BIKRA YANGU (40)

0
Mwandishi: Emmanuel F. Kway

SEHEMU YA AROBAINI
ILIPOISHIA...
Akili ya Catherine ilimtuma sehemu moja tu mifukoni mwa mwanaume huyo na kuitoa simu ndani ya mifuko ya suruali yake na kuzidi kumpagawisha ambapo alizidi kuichua koki yake.

SASA ENDELEA...
“Carlos!”

Sauti ya bosi wake ndiyo iliyo mshtua alijua kukutwa ndani ya chumba hiko angekosa kazi na pengine kuuliwa kabisa,

Alichomoka kama mkuki na kuiweka suruali yake mwilini haraka haraka na kutoka nje.

KITU cha kwanza alichofanya kuiweka namba ya mama yake mzazi kwenye simu sababu aliijua kichwani mwake,iliiita sana bila kupokelewa ,alijaribu tena mara nyingine lakini jambo lilikua lile lile tu,

Alipiga tena na kuzidi kuishiwa nguvu hasa baada ya simu ya mama yake kukuta haipatikani.

Kilichomshtua tena ni simu kuita alivyoangalia namba ilikua ni namba ngeni lakini ni ya Tanzania, haraka haraka aliiweka sikioni na kutulia.

“hallo”

Upande wa pili ulisikika wa simu na kuitambua sauti hiyo ilikua niya mama yake mzazi

“Mama mimi Catherine, tafadhali njoo unichukue. Mama nj… si.”

“Catherine upo wapi mwanangu siku sikii”

“Mam.. sijui nilipo tafadh..li njoo.., UNAONGEA NA NANI?”

Sauti ya Joyla ndiyo iliyomshtua na kumpora simu bila ya hata kusema ni wapi alipo.

Hakua na chaguo lingine zaidi ya usiku kuzinduka na kuanza kupanga vitu vyake kimnya kimnya, alishajua kuwa Catherime yupo katika hali ya hatari na muda wowote ule angeuwawa na baba yake mzazi, alishajua ukweli sasa, hakua na sababu ya kubaki Kwa Mama Andunje alijiona tayari keshapata nafuu kabisa,hakuna alichowaza ndani ya kichwa chake zaidi ya kumkumbuka Catherine mwanamke ambaye alimpenda kwa dhati kuliko yoyote Yule duniani, aliamini kuwa huyo ndiye mwanamke wake sahihi tena wa maisha yake isitoshe ni yeye ndiye aliye mtoa bikira yake, walisha pitia mengi sana.

Baada ya kumaliza kuweka kila kitu sawa alivuta karatasi na kuandika ujumbe juu yake na kuanza kunyata taratibu akitoka nje, alishika barabara kubwa na kuanza kutembea mpaka alipofikia bara bara ya lami hapo alijaribu kuomba msaada kwenye magari makubwa ya mizigo na baadae kupata usafiri wa gari kubwa la mbao linaloenda dar es salaam,

Njia nzima alikua akimuwaza Catherine tu na wala sio vinginevyo baada yamasaa manne walikua teyari wamefika Dar es salaam.

Kulikua teyari kumepambazuka na kutafuta moja ya bank ya CRDB hapo kimara ili kutoa pesa kidogo.
Alichoshukuru bado alikuta pesa zake zipo vile vile, alitafuta taxi na kunyoosha mpaka Bunju B nyumbani kwa Sabrina lakini hakukuta mtu wa aina yoyote ile,

ilibidi akae nje hapo asubiri mwenyeji wake aweze kuja.

Baada ya dakika tano alimuona mwanamke mwenye tumbo kubwa la mimba akishuka ndani ya gari na kuliendea geti.

“Shikamoo”

Aliamkia Enock

“Marahaba, nikusaidie nini?”

“namuulizia Catherine”

Kitendo cha kuuliza vile Sabrina aliinamisha kichwa chake chini, kupitia kitendo kile alijua kuna kitua ambacho sio cha kawaida kinachoendelea,moyo ulimwenda mbio sana hisia za kifo cha Catherine zilianza kupita ndani ya kichwa chake lakini hakutaka kuyapa nafasi mawazo hayo yateke akili yake.

“nime mkuta?”

“hapana”

“yuuu yuko wapi?”

“kwani wewe ni nani?”

“naitwa Enock”

Sabrina alimuangalia mtu aliye kua mbele yake na kukumbuka siku za nyuma alivyo ruka na kuyaokoa maisha ya Catherine, izo ndizo kumbu kumbu za haraka zilizo mjia akilini mwake kwa wakati huo na kuanza kusikitika sana.

