini,

“Mama mtoto wako huyu hapa”

Dokta Amir alijikaza kisabuni na kumkabidhi mtoto Yule Heather huku akiwa amemfunika na kanga,
Heather Alitoa tabasamu na kumbeba mtoto wake ila baada tu ya kumwangalia nayeye alishtuka na kumtupa chini na pale pale kuzimia baada ya kuona kiumbe hiko,sababu hakutegemea hata yeye.!

BAADA ya mazishi kuisha mkoani Kilimanjaro wakiamini kuwa mtoto wao Natu amefariki dunia, wazee wa kichaga walimkalisha kway na kuchinja mbuzi wawili kama mila zao za kichaga zinavyotaka zifuatwe, waliamini kuwa mtoto wao amepatwa na mkosi au balaa na kumpa Baraka zote,

Hawakuelewa kuwa mtoto wao kwa wakati huo ana pangiwa mipango mibaya ya kupelekwa nje ya nchi akachezeshwe filamu chafu za ngono, lakini licha ya yote walimuachia Mungu sababu yeye ndiye muweza wa kila kitu,

Baada ya taratibu zote za matanga kukamilika. Kway na mke wake Julia waliwasha gari na kuanza safari ya kurudi jijini Dar es salaam wakiwa hawana furaha hata kidogo,

Walifika usiku wa siku hiyo wakiwa wamechoka sana na kuanza kufanya juhudi za kuanza kutafuta mtoto mwingine kila siku ipitayo kwa Mungu,

lakini haikuwa rahisi kama alivyodhani,

“inatubidi tujaribu tena Mke wangu, najua leo upo siku za hatari”

“sawa”

Siku iyo tena walikula tunda la usiku kwa malengo na kwa nia moja tu kujaribu kutafuta mtoto mwingine,

Mwezi sasa ulipita bila kuona dalili yoyote ya Julia kushika mimba, ili bidi tu wanyooshe moja kwa moja hospitalini ili kuweza kujua nini tatizo,

Habari zilikua mbaya sana taarifa hizo zilionekana kumchanganya sana Kway na kutoelewa kama anasikia vibaya au anaota.

“mkeo ana ugonjwa unaitwa pyelonephritis deases, hii imetokana na mirija ya Fallopian kuziba ivyo inapelekea mbegu kutofika kwenye ovary na kutungisha yai, nina maana kwamba mkeo itachukua muda mrefu sana kupata mtoto au ataweza kuwa tasa kabisa”

Majibu hayo yaliukondesha moyo wa Kway Julia alipiga kelele za kilio na kushindwa kuelewa nini afanye.

“lakini dokta tulishawahi kupata mtoto inakua kuaje unavyo niambia ivyo, au mpime tena vizuri itakua umechanganya majibu, wakati mwingine binadamu tuna kuwa na mambo mengi, tuna pitiwa”
Kway alijitahidi kubadili ukweli,

KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

14 Bikra Yangu Simulizi
Jiunge kwenye mazungumzo
Chapisha Maoni