BIKRA YANGU (44)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA AROBAINI NA NNE
ILIPOISHIA...
Harufu za mizoga ya binadamu ndizo zilizo mshtua Enock aliye kua amelala fofofo, tayari kulikua kumekucha baada ya kutembea mwendo mrefu sana.SASA ENDELEA...
“hapa wapi?”
“tushaingia Demokrasia ya Kongo, bado kidogo tuna fika Kinshasa”
“huku umepajuaje blazza kway?”
“nilikua natafuta maisha”
Walizidi kusonga mbele ila Enock alipiga kelele baada ya kufika darajani na kupiga jicho lake chini, aliona Nissan Mkonge lenye namba za Uganda na kukumbuka kuwa aliambiwa kuwa Catherine ndiyo alisafirishwa kwa kutumia gari ya aina hiyo.
Walisimamisha gari na kushuka huku wakienda chini darajani kulikua kuna tisha sana, miti ilikua ni mingi mno, taratibu walijongea mpaka kwenye gari hilo bila ya kuona dalili ya kuwa na mtu yoyote Yule, ila ghafla walisikia kelele za watu,
Kitendo cha kugeuka nyuma waliowaona watu waliovaa majani wakiwa na mishale mikononi mwao na kuwaweka chini ya ulinzi.
Huku wakiongea lugha za ajabu na kucheka,
“hawa watu gani?”
“hata mimi sijui, ila kwa haraka haraka nimeelewa, wamesema kuwa wame pata vitoweo”
“unasema nini?”
Alihamaki Enock huku akitoa macho yake na kuzidi kuwashangaa watu hao wa ajabu mbele yake waliozidi kuwasogelea karibu yao wakizidi kucheka na kuruka ruka
Kitendo cha kugeuka nyuma waliowaona watu waliovaa majani wakiwa na mishale mikononi mwao na kuwaweka chini ya ulinzi.
Huku wakiongea lugha za ajabu na kucheka,
“hawa watu gani?”
“hata mimi sijui, ila kwa haraka haraka nimeelewa, wamesema kuwa wame pata vitoweo”
“unasema nini?”
Alihamaki Enock huku akitoa macho yake na kuzidi kuwashangaa watu hao wa ajabu mbele yake waliozidi kuwasogelea karibu yao wakizidi kucheka na kuruka ruka
Catherine Baada ya kuponea chup chup nchini Kongo na kuokolewa na jeshi la polisi la majini, hali yake ilikua mbaya sana na kupelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu, hapo ndipo alipo kutana na Julia au Mama Natu.
Alivyo ruhusiwa hospitali tu ili bidi achukuliwe na Julia sababu hakua na sehemu nyingine yoyote ile ya kuishi, shukrani alizompa shangazi yake huyo hazikua na mfano, hapo ndipo alipoanza kumueleza juu ya yaliyo mtokea na mpaka kukutana na Mwanae Natu,ndani ya jumba hilo wakiwa nchini Uganda.
“hapana sio kweli, Natu Alisha fariki”
“Kweli Anti”
“hapana, sio kweli sio kweli”
Julia alikataa katakata juu ya swala hilo, aliamini mwanae kasha fariki dunia hakutaka tena kukumbuka yaliyotokea katika maisha yake, sababu alisha anza maisha mapya!
Julia hakua na kinyongo cha aina yoyote ile juu ya Catherine alishajua kuwa mama yake alibeba mimba ya Kway, ili bidi tu amchukulie kama mwanae wa kumzaa hakua na jinsi yoyote ile ya kukataa ukweli hakutaka kumwambia chochote,
Alishakaa nyumbani kwa Julia BUKAVU siku tatu sasa, ambapo hapo alikua akiishi na kaka yake!
“Anti naomba niazime simu yako niongee na Mama, nimpigie simu”
Alisema Catherine
“sawa,”
Baada ya kupewa jibu hilo alikabidhiwa simu ya mkononi ili afanye mawasiliano na Mama yake mzazi, alibonyeza namba za mama yake na kuiweka simu sikioni.
“halloo Mama shikamoo!”
Baada ya simu kupokelewa Catherine alisalimia
“Nani, Catherine mwanangu upo wapi? Upo salama?”
“ndiio mama nipo salama”
“upo na Enock?”
Hilo ndilo swali lililo mfanya Catherine akae kimnya hakuelewa chochote juu ya Enock, hakuelewa kuwa mwanaume huyo alimfuata Mpaka Uganda kwa ajili ya kumuokoa
“hapana Mama”
“si alikufuata?”
“nani Enock? wapi?”
Catherine alitafakari kwa kitambo kidogo kabla ya kutoa jibu
“Uganda, kwani wewe upo wapi?”
“nipo kongo kwa Anti Julia, ”
Hapo ndipo ukimnya ulitawala, kumbu kumbu zili mpeleka siku aliyokua akimfokea Kway juu ya ujauzito wake kisha baada ya siku mbili Loyda alimwambia kuwa alipata ajali mbaya siku hiyo hiyo,aliomba simu ili amuombe msamaha, ilikua ni lazima afanye ivyo,
Baada ya kupewa simu alianza kuomba msamaha uku akijutia kwa aliyo yafanya alijua yeye ndiye chanzo cha kuvuruga ndoa yao hiyo ya watu hao wawili,ilibidi tu Julia atoe msamaha sababu aliamini yalisha pita hakukua na namna nyingine ya kuubadili ukweli, upande wa pili wa simu ulisikika mtoto akiwa analia hapo ndipo Julia alidondosha chozi.
“Mtoto ana itwa nani?”
Aliuliza Julia kwa sauti ya kinyonge huku akifuta machozi yake, Catherine aliyekua pembeni hakuelewa nini kinachoendelea hata yeye hakujua kuwa mama yake kajifungua mtoto. hakutaka kuuliza chochote zaidi ya kukaa kimnya lakini alihisi kuna kitu kinaendelea kati ya Julia na Mama yake, alihisi hawakuwa na maelewano mazuri, kupitia picha iliyokua mbele yake lakini hakutaka kuuliza, sababu aliamini hayamuhusu.
“anaitwa Christopher”
“sawa”
Baada ya kumaliza mazungumzo kwa njia ya simu wali tayarisha chakula kwa ajili ya kula usiku huo huku Julia akifanya taratibu za kumtafutia tiketi Catherine aweze kurudi Tanzania siku mbili zijazo fujo zikitulia.
Catherine hakuweza kulala usiku kucha aliwaza mambo mengi juu ya Enock, hisia zake zili mtuma atakua yupo sehemu amekwama au anateseka sana sababu ya mvua kali iliyokua ikinyesha,
aliwaza mambo mengi sana juu ya maisha yake yalivyokua yanaenda, vitu vingi sana alivikumbuka.
Kilicho mshtua zaidi ni kishindo kikubwa sana mithili ya bomu na kumfanya akurupuke kitandani, baada ya dakika chache alisikia milio ya risasi inarindima, alichungulia dirishani na kuona watu wanavyokimbia huku na kule,alivyotoka seblen alimuona Julia akijitaidi kufunga milango sababu hata yeye hofu ilimtanda.
“Anti kuna nini?”
“kuna vita,”
“vita!?”
“ndio, hawa bamutu ya huku kongo hawa wataki watu wa Rwanda, sasa naona wameamua kutumia njoo nguvu usiwe na wasi wasi juu la lolote”
Baada ya kuchungulia Dirishani waliwaona watu wafupi wakiwa na mitutu wapo nyumba ya jirani wamevunja mlango na kuwatoa vijana wawili wa Kinyarwanda, pale pale walipigwa risasi huku wengine wakipakiwa ndani ya gari,
Ilikua ni vita ya kutisha sana mara ya kwanza ilikua kama masihala, nyumba zili unguzwa na moto na watu wenye sura ndefu waliuwawa hawa kua na masihala hata kidogo,
“wewe ni Rwandee kaa chonjo”
Sauti hiyo ilipenya masikioni mwa Julia na Catherine wakishuhudia watu nje wakipangwa chini wakiwa wamepiga magoti yao, hapo ndipo mitutu ilikokiwa na watu hao kuuliwa pale pale kisha maiti kupakiwa ndani ya gari ili kwenda kutupwa. Ivyo ndivyo ilivyo kua walikua wakipita kila nyumba wakikagua,
Walipiga mlango teke na kufanya Julia na Catherine hofu iwatande.
Mtu mmoja mfupi mwenye misuli alimkata jicho kali Catherine huku wengine wakiwa wana kagua ndani ya nyumba hiyo.
“songa nasisi upesi!”
Aliamuru mtu huyo akiwa na mtutu dalili zilionesha kuwa walimuhisi Catherine ni raia wa Rwanda baada ya kuangalia pua yake ilivyo jichonga na sura yake iliyokuwa nyembamba kidogo.
“hapana huyo ni mutanzania”
Alidakia Julia akijaribu kumtetea
“shiii Funga,usiji fanye unajua”
Muda wote Catherine alikua akilia machozi akimuomba Mungu wake, aliamini huo ndio mwisho wa maisha yake, alichukuliwa na kusimamishwa nje ya uwanja mkubwa usiku huo ambao aliuita mwisho wa maisha yake!.
Akijimuika na wengine ambao baada ya muda mfupi wata pigwa risasi, watu takribani watano walisimama mbele yao wakiwa na mitutu mikononi mwao wameikoki tayari kwa kuachia risasi zao.
“Jamani mimi ni Mtanzania”
Aliropoka Catherine huku akijitoa kati kati ya kundi la watu akijaribu kuitetea nafsi yake hakufika mbali alipigwa na kitako cha mtutu kichwani na kumfanya adondoke chini na kuzirai, hapo ndipo kelele za mitutu zilisikika na damu nyingi kumwagika watoto kwa watu wazima walipo teza maisha yao siku hiyo.
Julia aliyekua dirishani alilia machozi sana baada ya kuona vile, alishuhudia wanavyo wapakia watu waliokufa akiwemo Catherine ndani ya karandinga na gari hilo kuondoka huku milio ya risasi ikisikika hewani!.
Sufuria kubwa sana lililetwa pembeni yao huku wakiwa wamefungwa kamba kwenye mti mkubwa. mbele yao kulikua kuna mwanaume wa kizungu nayeye kafungwa kamba pia , hawakuwa na ujanja tena walishajua wanaenda kuliwa nyama muda mchache ujao, hawa kutaka kuamini kuwa kuna binadamu kama hao bado wapo duniani!
Kway na Enock walizidi kustaajabu na kutandwa na hofu sana mioyoni mwao, kuni zilizidi kuchochewa na moto kuwa mkali, maji yaliyokua yanachemka yalizidi kutokota kumaanisha kuwa muda mfupi wange tumbukizwa ndani ya sufuria kubwa,
Mmoja wa watu hao aliye valia ngozi ya mnyama ili kuziba sehemu zake za siri alitembea huku akiwakagua mmoja baada ya mwingine kwa zamu ili kumchagua ni nani aanze, kila mtu alisali ndani ya moyo wake, macho yake yalitulia kwa kway, mijitu hiyo iliyovalia nguo za wanyama mwilini mwao ilianza kushangilia sana,
Kway alifunguliwa kamba na taratibu kuanza kupelekwa kwenye sufuria kwa ajili ya kuchemshwa, waliamini hapakuwa na masihali hata kidogo sababu aliona vichwa vya watu chini na baadhi ya viungo vya binadamu pembeni yake, walimfunga na kamba mwili mzima na kumpandisha juu huku taratibu wakimshusha kwenye sufuria, katika hali ya kushangaza walisikia milio ya risasi ziki pigwa hewani na wazungu kumi kuwazunguka.
Walivyotaka kutumia mikuki yao walisambaratishwa dakika hiyo hiyo na risasi ya mzungu
“Carlos! Are you okay?”
Mmoja wa wazungu aliita na kumfuata ndugu yake ambaye ilionekana ndiye waliyekuja kumuokoa, hapo ndipo walipo wafungua mateka wengine Kway na Enock Waliwashukuru wazungu hao sana, maana bila wao wangesha kuwa vitoweo na kuliwa nyama siku hiyo.
“Excuse me! may I use your phone?”(samahani naweza nikatumia simu yako”?)
Enock aliomba simu na kukabidhiwa sababu hawakuwa nazo kwa wakati huo, moja kwa moja alimtafuta Sabrina hewani kwa kujaribu kuvuta kumbu kumbu za namba zake kichwani sababu ndiyo ilikua ikimpigia mara kwa mara.
Nia yake ilikua ni moja tu kumjulisha habari za Catherine, kweli baada ya simu kupokelewa alimueleza kila kitu kilichokua kina tokea mpaka walipo fikia.
“Catherine yupo salama mbona, niliongea nae jana usiku, yupo Kongo!”
Alijibu Mama Catherine
“sasa nita mpata vipi?”
“subiri nakutumia namba za simu ili uweze kuongea nae”
“sawa nitashukuru sana”
Haikuchukua muda namba za Julia ziliingia kwenye simu yake na hapo ndipo alipoamua kumtafuta mwanamke huyo hewani mara moja,
Baada ya mazungumzo machache alianza kuhema juu juu huku mapigo yake ya moyo yakimwenda kasi, alihisi wenda hakusikia vizuri.
“unasema?”
“Catherine amefariki, ameuwawa na Masasi(risasi)”
Upande wa pili ulisikika wa simu kway aliye kua pembeni alimtizama Enock, kupitia macho yake alijua tu hakukua na taarifa nzuri hata kidogo, ilibidi apore simu na kuiweka sikioni.
“umesema Catherine kafanya nini?”
Aliuliza Kway
“Amefariki dunia, njoo kapigwa Masasi la…”
“Cherie. Mama Natu upo upo wapi?.”
Sauti ya mke wake hata siku moja haikuweza kumtoka wala kuisahau.
KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni