SEHEMU YA AROBAINI NA TANO
ILIPOISHIA...
“Amefariki dunia, njoo kapigwa Masasi la…”
“Cherie. Mama Natu upo upo wapi?.”
Sauti ya mke wake hata siku moja haikuweza kumtoka wala kuisahau.
SASA ENDELEA...
Hakuweza kuyazuia machozi yake yaliyo kua yakimbubujika kama mtoto wa miaka mitatu na kulowanisha mashavu yake yote mawili, maumivu makali aliyosikia ndani ya moyo wake hayakua na mfano wa kufananishwa na kitu chochote kile!,
“Hapana Catherine wangu, it is too early I have come for you my love!(bado mapema nimekuja kwa ajili yako mpenzi)”
Yalikua ni maneno yenye kutia huruma kutoka kwa Enock bado alikua aamini kama mwanamke anayempenda na aliyempigania kutoka Uganda mpaka kufika Kongo na leo anapewa taarifa kuwa amefariki Dunia!
Halikua jambo rahisi kabisa, aliupiga piga mti ulio kua pembeni yake huku akilia kwa machungu sana, tena kwa hisia, mambo waliyokua wakiyafanya hapo nyuma na Catherine ndiyo yalipita kichwani kwake na kujirudia rudia na kufanya kama mkanda wa.filamu unaosisimua, hakutaka kuamini kuwa Catherine amefarki bila ya kumuomba msamaha,ndoto za kufunga nae ndoa ya kifahari ambayo ingeongelewa na watu wote sasa ilianza kupotea na kuzimika kama mshumaa uliopulizwa na upepo.
“Enock!”
Aliita Kway akiwa pembeni yake hata yeye aliguswa vile vile.
“No Kway No, mpigie mkeo muulize tena”
“pole sana, yote tumuachie Mungu jikaze ita kubidi ukubaliane na matokeo, jikaze”
“siwezi Kway, inaniuma siwezi siwezi bratha”
Maneno hayo yalitosha kuonesha kuwa Enock aliguswa sana, aliserereka mpaka chini na kukaa kitako huku akilia sana machozi!
“Enock ujue nakupenda sana, wewe ndiye mwanaume wa maisha yangu”
Sauti ya Catherine ndiyo ilikua ikipita kichwani mwake huku akimuona siku hiyo wakiwa wote kitandani akiwa anatabasamu,
Ndani ya sekunde mbili alisimama kwa hasira huku akiwa anahema kifua kikipanda juu na kushuka chini na kupangusa machozi yake.
“nataka nirudi Tanzania sasa hivi!”
Alizungumza Enock
“mbona sikuelewi?”
“nataka nirudi Tanzania, tiketi nitakata wapi ya ndege?”
“inabidi turudi wote nisubiri!”
“hapana nenda kwa mkeo, mimi mtanikuta nikiwa hai sawa, ila nikiwa nime kufa basi”
Maneno aliyoongea Enock yalimchanganya Kway hakuelewa nini anazungumza, aliona wenda amerukwa na akili zake, alijitajidi kumzuia lakini hakuweza kufanikiwa neno Tanzania ndilo lilikua likitoka kinywani mwa Enock, japo hakutaka kusema ni kwanini anataka kurudi,
Hawa kuwa na haja ya kuendelea kulumbana ilibidi tu watoke msituni humo na kutafuta usafiri, ili Enock arudi Tanzania. Alianza safari vizuri baada ya kuingia ndani ya basi kubwa ambalo lilimpeleka mpaka Kinshasa hapo alichukua ndege mpaka Uganda akiwa amemuacha Kway,hapo alitafuta benki na kutoa kiasi kidogo cha pesa baada ya masaa mawili alikua teyari yupo angani na ndege hiyo kutua Tanzania Dar es salaam uwanja wa kimataifa mwalimu Nyerere safari nzima alikua hasemi kitu chochote mpaka anafika asubuhi.,
Mambo yaliyokua yana tokea katika maisha yake bado alikua anadhani anaota njonzi ndefu na muda mfupi angeenda kuzinduka,alicho kuwa anawaza wakati huo sio kitu kingine bali ni kumtafuta Baba yake mzazi mzee Mwasha, hisia zake zilimtuma kuwa yeye ndiye aliye sababisha mpaka maisha yake yame kua kinyume!.
Alishaamua kumchukia mazima aliwaza vitu vingi sana vilivyo sababishwa na baba yake, aliwaza jinsi alivyotaka kumuua,
Alitafuta taxi na kunyoosha mpaka nyumbani kwake, ila kilicho mshangaza ni baada ya kuona kuna sura ngeni kila aliye muona alimshangaa wengine walianza kukimbia huku na kule wakipiga kelele,
kwa mara ya kwanza hakuelewa nini kiliwa kimbiza watu hao lakini alikumbuka kuwa walidhani amekufa ivyo walimuona ni kama mzimu au mzuka,
hakua na muda wa kuongea na mtu yoyote alinyoosha mpaka ndani.
“Jamani majirani uwiii mzimu”
Kelele izo alizitoa Mdogo wake na Heather baada ya kumuona Enock kaingia ndani aliogopa sana hata yeye na kutoamini kuwa ana ona kitu cha ukweli mbele yake, alidhani wenda anaona maluwe luwe.
Bado alikua na hasira hakuweza kuongea chochote alinyoosha mpaka chumbani kwake haraka haraka na kufungua kabati,alikumbuka vizuri aliweka kisu kirefu cha kujikunja.
“nikishamuua na mimi najiua!”
Aliwaza Enock na kutoka nje haraka haraka, ndani ya akili yake aliwaza kitu kimoja tu kum-maliza baba yake mzazi na baadaye ajiue, mwanamke anayempenda Alisha kufa tayari aliona ni bora amfuate huko alipo ili waweze kuungana mbinguni na waweze kuendeleza mapenzi yao huko huko!.
Alitafuta taxi mpaka oysterbay nyumbani kwa baba yake mzazi, alishuka na kumkabidhi dereva pesa yake, kabla ya kuingia ndani ya geti alisimama nje na kuiangalia nyumba ya baba yake, alikumbuka mambo mengi sana akiwa mdogo akiwa na wazazi wake wote wawili wakiishi kwa furaha na leo hii anaenda kumuuwa baba yake mzazi hii yote yalisababishwa na Mapenzi.
Aliukunja mdomo kwa hasira na kuyabana meno yake na kulisukuma geti kwa nguvu, hakukua na mtu yoyote Yule ila aliliona gari la baba yake na kugundua kuwa yupo ndani!,
Alipita seblen na kumkuta Baba yake yupo na mwanamke mwingine
“Dad!”
Aliita huku akikitoa kisu kiunoni mwake
“Enock my son!”(Enock mwanangu)”
“No! am not your son,(hapana mimi sio mwanao)”
Alijibu Enock huku akizidi kusogea na kisu picha ilionesha kuwa alidhamiria kumuuwa baba yake tena kwa kisu
“unataka kufanya nini”?
“nataka kukuua , Nataka kukuua mbele ya Malaya wako, wewe sio baba yangu, wewe sio baba yangu, ulitaka kuniua kipindi nipo hospitali, umefurahi sasa Catherine amekufa, nakuuliza umefurahi, baba nini kimekukumbuka, mwanamke ndiyo anakufanya utake kuniua?”
Enock huku akilia kwa uchungu na Hasira za waziwazi haikua rahisi kutuliza hasira za mwanaume huyo aliyekua na kisu mkononi tayari kwa kuua.
“hapana mwanangu, mama yako ndiyo chanzo, Mama yako ndiyo chanzo!”
“usimtaje Mama yangu”
Alichomoka haraka haraka huku akiwa na kisu mkononi mwake kakishika vizuri tayari kwa kumchoma Baba yake mzazi, ilikua ni vita tayari, lakini alivyotaka kumchoma kilishikwa tayari na kuanza kushindana nguvu huku Mwasha akijaribu kukizuia kisu kisizame ndani ya tumbo lake,
Mwanamke mnene maji ya kunde aliyekua akishuhudia kitendo hiko aliokota kitu kilicho fanana na udongo cha kuwekea maua na kumpiga nacho Enock kichwani, hapo ndipo alipo dondoka na kelele kusikika huku damu nyingi kutoka kwa Enock zikichuluzika chini na kumfanya apige kelele za maumivu sababu ya kisu alichokua amekishika kuzama mwilini mwake!.
Tipa lililokua lime beba maiti lilibinuka kwa nyuma ili kumwaga maiti jalalani za wanyarwada waliokufa kwa kupigwa risasi na wakongo, lilikua nje kidogo ya mji wa Bukavu baada ya vita kubwa kutokea, hapo ndipo walipokua wana mwagwa maiti kisha kwenda kuchukua nyingine,
Alihisi mwili wake mzito sana miili ya watu waliokufa baada ya kupigwa risasi zilimkandamiza na kuzibana mbavu zake,kwa nguvu sana Catherine alizisukumiza na kuanza taratibu kusimama.
Alikua amepona ni baada ya kupigwa na mtutu kichwani na kuzirai hiyo ndiyo ilikua ponea yake,
Hakuelewa ni wapi alipo.Alikua amezungukwa na maiti nyingi pembeni yake zilizo kua zina toa harufu kali sana na kufanya pua zake zimuume mno!, bado ulikua ni usiku mnene wa kutisha mbalamwezi peke yake ndilo lililomsaidia kuona mbele, alianza kutembea akifuata matairi ya gari yalipo pita, alizidi kusonga mbele usiku huo akizipita maiti zilizo kua zina liwa na mbwa,alimuomba sana mungu amlinde aliamini bado anamtetea na isingekua yeye angesha kufa tayari na sio vinginevyo.
Alitembea mpaka alipo fika bara bara kubwa akiwa amechoka hana nguvu na kukaa pembezoni ili walau apate msaada wowote ule,
Kwa mbali alisikia muungurumo wa gari na kusimama ili aombe msaada, lakini alishindwa kujua afanye nini baada ya kuona ni tipa kubwa huku juu wakiwemo maaskari wakiwa na mitutu mikononi,
Alijua ni lazima walikua wakongo walioanzisha fujo na kuwauwa wanyarwanda vita ilikua bado ni kali bado.
Hapo ndipo alipogeuka na kuanza kukimbia ili kunusuru maisha yake, tipa lilisimamishwa na watu wanne kushuka na mitutu wakianza kumfukuzia kwa nia moja tu wam-miminie risasi ili wamuuwe.
Alizidi kusonga mbele akikimbia na kuingia ndani ya kimsitu kidogo chenye miti licha ya kukimbia lakini alisikia vishindo vya watu hao wakiwa nyuma yake wakimulika mulika tochi zao, bahati mbaya alikanyaga majani na kupiga mueleka hapo ndipo alipoanza kubiringika kama mpira kuelekea chini mabondeni.
Alijua ni lazima walikua wakongo walioanzisha fujo na kuwauwa wanyarwanda vita ilikua bado ni kali bado.
Hapo ndipo alipogeuka na kuanza kukimbia ili kunusuru maisha yake, tipa lilisimamishwa na watu wanne kushuka na mitutu wakianza kumfukuzia kwa nia moja tu wam-miminie risasi ili wamuuwe.
Alizidi kusonga mbele akikimbia na kuingia ndani ya kimsitu kidogo chenye miti licha ya kukimbia lakini alisikia vishindo vya watu hao wakiwa nyuma yake wakimulika mulika tochio zao, bahati mbaya alikanyaga majani na kupiga mueleka hapo ndipo alipoanza kubiringika kama mpira kuelekea chini.
“ongoza mbele, ukijaribu kupiga kelele tu nasambaratisha huo ubongo wako sasa hivi!”
Sabrina alitii amri hiyo kutoka kwa mtu mweusi mrefu sana mwenye makunyanzi usoni na mwenye makovu pia, uso wake ulijaa mabaka sana alionekana kabisa ni jambazi tena sugu,
Alisha muweka Sabrina chini ya ulinzi akiwa na bastola ndogo mkononi mwake, ndani ya akili yake Alisha jua kuwa anaenda kufa, na jitu lililokua mbele yake lilitumwa na Mwasha hakua na chaguo lingine zaidi ya kumbeba mtoto wake mchanga Christopher aliyekua akilia muda wote usiku huo alijua teyari vita imeanza kati yake na Mzee Mwasha.
“naomba niende na mwanangu”
“twende, twende”
Alimuweka mwanae mgongoni na kuamriwa abebe na funguo zake za gari, walitoka mpaka nje na ndiye aliyeamuriwa aendeshe gari huku jitu hilo jambazi likifuatia upande wa kushoto mkononi akiwa ame mbeba Christopher mtoto mdogo na mkono wake mwingine wa kuume ukiwa na bastola.
“washa gari”
“tunaenda wapi?”
“oysterbay, naomba usifanye kitu chochote cha kijinga, twende”
Kilicho fanya watu wa nje wasijue kinachoendelea ndani ya gari ilikua ni vioo vyeusi yaani tinted, walinyoosha barabara kubwa ya tegeta huku Sabrina njia nzima akiwa analia kwa kwikwi,
hiyo haikufanya jambazi aliyemuweka mateka abadilishe maagizo aliyo ambiwa na bosi wake.
“najua umetumwa na Mwasha”
Alizungumza Sabrina
“Kaa kimnya, ka kimnya endesha gari”
Gari lilizidi kwenda mpaka walipo fika Oysterbay kwenye nyumba kubwa ya gorofa kisha geti kufunguliwa, hapo ndipo alipo pata jibu la swali lake kuwa Mwasha ndiye aliye toa agizo la yeye kutekwa nyara baada ya kumuona amesimama nje anawasubiri,alivyo waona tu alitabasamu kumaanisha kuwa amefanikiwa.
“Ha!Ha!Ha!Ha!Ha! Sabrina, Sabrina, nafikiri unajua kwanini upo hapa, Kobelo mpeleke huyo stoo kule uwani,”
Alitoa kauli moja hiyo Mwasha na Sabrina kuanza kukokotwa mpaka nyuma uwani ndani ya stoo iliyo tumika kuifadhia spea za magari na kufungiwa kwa nje akisubiri kitu kimoja tu mwisho wa uhai wake.
KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA