Notifications
  • MWALIMU MKUU (6)
    Jina: MWALIMU MKUUMtunzi: __SEHEMU YA SITAILIPOISHIA...Hatimae rameki alipata nafuu alizinduka Mama ake alifurahi kumuona mwanae akiwa amepata fahamu“””Eeeee mungu kweli umesikia kilio changu asante sana(uku alifurahi)pole mwanangu””IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...“”Asante mama”alijibu ramekiMama rameki na mama loly walirudi nyumbani kumchukulia rameki chakula kwani tangu asubui akupata mlo.*********Upande wa bi sani alifurahi…
  • MWALIMU MKUU (5)
    Jina: MWALIMU MKUUMtunzi: __SEHEMU YA TANOILIPOISHIA...Mama roly alivyosikia rameki anataka kumwaga alimtema yule nyoka na kumficha pangoni mwake, rameki alimpambu mama roli kwa kasi ya ajabu kama ndege ya vita ikimbiavyo angani“Ramekiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!!! tombaaaa”rameki na mama roli walipiga madafu kama manne “heeee rameki siamini???!!”IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...“kwannn??”rameki aliuliza“DUDU LOTE HILI…
  • MWALIMU MKUU (4)
    Jina: MWALIMU MKUUMtunzi: __SEHEMU YA NNEILIPOISHIA...Mwalimu mkuu alistuka kuguswa na kitu kwenye makalio yake alijua rameki atakuwa kaweka mzigo nyuma yake rameki alivyoona ajakaa vizuri alisogea ili akae vizuri mwalimu mkuu alistuka kitu kama tango kikimgusa tena alipitisha mkono ili aone nn alistuka “MUNGU WANGUU”IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...Rameki alistuka mwalimu mkuu alivyoshika tango lake akapaza sauti“AAAAAA MWALIMU…
  • MWALIMU MKUU (3)
    Jina: MWALIMU MKUUMtunzi: __SEHEMU YA TATUILIPOISHIA...chausiku alishangaa kuziona zile sale “JAMANI NANI KAKUPA MWANANGUU??!!”aliuliza chausiku kwa mshangao“Kaka juma”alijibu ramekiIKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...“Oooh juma jamani mungu akubariki ooooh asante mungu”alitamka mama rameck uku akinua mikono juuRameck alizijalibu zile nguo hakika alipendeza sana adi mama ake alimfagilia kwa vigeregere “jamani juma mungu akuwekee…
  • MWALIMU MKUU (2)
    Jina: MWALIMU MKUUMtunzi: __SEHEMU YA MBILIILIPOISHIA...“MUNGU WANGU YULE SI MZEE ALINANI???!!!”aliuliza chausiku kwa mshangao chausiku alimuangaria mzee alinani ambae amepoteza furaha yake ya kusomaMzee alinani alikuwa anakuja kuangaria bishala zake pale sokoni kwa kina chausiku.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...Mzee alinani alistuka kumuona chausiku alikwepesha macho yake kwa aibu alitoka kwenye soko lile, chausiku alimpitia…
  • MWALIMU MKUU (1)
    Jina: MWALIMU MKUUMtunzi: __SEHEMU YA KWANZA“MAMA USIFE MAMA NITAISHI VP NA HII MIMBA MAMA”ilikuwa ni sauti ya mdada aitwae chausiku akimwambia mama ake asifee bado anamtegemea mama ake na mimba yakee“CHAUSIKU MWANANGU NAJUA MIMI NDIYO TEGEMEZI LAKOO NILIPAMBANA NA KILIMO ILI USOMEE LAKINI UMECHEZEA SHIRINGI CHOONI MWANANGU UMESHIKA MIMBA BADO MWAKA MMOJA TUU UMALIZE LAKINI NDO IVYO MWANANGU MIMBA NDO ISHAINGIA SINA BUDI KUKUFUKUZA INGALI UKO MOYONI MWANGU NAKUPENDA MWANANGU CHAUSIKUU ILA…
  • THE NIGHTMARE (9)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA TISAILIPOISHIA...“mmenifananisha, mimi ndio kwanza naigia ofisini mida hii.” Aliongea yule afande na kuigia kituoni.“sasa aliyekuwa anatuhoji ni nani kama sio huyo?”Alijikuta anajiuliza mwenyewe swali lililompa utata mkubwa kichwani mwake.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...Wakati wakiwa hawajui hili wala lile, walishangaa kuona maaskari wakijazana pale na ambulance ikafika…
  • THE NIGHTMARE (8)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA NANEILIPOISHIA...Walipofika feri, walipewa nahodha mwingine tofauti na yule aliyemuota na boti ilikuwa ndogo tu ya kawaida tofauti na ile aliyoiota.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...Sharji alijikuta anapiga makelele baada ya kumuona Balqis akiwa amejaa damu mdomoni huku ametoa makucha yake akimfata kwa nia ya kumdhuru.“AAAAAAAAAAAGH”Sharji alipiga kelele na kukurupuka.…
  • THE NIGHTMARE (7)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA SABAILIPOISHIA...“kha!!!!”Ulikua mshangao mkubwa kwa watu karibu wote baada ya kumuona Sharji akiwa na taulo akitoka chumbani kwa Balqis.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...Wengine walicheka na kaka yake alionekana kutoifurahia hali ile.“sasa wewe unatutia wasi wasi bure, si ungesema tu kama unaenda kulala kwa huyu dada?” aliongea kaka yake na kukirudia kile chumba alichompangia…
  • THE NIGHTMARE (6)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA SITAILIPOISHIA...“toa loud speaker bwana.”Aliongea Balqis baada ya Sharji kubonyeza kitufe cha kupaza sauti.“kwanini hutaki nisikie maongezi yenu?” aliongea Karimu kwa sauti ya ukali kidogo.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...“kwani kuna ubaya mimi nikiongea private na mdogo wako?” alijibu Balqis baada ya kuisikia sauti ya Karimu.“hakuna ubaya.” Alijibu Karim kwa sauti ya…

BIKRA YANGU (42)

Mwandishi: Emmanuel F. Kway

SEHEMU YA AROBAINI NA MBILI
ILIPOISHIA...
Katika hali ya kushangaza alihisi kitu kizito kime piga gari upande wa kushoto alivyo geuka nyuma aliona mti mkubwa uliodondoka na kufanya gari izidi kuhama bara barani,kila alipojaribu kucheza na usukani kushindana na hali hiyo hakuweza, ilibidi tu anusuru maisha yake na kujitosa nje huku akimuacha Catherine ndani ya gari hana fahamu na kushuhudia gari ikipelekwa na maji na kutumbukia kwenye maporomoko ya maji yaendayo kasi sana.
SASA ENDELEA...
“mi naona imeshindikana bratha Kway, bado anazingua huyo Demu na muda umekwenda”

“tunafanyaje sasa?”

“tutumie njia m-badala”

“kama ipi”?

“tutumie mabavu tu, sababu ukweli nisha jua mwanao pamoja na Catherine wapo kwenye hiyo nyumba”

“sawa!...mabavu kivipi?”

“tuvamie tu, hakuna njia nyingine, ile nyumba ina lindwa sana”

“kumbuka tupo katika nchi ya Watu”

“hata kama, hata kama lazima tuwaokoe Natu na Catherine tena leo hii”

Maneno aliyokua akiongea Enock hayakuwa na mzaha ndani yake, kway hakua na namna yoyote ya kumzuia hata kidogo aliongea akimaanisha sana.

Mipango waliyopana ya kumlaghai mwanamke Joyla ambayo walipanga Enock amuendee na kumtongoza na wawe wapenzi kisha baadae aweze kujua siri viligonga mwamba baada ya mwanamke huyo kuonekana bado mgumu,sasa waliamua kutumia mabavu tu ni baada ya kujua teyari nyumba anayo ishi mwanamke huyo mwenye dangulo yeye na mume wake Mullosi mwenye uraia wa Jamaica ipo Namugongo.

Wanaume hao wawili kila mtu aliyekua na maumivu yake moyoni walitoka nje na kwenda mjini kampala kununua silaha kama mapanga, visu, suluu na plies hawa kuwa na uhakika kwamba silaha hizo zingefanya kazi.

“ninge kuwa na bastola yangu ingekua rahisi sana”

Alizungumza kway wakiwa kwenye moja ya mgahawa wakila chakula baada ya kufanya manunuzi ya silaha izo.

“iko wapi kwani?”

“nimeiacha Mwalimu Nyerere!”

Walikula chakula ila ghafla mvua ilianza kunyesha kali sana na radi kupiga na kufanya hofu kutanda, kitendo cha dakika mbili kilifanya maji yaanze kujaa.

“sasa tuna fanyaje blazza kway?”

Alihoji Enock kwa sauti ya Juu

“si unaona kuna mvua tufanye kesho”

“hapana haiwezekani, leo hii lazima tuka waokoe”

“sasa tutaendaje?”

Kway aliuliza!

Wote walitoka nje nakuona ni jinsi gani magari tayari yalianza kusombwa na maji ilikua ni mvua kubwa hatari,yenye nguvu na maajabu vile vile, hata wao walishindwa kuelewa na kufikiria nini cha kufanya,

Baadaye walikua teyari wameshapata jibu kamili kuwa watafute helikopta ya kukodi ili waweze kufanya uvamizi, waliona bora wafanye ivyo. Ili kua ni lazmia waende Entebbe nje ya mji wa KAMPALA na huko ndipo wata pata helikopta ya kukodi.

Kwa bahati nzuri walipata usafiri wa gari kubwa na kuingia, mpaka usiku unafika walikua bado njiani kutokana na mvua hiyo kubwa sana iliyo sababisha maafa.

Walifika moja kwa moja na kuonana na mkurugenzi wa usafiri huo wa kukodi Kanyika Amoti japo kwa mara ya kwanza aliweka mgomo.

“sawa ni milioni moja kwa saa!, mutatumia muda gani?”

Alihoji mkurugenzi huyo

“masaa kama matano,”

“sawa milioni tano”

“BARCLAYS bank ipo wapi?”

“ipo hapo nyuma”

Kwa siku iyo waliweza kutoa milioni mbili peke yake ambayo kway nayeye alichangia, hawakuweza kutoa pesa izo zote kwa mkupuo kwenye mashine,

Walitoa nusu ya malipo nakupewa dereva, baadaye walikua wapo angani helikopta ikipiga kelele huku ikizungusha mapanga boi yake kuelekea Namugongo,bado mvua ili kua kubwa sana, walitoa maelekezo wakimuelekeza dereva huyo mpaka Helikopta hiyo ilivyotua juu ya gorofa ya nyumba hiyo.

Sababu ya mvua nyingi sana haikua raisi kusikia mlio wa helikopta ikipiga kelele zake!

Walishuka wakiwa na silaha zao mikononi na kuingia mpaka ndani ya nyumba hiyo kubwa sana kimnya kimnya kama makomandoo,harakaharaka walifungua kila chumba na kukosa watu wanaowatafuta Catherine na Natu,Enock alimvaa mmoja wa kijana aliyekua lindo na kumuwekea kisu shingoni. 

Kwa uwoga ilibidi asonte kidole mlango unaofuata na ndo hapo walipoupiga teke na kukuta wanawake kwa watoto wengi wakiwa ndani!.

Kila mtu alipiga jicho kumtafuta mtu wake.

“Daa….d(baba)”

Sauti ya mtoto mdogo ndiyo iliyosikika na Natu kutokeza alimrukia baba yake na kuanza kulia machozi. Kway alilia japo hakujua ni kwanini alilia machozi hayo yaliyokua yaki mbubujika machoni mwake na kulowanisha mashavu yake kwa kumpata mwanae ambaye aliamini Alisha kufa tayari na walisha fanya mazishi.

“Catherine, Catherine, Catherine”

Aliita Enock akiwa bado anamtafuta Catherine ni wapi alipo aliwapangua pangua wanawake waliokua hapo bila kumuona mwanamke huyo aliye mpenda sana na kumfanya afunge safari yake kutoka Tanzania mpaka hapo Uganda.

“Da..d dada Catherine hayupo humu!”

Alizungumza Natu.

“yuko wapi”?

“wameondoka nae jana Dad,”

“Wapi?”

Alidakia Enock kabla ya kway kusema lolote!

“sijui ni wapi , ila nilisikia neno Kinshasa”

Japo Natu alikua ni mtoto lakini aliweza kutoa maelezo yaliyonyooka.

Haraka haraka walianza tena kutoka nje bado walikua na safari ndefu ya kumtafuta Catherine walipanda ngazi na kukuta Helikopta inazungusha mapanga boi yake,

Derevaakiwa tayari kuuinua ili ipae angani,

Walimuingiza Natu na Enock kufuatia kabla Kway hajaingia zilianza kusikika risasi kutokea upande wa nyuma, Dereva hakua na chaguo lingine zaidi ya kuinua helikopta nakupaa angani ,hapo ndipo walinzi walipoanza kuishambulia Helikopta hiyo na risasi upande wa nyuma ya injini. ilianza kutoa moshi mzito haikuchukua dakika hata tatu ilipoteza uelekeo na kulipuka vipande vipande na kusababisha Moto mkali sana.

“Natuuuuuuuuuuuuu!”

Kway alipiga kelele nyingi baadaya kushuhudia Helikopta aliyo kuwemo Enock na Natu imelipuka na moto baada ya kusha mbuliwa na risasi na walinzi hao na hapo ndipo watu wenye ngozi nyeusi walipomfuata na kumzunguka wakiwa na mitutu Mikononi mwao na hasira nyingi usoni mwao.

Mafuriko ya Maji ndiyo yalimzindua kutoka katika usingizi mzito na wala sio kitu kingine!, hakuelewa ni wapi alipo ila alikua ndani ya gari bado likielea juu juu,maji yalikua tayari yamejaa ndani ya gari, kumbu kumbu za haraka haraka zilianza kumjia na kukumbuka kuwa alikua yupo ndani ya gari wanasafiri barabarani na baada ya kuzinduka alichomwa sindano na kutojua kilichoendelea kuanzia hapo.

Jambo alilofanya ni kuhangaika kutoka ndani ya gari akijaribu kufungua mlango, maji yaliyomzidi kimo yalizidi kumsonga na kumzidi nguvu,alibana pumzi zake na kuyafumbua macho yake akijaribu kuufungua mlango, alivyoibua kichwa chake aliona ni jinsi gani maji yalivyokua yanaenda kasi na mbele yake kulikua kuna maporomoko, ilikua ni lazima afungue mlango huo na kutoka nje vinginevyo angepoteza maisha yake humo ndani ya gari.

Alihesabu mpaka tatu na kuzamisha tena kichwa chake chini akijaribu kupapasa papasa kitasa, bahati nzuri aliweza kukiona na kwa nguvu zake zote alifungua mlango na kutoka nje huku akianza kuogelea taratibu.

Haikupita hata sekunde mbili maji yalimpeleka mpaka kwenye maporomoko na kumrusha hakua na jinsi ya kufanya zaidi ya kumkumbuka mwalimu wake wa St, Marrys Jonas, alivyomfundisha kucheza na maji, alisimama wima na kuibana miguu yake na mikono pia akiwa amenyooka kama mti na kuyafumba macho yake.

Na kujikuta amejikita ndani ya maji mpaka chini kisha kuibuka juu akitoa kichwa chake akiangalia jinsi ya kutoka nchi kavu,kuogelea akitafuta atoke nchi kavu lakini hakuweza na maji kuzidi kumshinda nguvu,maji yaliyo kua yanazunguka kwa nguvu sana hakuweza kushindana nayo na taratibu kuanza kunywa maji, hapo ndipo alipo jua kuwa masaa machache anaenda kufa,

licha ya kuishiwa nguvu hakutaka kufa bado alijipa moyo kuwa atapata sehemu ili anusuru roho yake, kwa mbali aliona gogo la mti na kuanza kuogelea kulifuata.

Alipo lifikia aliweka kichwa chake juu ya gogo hilo aliloamini kuwa ndilo litakua msaada pekee kwake!

Akiwa anatetemeka sana huku meno yake yakiwa yanagongana kutokana na baridi kali, alizidi kusogea mbele na gogo hilo,harufu kali sana za maiti ndizo zilimuumiza pua zake, aliona miili ya watu ikipelekwa na maji na kumfanya azidi kuogopa, bado mvua ilizidi kunyesha usiku huo bila kuacha.

Matumaini ya kupona yalipotea baada ya maji makali kulipiga gogo la mti ambalo aliweka kichwa na mikono yake kwa juu na kufanya lihame, hapo ndipo maji yaliyokua yana zunguka yalianza kumzungusha aliibuka mara moja! Mara ya pili. Ya tatu! Alikua teyari kasha ishiwa nguvu zake kabisa,
Hakuna alicho subiri zaidi ya umauti kumkuta alimkumbuka Mama yake mzazi, alimkumbuka Enock na vitu vingi vilivyotokea katika maisha yake.

“Ehh Mungu!, naomba unisamehe dhambi zangu zote kabla hujaichukua roho yangu na kuungana na Baba yangu huko alipo”

Alisema maneno hayo ndani ya moyo wake huku akizidi kunywa maji hayo na taratibu kuanza kumpeleka,miguu na mikono yake vyote vilishindwa kufanya kazi kabisa. Umauti tu ndio kitu pekee alichojua kinachofuata baada tu ya muda mfupi ujao, giza nene lilianza kutanda juu ya macho yake na mapigo yake ya moyo kumwenda taratibu sana huku akizidi kuzama chini ya maji baada ya kunywa maji mengi na kujaa kwenye mapafu yake!,

yalimfanya awe mzito hapo ndipo macho yake yalipo funga na giza nene kutawala mbele yake baada ya kuteseka sana na kukosa pumzi pia!

“Noo msimuuwe!”

Kauli ya mwanamke huyo ndiyo pekee iliowazuia watu hao weusi wenye hasira kushusha mitutu yao chini na hapo ndipo Kway alipokua ameponea chupchup!

akiwa amepiga magoti huku bado mvua inanyesha, walimchukua na kuingia nae ndani ya nyumba hiyo kisha kumfungia ndani ya chumba kidogo,

Bado alikua na machungu baada ya mtoto wake Natu pamoja na Enock kulipuka ndani ya helikopta, aliona kuja Uganda alifanya kazi bure ni bora angebaki, alishampata tayari mtoto wake mikononi mwake na kuuwawa mbele ya macho yake,alibaki akijilaumu sana, akiwa amefungwa juu ya kiti mikono yake ikiwa kwenye kamba kwa nyuma.

Alitulia kidogo baada ya chumba kufunguliwa na mwanamke mwenye macho makubwa kuingia.

“Joyla, nini unafanya?”

Aliuliza kway akiwa katika maumivu moyoni.

“ha ha ha ha Dear X Kway, nilikupenda sana wewe mwanaume, nilikupenda sana, alafu nilikua sijui kuwa ulimfuata mtoto wako, lakini pole sana, vipi mkeo hajambo?, nilivyosikia unaoa nilitaka nije kwenye harusi yako ila nilishindwa”

“Joyla naomba niache niende”

“hapana huwezi kwenda popote pale”

Taratibu mwanamke huyo aliye kua anajiamini alisogea midomoni mwa Kway na kuanza kumnyonya mdomo wake.

“bado nakumbuka mengi tuliyo yafanya Kway, namkumbuka Marehemu Ramsey rafiki yako, juzi ndipo niligundua kuwa Catherine ni mtoto wake, lakini kabla sijakuua naomba nikwambie ukweli, nilisha toa mimba zako tatu,”

Aliongea kwa majigambo huku akitembea tembea huku na kule kwa dharau na kebehi sana. Mwanaume aliyekua juu ya kiti walikua wapenzi kipindi cha nyuma kilicho pita lakini sasa hivi hakua na mapenzi nae tena ilikua ni lazima amuuwe tu na ndo hiko kilikua ndani ya moyo wake.

KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

14 Bikra Yangu Simulizi Z14
Jiunge kwenye mazungumzo
Chapisha Maoni