Notifications
  • MY DIARY (42)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA MBILITULIPOISHIA...Uzalendo ulinishinda ikabidi nimuulize ni kwanini bado wanatumia njia hiyo ya kizamani kutunza kumbukumbu wakati siku hizi kuna kitu kinachoitwa Human Resource Informaion system ambapo kumbukumbu zote za wafanyakazi kama waliochishwa kazi, wagonjwa, walioenda likizo ,waliopandishwa vyeo na taarifa nyingine muhimu uhifadhiwa kwa kutumia komputa.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (41)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA MOJATULIPOISHIA...Mark anashangaazwa sana na mwanamke huyo lakini kwa kuwa shida yake ilikuwa ni hela anaamua kuachana nae na kuanza maisha mapya hapo jijiini Dar es salaamMaisha yanaendela lakini Mark amekuwa tajiri na mtu mwenye mafanikio sana kiuchumi.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Pamoja na mafanikio hayo ni mtu ambaye mapenzi bado yalikuwa yakimuumiza siku hadi siku.Filamu…
  • MY DIARY (40)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINITULIPOISHIA...Alikuwa akinyata kwa kweli. Kweli hata mimi nilimkubali tu siku ya kwanza ingawa bado nilikuwa sijajua ufanisi wake wa kazi.Nilikaa nae hapo kwangu kwa mda wa siki tatu huku asubuhi tukiamka na kuendelea na kazi.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Ndani ya mda huo nikagundua kuwa alikuwa na uzorfu mkubwasana hivyo kazi hiyo alikuwa akiimudu kabisa.Hapo sasa nilimkubali sana…
  • MY DIARY (39)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA TISATULIPOISHIA...Nilikuwa na furaha sana huku nikiamini kuwa ndoto zangu za kuja kuwa mtu maarufu zinaweza kufanikiwa hata kabla ya kuyapata yale madini. Sikutaka mbwembwe niliamua kuikopi na kuipesti hiyo stori kama ilivyo na kuifowadi kwa Mark.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Baada ya kama lisaa hivi Mark alipiga na kuniuliza kama kweli ilikuwa nai mimi nimetunga hiyo…
  • MY DIARY (38)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA NANETULIPOISHIA...Usiku nilishituka usingizini baada ya mbu kuning’aata na kunisumbua sana. Niliwachukia sana hao mbu kwa sababu walinikatisha ndoto yangu ambayo nilikuwa nikiota.Ndoto ilikuwa ikielezea jinsi harusi yangu na Mark itakavyokuwa. Ndoto ilikuwa tamu sana maana ilinipa taswira ya picha halisi ya maisha yangu ya mbeleni.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nilishusha neti…
  • MY DIARY (37)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA SABATULIPOISHIA...Hapo alitulia tulii kama mtu aliyeaamia dunia ingine. Kimoyo moyo nikawa najisemeha kama amehamia dunia ingine na kuanza kuwaza ujinga sahuri yake mimi nipo kazini bwana acha nitafute hela. Ndio ni lazima nifanye kazi kwa utaalamu na utundu wa hali ya juu ili waendelee kusimuliana huko mjini ili niendelee kupata hela.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Wewe…
  • MY DIARY (36)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA SITATULIPOISHIA...Sasa wewe fikiria mimi niliyeletewa zawadi sikujua ni zawadi gani lakini yeye tayari alishafungua na kuchungulia na kujua nini kilifungwa huko ndani.Basi nikaendelea kumuhudumia yule mama huku na yeye akiniambia kuwa itabidi nikimmaliza hizo zawadi tusifungue hapo hapo na waniimbie wimbo wa happybirthday.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Tuliendelea na stori mbili…
  • MY DIARY (35)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA TANOTULIPOISHIA...Tatu niliambiwa kuwa ndugu zake na wazazi wake walihusika kwenye mipango hiyo hivyo walibariki kabisa huyo binti kuniacha mimi mumewe wa ndoa na kuamua mtoto wao aolewe upya. Nne ni kwamba huyo mzungu amewaamishia wazazi wake mjini na amewajengea nyumba ya kifahari.Kwa hiyo mimi ninavyowapigiana simu na kuwajulia hali kumbe wenzangu huwa wananichora tu.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (34)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA NANETULIPOISHIA...Hapo nikakumbuka kuwa zile zana zangu za kazi nilikuwa nazo ni vile vifaaa vya kupimia ukimwi ambavyo huwa navitumia kabla ya kukutana na mwanaume yeyote nisiyemfahamu. Nikaamua kumkubalia huku nikiamini kuwa hiyo ndo kinga yangu pekee iliyobaki kama mwanaume huyo atataka kuzini na mimi usiku huo.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Basi tuliondoka na kwenda sehemu…
  • MY DIARY (33)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA TATUTULIPOISHIA...Nilikuwa nachanganya staili za kijamaika na hizi za kwetu, sikuacha pia zile za Nigeria hapo nikapata vitu vyangu vya tofauti kabisa. Basi baada ya kujihakikishia kuwa nipofiti kwa mastahili yangu hayo nilisubiri siku ya shindano ifike nikafanye yangu. Siku ya shindano ilifika na mimi nilikuwa miongoni mwa washiriki walioingia tatu bora.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…

BIKRA YANGU (32)

Mwandishi: Emmanuel F. Kway

SEHEMU YA THELATHINI NA MBILI
ILIPOISHIA...
Catherine aliita huku akimzabua kofi kali lililolia kwa nguvu sana, kitendo kile haki kumfurahisha hata yeye na ili bidi afanye vile kuzuga kwa wakati huo mzee mwasha Alisha pandwa na hasira sana na kuzidi kumlaani mwanae.
SASA ENDELEA...
“Beatrice au Catherine what ever, kapange nguo zako turudi Tanzania,samahani kwa yaliyo jitokeza huyu mtoto wangu keshaanza kuharibikiwa sana na mabangi anayo vuta, ninge kua na bastola ningemtandika nayo”

Alizungumza Mwasha huku akiwa mwenye hasira nyingi sana, walirudi na Catherine ndani ya chumba chao na kuanza kupanga nguo kwa ajili ya kurudi Tanzania,

taratibu za kuanza kukata tiketi zilianza mara moja na kwa bahati nzuri walipata ndege siku hiyo inayoondoka saa tano za usiku,

japo ilikua ya kuunga ilikua ni lazima mzee huyo aondoke Brazil siku iyo iyo ili amuweke mbali Catherine na Enock aliye amini kuwa anavuta bangi,

Usiku ulifika na tayari walifika uwanja wa ndege na sasa kuingia na kurudi wakiwa na Ngowi pamoja na Betty rafiki yake kipenzi.

Kesho yake saa kumi za jioni walifika uwanja wa ndege mwalimu Nyerere na moja kwa moja kunyoosha mpaka nyumbani kwake oysterbay akiwa na Catherine.

“nawewe sitaki kukuona una zungumza na Enock, hata siku moja iwe mwanzo na mwisho”!
“mbona unanifokea lakini”?

“samahani kipenzi, hapa nisha changanyikiwa”

Mwasha alimsogelea Catherine na kumuendea mdomoni lakini aliukwepesha mdomo wake na kuangalia pembeni.

“humu chumbani kwako kupo rafu sana, ngoja nikusaidie kupanga panga”

Catherine alizuga na kuanza kupanga panga ndani ya chumba hiko cha Mwasha ila baada ya kuvuta droo ya kwenye kitanda alikutana na bahasha kubwa sana,

Hakutaka kupitwa aliitoa bahasha ile na kukutana na picha sita,

Moyo ulimwenda mbio sana baada ya kuona picha ya baba yake mzazi Ramsey akiwa na mwanamke wame kombatiana, lakini hakuelewa Yule mwanamke ni nani,

Alizidi kuziangalia picha nyingine na kuanza kulia kwa sauti hii ni baada ya kuona picha ya baba yake ambaye ni marehemu akiwa amefungwa kamba huku akiwa na damu nyingi sana mwilini mwake,!

Pembeni ya picha ile alionekana mwanamke amepiga magoti analia huku nyuma yake akiwa amesimama Mwasha na bastola mkononi mwake,

Kwa haraka haraka kupitia picha zile aliweza kuunga unga matukio na kumfanya apatwe na hasira sana.

“vipi mbona unalia”?

Aliuliza mwasha baada ya kuingia ndani chumbani.

“huyo ndiye mwanaume niliyekwambia, alitembea na mke wangu huyo hapo, nili mfanya vibaya sana najua amekufa namimi ndiye niliye fanya ivyo mpaka nikafungwa jela, ila bado nina kisasi na familia yake , mke wake nishamfahamu na ana mtoto wa kike niliambiwa, lazima niwafanye vibaya hapo nafsi yangu itatulia”

Maneno aliyo zungumza mzee Mwasha yalikua ya kutisha sana yalikua ya kuogopesha kuliko kawaida,
Hakuelewa kuwa mwanamke aliyekua ameketi pembeni yake ndiye aliye paswa kumuuwa au ndiye aliyekua akimzungumzia.,

maneno aliyokua akiongea yalimaanisha sababu aliongea akiwa mwenye hasira za wazi wazi.
Moyo wa Catherine ulizidi kumwenda mbio sana na kuelewa kuwa alikua kesha nasa kwenye mtego mkali na kutoka ilikua vigumu, ilikua ni lazima atoke kwenye mtego huo na kumueleza mama yake mzazi ili amuokoe….

“kway uko wapi rafiki yangu”?

“vipi kwani Ali?”

“sijui kuna gari nime ifananisha hapa ubungo, nafikiri nime ifananisha, za masiku”?

“ngo ngo ngo ngoja kwanza,. Gari yangu umeiona wapi ile vitz?”

“ndio! hapa ubungo mataa imepata ajali,kwani wewe upo wa …tititi”

Mapigo ya moyo ya Kway yalilipuka na kuanza kuhisi joto kali mwilini mwake na kuikata ile simu, hakuna alichowaza zaidi ya kujua kivyovyote vile mke wake ndiye kapata ajali kutokana na hali aliyoondoka nayo dakika chache zilizo pita hapo nyuma!,

moja kwa mojalichomoka kama kichaa na kutoka nje ya geti, bahati nzuri alikutana na boda boda na kuiparamia.

“twende ubungo mataa fanya fasta, nahitaji kufika hapo sasa hivi”

“sawa shilingi elfu kumi na tano”

Japokua alikua anajua anapigwa mzinga sababu haikuwa bei ya kutoka kimara mpaka ubungo, hakutaka hata kujaribu kupunguza bei kama afanyavyo, kutokana na haraka aliyokua nayo hata angetajiwa shilingi elfu hamsini angetoa mara moja,

Piki piki iyo ilizidi kwenda kasi huku kway akizidi kumsihi dereva Yule awahi kufika, walipita katikati ya magari mengine kwa kasi sana, baada ya dakika kumi alifika ubungo maji na kwa mbali aliona watu wengi,

hakutaka kujiuliza alijua kivyovyote ni watu walioshuhudia ajali ile, alimkabidhi dereva Yule elfu ishirini bila kudai chenji na kuanza kukimbia haraka haraka eneo la tukio,

Chini aliona bangili ya Julia juu ya lami ambayo ilikua na kidani cha jina lake, alikiokota na kuzidi kusogea huku akiwa pangua pangua watu waliokuwa wamezunguka kushuhudia ajali hiyo mbaya sana!,
“jamani naombeni kupita, naomba njia naomba kupita”

Alizidi kuwapangua watu hakuamini alichokiona walikua ni watu watatu wakisaidiana kulivuta gari ili wamtoe mke wake Julia aliye kua amebanwa ndani hasemi chochote kile,

damu nyingi zikiwa zime tapakaa chini yake na kufanya sura yake isionekane kabisa, aliweka kiganja chake machoni huku akilia kwa machungu, alizidi kuishiwa nguvu sababu mpaka dakika hiyo hakuelewa kuwa kama mke wake ni mzima au keshakata kauli tayari, alipita mpaka kwa wale vijana na kuanza kusaidiana nao kumtoa Julia ndani ya gari ambao ilionekana amekandamizwa na m-bonyeo wa gari hilo.

Machozi yalimtoka Catherine bado picha ya baba yake mzazi ili mjia kichwani japo kua hakuwahi kupata malezi kutoka kwake lakini alijua kivyovyote vile kifo chake alikufa akiwa ana teseka sana,
na aliyesababisha hayo yote ni mzee huyo ambaye sasa hivi yupo mbele yake na isitoshe wana mahusiano ya kimapenzi.

Maneno ya mzee Mwasha yalizidi kuukoroga ubongo wake alijua ni kisasi ndicho analipiza kwa sasa hivi na si vinginevyo, alisimama na kuomba ruksa ya kurudi hostel huku akijaribu kuficha uso wake.!
“unalia nini”?

“no kuna kitu nime kumbuka tu, alafu mafua yana nisumbua wala usijali baby”

“niambie kama unaumwa nikupeleke hospitali”

“nipo sawa”

Alijibu Catherine huku akizuga na tabasamu la bandia,alimbusu Mzee Mwasha mdomoni na kutoka nje akiwa mwenye wasi wasi,

hakuna alichowaza hapo zaidi ya kutafuta usafiri mpaka kwao Bunju B kisha akamueleze mama yake juu ya kile alicho sikia kutoka kwa Mwasha,

Lakini hakuelewa kama mama yake ange muelewa au angemchukuliaje.

“lazima nimwambie mama yangu, inabidi nimuokoe kabla hayajatokea makubwa, asipo niamni basi”

Alizidi kuwaza Catherine na kufika kwao Bunju lakini kwa bahati mbaya hakumkuta mama yake, alimtafuta kwenye simu na kukuta haipatikani hewani!,

Wasiwasi ulizidi kumtawala moyoni mwake hisia mbaya juu ya kukamatwa kwake vilizidi kujijenga ndani ya mtima wake.

“dushwa dushwa dushwa kufa kufa kufa… hiii mbona mnanitazama hamnijui, halloo eeeh kamuzubanda.. ha ha ha ha ha ha ha ha hihiihihihi. Nataka nivue samaki, nyie tokeni tokeni mnazama!”

Maneno hayo yalitoka kinywani mwa mwanamke Heather akiwa ameshika kiatu kikubwa mkononi huku kikiwa sikioni akiifanya kama simu,

hii iliashiria tosha teyari amerukwa na akili amekuwa chizi kabisa au mwehu, nywele zake tim tim akiwa juu ya kitanda cha hospitali , wakijaribu kumtuliza,

baadae walimfunga kamba, kila mtu alishika kichwa chake baada ya kumuona mwanamke huyo.
“Mganga kalumanzila…huyu hapa bruuuchaha cha cha”

Alizidi kuongea Heather maneno yasiyo eleweka kabisa.

Enock teyari Alisha tua kutokea Brazil na kunyoosha moja kwa moja hospitali kabla ya hata kupumzika, alishtuka hata yeye baada ya kumuona mke wake yupo katika hali ile,

Ilikua ni fedhea kwake pia, alimtizama mwanamke wake na kuomba mtoto wake aliye jifungua, ila alistaajabu baada ya kuletewa kiumbe kisichoeleweka, na kumkana mtoto Yule pale pale.

Shangazi yake Heather aliyeitwa Rehema alikua pembeni ameji kunyata bila kuongea chochote kile, babamzazi mzee mpelembe na mama yake mzazi Heather walimtupia jicho kali Enock wakimshtumu na kumtuhumu kuwa amemroga mtoto wao.

“Enoock kamata kamata ha ha ha ha ha ha, Mama Enock huyo dushwa dushwa kufa tena.. haha mimi ndiye niliye kuuwa ndiyo dushwa dushwa nita kuua tena”

Enock taratibu alianza kusogea karibu yake na kusikia habari hizo kutoka kwa mke wake Heather, kwa mara ya kwanza alidhani ni uwendawazimu ila alizidi kurudia maneno yale yale kuwa alimuuwa mama Enock, na kuanza kutoa siri zote huku akimtaja na Zahara wakati mwingine.

Hasira zilizidi kumkaba Enock na kuzidi kusogea, alimfuata na kuanza kumkaba kwa hasira pale pale kitandani alipokua amelala, na kufanya watu wamfuate wakimzuia asichukue hatua hiyo kali.

“bosi tumeshapata picha kamili ya mtoto wa Ramsey”

“mumeipata wapi”?

“tume chunguza si ulipita iyo kazi mimi”?

“kabisa”

“ngoja nikutumie watsap”

“poa”

Yalikua ni mazungumzo baina ya simon na Mwasha kisha baada ya muda mfupi ujumbe uliingia kumaanisha kuwa teyari picha ime tumwa.

Baada ya kufungua simu yake hakuamini picha aliyoiona ilikua ni ya mwanamke Catherine tena akiwana mama yake Sabrina,

Alishindwa kuelewa ni kitu gani afanye, lakini ilibidi tu alipize kisasi ilikua ni lazima aweke hisia zake pembeni na amalize kile alicho kipanga muda mrefu,

Kweli alikua na chuki sana na marehemu Ramsey ilikua ni kama alitoneshwa kidonda kilichopoa muda mrefu,

alimkumbuka sana mke wake Josephine alivyokua mzuri walivyokuwa wenyeupendo lakini upendo wao ulikatishwa na Ramsey,

Alivuta droo na kutoa bastola yake na kuikagua kama ina risasi alivyo hakikisha kila kitu kipo sawa aliiweka kiunoni na kuanza safari ya kutoka nje,

Alipewa maelekezo vizuri sana nyumbani kwa Sabrina na sasa alikua njiani kuelekea bunju B kwa nia moja tu kuteketeza familia hiyo ya Ramsey akiwemo Sabrina na Catherine.!

Baada ya dakika chache Alisha fika teyari bunju jioni hiyo ya saa kumi na kuweka gari pembeni na kuweka bastola yake sawa sawa.

Baada ya kumtoa Enock shingoni mwa Heather alikasirika sana na kuondoka zake kwa nia moja tu kuelekea kwa Catherine, bado alikua na mapenzi nae mengi moyoni,

Aliwasha gari na kufika mpaka nyumbani kwao, ila aliona gari la baba yake nje bila kuhofia chochote nayeye aliingia ndani ya geti, ila alisita kidogo baada ya kusikia baba yake anafoka na kuongea maneno ya ajabu,

Alinyata kidogo na kuchungulia dirishani hakuamini alichokiona hii ni baada ya kumuona baba yake ana bastola mkononi amewaweka chini ya ulinzi Sabrina na Catherine.

“ni lazima niwauwe, na sito wapa hata nafasi ya kusali sala ya mwisho, kwa ajili ya Ramsey nimeamua kufanya ivii, kacha kacha paaa paaaa”

Pale pale Mzee Mwasha alifyatua risasi ila hakuamini alichokiona baada ya tu kuona aliyekua akivuja damu mbele yake alikua ni Enock,

kitendo cha kufya tua risasi ile Enock alimrukia Catherine na risasi mbili kupenya ndani ya tumbo lake na kubaki chini anavuja damu nyingi sana,

kilikua ni kitendo cha ghafla hata yeye alishindwa kuelewa Enock aliingiaje humo ndani,.

Mzee Mwasha alizidi kuyatoa macho yake huku akimtizama mwanae aliye kua chini anavuja damu nyingi sana mdomoni na tumboni mwake, huku akitafuta pumzi kwa shida sana……
KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

14 Bikra Yangu Simulizi
Jiunge kwenye mazungumzo
Chapisha Maoni