Ilikua ni kama ametoneshwa kidonda kilichokua ndani ya moyo wake.hakuna alicho fanya zaidi ya kumkaribisha ndani na kuanza kumuelezea kila kitu tangu alivyoanza kumtafuta Catherine bila kuficha chochote,pia hakuacha kumshukuru kwa kitendo cha yeye kuyaokoa maisha ya mwanae kwa kitendo cha kumrukia japokua hakua na kitu cha kumpa, halikua jambo la kawaida kwa mtu yoyote kuamua kupoteza maisha kisa mapenzi.

“Mama nampenda sana catherine, nita hakikisha nita mtafuta mpaka pale nitakapo mpata, hata kama nikifa sawa tu”

Alizungumza Enock akiwa mwenye hisia sana moyoni mwake.

“ninavyo kwambia hapa leo hii kanipigia simu ila sikuweza kuongea nae vizuri”

“unasema ukweli Mama?”

“ndio, nilitaka nipite polisi lakini hali yangu haikuwa nzuri sana”

“hiyo namba iko wapi?”

“hii hapa”

Sabrina alipekua pekua simu yake na kumkabidhi Enock

“hizi code za Uganda,, mimi nitaenda hata leo”

“hapana mwanangu huoni ni hatari”

“siwezi kukaa hapa lazima niende, nachokuomba usiwaambie polisi chochote kile, na hapa naomba uhame”

“kwanini?”

Sabrina aliuliza, na hapo ndipo Enock alianza kumueleza nia na mipango ya baba yake ya kutaka kumuuwa kabisa hata yeye habari zile aliziona ngeni kwake,

Kabla ya kukaa sawa walihisi geti limefunguliwa Enock alisimama na kuwaona watu wawili wakiwa wamevalia miwani na makoti, hapo ndipo alipo mshika mkono Sabrina na kutoka nae mlango wanyuma taratibu sana,

walitembea kimachale na kutoka nje mbio mbio na kulipalamia Geti.

“nipe funguo za gari”

Enock aliingia ndani ya gari na Sabrina kisha kutoa mbio za ajabu huku majambazi hao wakibaki kulishangaa gari hilo likitoa mbio.

“wale ni akina nani?”

“bila shaka ni watu wa mzee”

“sasa itakuaje?”

“inabidi tutafute sehemu ya kujificha”

Enock tayari aliamua kumsaidia Sabrina mama mzazi wa Catherine dhidi ya mkono wa baba yake Mwasha ilikua ni lazima awalinde watu hao wawili akitumia jicho lake la tatu,

Walitafuta Hotel iliyokua nje ya mji kidogo na kila mtu kutafuta chumba chake, lakini kwa Enock bado alikua na nia moja tu aanze safari ya kwenda nchini Uganda mara moja, japo hakujua ni wapi atafikia,
Baada ya siku mbili alikua kisha kamilisha safari yake ya kukata tiketi na ilibaki siku moja tu ili safari yake iweze kuanza.

Siku iyo ilivyofika aliwasha gari na kushoto alikaa Sabrina wakielekea uwanja wa ndege kwa ajili ya safari, katika hali ya ajabu Sabrina alianz kupiga kelele huku akishika tumbo lake kubwa lenye mimba kuashiria kuwa kivyovyote vile tayari anahitajika kuwaishwa hospitali,

Hapo alikua na mambo mawii ya kuchagua amuwaishe hospitali Sabrina au awahi ndege ambayo zilibaki dakika kumi tu iweze kuondoka.

Japokua kifo cha Enock kiliwasikitisha wengi mamia na maelfu ya watu hasa kwa waliomfahamu, kijana mdogo aliyekua na mafanikio makubwa hapo mjini kufa mapema ili kua ni vigumu watu kuamini,kuna waliosikika chini kwa chini kuwa kuna ndumba! Kuna wengine walisema alikua freemason chama kinacho tumia nguvu za giza na alimtoa mama yake mzazi kafara kisha akamfanya mke wake awe mwenda wazimu, na kukosea masharti hapo ndipo umauti ukamkuta.

Anderson Peter rafiki yake kipenzi ndiye yeye tu aliamini kuwa moto uliotokea hapo hospitali wenda zilikua itlafu za umeme aliwa pingasana waliokua na imani potofu juu ya msiba wa Enock kila siku!.

“Ndumba izo hakuna kitu, Enock alikua mchawi alikua mkuu wa Freemason,”

Ilisikia sauti ya kijana mmoja siku iyo katika kilabu cha pombe

“kwanini watu wanakua wanamkosea Mungu, kamtoa mama yake kafara, kamgeuzia mke wake awe chizi, maskini watu wana laana sana!”

Ivyo ndivyo wengi walivyofikiria juu ya mambo yaliyo tokea, kila mtu aliyekua akipewa historia hiyo fupi nakuunga unga matukio basi huamini asilimia mia moja kabisa.

Hakuelewa kuwa Siri kubwa aliibeba Zahara peke yake juu ya uchizi wa Heather mpaka kifo cha Mama Enock hakutaka kuongea chochote kile,hakutaka kuthubutu kufungua kinywa chake kuzungumza kitu cha aina yoyote ile kuhusiana na mambo yaliyo tokea hapo nyuma yake,

Heather Alisha kuwa mwenda wazimu yupo milembe na wodi ya vichaa, ndugu zake wakiwa teyari wametaifisha nyumba ya Enock na kujimilikisha magari yote ya kifahari,

“Alafu hili gari tuuze au?”

Aliuliza Sakina mdogo wake Heather siku iyo usiku

“uuze lako, alafu nakushangaa sana Dada Sakina mali izi zote sio zako ni za Dada Heather, hata kama ana hali ile sio vizuri”

“wewe una jua nini kaa kimnya, sasa unafikiri atapona tena”

“hata kama, na usinishirikishe wala nini”

“poa utajijua”

Hayo ndiyo yalikua mabishano baina ya watu hao wawili kila kukicha wakitaka kuuza mali, walishauza shamba moja la Enock la mpunga Kilosa, Morogoro na kuanza kuuza sasa baadhi ya hisa za kampuni ya Nissan chini kwa chini. Hayo ndiyo yalikua yakiendelea.

Aliona ni bora amuwaishe Sabrina Hospitali wala sio vinginevyo, roho ya huruma ilimuingia hapo hapo, alizungusha usukani na kunyoosha mpaka hospitali ya hapo karibu,

Kitendo cha kufika tu alimchukua Sabrina na kumkokota mpaka ndani hospitali, ambapo alipelekwa na wauguzi na moja kwa moja kumuwaisha ndani wodi ya wamama wajawazito madaktari wote sasa walikua bize kumshughulikia.

Alivyoangalia saa yake ya mkononi alikua kasha chelewa teyari hakua na jinsi zaidi ya kutulia na kughaili safari siku iyo,

Alikaa juu ya benchi ili asubiri nini kitaendelea. Mwanaume mmoja aliye valia kotijeupe la kidaktari alimuita na kuanza kuongozana wote ofisini yeye nyuma daktari mbele mpaka ofisini kwake na kuketi pembeni ya kiti, ili kusubiri nini daktari huyo angesema kwa wakati huo.

“amejifungua salama bila matatizo yoyote yale, unaweza kwenda kumuona”

Hilo jibu moja tu lili mfanya asimame na kunyoosha mpaka wodi ya wanawake waliojifungua na kuketi pembeni mwa Sabrina ambaye alionekana kuchoka sana akiwa ameshika kichanga mikononi mwake.

Enock ndani ya moyo wake alitamani kuuliza ni nani baba wa mtoto huyo, lakini aliona hilo yeye alimuhusu kabisa, alimpa pongezi za dhati kwa kujifungua mtoto wa kiume mwenye afya.

“Ahsante sana, unaonekana ni kijana mkarimu”

Alizungumza Sabrina akimshukuru sana Enock japo walizoeana kwa siku chache lakini alishajua tabia za kijana huyo ambaye aliokoa maisha ya mwanae kipindi cha nyuma kilichopita.

Baada ya kumpa pongezi ilibidi tu amkumbushie kuwa bado anasafari ya kuondoka kesho asubuhi sana mpaka Uganda ili aweze kumuokoa Catherine mwanamke anaye mpenda kuliko mtu yoyote Yule chini ya jua la Mungu!.

Alitafuta Hotel huku akiandaa mipango ya tiketi siku inayofuata, alipata ndege ya asubuhi na kumfanya afurahi sana,

Hakuona jambo la busara kuondoka bila ya kumuona Sabrina hospitalini na kumuaga Mama huyo.
“Nakutakia safari njema huko uendako”

“sawa Mama ubaki salama, naomba nikirudi na Catherine nifunge nae ndoa!”

“mimi sina kipangamizi kila la kheri mwanangu!”

Baada ya kujiridhisha na majibu hayo aliweka begi lake dogo mgongoni na kuanza kuondoka, alitafuta taxi mpaka uwanja wa ndege na baada ya muda mchache alikua ndani ya shirika la ndege la AIRUGANDA,ilitembea angani kwa masaa Manne na kutua uwanja mkubwa wa Entebbe nchini Uganda na kushuka taratibu ngazi huku akizidi kushangaa,

Ki ukweli hakua mwenyeji wa nchi hiyo lakini alisha weka nia ndani ya moyo wake kwa gharama yoyote ile ni lazima arudi na Catherine nchini Tanzania na waweze kufunga ndoa,

KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)