SEHEMU YA AROBAINI NA SITA
ILIPOISHIA...
Alitoa kauli moja hiyo Mwasha na Sabrina kuanza kukokotwa mpaka nyuma uwani ndani ya stoo iliyo tumika kuifadhia spea za magari na kufungiwa kwa nje akisubiri kitu kimoja tu mwisho wa uhai wake.
SASA ENDELEA...
Alimnyonyesha mtoto wake maziwa aliyekua akilia, alivyo hakikisha amelala alisimama na kuanza kuchungulia nje akiya lazimisha macho yake kuona mbele kutokana na giza totoro,ilikua ni lazima atoroke au aondoke, alipitisha mkono wake kwenye kitundu kidogo na kupapasa kwa nje, ila alikata tamaa baada ya kugusa kufuli kubwa na kuishiwa nguvu zote mwilini mwake,alirudi kinyume nyume mpaka ukutani na kumbeba mtoto wake mikononi akitafakari nini cha kufanya alivyo papasa papasa pembeni aligusa kitu kama chuma alivyo kitizama vizuri aligundua ni exsozi ya gari, alitafakari kwa kina na kutulia kimnya, hakuweza kulala mpaka kunakucha.
Parakacha za mtu kutokea nje ya stoo ndizo zilimfaya akamate chuma hiko vizuri nyuma ya mikono yake tayari kwa kujiokoa, ilikua ni lazima ajaribu kujiokoa ili hata akifa ajue kuwa alijaribu kujitetea lakini alishindwa, hakua na uhakika kwa kile alichotaka kukifanya kitafanikiwa, lakini alipiga moyo konde!,alisogea mpaka kando ya mlango na kumsubiri mtu anaye kuja,
Bila kujiuliza mara mbili mbili alikishusha chuma juu ya utosi wa Kobelo aliyekua na bastola mkononi mwake kutokana na kutokujiaandaa alidondoka chini puuh!
Hapo ndipo alipo chukua bastola na kuishika vizuri lilikua ni jambo la ujasiri hata yeye hakuelewa ujasiri huo kautolea wapi, alitoka nje na kuchungulia usalama kisha kurudi ndani kumchukua mwanae, alimfunga vizuri mgongoni mwake na kuanza kutembea taratibu lakini kabla ya kupiga hatua, dirishani alisikia sauti ya mtu akilumbana,
Alivuta kumbu kumbu na kuchungulia dirishani, hakuamini baada ya kumuona Enock akiwa amesimama ameshika kisu kisha baadae mwanamke aliyesimama kumpiga Enock kichwani,hayo yote yakiwa yanatokea aliya shuhudia kwa macho yake yote mawili, kitendo cha Kumuona Enock alijua kabisa lazima Catherine atakua kasha rudi nae tena salama salmin, ilikua ni lazima afanye jambo ili amuokoe mwanaume huyo.
“Bastola yangu iko wapi?”
Sauti hiyo ilifoka kutoka kwa Mwasha baada ya kumuona Enock yupo chini hoi anavuja damu mkononi baada ya ncha ya kisu kuzama, alivyo weka mkono wake kibindoni hakuiona bastola yake,
“ipo ipo juu pembeni ya t.v”
Alijibu mwanamke wake huku akitetemeka sana, hapo ndipo Mwasha alipandisha ngazi kwa hasira akiiendea silaha yake.
“ganda ivyo ivyo, nipe funguo za gari!”
Sabrina aliongea na kumuweka Mwanamke huyo chini ya ulinzi akiwa na bastola, alimuamuru akafunge mlango mkubwa ili Mwasha ashindwe kutoka,
Ilibidi atii amri hiyo mara moja.
Jambo alilofanya ni kumuinua Enock aliyekua chini anavuja Damu na kuanza kumkokota mpaka kwenye gari, alimuweka na mtoto wake Christopher kisha yeye kuliendea geti na kulifungua,
Alirudi ndani ya gari na haraka haraka kupiga gia akitoa kasi ya ajabu moja kwa moja nje.
“Enock pole sana, ina kubidi nikupeleke Hospitali”
“hapana, hapana usifanye ivyo tutakamatwa tu, alafu ulifikaje hapa, ulijuaje kama nimerudi?”
“nitakwambia ni stori ndefu sana, sasa tuta fanya nini kama hutaki nikupeleke hospitali?”
“hata ivyo ungeniacha tu baba yangu aniue, sababu sioni haja ya kuishi”
“hapana usiseme ivyo, na Catherine yuko wapi?”
“cat..herine amefariki, Catherine ameuwawa nchini Kongo Mama!”
Aliongea Enock bila kuchuja maneno hayo mazito yaliyo penya masikioni mwa Sabrina na kubaki akimtolea macho yake Enock na kudhani wenda alisikia vibaya maneno yaliyo tamkwa!
Alizidi kubiringika kuelekea mabondeni kama mpira na kujigonga gonga na miti mpaka kufika chini kwenye matope na kutulia tuli, alihisi tena maumivu kwenye mguu wake wa kulia na kuona miale miale ya tochi ikiangaza huku na kule ilibidi atulie,alielewa kabisa kitendo cha kujigusa angemiminiwa risasi na kufa hapo hapo, hofu ili zidi kumtanda huku akimuomba Mungu wake aliye juu aitetee nafsi yake,
Kwa uwoga alijikuta akikaa bila kujigusa mpaka kuna kucha, taratibu sana alisimama na kutembea huku akichechemea akienda asipo pajua,njaa tayari ilianza kumtafuna na kuhisi nguvu zina muishia mwilini mwake, ilibidi akae chini ya mti ili akusanye nguvu ili azidi kusonga mbele,kitendo cha kukaa na kutafakari hapo ndipo usingizi uka mchukua kutokana na uchovu aliokua nao.
Kilicho mshtua ni kitu kama kichuma cha moto usoni mwake alivyo yafumbua macho yake alikutana na mdomo wa mtutu umeshikwa vizuri na mtu mmoja mfupi mwenye misuli mikononi, moyo ulimdunda sana vikiambatana na jasho jembamba usoni baada ya kujua huo ndio mwisho wa Maisha yake!.
“naomba usiniue tafadhali! Nita kupa chochote unachotaka!”
Alisema Catherine akijaribu kumshawishi Mwanaume aliyekua mbele yake amekunja sura hacheki wala kuongea lolote.
Mzee wa Makamo Mfupi alianza kujilamba midomo yake na kumtizama Catherine kuanzia juu mpaka chini.
“simama juu”
Aliamuru mzee huyo akiwa na mtutu mkononi mwake nyuma ya Catherine huku akizidi kumkagua jinsi Mungu alivyo mpendelea kila sehemu,
walizidi kusonga mbele maili moja na kufika kwenye kijiji kilichokua kina vibanda vibanda vilivyo tengenezwa katika mfumo wa Nyasi,
Baadae alitoka na mwanamke mwingine mtu mzima!.
“Mtanzania mwenzako huyu Mama Abushiri, nime mtosha kule juu. Kiswahili yake tu ilinifanya nijue kuwa ni mtanzania, Binti karibu sana hii fasi tunaishi kwa kujificha sana, kabla ya kukuchosha naomba kwanza ukanawe kisha njoo uje upatiwe chakula”
Maneno yaliyokua yanatoka kwa mzee huyo hata yeye alishindwa kuyaamini alijua wenda baadae wange mgeuka na kumuuwa ila mpaka wakati huo hakukua na dalili yoyote ya picha mbaya.
“karibu sana, jina lako nani?”
Aliuliza Mama Abushiri
“Mimi,? Mimi naitwa Catherine, naitwa Catherine Ramsey”
“twende kwanza ukajimwagie maji, alafu ule chakula niweze kukukanda mguu wako jisikie upo nyumbani”
Alioneshwa chumba cha kubadilishia nguo na kupewa maji ya kuoga baada ya hayo kufanyika alirudi na kukuta ugali na samaki,kula kwa haraka haraka ndipo kulidhihirisha kuwa ana njaa sana, mpaka alipo shiba Alisha kula sahani tatu peke yake na kuomba maji ya kunywa.
“ilikuaje mpaka umefika kongo”?
“ni stori ndefu sana”
“niadisie taratibu huku namalizia kukukanda mguu wako”
Hapo ndipo Catherine alimuelezea alivyokua kwa shangazi yake julia na kundi la waasi kudhani kuwa yeye ni mnyarwanda, alielezea historia hiyo kwa ufupi huku akilia machozi na kutoamini kuwa mpaka wakati huo anapumua na mzima wa afya.
Mpaka ina fika usiku aliweza kuzoeana na baadhi ya majirani zake, kweli alionesha uchangamfu sana na kupendwa na watu.
Alioneshwa sehemu ya kulala ili apumzike baada ya kukandwa mguu wake uliokua na maumivu,
Alisali sala ya usiku kabla ya kulala akiomba Ulinzi kwa Mungu baba aliye juu mbinguni na kuweka kichwa chake juu ya mto mdogo, kabla ya kukaa sawa alihisi watu wakipiga kelele nyingi nje na kuanza tena kuogopa,
Alivyo chungulia nje aliwaona watu wawili wakiwa na mitutu yao mkononi.
“kuna mwanamke njoo tuna mtaka musifanye muchezo, tutaua kijiji kizima, ako wapi?”
Liliuliza jitu moja la kikongo! Moyo ulimlipuka paa! Na kuanza tena kudondosha machozi sababu alishajua kuwa anayeuliziwa ni yeye na sio mtu mwingine.
Ilikua ni kilio cha uchungu Kwa Enock baada ya kusimulia historia fupi tangu alivyofika nchini Uganda mpaka umauti wa Catherine kumkuta,aliumia ndani ya mtima wake, hata yeye hakuelewa ni mambo gani yalitokea katika maisha yake alijaribu kuvuta kumbu kumbu juu ya mambo yaliyo pita nyuma na kuchukiana mpaka na baba yake mzazi juu ya kutetea penzi lake kutoka kwa Catherine aliyemtoa bikira yake yeye mwenyewe na kupanga aje kuwa mke wake hapo baadaye!,
Ila mambo yalienda kombo baada ya Heather kuingilia kati akitumia ndumba au nguvu za giza ili kumkamata na kufanikiwa kuichukua akili yake, ni kweli! Alipitia misuko suko mingi sana mpaka hapo alipofikia, hata kwa Sabrina alilia sana kwa kupotelewa na mtoto wake wa kike ambaye alikua kama ndiyo kumbu kumbu yake kwa marehemu Ramsey aliyemzalisha kipindi wanasoma Morogoro,
alilia machozi huku mtoto wake mwingine akiwa juu ya kochi, pole haikutosha kuzuia uchungu aliokua nao.
“Enock!”
Sabrina alimuita
“Naam Mama!”
“una uhakika na unachokisema?”
“ndio Mama nina uhakika?”
“Kway ulimuacha wapi?”
“nili muacha, yeye alirudi Congo Bukavu kwa mke wake, tulikua wote na tuka muokoa vizuri mtoto wake Natu, lakini alisema anaenda Congo kwa mke wake, sidhani kama alifika salama sababu kuna vita kali”
“wewe ulishuhudia Catherine amekufa?”
“niliambiwa”
“na nani?”
“na mke wa Kway”
Bado Sabrina hakutaka kukubaliana na mambo anayo sikia aliangua tena kilio kwa sauti ya juu sana huku akianza kupiga simu kwa ndugu jamaa na marafiki kwa uchungu sana, mpaka inafika jioni ya saa kumi na mbili watu walifurika nyumbani kwake wakimpa pole,ila wengi walimfuata Enock na kutaka kujua nini kilicho tokea mpaka umauti uka mkuta msichana mrembo Catherine,
Kila mtu aliye sikia historia hiyo fupi kutoka kwa Enock alitingisha kichwa chake na kuoneshwa kuguswa mpaka ndani ya moyo wake, Loyda Alisha fika teyari na ndiye aliye fanya watu waanze kulia upya alionekana ndiye mwenye maumivu kuliko mtu yoyote kwa kuondokewa na Mtoto wa kaka yake ambaye ilikua ni kama ukumbusho kwake,mpaka dakika hiyo hawa kuweza kuuona mwili wowote, siku mbili nzima walibaki wakiomboleza na kulia tu,
Kwa Enock alishalia sasa mpaka machozi kumkauka machoni mwake, bado alikua haamini, alikua amekaa na vijana wengine ameganda kama barafu mdomo kauacha wazi akiwa na fikra nyingi sana kichwani mwake alijiona ni mwenye mkosi duniani na kujuta ni kwanini alizaliwa,
licha ya hayo yote alimlaumu sana baba yake mzazi mzee Mwasha, alimuhesabia kuwa yeye ndiye chanzo cha hayo yote yanatokea katika maisha yake.
“nita kuua kwa mikono yangu”
Aliwaza Enock kichwani mwake.
Kelele za watu ndizo zilimkurupua Baba Abushiri kitandani kwake na kumziba mke wake mdomo, alijua teyari kuna jambo baya linaendelea nje, alitembea hatua chache tu na kuchungulia nje, hapo ndipo alipata majibu sahihi ya maswali yake aliwaona watu watatu wameshika mitutu wamewaweka baadhi ya watu chini ya ulinzi, ilikua ni lazima afanye jambo sababu ndiye aliye tegemewa ndani ya kijiji hiko,
Alitembea mpaka uvunguni na kuinua gobole na kushika kisu sawa sawa mkononi mwake alivyo fanya hayo yote alitembea taratibu sana nje, na kumfata mmoja wa waasi na kutumbukiza kisu ndani ya shingo yake,kabla ya mwingine kushtuka alimvuta na kumtwanga kichwa puani na kuzungusha teke lililo mfikia mwingine aliyesimama nyuma yake kabla ya kufanya lolote, alichukua gobole na kuwamaliza papo hapo,
KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA