SEHEMU YA THELATHINI NA SITA
ILIPOISHIA...
“hapana, tumeelekezwa na Mh.Msulwa hata ivyo tulikua tukiongea nae kwenye simu muda mchache uliopita”
“ahaa okay karibuni ndiye mimi”
SASA ENDELEA...
Walikaribishwa na mwanamke huyo na pale pale kuanza kueleza shida iliyowapeleka hapo, baada ya maelekezo kutolewa mwanamke huyo alivuta pumzi ndefu kisha kuwatizama kila mmoja wao.
“kazi ndogo sana hiyo, mwanao ni lazima atakua ametekwa na kikundi kinachoitwa BITCH HUNTERS,NITAFUTIENI milioni tano kazi yenu itakua imekamilika kesho kutwa nitakua nisha jua mwanao alipo na utampata”
Alizungumza Sasha akiwa anaamini na kile anachokiongea kutoka kinywani mwake, hakukua hata na mzaha ndani ya maneno aliyokua akiongea hapo.
“huwezi kupunguza kidogo?”
“hapana kway iyo ni kwasabu tu ya mheshimiwa Ila wengine huwa wananipa mara mbili ya hapo, nenda kajipange ukiwa tayari uje”
“nipo tayari sasa hivi”
“kama upo tayari utalipa Advance milioni moja utaiingiza ndani ya hii account, naona una wasi wasi ngoja nikutoe wasi wasi., mwanao utampata niamini mimi,”
Alizungumza mwanamke huyo na kumtoa wasi wasi kway aliyekua anatoa mimacho na kushindwa kumuamini mwanamke huyo anayeongea maneno ya kijasiri sana na mwenye kujiamini kuliko kawaida,
Siku inayo fata ilibidi aanze kukamilisha malipo aliyoambiwa na tayari kumuingizia pesa kwenye account na kumpa taarifa hiyo.
Baada ya siku mbili aliitwa mpaka Boko ili akapewe taarifa ni wapi alipo fikia, taarifa alizosikia zilizidi kumchosha sana akili yake moyo ulimwenda mbio kupita kawaida.
“kabla ya kukuta ule mkono wa mwanao, siku mbili nyuma kuna maiti iliokotwa baada ya kufanya uchunguzi wangu sikupewa ushirikiano ikanibidi niibe risasi iliyotumika kumuuwa huyo mtu, sasa hapa una kazi kidogo, kuna uhusiano baina ya hiyo maiti na koplo Mwita”
Kumbu kumbu za haraka haraka zilimjia kway na kumpeleka mpaka siku hiyo walivyokua na Natu mtoto wake mdogo akimnyooshea kidole Mwita, jambo alilokua analiona mbele yake ulikua ni kama mkanda una pita na kucheza mbele ya macho yake,
na hapo ndipo alipo anza kuunga unga matukio alijua kivyovyote vile ni lazima askari huyo alikula njama.
“nime nime kumbuka ki..”
“subiri nimalize sasa, huyu Mwita ni askari lakini ni jambazi sugu ana toa michoro mbali mbali historia yake ninae kwaio hili halikunishtua sana”
“sasa kwanini kama unawajua hao majambazi usiwakamate”?
“siwezi kufanya ivyo bila kibali, kumbuka mimi ni mpelelezi wa kujitegemea, sasa hapa hatuna jinsi inabidi tutumie nguvu za ziada ili huyu mtu ataje”
Baada ya maongezi hayo taratibu zilianza mara moja za kumtafuta Koplo Mwita hakuna njia watakayo tumia zaidi ya kumteka nyara ili wafanikishe.
Hali ya Enock ilizidi kuonesha faraja, sasa aliweza kufumbua macho yake lakini alishindwa kuongea chochote kile alichoweza kukifanya ni kutingisha vidole tu huku akimtizama kila mtu aliye kua akimzunguka mahali hapo,
licha ya hayo yote lakini bado hakuweza kupumua bila kutumia msaada wa mashine,
Jambo lililowashtua wauguzi ndani mule ni baada ya kumuona akitabasamu hasa alipomtizama mwanamke mzuri aliye simama mbele yake aliyevalia sketi nyekundu ndefu na shati jeupe huku mkononi akiwa ameshika maua alikua si mwingine bali ni Catherine Ramsey,
Wauguzi wote walibaki wakimwangalia
“dada wewe ni nani yake”?
Ilibidi nesi mmoja aulize
“ni rafiki yake tu”
“hapana haiwezekani, huyu mgonjwa hakuwahi hata kutabasamu lakini alipokuona wewe tu baasi akatabasamu, usitufanye sisi watoto”
Zahara aliyekua pembeni wivu ulimwingia na kuhisi ni lazima kuna kitu kinaendelea kati ya Enock na Catherine alitoka nje bila kuongea chochote kile,Catherine aliweka maua yake pembeni na kumsogelea Enock huku akiwa anatabasamu na kufanya kishimo cha shavu la kushoto kuingia ndani, alimsogelea Enock karibu na kukaa kitako juu ya kitanda kile huku akiwa mwenye huruma sana.
Ila katika hali ya kushangaza mashine ilianza kupiga kelele sana kwa sauti kuashiria kuwa mapigo ya moyo yanazidi kushuka kwa kasi,wasi wasi ulizidi kumuingia kila mtu, hasa baada ya kumuona Enock anatingisha miguu kuashiria kuwa roho yake inaacha mwili, alizidi kuweweseka akiwa juu ya kitanda.
“dada naomba utoke nje tafadhali, nenda kamuite Dokta haraka sana Mage”
Walimtoa Catherine nje huku wakizidi kushughulika na Enock, mapigo ya moyo ya Catherine yalizidi kwenda mbio sana katika akili yake alitafsiri lile tabasamu la Enock ndilo lilikua la kumuaga.
“umefikia wapi Dokta saki”?
“mambo yapo sawa sasa, nilimchoma sindano ya sumu ambayo itakua inamuua taratibu sana, hakuna atayeweza kuhisi, na sasa hivi tunavyoongea ndio itaanza kufanya kazi, usijali mzee andaa kitita changu”
“sawa saki nakuaminia”
Mzee Mwasha alitabasamu baada ya kusikia majibu kutoka upande wa pili yaliyo mfanya azidi kufurahi, kweli alidhamiria kumuua mwanae kipenzi akisha maliza hapo afuatie Sabrina na mtoto wake Catherine alishavaa ngozi ya Simba sasa.
“ndio mwanangu anaitwa Catherine Ramsey. Tangu juzi alivyotoka nyumbani hakurudi tena”
“Mama punguza jazba nieleze vizuri,nimekuuliza hivi alivyoondoka alikuaga”?
“hapana hakuniaga”
“ana umri gani”?
“anamiaka ishirini na tatu”
“anasoma”?
“ndio”
“wapi”?
“C.B.E”
“ulishawahi kwenda hapo chuoni kumuulizia”?
“ndio ndio nilishaenda hapo na hapa nimetoka chuoni kwao”
Askari huyo aliyekua zamu jioni hiyo alizidi kuyachukua maelezo ya Sabrina akiyaandika vizuri juu ya karatasi maalumu na kuzidi kuhoji maswali ambapo kila lililosemwa aliliandika vizuri alisikiliza vizuri kwa umakini mno.
Catherine siku kadhaa sasa hakuonekana nyumbani, Sabrina alizidi kuingiwa na hofu aliamua kumtafuta chuoni na sehemu zote alizojua kuwa mwanae anaweza kuwepo lakini hakuweza kumpata na kumfanya azidi kuingiwa na wasi wasi sana,ndipo alipoamua kunyoosha mpaka kituo kidogo cha polisi Tegeta.
“lakini afande”!
“naam”
“nina mashaka na mtu mmoja”
“enhee nani huyo”?
“anaitwa mwashii sijui mwasha David”
“kwanini”?
Hapo hapo Sabrina alianza kumuelezea askari huyo kila kitu mpaka alipo taka kumuua mtoto wake Catherine hakua na jinsi ya kuficha kitu chochote kile ilikua ni lazima aweke mambo wazi ilikua ni lazima afanye jambo hilo ili mwanae aliyeamini ametekwa nyara aweze kumpata.
“mama una uhakika na unachokiongea”?
“ndio”
“Mwasha David si ndio, huyu ninae mfahamu mimi au mwingine, mrefu hivi ana mvi kwa mbali sana”
“ndiye mwenyewe”
Askari Yule baada ya kuchukua maelezo ya Sabrina alimruhusu aende na kumu hakikishia kuwa kila kitu kitaenda sawa na Catherine kupatikana mara moja.
Baada ya Faisal kutumia kila jitihada kumnasa Catherine kushindikana ili mbidi atumie njia nyingine tu ya kumteka nyara,
Alimsha mfukuzia na kumrubuni na vitu vingi sana kila siku akibadili magari ya kifahari lakini aligonga mwamba na kushindwa kuelewa nini binti huyo aliringia hasa.
Siku hiyo akiwa amepaki gari Mwenge mwisho baada ya kumfuatilia akiwa anatoka Hospitaali ya Lugalo alishuka ndani ya gari na kumuongelesha lakini bado alitolewa nje.
“siwezi kupanda kwenye gari yako, sitaki sitaki sitaki”
Aliropoka Catherine na kufanya abiria waliokua stendi iyo wanasubiri usafiri wa dala dala wageuze shingo zao nyuma kuwatizama wawili hao,
walitizama gari hilo la kifahari aina ya BMW X6 ikiwa pembeni na kustaajabu kwanini Catherine alikataaa kuingia ndani ya gari wakati usafiri ulikua mgumu siku hiyo.
Wasichana waliokua pembeni udenda uliwatoka na kumuona Catherine anapoteza bahati walitamani walau ingekua bahati yao lakini haikuwa ivyo.
“sawa hakuna neno,”
Alijibu kifupi na kuingia ndani ya gari na kuliondosha mbio, alifika na kuliegesha gari lake nje, mbali kidogo na geti anapoishi catherinekisha kunyunyizia madawa makali ya usingizi juu ya kitambaa cheupe na kumsubiri catherine,
aliona njia hiyo ingekua bora zaidi, sababu Alisha kula nusu ya pesa ili tu kufanikisha zoezi la kumteka Catherine Ramsey na asafirishwe mara moja.
Jioni ya saa moja ilipofika kwa mbali aliweza kumuona na kushuka ndani ya gari nyuma nyuma alimfuata taratibu kisha kumkaba shingo yake na kukiweka kitambaa kile puani mwa Catherine,
haikuchukua hata sekunde mbili Catherine alihisi kizungu zungu kizito na kupoteza fahamu zake pale pale.
Moja kwa moja aliiingia nae ndani ya gari na kutoka nae mbio, sehemu ya kwanza alifika nae mpaka chumbani na kumvua nguo zake zote nayeye kuvua nguo zake,
Aliipanua miguu ya Catherine na kuanza kumuingilia kimwili vile vile bila fahamu zake kumrudia, baada ya hapo alimpiga picha akiwa utupu,na kuingia bafuni kuoga alivyomuangalia tena Catherine jinsi alivyokua mzuri na mweupe, hisia kali zili mpanda tena na kumpandia kwa juu na kuingiza MASHINE yake ndani ya MGODI na kuzidi kujiburudisha kimwili.!
Kwa mbali sana alihisi kichwa chake kizito kabla ya kufungua macho yake alihisi kitu tofauti kabisa, na taratibu kuanza kufumbua macho yake hakuamini alichokiona,hakuamini baada ya kumuona Faisal yupo juu yake ndio anamalizia kurusha risasi zake juu ya tumbo lake, aliinuka haraka haraka na kushindwa kuelewa alifikaje fikaje chumbani humo,alijaribu kuvuta kumbu kumbu zake nyuma taratibu na kukumbuka mara yamwisho alikua na Enock hospitalini kisha kupanda gari mpaka nyumbani kwao, ila baada ya hapoa alishindwa kuelewa nini kimetokea na kufika hapo kitandani.
“turudie tena”
Alizungumza Faisal lakini aliambulia kofi la shavu zito na kumfanya Catherine alie machozi alielewa ni kitu gani kilitokea hapo nyuma,
alielewa ameingiliwa kimwili bila ya ridhaa yake na kuzidi kupandwa na jazba.
Na kujikuta anashindwa kuongea sababu ya kwikwi
“umeridhika, umer..idhika sasa”?
“kidogo sio sana”
Alijibu Faisal kwa dharau
“sasa umepata faida gani fala wewe, wana ume wenzako hawapo iv..yo”
Catherine aliongea kwa hasira na kusimama akitafuta nguo zake, alivyo zipata alizivaa na kuzidi kumtolea maneno machafu Faisal aliyekua kitandani yupo uchi wa mnyama.
“nipe funguo niondoke”
Alisema Catherine baada ya kukuta mlango umefungwa, baada ya kutoa funguo Faisal alitoa simu yake mfukoni na kuipiga.
baada ya dakika thelathini walitokea wanaume watatu na kuingia baada ya kufungua mlango kwa nje,
Kitita cha pesa kilirushwa na Faisal kukipokea mpaka dakika hiyo Catherine hakuongea kitu chochote kile ila baadae aligundua kinachoendelea,alishaelewa kuwa anauzwa na kubaki akilia machozi mengi akiomba msamaha ili wasifanye wanachotaka kukifanya.
“Binti Catherine tuondoke, ushauzwa tayari”
Aliongea mmoja wa watu hao walioingia ndani.
“tafadhali msifanye ivyo, kama mnataka pesa nitawapa”
Hawa kutaka kubishana nae walichofanya walimshika kwa nguvu na kumchoma sindano kali ya VALIUM baada ya dakika mbili tayari alipoteza fahamu zake na kum-beba begani na kuondoka nae….
“hapana sitaki kuamini, mnanidanganya”
“ukweli ndio ivyo mzee!”
“ilikuaje”?
“hata sisi tuna shindwa kuelewa ni moto wa ghafla ulitokea kwa bahati mbaya tulijitahidi kumuokoa lakini ilishindikana, ameteketea na moto, samahani mzee mwanao pia alikua ndani ya chumba”
“hapana, My s..on! haiwezekani”
Mzee Mwasha aliserereka mpaka chini akitumia mgongo wake hapo ukutani asubuhi ya saa kumi na mbili ni baada tu ya kusikia taarifa mbaya kutoka hospitalini hapo kuwa mwanae Enock alikuwa ndani ya chumba maututi ambacho kiliwaka moto usiku wa kuamkia jana yake,
KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA