SEHEMU YA AROBAINI NA SABA
ILIPOISHIA...
Alitembea mpaka uvunguni na kuinua gobole na kushika kisu sawa sawa mkononi mwake alivyo fanya hayo yote alitembea taratibu sana nje, na kumfata mmoja wa waasi na kutumbukiza kisu ndani ya shingo yake,kabla ya mwingine kushtuka alimvuta na kumtwanga kichwa puani na kuzungusha teke lililo mfikia mwingine aliyesimama nyuma yake kabla ya kufanya lolote, alichukua gobole na kuwamaliza papo hapo,SASA ENDELEA...
Yote yaliyokua yanaendelea Catherine aliya shuhudia alipenda sana jinsi baba Abushiri alivyokua anapambana na watu hao mpaka kuwauwa, hakuwahi kuona mtu akipigana ivyo zaidi ya kuwaona wacheza muvi wakina Steven Seagal na Don Yen, hapo ndipo alipo tamani nayeye kujua kupigana ili awe anajiamini na kujihami.
“Ahsante!”
Alishukuru Catherine
“usijali rudi ukalale”
“nilikua naomba kitu kimoja kutoka kwako”
“kitu gani?”
“naomba nijue kupambana kama wewe”
Kauli hiyo ilimshtua sana Baba Abushir hakutegemea hata yeye kwa msichana mdogo kama Catherine kutaka kucheza michezo hatari.
“hii michezo hatari sana, hautaweza”
“nitaweza tu, nakuomba tafadhali”
Huo ndio ulikua mwazo wa kumsumbua Baba Abushir kila siku akimuona, wiki sasa ili katika akizidi kumsihi na kutaka kujua mbinu za kupigana japo aliambiwa kuwa ni kazi na ingemchukua muda,
lakini hakujali hata kidogo hata ingechukua miaka mia, ili mradi alishajua kile anacho kitaka, alishataka kujua jinsi ya kupambana kutokana na maisha aliyo pitia nyuma na kufanya awe na maadui wengi alijua iyo inge msaidia sana mbele ya safari.
“beba huo mti twende msituni”
Alisema Baba Abushir siku hiyo asubuhi sana.
“sawa”
“kwanini unataka kujua kupigana?”
“napenda kujua, kwanza moja self defence, alafu mchezo huu nilikua naupenda tangu muda mrefu sana”
“sawa, utajua tu ila inakubidi uwe mvumilivu”
“nakuhaidi nitakua mvumilivu”
“sawa twende huku ukaanze mazoezi leo”
Walitembea msituni mpaka walipofika kati kati hapo ndipo Catherine alianza kuambiwa aanze kufanya pushup ili kutanua misuli yake,kwake lilikua jambo gumu sana sababu ilikua siku yake ya kwanza hata Baba Abushir hakutaka kumkatisha tamaa, walizidi kufanya mazoezi wote kwa pamoja mpaka ikakatika wiki nzima Catherine alikua anaweza kupiga pushup nyingi hapo, hio ilimpa sana faraja Baba Abushir na hatua nyingine kufuata,kila asubuhi walikua waki kimbia mbio ndefu ili kuongeza pumzi, siku zilikatika na mwishowe kuanza mazoezi rasmi ya kupigana ndondi.
“hapana ngumi haikunjwi ivyo, ukitaka kukunja ngumi, hii ngumi moja unaiweka karibu na usoni huku ukitingisha tingisha miguu, alafu kitu kingine ukiwa una pambana na adui yako, jua kumsoma akili”
“kivipi?”
“uwe una muangalia sehemu kuu mbili, machoni na miguuni, mfano mimi nikikuangalia miguuni nitajua unarusha ngumi ipi ya kulia au kushoto,embu rusha ngumi”
Catherine alivyo rusha ngumi ilidakwa na kujikuta yupo chini bila kujua kadondoka vipi.
“inuka”
Hayo ndiyo yalikua mazoezi kila siku iendayo kwa Mungu mpaka miezi miwili ilivyokatika Catherine alikua amekwiva sana, alishajua jinsi ya kutumia bastola na kulenga shabaha,alishajua jinsi ya kurusha mateke na kupambana na mtu yoyote Yule hata mnyama mkali, kitu ambacho alisisitizwa na Baba Abushir ni ujasiri na asiwe mkorofi.
Uzuri Mungu aliumba kitu wakati na kusahau, ivyo ndivyo ilikua kwa Enock ilibidi tu asahau na kuchukulia kuwa ni sehemu ya Maisha kufiwa,sababu kama ulizaliwa ni lazima ufe na mwisho wa siku kila mtu ataonja umauti!, alishaamini kuwa Catherine amesha fariki Dunia, kama mama yake mzazi Alisha fariki na kumsahau kwanini isiwe kwa mwanamke huyo,
Alisha rudi kwenye nyumba yake na kuwatimua watu wote aliowakuta, kila aliye msimulia kilichotokea katika maisha yake alibaki kinywa wazi asijue cha kufanya, lakini licha ya yote mara kwa mara alikua akienda wodi ya vichaa kumuangalia mke wake Heather hali yake ina endeleaje, hakua na kinyongo chochote juu ya mwanamke huyo,
Baba yake Mzee Mwasha Alisha kimbia na kutokomea kusipofahamika jeshi la polisi lilikua bado lina mtafuta bila mafanikio yoyote yale,ilibidi kila mahali atembee na walinzi aliowaajiri kwa ajili ya usalama wake sababu aliamini baba yake mzazi yupo na muda wowote anaweza akamuuwa, na huo ndio ushauri aliochukua kutoka kwa rafiki yake kipenzi Anderson Peter.
Bado Zahara alionesha kumpenda sana Enock alimsisitiza lakini mbinu zake hazikuzaa matunda.
Baada ya kuingia ndani ya gari kutoka ofisi za Nissan siku hiyo Enock alinyoosha mpaka kwenye moja ya baa ili akapumzishe akili yake iliyokua na msongo wa mawazo,ndani ya akili yake alihitaji mke mwema ili baadae aje kumzalia watoto japo ilikua vigumu kumpata mwanamke kama Catherine,
“dada naomba kaniitie Yule binti aliyevaa shati jeupe”
Enock alimwambia muhuhdumu
“sawa anco, vipi tuongeze kinywaji,?”
“ndio niongezee alafu umsikilize anataka nini”
“sawa”
Baada ya dakika moja msichana mrefu maji ya kunde alikua mbele yake ameketi na kuanza kuulizana maswali huku wakipiga stori mbali mbali za maisha, walizoeana na muda mfupi walifahamiana majina.
“nafanya kazi bank,kama cashier”
“sawa Naomi mimi nipo NISSAN posta pale kama mkurugenzi, muda umesha kwenda naomba nikuache”
“sawa usiku mwema”
Hapo ndipo urafiki ulipo anzia na baadaye haukuwa tena urafiki, walikua wapenzi tena wenye mapenzi ya dhati, taratibu alianza kumsahau Catherine na mwishowe kusahau yote yaliyo tokea na hisia zake kuhamia kwa Naomi hakua anasema wala kuongea juu ya mapenzi aliyopata,ila kwao kipingamizi kilikua ni kimoja tu Heather ambaye aliaminika kuwa ni mke wa ndoa kama mkristo hakutakiwa kufunga ndoa mara ya pili. Kila mtu ndani ya moyo wake alitamani swala la ndoa litokee.
“lazima nifanye kitu, nampenda sana Enock nataka anioe”
Aliwaza siku iyo Naomi akiwa chumbani kwake amelala baada ya kukata simu ya Enock wakitakiana usiku mwema.
Mwanamke Naomi alishazama kabisa kihisia, Alisha mpenda sana Enock kupindukia kutoka ndani ya moyo wake na kutamani kufunga nae ndoa aishi nae kihalali na hapo baadaye amzalie watoto wajenge familia waishi kama baba na mama mpaka kifo,
lakini jambo moja ndilo lina muumiza kichwa ni Heather mke wake na Enock ambaye alikua yupo wodini amerukwa na akili zake kabisa, mwanamke huyo ndiye alikua kikwazo kikubwa cha safari yake ya ndoa kutimia, kama maandiko ya biblia yalivyoandikwa kuwa ni kifo tu ndiko kitawatenganisha wana ndoa na wala sio kitu kingine,
Alitamani muda wowote ule Heather afe ili yeye aweze kuolewa, ilishapita wiki nzima akitafakari ni kitu gani akifanye. sio yeye tu Hata Enock alishafikiria ni kitu gani akifanye lakini akili yake iligota na kugonga mwamba alishindwa kufikiria nje ya boxi,hata kama mwanamke huyo alihusika kumuuma Mama yake mzazi hakupaswa kulipiza ubaya,kasha kua mwendawazimu aliamini hiyo ni adhabu tosha kutoka kwa Mungu!
“sasa itakuaje Mpenzi?”
Naomi alimuuliza mpenzi wake
“kuhusu nini?”
“kuhusu ndoa yetu”
“kama nilivyo kwambia ina bidi tuwe na subira si nilishakwambia nina mke, nipe muda kwanza nifikirie cha kufanya alafu nitakujibu, haya mambo sio ya kwenda pupa”
“Enock unanipenda?”
“nakupenda sana hilo sio la kuuliza”
“nikuulize kitu?”
“ndio mpenzi wangu”
“mimi na Yule kichaa wako unampenda nani?”
“nakupenda wewe Naomi”
“sasa mbona una kua mzito wa kufikiri,kama hauna malengo namimi uniambie sio unanipotezea muda wangu bure”
“nipe muda nitajua cha kufanya”
Ivyo ndivyo kila siku Naomi alikua akimsumbua mpenzi wake Enock juu ya yeye kumuoa, ni kweli kabisa alitamani ndoa kuliko kitu chochote kile duniani,
Enock alishachanganyikiwa hakujua ni kitu gani afanye kila siku alikua akiwaza ni kitu gani akifanye juu ya Heather alitamani afe mara moja ili yeye apate mwanya wa kuishi na kufunga ndoa na Naomi,
ofisini alikua hapakaliki tena kila kukicha Naomi alikua akimsumbua juu ya yeye kafikia uamuzi gani na kufanya iwe kero na kumtishia kuwa atamuacha muda wowote.
“kama hutaki basi tuachane!”
Naomi alitingisha kiberiti siku hiyo na kuona ni jinsi gani Enock alivyo shtuka akimuomba msamaha
“sasa huko umefika mbali sana”
“ndio ivyo”
“Naomi usifanye ivyo”
“basi kama hutaki niruhusu nifaye kitu kimoja”
“kitu gani?”
“naenda kumuuwa”
“nini?”
“kama ulivyosikia”
“hapana usifanye ivyo”
“Enock hunipendi bado unampenda Yule kichaa wako, na usinitafute tena”
Baada ya kumaliza maneno hayo Naomi alisimama akiwa amekasirika sana, siku mbili nzima walinuniana kila mtu hakumsemesha mwenzake kabisa,
lakini mmoja wapo kati ya hao wawili alionesha kuumia zaidi kuliko mwenzake si mwingine bali ni Enock siku mbili bila ya kuongea na Naomi alihisi kuumwa sana,baada ya siku mbili kupita mpaka ina fika mtondogoo ndipo alipompigia simu na kumuomba msamaha japo alijua hakufanya kosa la aina yoyote ile,ili mbidi awe mdogo na kujishusha.
“kwaio umeamuaje?”
Aliuliza Naomi
“fanya unavyo jua ili tufunge ndoa”
“okay baby wangu”
Baada ya kukata Simu Naomi alikua mwenye furaha sana, ,kichwani mwake hakuwaza kitu kingine bali ni kufanya mauaji japo hakuwahi kufanya kitendo hiko kabla, lakini mapenzi ndiyo yalimpelekea akachukua maamuzi ya kutaka kutoa uhai wa Heather ambaye alikua ndiye kikwazo peke yake.
Siku hiyo hiyo aliwasha gari mpaka wodi ya vichaa Muhimbili ili kumuona Heather,
ivyo ndivyo alivyo fanya siku iliyo fuata, alijaribu kujenga urafiki wa karibu na mwanamke huyo mwendawazimu, alionesha sura ya ukarimu hata wauguzi waliomuona walimuonea huruma sana Naomi.
“Dada angu anaendeleaje?”
Aliuliza Naomi
“kama unavyomuona ivyo, tunajaribu kumpa mpa dawa zitakazo msaidia”
Alijibu muuguzi wa kikealiyevalia sare za rangi ya bluu
“Mungu amsaidie dada yangu apone, sijui kwanini imekua ivi. EEh Mungu nini nime kukosea nini kakukosea Heather, kwanini umeamua kumpa Adhabu hiyo”
Alizungumza Naomi akitia huruma sana hata muuguzi aliye kua nae pembeni alimuonea sana huruma moyo ni kiza kinene huwezi kujua yupi mkweli yupi muongo!, hakuna hata punje ya neno moja lililokua lenye ukweli ndani yake, mambo aliyokua akiongea Naomi haya kushahabiana na moyo wake hata kidogo,
Ndani ya moyo wake alitamani Heather afe muda huo huo, wiki nzima alifululiza kwenda wodi ya vichaa mpaka wauguzi kuanza kumzoea.
“Mimi na kamazubanda banda banda, njoo hapa hi hi hi hi hi hi, what is biology? Njoo tuvue samaki, unajua kuimba Mungu ibariki njoo tuimbe oooh Baba wa taifa nime kukumbuka sana baba yangu, unavikumbuka vita vya maji maji ha ha ha ha ha viliongozwa na kinjeketile. Inabidi nimpigie simu”
Maneno hayo yalimtoka Heather akijaribu kuongea vitu visivyoeleweka akichanganya habari,
Naomi aliyekua pembeni yake alimkata jicho kali la chuki za wazi wazi, kwakua wauguzi walimzoea tayari walimuacha chumba kimoja na wao kuondoka zao,
KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA