BIKRA YANGU (31)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA THELATHINI NA MOJA
ILIPOISHIA...
“lakini dokta tulishawahi kupata mtoto inakua kuaje unavyo niambia ivyo, au mpime tena vizuri itakua umechanganya majibu, wakati mwingine binadamu tuna kuwa na mambo mengi, tuna pitiwa”
Kway alijitahidi kubadili ukweli,
SASA ENDELEA...
“hapana nime mpima mara mbili mbili, najua kuwa alishawahi kushika mimba,nime mpima na x ray pia ina onyesha kuwa kuna uchafu wa damu iliyo vulia tumboni na majeraha, sina uhakika kama hajawahi kuanguka au mtu kumpiga maeneo ya tumboni”
Kumbu kumbu zake zili mpeleka moja kwa moja kwa majambazi waliowahi kumteka mke wake na kumtesa sana, hasira na chuki vilizidi kujijenga ndani yake na kumfanya ayabane meno yake.
“kweaio hatoweza kushika mimba”?
“sijasema ivyo lakini itachukua muda sana, nita mpa dawa za kutumia”
“ahsante dokta”
Walitoka ndani ya chumba hiko wakiwa wenye huzuni mwingi na kurudi kupumzika nyumbani.
“happy Birthday Natu”
“Dad Dad thank you, DaD YOU’RE THE best Dad I love you, Noo Dad Mom anakula keki yangu mimi chitaki”
Alikua ni kway usiku huo akiangalia mkanda wa video wa mtoto wake huku akilia machozi, alijiona alivyokua akipakwa keki usoni na mtoto wake huku wakiwa wenye furaha na mke wake Julia siku hiyo ya sherehe alipokua akitimiza miaka mitano wakiwa nchini Malaysia,
Alijikuta akilia na kuzima t,v ile sababu alihisi bado uchungu moyoni mwake.
“sasa kway, mbona nashindwa kukuelewa”?
“kunielewa kivipi?”
“hujui, hujui kuwa nina mimba yako au unajitoa fahamu”?
“sasa ndo umeamua kuni fuata mpaka nyumbani”
“ndio! naona hunipigii simu, hupokei simu zangu, nimeamua kuja”
Sabrina alizidi kupayuka kwa sauti huku akiwa mwenye jazba nyingi sana mdomoni, alionekana kabisa alimuwekea kway maneno mdomoni mwake na sasa aliamua kufunguka,
Julia akiwa dukani alirudi kimnya kimnya na kusita kidogo baada ya kusikia malumbano hayo, akiwa dirishani aliweza kusikia kila kitu na kuanza kulia machozi ya uchungu sana.
Bila kuongea chochote aliwapita na baadae kutoka na mabegi yake mkononi, dalili zilionesha kuwa alikua akiondoka mazima.
“mke wangu unaenda wa…”
“funga, nyamaza niache niende kwetu, siyauwa”
Aliongea Julia akiwa mwenye machozi machoni mwake na kuzidi kuburuza mabegi.
Catherine alizidi kutetemeka kwa hofu sana baada ya Enock kumsogelea baba yake mzazi na kutaka kupasua jipu lililokua lina muuma siku nyingi sana.
“Dad huyu ni mwana mke wangu, kama ulikua hujui nakwambia leo hii hii, nampenda sana,”
“lini umeanza kuvuta bangi na kukosa heshima mpuuzi mmoja huna akili,blood full, huo umalaya umerithi wapi, huyo ni mama yako, nilishakwambia tangu siku ya kwanza huyu ni mama yako, sijui hiyo tabia ya umalaya umeitoa wapi, umeitoa wapi, pumbavu zako mkosa adabu mimi sina tabia hiyo, hiyo tabia najua umerithi kutoka kwa mama yako, Mama yako ndiyo alikurithisha hiyo tabia ya umalaya ya hadi kutamani mke wa baba yako mzazi,”
Maneno aliyokua akiongea Mwasha baba yake mzazi na Enock yalikua makali sana na kumfanya Enock azidi kupandwa na hasira mno,alishindwa kuzizuia hasira zake na kuchanganya na wivu aliokua nao, baada ya kusikia mama yake anazidi kutukanwa alijikuta ana kusanya nguvu na kukunja ngumi na kumtwanga baba yake mzazi ya mdomo pale pale na kumfanya aende chini na kudondoka chini kama mzigo puuh!
Biashara chafu inazidi kutikisa nchini Tanzania watoto wa kike walizidi kupotea katika mikoa mbali mbali na kufanya hofu kuzidi kutanda sana ndani mioyoni mwa wazazi wenye watoto wa kike, bado hali ya sitofahamu inazidi kuzua gumzo na kujijenga ndani ya mioyo ya kila mtanzania,kesi zilizidi kila kukicha, kila mwana mama sasa alikua makini na binti yake wa kike, wazazi walizidi kugongana vikumbo vituo vya polisi kufungua majarada juu ya upotevu wa watoto wao wa kike wadogo kwa wakubwa.
“Mama ulisema mtoto wako anaitwa nani”?
“anaitwa Linda, ana miaka ishirini na mbili”
“hii wiki inakuaje kuna mfululizo wa watoto wa kike kupotea hapa kuna kitu lazima, alipotea lini”?
“tangu juzi hajaonekana nyumbani nilimtuma dukani basi hakurudi tena”
Mama Linda alizidi kutoa maelezo yake kituoni huku akilia kwa uchungu, bado jeshi la polisi lilizidi kuumiza kichwa sana na bongo zao, hawakuelewa ni kwanini tukio hilo lina tokea, ulinzi ulizidi kuboreshwa ili wakamate mtandao huo unaoteka mabinti bila kujua nini wanachokitaka,ivyo ndivyo ilivyo kua bila kuelewa kuwa kuna mtandao mkubwa sana hapo nyuma wenye nguvu,
“unamuonaje huyu”?
“huyo safi sana, embu nitumie picha yake akiwa amesimama”
“ahaaa poa poa, sasa hivi subiri niichukue facebook”
Baada ya dakika chache picha ilitumwa ya mwanamke mrembo sana akiwa amekamilika na mwenye makalio makubwa kiasi.
“nime muona huyo atafaa sana”
“kwaio , subiri nipe muda kidogo kila kitu kitaenda sawa”!
Yalikua ni mazungumzo kupitia mtandao, huku picha ya Catherine Ramsey ikirushwa kumaanisha kuwa anatakiwa kwa gharama yoyote ile kutokana na uzuri wa kipekee aliokua nao,
walizidi kufanya mawasiliano baada ya kuhafiki na kupatana bei sasa ilibaki kazi moja tu kumtafuta Catherine Ramsey kwa wudi na uvumba.
“Julia unaenda wapi sasa!,yaka tusolola Mama Natu(njoo tuongee Mama Natu)”
Alizungumza kway huku akiwa nyuma ya mke wake huyo akijaribu kumshika mkono na kuzuia mabegi yake asitoke nayo nje, hakujua kama juhudi zake zingezaa matunda ilikua sio rahisi kumtuliza mwanamke wake akiwa na hasira,
Hilo alilijua ila kama mume ilibidi ajishushe ili amruhusu shetani aende zake.
“kisa mimi sizali si ndio sawa tu, tikanga nazo kyende,restre avec ta pite(niache niende,baki na Malaya wako).
Aliongea akichanganya lugha ya kwao lingala na kifaransa huku akilia machozi mengi, iyo iliashiria ni jinsi gani alikua mwenye hasira,alijiona hana thamani tena mbele ya mume wake kutokana na kutokuzaa kwake, hiko ndiko kilicho kua kichwani mwake kwa wakati huo ni baada tu ya kugundua kuwa Sabrina kashika mimba ya mume wake,ilikua ni bora aende zake kuliko kuendelea kubaki nyumbani hapo. akiwa mwenye machungu mengi, hilo lilikua ni pigo jingine tosha,ndoa haikua tamu tena ilikua ni shubiri alijilaumu ni kwanini alikubali kuja Tanzania, alishindwa kuongea na kubaki kulia kwa kwikwi.
“pardon Mama Natu(nisamehe Mama Natu), nita kuelezea kila kitu kilicho tokea”
“Kway niache mi yangu nijiendee, ni…ache”
Aliongea na kumsukumiza kway kisha kuendelea kuburuza mabegi yake mpaka nje na kuanza kuyapakia ndani ya gari huku bado akilia machozi na kuongea lugha ya kwao akionesha hasira za wazi wazi na kumwambia mlinzi wa getini afungue geti ili yeye atoe gari.
“Masai acha usifungue geti”
“em..bu nif..ungulie wewe Masai”
“Masai usifungue geti”
Julia kuona vile alishuka ndani ya gari na kulifungua geti kisha kurudi ndani ya gari na kuliwasha, alitia milango lock, huku akimuangalia mumewake aliyekua nje akiomba msamaha lakini yeye aliona kama ni unafki,
Sabrina aliyekua pembeni alianza kujuta sana kwa kitendo alicho kifanya kilicho sababisha ugomvi mkubwa uliokua ukiendelea juu ya wanandoa hao,!
Hakuamini alichokiona baada ya kumuona Kway amesimama na kutanda mbele ya gari ili kutoruhusu Julia asilitoe gari nje,
“piii piiiiii”
Honi ya gari ilisikika mara mbili na kilicho fuata hapo ni gari kutolewa kwa kasi sana, Sabrina hakuamini alichokiona baada ya kumuona kway kagongwa na gari na kutupwa upande wa pili,
hakuamini kuwa mke wake Julia ana hasira kiasi kile na kufikia hatua ya kumgonga mume wake.
Masai aliyekua getini alishika kichwa baada ya kumuona bosi wake yupo chini akilia machozi yaliyo changanyika na maumivu makali sana,
Aliinua kichwa chake na kushuhudia mke wake Julia akiishia bila hata kupunguza mwendo kasi wa gari na kutokomea akiacha vumbi kwa nyuma yake.
“juliiaaaaaaaaaa”!
Aliita kway huku akilia machozi mengi, Sabrina aliyekua juu kibarazani ilikua ni kama anaangalia filamu ya kihindi yenye kusisimua sana na starring wa picha hilo alikua shurkhan!,
Alibaki chini akiwa na maumivu mengi sana alivyotaka kusimama alirudi tena chini baada ya kuhisi maumivu makali sana mguu wa kulia,alimkata Sabrina jicho kali sana lenye kuonesha chuki na maumivu makali mengi.
Alisimama tena kwa hasira na kupapasa kiuno chake na kufanya Sabrina aingiwe na hofu sababu alijua nini maana yake, alielewa sasa ni kifo ndo kina fuata tena cha kupigwa risasi.
Alivyo papasa kiunoni hakua na bastola yake kweli alidhamiria kumpiga risasi mwanamke huyo aliyesababisha balaa. alikua sio yeye tena zilikua ni hasira sasa, alinyoosha mpaka ndani na baadae kurudi na bastola yake mkononi lakini hakumuona tena Sabrina.!
“yuko wapi, wewe masai yuko wapi Yule mwanamke?”
“amesakimbia bosi amesakimbia, ametoka nje, nimkimbise?”
Kway aliachia misonyo na kurudi ndani huku bado akiwa mwenye hasira sana kupita kiasi.
Vitz ya rangi ya bluu ilizidi kukoleza mwendo ndani ya gari alikua mwanamke Julia huku akilia machozi mengi yaliyojaa hasira sana na kufanya yamzibe machoni aliyapangusamachozi yake na kutoa simu yake ya mkononi.
“yaya Bo…..zi na..zoya Lobi na airport ya ndjili(kaka Bozi naomba uje kunipokea kesho uwanja wa ndege ndjili).
Alizungumza Julia huku akiwa analia sana na kuongea kwa kigugumizi akijaribu kuficha hisia zake moyoni!.
“problem ezala nini?,(kuna tatizo gani”) nipo Lubumbashi mbona unatoa machozi uko nini umefanya sasa julia,?”
“kuja nitwala iyo Kes….ho yaya. Ikol….”
Hakuweza kumalizia maneno anayoongea kutokana na kulia sana. hakuweza kujua kua taa za rangi nyekundu zime waka hapo ubungo mataa kuashiria kuwa asimamishe gari ili magari mengine yapite kama sheria za barabarani zilivyowekwa,ivyo alipita kwa kasi sana, tipa la michanga lililokua linatokea upande Gongo la mboto kuelekea mwenge likiwa kwenye kasi sana, lilipiga honi mfululizo na kuonekana dereva Yule kushindwa kulisimamisha tipa hilo kwa wakati huo,
Kilicho tokea hapo zilikua ni kelele za watu na wengine kushika kichwa, ilikua ni ajali mbaya sana sababu vitz aliyokua akiendesha Julia ilisagika vibaya mno ikiwa uvunguni mwa tipa,raia walioshuhudia ajali ile hapo ubungo walianza kutokea ili kujua kinachoendelea kama kawaida ya wabongo, wenye simu zao walitoa ili wapige picha na kurushiana katika mtandao wa watsap,
Walichoona pale zilikua ni damu zime tapakaa kwenye lami ilikua ni ajali ya kutisha ambapo usingeweza kuiangalia mara mbili kama ulikua na moyo mwepesi.
Ngowi aliingilia ugomvi ule ambapo Mwasha alikua akipigana na mwanae Enock kisa mwanamke Catherine, kila mtu alimpenda sana mwana mke huyo hakuna hata mmoja aliyetaka kumuacha kirahisi na kutengeneza chuki kati ya mtu na baba yake.
“huyu ni mwanamke wangu, alishawahi kuwa mpenzi wangu”
Alizungumza Enock huku akiwa ameshikwa na Ngowi akitaka kujitoa.
“Enock”!
Catherine aliita huku akimzabua kofi kali lililolia kwa nguvu sana, kitendo kile haki kumfurahisha hata yeye na ili bidi afanye vile kuzuga kwa wakati huo!.
Mzee mwasha Alisha pandwa na hasira sana na kuzidi kumlaani mwanae.
KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni