Notifications
  • MY DIARY (39)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA TISATULIPOISHIA...Nilikuwa na furaha sana huku nikiamini kuwa ndoto zangu za kuja kuwa mtu maarufu zinaweza kufanikiwa hata kabla ya kuyapata yale madini. Sikutaka mbwembwe niliamua kuikopi na kuipesti hiyo stori kama ilivyo na kuifowadi kwa Mark.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Baada ya kama lisaa hivi Mark alipiga na kuniuliza kama kweli ilikuwa nai mimi nimetunga hiyo…
  • MY DIARY (38)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA NANETULIPOISHIA...Usiku nilishituka usingizini baada ya mbu kuning’aata na kunisumbua sana. Niliwachukia sana hao mbu kwa sababu walinikatisha ndoto yangu ambayo nilikuwa nikiota.Ndoto ilikuwa ikielezea jinsi harusi yangu na Mark itakavyokuwa. Ndoto ilikuwa tamu sana maana ilinipa taswira ya picha halisi ya maisha yangu ya mbeleni.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nilishusha neti…
  • MY DIARY (37)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA SABATULIPOISHIA...Hapo alitulia tulii kama mtu aliyeaamia dunia ingine. Kimoyo moyo nikawa najisemeha kama amehamia dunia ingine na kuanza kuwaza ujinga sahuri yake mimi nipo kazini bwana acha nitafute hela. Ndio ni lazima nifanye kazi kwa utaalamu na utundu wa hali ya juu ili waendelee kusimuliana huko mjini ili niendelee kupata hela.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Wewe…
  • MY DIARY (36)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA SITATULIPOISHIA...Sasa wewe fikiria mimi niliyeletewa zawadi sikujua ni zawadi gani lakini yeye tayari alishafungua na kuchungulia na kujua nini kilifungwa huko ndani.Basi nikaendelea kumuhudumia yule mama huku na yeye akiniambia kuwa itabidi nikimmaliza hizo zawadi tusifungue hapo hapo na waniimbie wimbo wa happybirthday.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Tuliendelea na stori mbili…
  • MY DIARY (35)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA TANOTULIPOISHIA...Tatu niliambiwa kuwa ndugu zake na wazazi wake walihusika kwenye mipango hiyo hivyo walibariki kabisa huyo binti kuniacha mimi mumewe wa ndoa na kuamua mtoto wao aolewe upya. Nne ni kwamba huyo mzungu amewaamishia wazazi wake mjini na amewajengea nyumba ya kifahari.Kwa hiyo mimi ninavyowapigiana simu na kuwajulia hali kumbe wenzangu huwa wananichora tu.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (34)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA NANETULIPOISHIA...Hapo nikakumbuka kuwa zile zana zangu za kazi nilikuwa nazo ni vile vifaaa vya kupimia ukimwi ambavyo huwa navitumia kabla ya kukutana na mwanaume yeyote nisiyemfahamu. Nikaamua kumkubalia huku nikiamini kuwa hiyo ndo kinga yangu pekee iliyobaki kama mwanaume huyo atataka kuzini na mimi usiku huo.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Basi tuliondoka na kwenda sehemu…
  • MY DIARY (33)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA TATUTULIPOISHIA...Nilikuwa nachanganya staili za kijamaika na hizi za kwetu, sikuacha pia zile za Nigeria hapo nikapata vitu vyangu vya tofauti kabisa. Basi baada ya kujihakikishia kuwa nipofiti kwa mastahili yangu hayo nilisubiri siku ya shindano ifike nikafanye yangu. Siku ya shindano ilifika na mimi nilikuwa miongoni mwa washiriki walioingia tatu bora.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (32)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA MBILITULIPOISHIA...Lakini kuchepuka kwangu na kuingia mgombani haikumaanisha kuwa sheria ingeniacha hivi hivi.Ilifika mahali ikabidi nizime gari na kutulia tulii kusikilizia nini kitafuata.Tayari nilikuwa nimezungukwa na mapolisi ambao walikuwa wakinifuatilia kwa kutumia pikipiki.Kwa bahati nzuri dereva wa lile gari na yeye alishafika hapo na alishawaambia polisi kuwa mimi naugua ukichaa na nilifufuka kutoka mochwari.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA…
  • MY DIARY (31)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA MOJATULIPOISHIA...“marehemu pia alinieleza kuwa ana miliki duka la vitu vya urembo wa kike ambalo pia Leah analisimamia ila hilo apewe mdogo wake Marry ambaye yupo hapa. Mama mdogo huyo mara baada ya kuyasema hayo alikaa zake chini. Baba mdogo ambaye hakurizika na maelezo hayo alisimama na kusema “kwa hiyo kama marehemu alijua kuwa atakufa hivi karibuni kwani nini hakufuata taratibu za kisheria za kuandika wosia na kurithisha mali.IKIWA UNASOMA…
  • MY DIARY (30)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINITULIPOISHIA...Baada ya hapo Nnilimwomba mama mdogo ajikaze na kuwatarifu ndugu wengine habari hizo za msiba.Tulisaidiana hivyo hivyo maana sio siri kila mmoja alikuwa na uchungu sana kutokana na mazingira ya kifo hicho. Habari zilizidi kusambaa kwa kasi na majirani walianza kukusanyika hapo kwa mama mdogo.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Msiba ni msiba tu na ukitaka kujua binadamu…

BIKRA YANGU (35)

Mwandishi: Emmanuel F. Kway

SEHEMU YA THELATHINI NA TANO
ILIPOISHIA...
Sio kway peke yake hata kwa madaktari na wauguzi walishaanza kuingiwa na hofusana babadaya mwanamke waliyekua wakimpa matibabu kutokuzinduka kwa siku nne kitandani, ilikua ni jambo la ajabu sana walivyo mchoma nusu kaputi hakuweza kuzinduka tena lakini kilichokua kinawapa moyo ni mapigo yake kudunda wakiamini kuwa hali yake ni nzuri sana,
SASA ENDELEA...
Kila mtu sasa alimtupia lawama Kway sababu waliamini Julia akitoweka duniani ni yeye atakua amesababisha, walimzuia hata asiweze kukanyaga hospitalini hapo, kila alipokuja walimfukuza mbali sana, sio wengine bali ni ndugu zake na julia,

moyo ulimuuma sana kutokuruhusiwa kumuona mke wake Julia., hakua na la kufanya zaidi ya kukubaliana na hali hiyo hakutaka kugombana na ndugu wa mke wake.

Ilikua kila siku ni lazima apige simu hospitalini hapo kuuliza hali ya mke wake ila alijibiwa nakuambiwa kuwa bado hali ni ile ile,

Habari iliyo mchanganya siku hiyo ni baada ya kupiga simu na kuambiwa kuwa mke wake alihamishwa hospitali kimnya kimnya na hata madaktari hawakujua ni wapi wazazi wake walimpeleka,

alijua nini maana yake alijua tu ni lazima zilikua ni njama za kumtenganisha mke wake na yeye.

“mpeeeeenzi waaaaangu naaaaomb……a nikue….leze pendo langu lililo moyoni mmmh moyoni mwangu…..Mweeeenyezi Muuungu muumba ardhi na Mbingu ndiye shahidi wa pendo mmmh moyoni mwangu”!

Alikua ni kway akiimba nyimbo hiyo huku mkononi akiwa ameshika chupa ya pombe kali mdomoni akiwa na sigara, aliamini vitu ivyo ndivyo vinge mpunguzia mawazo, kila alichokipenda sasa hakikuwepo Duniani,

aliimba huku akiangalia chupa yake ya pombe huku akisimama wakati mwingine akicheza usiku huo ndani ya baa iliyoitwa Mandela, nyumba yake aliiona chungu pengine kuliko shubiri,

Alikua ni mtu wa kukesha baa na kulewa na watu aliowakuta, aliimba nyimbo iyo ya wana Njenje huku akicheua cheua.,ndugu jamaaa na marafiki walisha mshauri ila wote aliwapuuzia

“mapenzi niiiii kuvumilianaaaaa nami mpenzi nimekuvumilia,…..,tulizana mpenzi Tupendaaanee,wewe dada kuja hapaaa hii chupa imeekwishaaaa, alaaafu moja, mbili Yule pale wape bia mbili mbili hawa kwenye bili yanguuuuuu”

Aliongea kway akiwa bwii pombe zime mshika kichwani akitoa agizo hilo mara moja.

“Kway bratha nini una fanya?, mpaka muda huu upo baa pombe sio suluisho, achana na mapombe twende nikupeleke nyumbani, sawa una matatizo lakini wewe sio mwenye matatizo peke yako hapa duniani,”

Alizungumza binamu yake aliye fika hapo na kumkuta ndugu yake akiwa chakali.

“Jamesss ulishawahi kuninunulia pombe, jibu ni hapana, kwaiiiooo kama unataka pombe niambie nikununulie sio una kuja unazuunguka mbuyu,”

Ilibidi binamu yake James atumie akili kumuelewesha kuwa anachokifanya anaji dhalilisha, kwa mara ya kwanza ilikua vigumu sana kumuelewa ila baadae taratibu waliinuka na safari ya kumpeleka kway kwake kuanza.

kitendo cha kufika alijitupa kitandani na kuanza kulitaja jina lamke wake julia huku akilia machozi,
Picha ilionesha kuwa bado alikua akimkumbuka.

Asubuhi aliamka akiwa amechoka sana na kuamua kwenda kwenye album za picha akitizama picha za mke wake na mtoto wao Natu,alivuta droo na kutoa baasha kubwa ya picha alizopigwa Natu akiwa amefariki aliangalia mkono ule wa Natu na kusita kidogo.

“Mhhhh”

Alijikuta akiguna baada ya kuuchunguza mkono ule vizuri na kugundua kuwa hauna kidoti cheusi kwenye kiganja,

alichukua picha nyingine na kulinganisha kucha za mtoto wake Natu na kufikicha macho yake,
Ili kuhakikisha ni kweli au anaona vibaya, alitizama tena na kugundua ni vitu viwili tofauti.

Alichukua simu yake ya mkononi na kumtafuta Molito rafiki yake wa karibu na kumuita ili nayeye aweze kumwambia nini cha kufanya ndani ya dakika arobaini alikua keshafika haikuwa na haja ya kuficha aliweka kila kitu wazi.

“sikia nikwambie kitu kway, si alizikwa Moshi?, kama una uwezo tutaomba kibali maiti ile ifukuliwe tupime DNA hapo ndo tutajua, na tutajua pa kuanzia”

“sawa ndugu yangu ngoja nita fanya ivyo,”

Siku hiyo hiyo alinyoosha mpaka kituo cha polisi na kuomba kibali hiko na kuambiwa kuwa akaonane na maaskari wa mkoani Kilimanjaro hapo Himo.

Asubuhi ya saa kumi na mbili kesho yake alishafika ubungo na kupanda basi la kampuni ya MERIDIAN na sasa alikua njianni kuelekea mkoani Kilimanjaro,

ndani ya kichwa chake alikua mwenye mawazo mengi sana na kusinzia pale pale.

Masaa saba yalivyopita tayari alikua njia panda na kushuka, hapo alitafuta usafiri mwingine mpaka hapo Himo na kutoa kibali kile,

kutokana na kazi iyo kuwa ngumu askari walimshauri kesho yake wangeanza kazi wakiwa na daktari maalumu kwa ajili ya kupima DNA yalikua ni maamuzi yaliyokua yanaitaji ujasiri sana.

Masaa yalienda mwendo wa kinyonga kwake kisha asubuhi kufika alinyoosha mpaka kituoni hapo na kuondoka na defender mpaka kijijini Mwika,

wanakijij waliowaona waliwashangaa ila yeye moyoni mwake alijua anacho kifanya.

Zoezi lilianza mara moja la kufukua maiti hiyo na kufika chini huku wakiwa na vitambaa puani mwao kutokana na harufu kali.

“sasa mbona tume kuta mkono”?

Aliuliza askari mmoja wao

“ndivyo tulivyozika”

Waliuchukua mkono ule na kwenda nao mpaka maabara na kuanza kuupima, walichukua na damu kubwa ya kway kisha kumwambia aje jioni yake..

“Majibu kweli yanaonesha wewe na huyu aliyezikwa hamna uhusiano wowote ule”

Moyo wa kway ulimlipuka kuna picha ilimjia kichwani kuwa mwanae Natu yupo mahali anateseka sana hakujua ni wapi hakujua ni wapi aanzie kumtafuta.

Hali ya Enock bado ilizidi kuwa mbaya sana baada ya mashine zile kurudiswa mwilini mwake, ilibidi ulinzi mkali uwekwe hospitalini hapo wakiamini kuwa kuna watu wabaya wana taka kuyapoteza maisha ya mwana ume huyo,

Zahara Alisha fika hospitalini baada ya kupata taarifa juu ya hali aliyokua nayo Enock mwanaume anaye mpenda sana.

Aliangua kilio sana, pembeni yake alimuona mwanamke mmoja mweupe aliyekua na majonzi alionekana kama alikua akimfananisha ilibidi tu amsogeleee na kumuuliza kama wana fahamiana.
“ndio nakufahamu tulishawahi kukutana kituo cha polisi, wewe ni anti yake na Suzi”?

“basi nishakumbuka”

“hali yake vipi”?

“kama unavyo muona tangu aletwe hajaweza kusema chochote”

“hawa majambazi hawa…”

Alijisemea Zahara bila kujua ukweli wa mambo. kwa Catherine alimuona mzee wa makamo hakuweza kuisahau sura yake hata kidogo japo alivalia miwani kubwa na kofia,

alikua ni mzee Mwasha, alivyo muona hata yeye aliinamisha kichwa chake chini, na kujificha nyuma ya zahara.

“naomba nimuone mwanangu”

Aliomba Mzee Mwasha baada ya kukutana na Mlinzi akiwa mlangoni hapo chumba alicholazwa Enock, alitoa kitambulisho na kweli ilionekana kabisa alikua ni baba yake mzazi,hakukua na haja ya mlinzi Yule kuweka aina yoyote ya kipingamizi bila kujua kuwa anamruhusu israeli atoe roho ya Enock hapo kitandani.

Ndani ya Moyo wa Mzee Mwasha alishaa apa ni lazima amuuwe mtoto wake ili kupoteza ushahidi wa mambo japo kwake ulikua ni uamuzia mgumu sana lakini ilimbidi afanye ivyo ili mkono wa sheria upite mbali, aliingia ndani ya chumba hiko na kumkuta mwanae amelala mashine ndizo zina piga kelele peke yake.

“Mwanangu Enock naomba unisamehe kwa kitendo nitakacho kifanya hapa sina jinsi, REST IN PEACE MY LOVELY SON(pumzika kwa amani mwanangu kipenzi)”

Alizungumza mwasha na kuibana mashine iliyokua puani mwa Enock akizuia hewa iyo ya Oxygen isipite ndani ya mfumo wa upumuaji,…

Akili yake ilicheza kama umeme ilikua ni lazima afanye jambo ilikua ni lazima atumie akili ya ziada sababu alishajua ni lazima mzee Mwasha aliyeingia ndani ya chumba alichokua Enock alitaka kummaliza ivyo ndivyo akili yake ilimtuma.

Alihisi moyo wake una muuma sana hakutaka jambo lile litokee hata kidogo, pale pale aliruhusu miguu yake itembee haraka haraka na kwenda mpaka kwa askari aliyesimama mlangoni na kupiga kelele nyingi.

“naomba niingie humu ndani, naomba niingie jamani uwii”

Ilikua ni lazima apige kelele zile ili amuokoe Enock aliamini kelele zile zinge mshtua Mwasha aliyekua ndani ya chumba alicholazwa Enock, maaskari walizidi kusogea eneo hilo na kumshika Catherine aliyekua akilia sana,

hakuna hata askari mmoja aliyeweza kujua nini kilimfanya mwanamke huyo alie kwa sauti huku wakati mwingine akilitaja jina la Enock.

“binti wacha kupiga kelele”

Alifoka askari mmoja kati ya wengene nane waliofika eneo hilo, moyo wake uliingiwa na amani japo sio sana baada ya kumuona Mzee mwasha akiwa ametoka nje ya chumba alicholazwa Enock macho yao yaligongana na kuangaliana kwa kitambo kidogo na kumfanya mzee huyo aachie misonyo mikali kisha kuondoka zake akiwa bado na hasira nyingi sana kutokana na kukatisha kitu alichokua anakifanya cha kutaka kumuua mtoto wake wa kiume.

“naomba nimuone Enock tafadhali”

“hurusiwi embu kaa hapo, na unyamaze”

Alizidi kufoka askari huku akiwa amekunja ndita laiti wange jua kuwa kelele alizokua akipiga Catherine ndizo zilimuokoa Enock ambaye alikua anaenda kufa,

Tayari alishajua ukweli juu ya mtoto waliyemzika hakua yeye ni baada ya kupima DNA chini ya usaidizi wa jeshi la polisi, ilikua ni lazima afanye jambo na kujua ni wapi mtoto wake Natu alipo kua, kweli alidhamiria kufa au kupona ili mtoto wake arudi mikononi mwake,

hapo ndipo siku inayo fuata aliingia kwenye basi na kurudi mkoani Dar es salaam ili ajue ni wapi atakapo anzia juu la swala lake,

Hakua na msaada mwingine zaidi ya kumfuata Molito na kumueleza juu ya swala zima jinsi ilivyokua, hawakukaa sana walinyoosha mpaka kwa waziri wa mambo ya ulinzi hapo nyumbani kwake masaki aliyeitwa Eddizaria Msulwa ambaye alikua ni mjomba wake na Molitto, kisha kumuelezea kila kitu.
Ilibidi Molito aongee shida ya rafiki yake huyo kway ili wampate mtu atakae weza kuwasaidia, walikaribishwa vizuri na kuelekezwa mpaka nyumbani kwa mpelelezi aliyejitegemea nje kidogo maili kadhaa kutoka hapo mjini Dar es salaam,

“nawatakia mafanikio mema nina imani huyu mtu atawasaidia sana, mwambieni mimi nimewatuma”

Aliongea Mh. Edizaria Msulwa huku akiwapa mkono wote wawili kisha kuketi, hata yeye alisikitishwa sana na kuguswa na mkasa aliousikia kutoka kwa Kway hakua na kinyogo chochote ilibidi awape mpelelezi wake binafsi anaemtumiaga katika kazi zake za kutaka kujua baadhi ya siri za nchi yake.
“sawa ahsante sana Mheshimiwa Mungu akubariki”

Kway alijibu kisha kusindikikzwa mpaka nje na walinzi, hakukua na sababu yoyote ile ya kusubiri siku inayo fuata waliendesha gari mpaka boko na kumtafuta mpelelezi huyo waliyetumwa kwake,

Walipewa maelekezo mpaka ndani kidogo kati kati ya kipori kidogo kwa njia ya simu. walishuka na kuanza kutembea kwa mguu,

Kulikua kuna nyumba moja peke yake iliyo zungushiwa ukuta mrefu sana kwenda juu waligonga na kelele kusikia za mbwa wanabweka kisha baadae kutoka mwanamke mmoja mrefu kidogo mwenye macho makubwa ya duara.

“samahani habari yako, tuna muulizia sasha, tumemkuta?”

“nyie mkimuona mtamjua”?

Mwanamke huyo badala ya kujibu swali nayeye aliwapiga swali huku akiwatizama wote wawili kwa zamu

“hapana, tumeelekezwa na Mh.Msulwa hata ivyo tulikua tukiongea nae kwenye simu muda mchache uliopita”

“ahaa okay karibuni ndiye mimi”

KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

14 Bikra Yangu Simulizi
Jiunge kwenye mazungumzo
Chapisha Maoni