BIKRA YANGU (41)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA AROBAINI NA MOJA
ILIPOISHIA...
Ki ukweli hakua mwenyeji wa nchi hiyo lakini alisha weka nia ndani ya moyo wake kwa gharama yoyote ile ni lazima arudi na Catherine nchini Tanzania na waweze kufunga ndoa,SASA ENDELEA...
Alimpenda sana Catherine ndani ya moyo wake aliwaza vitu vingi sana akiwa nje katika maegesho ya magari.
“Jebalekoo sebbo?”(habari yako muheshimiwa?”)
Sauti ya kiume dereva taxi ndiyo iliyo mshtua akiwa ameduwaa asielewe nini cha kufanya.
“I don’t speak your language(siongei lugha yenu)”
“sawa habari!”
“nzuri tu”
“taxi ipo hapa, kwa mubei ya muzuri sana sema twende”
“nipeleke hotel nzuri”
“sawa twende ingia twende”
Enock aliingia mlango wa nyuma na begi lake mgongoni huku dereva huyo akiwa anamchangamkia sana akimuongelesha na kumuuliza maswali ya hapa na pale akijaribu kumzoea mpaka walipofika jiji la kampala hotel ya nyota tano iliyoitwa Serena na gari kuingia kwenye maegesho maalumu.
Alimpatia dereva pesa yake na kuingia mapokezi
“for how long are you going to stay?( unatakaa kwa kipindi gani)?”
Alihoji dada wa mapokezi
“actually I don’t know,!probably two to three days(ki ukweli sijajua, ni kama siku mbili mpaka tatu)”
Baada ya kutajiwa malipo Enock alipewa funguo zake na kuingia ndani ya lift kisha kubonyeza namba ukutani na lift kuanza kupanda juu,
Ilivyo fika gorofa ya saba lift ilijifungua na mwanaume mwenye ndevu kiasi mfupi wa wastani mweupe kuingia huku akiwa anaongea na simu kwa Kiswahili fasaha kabisa.
“ndio, hata sielewi itakuaje, ila nishajua pa kuanzia ndio ndio, nitakucheki mida basi!”
Enock alizidi kumtizama mwanaume huyo kwa umakini na baada ya lift kujifungua alitoka nje na kumuacha ndani,Baada ya kufika namba ya lift aliyobonyeza ilijifungua na kutoka nje na kuanza kutafuta chumba chake,baadae alivyo kipata aliingia na moja kwa moja kujitupa kitandani akiwa na mawazo mengi kichwani mwake.
Aliwaza juu ya ndoa kubwa na sherehe kubwa atakayo fanya na Catherine siku chache atakapo mpata, licha ya kuwaza yote hayo ilikua ni lazima afanye jambo juu ya baba yake mzazi,
Alisha mchukia sana, aliwaza vitu vingi vilivyo pita katika maisha yake na kujiona kama anaota ndoto, ni kweli alipitia mambo mengi yaliyokua kama historia kwake tena iliyo bidi iandikwe au kuaktiwa na wasanii hodari kama Juan Miguel wa kwenye tamthilia ya DON’T MESS WITH AN ANGEL ,
Usiku kucha hakupata hata lepe la usingizi, sura ya Catherine ndiyo ilikua imetawala mbele yake alitamani wawe wote kitandani hapo wakiongea na kucheka pamoja kama walivyo fanya hapo nyuma,
Alichukua mudakidogo na kumkumbuka mama yake mzazi Josephine ambaye alikua tayari amefukiwa mavumbini ametangulia mbele ya haki, na aliye katisha maisha yake alikua ni Heather Mke wake na sasa hivi amewehuka na akili zake,
Aliwaza jinsi miaka ya nyuma walivyokua wakiishi vizuri na Wazazi wake wakiwa wenye furaha sana, lakini sasa hivi mambo yalibadilika kabisa, mambo yalikua juu chini chini juu.
Usingizi mkali sana ulimchukua hapo hapo baada ya kuwaza mambo hayo yote usiku huo.
Alikurupuka asubuhi na kuingia ndani ya lift ili aende kula asubuhi yake.
Aliagiza chakula na kuanza kula ila kwa mbali alimuona mwanaume aliye kua anaongea Kiswahili usiku wa jana ndani ya lift, aliamini kuwa huyo ndiye atakae kuwa mwenyeji wake,
Alisimama na kwenda kwenye meza aliyokua mwanaume huyo.
“Ndugu habari?”
Enock alisalimia.
“safi tu,za kwako?”
“salama, Wewe ni Mkenya au Tanzania?”
Alizidi kuhoji Enock
“TANZANIA, natokea Tanzania”
“hata mimi!, naitwa Enock”
“Kway,!”
“upo huku kwa muda gani”?
Alizidi kudadisi Enock
“muda kidogo,wewe je?”
“nimeingia tu jana hapa”
“okay sawa, wacha niwahi kuna sehemu nawahi, tutakuja tuzungumze, nipo chumba namba 105”
“ahsante sana”
Enock alitabasamu sana kupata mwenyeji wake ambaye angeweza kumtembeza maeneo tofauti ya huko hakuelewa kuwa wapo safari moja ya kuwatafuta watu waliopotea siku nyingi zilizo pita!.
“Hodi ndugu nimekuja”
“karibu karibu sana, pita ndani Enock!”
Alijibu Kway usiku huo na kumkaribisha Enock chumbani, hakua na sababu ya kumuwekea mashaka ilibidi tu wazoeane sababu walitokea nchi moja Tanzania,waliulizana maswali mengi tofauti ya hapa na pale, Kisha baadae Enock kuamua kusema jambo lililo mleta Uganda na kutoa picha ya Catherine mfukoni mwake na kumuonesha Kway.
Picha ile aliichukua na kuitizama kwa karibu sana na kumtizama mwanaume Enock aliye kua anaongea kwa hisia zote juu ya mwanamke huyo Catherine.,
kumbu kumbu zake zilianza kurudi nyuma na kukumbuka sikuambayo Catherie alikua Hospitali akisema kuwa Enock ndiye aliye fanya mpaka atake kujiua,
Alizidi kuvuta vitu vingi sana juu ya Enock aliye kua ameketi juu ya sofa akizidi kubwabwaja maneno mengi juu ya mapenzi aliyokua nayo juu ya mwanamke huyo.
Kway alishusha Pumzi ndefu na kukuna kichwa chake kidogo.
“Catherine Ramsey Kidhirwa, namfahamu sana”
Alijibu Kway na kumfanya Enock akae vizuri akiyatoa macho yake makubwa na kukaa sawa juu ya sofa baada ya kusikia habari hizo mpya kwake!.
Catherine Ramsey msichana mrembo anayetikisa jijini Dar es salaam ameshatekwa tayari yupo Nchini Uganda ana chezeshwa filamu chafu za Ngono, wana mtishia kumuuwa pale atakapo kataa kuonesha ushirikiano kutokana na uzuri usiokua na mfano aliokua nao, hakua na jinsi zaidi ya kukubali ili tu aweze kunusuru maisha yake kwani aliamini kuishi ni mara moja. Enock ana zinduka kitandani na kupewa taarifa hizo mbaya za kupotelewa na mwanamke aliyempenda, baada ya kufanya uchunguzi anagundua kua yupo nchini Uganda anaamua kufunga safari moja kwa moja Mpaka Uganda ili tu kumuokoa mwanamke catherine, aliyekiri kuwa ndiye atakae kuja kumzalia watoto hapo baadae.
Mvua kubwa sana ambayo haikuwahi kunyesha miaka mingi iliyopita sasa ilinyesha siku tatu mfululizo bila kuacha ikiambatana na radi kubwa sana, watu walipelekwa na maji mamia na maelfu ya watu walipoteza maisha yao pamoja na mali nyingi sana zilisombwa na mafuriko.
Usafiri wanchi kavu ulikua shida mno hakukua na usafiri wa aina yoyote ile kila raia waNchi hiyo ya Uganda alishindwa kutoka nje kutokana na mafuriko hayo yaliyokua hayana mfano wake!.
“sisi tumekwama hapa”
“Mmefika wapi?”
“tuna karibia Gatuna mpakani! kuna mafuriko sana, njia hazipitiki, kuna daraja limevunjika”
“tafuteni hoteli mlale”
Larry dereva aliyekua akiendesha Landcruiser mkonga mvua hiyo kubwa ilimkuta njiani, akishuhudia magari mengine yakisombwa na maji na kupinduka, hofu ili mtanda na kuamua kumpigia simu Bosi wake Joyla ili wajue nini cha kufanya.
Walishaamua kumuuza Catherine Ramsey kwa pesa nyingi sana na sasa hivi walikua njiani wakipitia njia boda ya Congo ili wakutane na tajiri mkubwa sana wa Kigerman Karl Martin hapo Kinshasa, ili wamkabidhi Catherine ,
Mvua peke yake ndiyo iliyo leta kikwazo na kufanya gari hilo litembee mwendo wa kinyonga, mambo yote hayo yanatokea Catherine hakua anaelewa kitu chochote kile alichomwa sindano kali sana ya madawa ya usingizi na kulala kwenye viti vya nyuma, alikua ni kama aliyekufa hajui kinachoendelea,
Hakua anaelewa ni wapi anaenda hakuelewa kuwa tayari kasha uzwa na siku chache atakua nchini German. Baada ya kusimama masaa mawili Dereva anapata ufumbuzi wa njia nyingine japo ilikua na mafuriko lakini alizidi kusonga mbele ivyo ivyo akizidi kushuhudia jinsi magari yanavyosombwa na maji yakielea juu juu,ilikua nil lazima amfikishe Catherine Kinshasa na hiyo ndiyo ilikua kazi kubwa aliyokua nayo. Kwa mwendo wa kobe alifanikiwa kufika boda ya Gatuna, hapo hawa kuwa na shida yoyote ile na maaskari wa hapo kutokana na walisha fanya mawasiliano juu ya ujio wake,walipita bila wasiwasi na kuingia Rwanda usiku kucha gari lilizidi kuchanja Mbunga kutokana na hali kuwa shwari kabisa mpaka mjini Kigali walifika salama salmin!,
Jioni ya saa kumi na moja walifika boda ya Ruzizi na kusimamishwa na askari kwa ajili ya ukaguzi hapo mpakani.
“Naomba niongee na Hafsa Kaijage”
Alisema Larry dereva baada ya kuona askari huyo anamuwekea mashaka juu ya msichana catherine aliyekua amelala viti vya nyuma.
Mkuu wa kikosi cha ulinzi hao boda alikuja baada ya kuitwa.
“nime tumwa na Don Mullosi, huu hapa mzigo wako”
Baasha ya kaki ilitolewa na askari huyo kupewa hongo ili tu aruhusu gari hiyo ipite, Don Mulllosi alijulikana kote hakuna mtu aliyeweza kuigusa gari yake,walijua kufanya ivyo wange poteza vibarua vyao, walijua ni kiasi gani alikua na pesa za kutisha.
“Bimaa! Bimaa!(nenda nenda)”
Aliamuru Hafsa wa polisi
“Merci”(shukrani)
Gari taratibu lilianza kuondoka lakini kabla ya kufika mbele askari wengine walikuja na kulizunguka gari hilo wakiwa na mitutu mikononi mwao na kufanya dereva huyo hofu izidi kumtanda alisimama na kusubiri nini kinge fuata,hofu na mashaka moja kwa moja vilitua juu ya Catherine alijua hapo ndipo angepewa kesi ya utekaji nyara, hakujua afanye nini.
“weka gari kando saa hii”
Aliamuru askari mmoja mfupi wa kikongo na gari kuwekwa pembeni.
“kuna shida gani afande?”
“una kwenda fasi gani?”
“Kinshasaa,Gombe, kuna problema?”
“hurusiwi kutembea saa hii ina kubidi ulale hapa, huko hali ya hewa haiko shwari.”
“nina haraka afande, embu pata hizi mkanywe supu”
Ilibidi tu atoe hongo nyingine hapo mpakani na kuruhusiwa apite,licha ya kuchukua pesa zake lakini walimsisitiza kuwa kuna mvua kubwa sana huko anapoenda, lakini ili bidi asonge mbele.
Alisha tembeza gari takribani masaa matatu njiani na kuamua kwenda kujaza mafuta na kutafuta chakula .
“huko njia habiko bien, ni mubaya saana,”
Mjaza mafuta alisema.
“ni mbaya sana?”
Nayeye aliuliza tena
“haifai kabisa”
Alipuuzia na kupiga gia na kuondoka, huyo ni mtu wa nne sasa kumwambia habari izo za bara bara kuwa mbovu.
“tu..naenda wapi?”
Sauti ya Catherine ndiyo iliyomshtua baada ya kutoka usingizini, alichofanya bila kujibu chochote alimdunga sindano ya usingizi nyingine na kuzidi kusonga mbele, kila alivyozidi kusonga mbele kiza nene lilizidi na wingu zito kuonekana,baada ya sekunde chache mvua kubwa ilianza kunyesha iliyo ambatana na radi kali usiku huo, hakutaka kusimamisha gari alizidi kusonga mbele alikua amebakiza masaa manne tu aufikie mji mkuu wa Kongo Kinshasa hiyo ili mpa moyo sana.
Upepo mkali sana ulizidi kuvuma kuelekea upande wa magharibi ya kaskazini na kufanya kitu kama kimbunga, vitu vilianza kuchukuliwa na maji.
Katika hali ya kushangaza alihisi kitu kizito kime piga gari upande wa kushoto alivyo geuka nyuma aliona mti mkubwa uliodondoka na kufanya gari izidi kuhama bara barani,kila alipojaribu kucheza na usukani kushindana na hali hiyo hakuweza, ilibidi tu anusuru maisha yake na kujitosa nje huku akimuacha Catherine ndani ya gari hana fahamu na kushuhudia gari ikipelekwa na maji na kutumbukia kwenye maporomoko ya maji yaendayo kasi sana.
KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni