BIKRA YANGU (43)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA AROBAINI NA TATU
ILIPOISHIA...
Aliongea kwa majigambo huku akitembea tembea huku na kule kwa dharau na kebehi sana. Mwanaume aliyekua juu ya kiti walikua wapenzi kipindi cha nyuma kilicho pita lakini sasa hivi hakua na mapenzi nae tena ilikua ni lazima amuuwe tu na ndo hiko kilikua ndani ya moyo wake.
SASA ENDELEA...
“Fuc** you Joyla!,Fuc** you once again fuc*** you I said!”
Kway aliongea kwa hasira sana akitukana! na kutamani kutoka juu ya kiti alichowekwa sababu aliongea huku akijaribu kusimama lakini alishindwa, hasira tayari zilisha mtawala na misuli ya kichwani kumsimama
“unasema?”
Alihoji Joyla
“Fuc** you”
Pale pale alipokea kofi kali sana la shavu na kumfanya adondoke chini mzima mzima kama gogo na kiti alicho fungwa,
Joyla alitembea mpaka nje na kurudi akiwa na bastola mikononi mwake hapo ndipo alipo ikoki na kumuwekea kway usawa wa kichwa bila kuuliza chochote alifyaatua,
Lakini katika hali ya kushangaza akiwa chini kwenye kamba zake baada ya risasi hiyo kusikika hakusikia maumivu yoyote yale na kushindwa kuelewa nani aliye pigwa na risasi, alivyofumbua macho yake alimuona Joyla yupo chini. Amedondoka chali!.
“usiondoe Helkopta, si unaona kuna mtu bado hajaingia, acha upumbavu!”
“hapana siwezi tuta kufa”
“nimesema tumsubiri”
“hapana wewe niue tu”
Dereva wa helkopta japo aliwekewa kisu shingoni mwake, hakutaka kubaki chini baada ya kuona wana shambuliwa na risasi kutoka kwa walinzi,
Natu alilia sana baada ya kuona wana muacha baba yake chini hakukua na jinsi tena ya kurudi sababu ya walinzi kuanza kuwa wengi na kuishambulia Helkopta hiyo, ambapo baada ya sekunde nne ilianza kutoa mlio kuashiria kuwa injini ina matatizo ivyo kuna mawili tu ilibidi yafanyike,
waruke nje au watue chini na helikopta, japo wazo la pili hawakudhani kama lingefaa hapo ndipo Enock bila kujifikiria alimshika Natu vizuri na kuruka nje huku nyuma akiacha mlipuko mkubwa wa helkopta,
Walitua mpaka juu ya maji na kumuweka Natu vizuri mgongoni mwake na kuanza kupiga mbizi mpaka alipo fika sehemu salama.
“Natu naomba nisikilize, wewe ni mtoto mzuri sana, naomba unisubiri hapa sawa, usitoke naenda kumchukua baba yako”
Alizungumza Enock na kumuweka Natu sehemu ambayo haitoweza kuingia maji ili yeye arudi mwenyewe kwenda kumuokoa Kway.
Alivyo maliza hayo yote alijitosa ndani ya maji na kuanza kupiga mbizi mpaka ndani ya nyumba hiyo kubwa na kumkuta mlinzi getini alimvuta na kumkaba shingo kisha kuchukua silaha yake, na ndo hapo alipoanza kuwa uwa walinzi wote mpaka kuingia chumba alichokua ame fungwa Kway na kumkuta Joyla kashika bastola mkononi,
kabla ya kufyatua bastola yake alimpiga teke na kumfanya Adondoke chini.
“bratha Kway, upo salama?”
Aliuliza Enock akiwa na bastola yake mkononi
“nipo salama”
Jibu hilo lilimfanya amgeukie Joyla na kumpiga teke la tumbo bila huruma, Alisha changanyikiwa tayari alicho taka kujua kwa wakati huo ni wapi Catherine alipo na wala sio kitu kingine, alizidi kumpiga mateke na kumsimamisha mpaka ukutani.
“paaaaaaaa”
Bila huruma alimfyatua bastola ya mguu pale pale na kufanya Joyla atoe siri zote.
Watu walizidi kusombwa na maji na hali kuwa tete, ilibidi tu jeshi la polisi watumie maboti maalumu ili kuokoa maisha ya watu, hapo ndipo walianza kutembeza boti zao huku wakitafuta watu usiku huo huo wakiwa na tochi kubwa sana, walizidi kupiga patro na kufanikiwa kuokoa baadhi ya watu.
“jamani sio mtu Yule!?”
Aliuliza Askari mmoja wao huku akiwashtua wenzake wote walipiga tochi zao na kuona mtu kwa mbali, walianza kupeleka boti zao, ila walipo fika mahali walipo muona walishangaa kutokumuona tena.
“si alikua hii fasi?”
“ndio!”
“sasa amekwenda wapi?”
“embu tusubiri”
Walizidi kupiga tochi zao huku na kule walivyoangaza ndani ya maji waliweza kumuona Catherine akiwa taratibu anazama chini ya maji, hapo ndipo mmoja wa askari alipojitosa na kuingia mpaka ndani ya maji,
Baada ya sekunde kadhaa aliibuka nae akiwa amemshika kiunoni walisaidiana mpaka kumuingiza ndani ya boti hio HUKU WAKIMUONEA HURUMA jinsi alivyo kua na hali mbaya sana ameya fumba macho yake,
hakuna walichofanya zaidi ya kuanza kumpa huduma ya kwanza wakimkamua maji yaliyokua yamejaa tumboni mwake., waliendelea kusaka watu. mpaka kunakucha waliweza kuokoa idadi ya watu hamsini na mbili huku watu themanini wakiwa teyari wamepoteza maisha yao baada ya kufamaji.
Kulivyokucha asubuhi walimuwaisha Catherine Hospitali sababu ndiye yeye peke yake alionekana kuwa na hali mbaya kuliko wenzake wote, moja kwa moja aliingizwa chumba cha wagonjwa maututi na matitabu kuanza harakaharaka!,
Baada ya siku mbili hali yake ilizidi kuwa nzuri sana,
“hali yako iko aye, uko bien”?
Sauti hiyo ndiyo iliyo mfanya ayafumbue macho yake sababu aliitambua sana haikua ngeni katika masikio yake, aligeuza shingo yake na kumtizama mwanamke aliye kua amefunga tenge kubwa akiwa pembeni ya kitanda ana muangalia mgonjwa mwingine!.
“Anti Julia?”
Aliita Catherine baada ya kumuona mwanamke huyo pembeni yake!
Alikua ni MWENYE furaha muda wote usoni mwake mpaka ndani kabisa ya moyo wake, lakini kilicho mchanganya zaidi ni kuhusu baba wa mtoto aliye jifungua ambaye alikua ni Kway mpaka wakati huo hakua na mawasiliano mazuri na Mwanaume huyo aliyembebesha mimba mpaka akajifungua,
Bado alikua amelala kitandani akipatiwa matibabu na madaktari ndani ya hospitali ya Mico hapo sinza, ndugu jamaa na marafiki walifika ili kumpa pongezi kwa kujifungua kichanga ambaye alimpa jina Christopher alimpenda sana mtoto huyo japo hakuzaa na Ramsey, aliamini kile kilicho tokea kwa wakati huo ni mipango ya Mungu aliye juu mbinguni!
Wifi yake aliyeitwa Loydah dada yake na marehemu Ramsey pia alikua amesimama wima pembeni ya kitanda chake, ndani ya akili yake hata yeye alitaka kujua ni nani muhusika wa mtoto huyo haswaa!
Bado alikua na alama ya kiulizo ndani ya kichwa chake alisubiri watu waondoke kisha kusogea karibu na kuanza kumuhoji Sabrina maswali.
“una jisikiaje na hali wifi yangu?”
Aliuliza Loyda
“Mungu ni mwema!,”
“lakini bado sija jua baba yake na huyu mtoto ni nani?”
“utamjua tu usijali wifi yangu”
Majibu hayo ndiyo yalimfanya anyamaze . Loyda alimshika mtoto huyo mtoto na kumuweka mikononi mwake.
“anaitwa nani?”
“Christopher, jina la babu yake”
“mmmh ahhhhhaaa…jina zuri sana”
Aliitikia Loydah, lakini ilionekana kabisa hakufurahishwa na mtoto huyo kuzaliwa na wifi yake, kitu kama dharau au nyodo ndicho alicho kitafsiri ndani ya akili yake kupitia Sabrina kuzaa mtoto huyo,
alimkumbuka kaka yake Ramsey ambaye kwa wakati huo alikua amefukiwa mavumbini ametangulia mbele ya haki kisha kumtizama tena Sabrina,
“nataka kujua mtoto huyo ni wa nani Sabrina?”
Safari hii aliuliza akionyesha hasira za wazi wazi
“wifi subiri hali yangu ni mbaya ila nita kwambia tu”
“sawa, nitarudi kesho ili uniambie”
Maneno aliyo kua akiongea haya kua hata na punje ya masihala ndani yake, ndani ya nafsi yake alitaka kweli kumjua mwanaume aliyemzalisha wifi yake, japokua hakujua akimjua ni kipi amfanye!
Sabrina hakutaka kulifikiria sana hilo, alimuacha mtoto wake kitandani na kutoka nje akielekea msalani kujisaidia , baada ya kurudi alishtuka sana baada ya kuona sura ya mzee Mwasha ikiwa mbele yake tena amemshika Christopher mikononi mwake na kutabasamu.
“hongera Sabrina,!”
Alisema Mzee Mwasha
“Ahsante!”
Kitendo cha kujibu ivyo alimvaa na kumpokonya mtoto huyo mikononi mwa Mwasha sababu alijua mzee huyo ni hatari sana na alikuja hapo hospitali kwa nia moja tu kulipa kisasi, aliyakumbuka yote yaliyo tokea kipindi cha nyuma, kama aliweza kumtandika risasi mtoto wake wa kumzaa Enock hatoshindwa kumuuwa Christopher au yeye hapo alipo,
Hofu ilizidi kumtawala ndani ya moyo wake huku akimtizama mzee huyo aliye simama mbele yake ana tabasamu.
“mbona umeni pokonya sasa mtoto?”
“sitaki! kaa mbali na mwanangu”
“ha! ha! ha! ha! ha! ha!, Catherine yuko wapi?”
“sijui, naomba uwende”
“okay, mimi naenda lakini…….”
Maneno hayo hakuweza kumalizia na taratibu kuanza kuondoka huku akimuoneshea Sabrina ishara ya kumkata kichwa baada ya kupitisha mkono wake shingoni akimpa kama ujumbe,
Alisha dhamiria kuteketeza uzao wa Ramsey na hiko ndiko alicho jiapizia miaka mingi iliyo pita mtoto mchanga aliye ji fungua Sabrina alikua teyari kasha ingia kwenye huo mkumbo,
ilikua ni lazima nayeye amuangamize kwani ni kizazi cha Ramsey, ni mtoto wa Sabrina!.
Masaa yalienda huku bado akiwa na hofu sana moyoni mwake bado alimfikiria mwanae Christopher aliye kua bado mdogo sana kuingia ndani ya matatizo hayo makubwa yaliyo sababishwa na Ramsey!.
Walisha shauriana vya kutosha na kupata muafaka kuwa wampakie Natu ndani ya ndege ili wao waendelee na msako wao, sababu hatua ya kwanza ilikua teyari ime kamilika kilicho baki hapo ni kitu kimoja tu kumtafuta Catherine kwa wudi na uvumba.
Enock alishaamua kujitoa muhanga iwe kufa au kupona ili mradi ampate Catherine ndipo moyo wake uta tulia hakuna alicho fikiria zaidi ya kufunga ndoa kubwa itakayo weka historia hata nje na ndani ya Afrika!,
Hali ya hewa kidogo ilikua shwari! Magari machache ndiyo yaliweza kutembea barabarani na kupata usafiri mmoja ulio wapeleka mpaka Entebbe uwanja wa ndege ili wampakie Natu afike Tanzania.
“Hallo Molito, ndio nishampata, Ahsante kaka, ndio atafika hapo jioni saa kumi na AIRUGANDA, ndio mpaka nitakapo rudi, sawa ndugu kazi njema Mungu akubariki”
Baada ya kukata simu alimkombatia mtoto wake na kumkabidhi kwa mmoja wa waudumu wa ndege ili ahakikishe usalama wa mwanae mpaka atakapo fika.
“when you reach, call this number(ukifika piga hii namba)”
Aliongea Kway akimuachia namba mhudumu wa Ndege hiyo akimkabidhi Natu,baada ya taratibu hizo kukamilika, walirudi akiwa pamoja na Enock kwa kazi moja tu kuanza safari ya kumtafuta Catherine wakitumia usafiri wa gari la kukodi,
Ilikua ni lazima warudi Tanzania na Catherine ndipo roho ya Enock itulie, Kway alikua juu ya usukani huku kushoto akiwa ameketi Enock.
“Blazza kway ahsante sana, napenda kukuhaidi kuwa kama mkwe sijui niseme.., niki mpata Catherine nita fanya harusi kubwa sana utashangaa mwenyewe, nitakupa zawadi kubwa sana,”
Aliongea Enock kwa hisia sana huku akimaanisha
“Enock ndugu yangu, mimi sio wa kunipa zawadi hio ina takiwa umkabidhi Mama yake”
“alafu kuna kitu nilikua sija kwambia”
“kitu gani?”
“Mama yake kaji fungua mtoto wa kiume”
“Mama yake nani?”
Aliuliza Kway huku akimtizama Enock machoni mikono yake miwili ikiwa juu ya usukani
“Mama yake na Catherine”
“ahaaaa okay!”
Hakutaka kujua mengi sababu Alisha jua kuwa mtoto huyo ni wake na wala sio vinginevyo alirudisha macho yake mbele na kuzidi kusonga mbele, walisha tembea sasa masaa takribani matatu barabarani walifika Gatuna na kupiga passot zao mihuli kisha kuzidi kusonga mbele,
baadaye walifika Ruzizi boda ya Congo na kuzidi kusonga mbele,
Harufu za mizoga ya binadamu ndizo zilizo mshtua Enock aliye kua amelala fofofo, tayari kulikua kumekucha baada ya kutembea mwendo mrefu sana.
KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni