SEHEMU YA AROBAINI NA NANE
ILIPOISHIA...
Naomi aliyekua pembeni yake alimkata jicho kali la chuki za wazi wazi, kwakua wauguzi walimzoea tayari walimuacha chumba kimoja na wao kuondoka zao,SASA ENDELEA...
Hiyo ndiyo ilikua nafasi yake pekee ya kutimiza kile alichotaka kukifanya siku nyingi, sumu kali ya panya DDT poison aliyokua akitembea nayo kila siku kwenye pochi yake aliitoa na kuimimina ndani ya maji ya kunywa na kumkabidhi Heather anywe.
“kunywa maji matamu sana”
“tamu?”
“Tamu ndio shika”
Hakuelewa kuwa amewekewa sumu kali na kuanza kuyanywa maji kwa mkupuo mpaka chupa yote kuisha, haikupita hata sekunde mbili Heather alikua akipiga kelele za maumivu ya tumbo huku akigala gala chini,
Alishajua kuwa dawa yake inafanya kazi alimsogelea karibu yake na kumziba pua ili aweze kummalizia kweli alikua na roho ya kijasili pepo mchafu alishamuingia,alivyo hakikisha Heather katulia hasemi alitoka nje nakuanza kupiga kelele nyingi sana za msaada.
“nini?”
“amekunywa maji yaliyokua yana sumu ya panya nilitoka nje kwenda chooni”
“kwanni umekuja na sumu sasa?”
“nyumbani kwangu kuna panya nilinunua ili kuwategeshea”
Ivyo ndivyo alivyokua akijitetea Naomi hata alipohojiwa na mtu yoyote Yule aliyemuuliza juu ya kifo cha Heather,alilia machozi ya uwongo wauguzi waliomzoea walimpa pole nyingi huku wakimpa matumaini, ndani ya moyo wake alijiona mshindi sana na kuona ataweza kuishi vizuri na Enock wakiwa na maisha mazuri sababu ya uwezo wake kifedha.
Baada ya mazishi ya Heaher kuka milika kila kitu na kutoa matanga sasa ilibaki kazi moja tu kufunga ndoa na Naomi,lakini ilibidi kidogo avute muda ili ndugu wa upande wa Heather wasiweze kumfikiria vibaya,
Mwezi ulikatika na sasa kuanza kuishi nyumba moja na Naomi kama mume na mke wakisubiri tu Ndoa ifanyike hayo ndiyo yalikua mawazo katika kila akili ya mmoja wapo.
“Mama shikamoo, Mimi Catherine”
Upande wa pili wa simu ulisikika baada ya Sabrina kuweka simu yake sikioni, alistaajabu aliitoa simu sikioni na kuiangalia tena sababu hakuamini sauti aliyo sikia , alijua wenda yupo kwenye njozi.
“Catherine yupi?”
“Catherine mwanao”
“hapana sio kweli Catherine mwanangu ameshafariki na tushamzika kama unanichezea akili naomba uniache binti”
“Mama mimi sikufa,nipo Kongo nilipona ni historia ndefu sana, lakini nacho kuomba usimwambie mtu yoyote Yule mimi nakuja kesho nishakata tiketi ya ndege”
“Mungu wangu, Mwanangu Catherine njoo nikuone, nililia sana kwenye msiba wako, kumbe haukufa? Eeh Mungu wangu”
Bado hakutaka kuamini kuwa mwanae yupo hai na ametoka kuongea nae sekunde chache zilizopita, alitembea mpaka kwenye sink la maji na kunawa uso ili kuhakikisha kuwa kama ni kweli au yupo kwenye njozi,ukweli ni kwamba hakua ndotoni alimtizama Mwanae Christopher ambaye alishaanza kutambaa sasa na kuweza kuita Mama,
Usiku kucha aliwaza bila hata ya kupata lepe la usingizi akisubiri kukuche na kwenda kumpokea Mwanae Catherine uwanja wa ndege mwalimu Nyerere,masaa yalienda na kukucha tayari. alimpa Christopher uji na kumuogesha kama afanyavyo kila siku,
Mchana ulivyo fika kweli simu yake iliita na kuongea na Catherine kuwa kasha fika uwanja wa ndege mwalimu Nyerere, hapo ndipo alipoamini kuwa hayupo ndotoni. Aliwasha gari na kunyoosha mpaka uwanja wa ndege.
Alishuka haraka haraka akiwa na Christopher mkononi mwakempaka macho yalivyotuwa machoni mwa Catherine walikimbiliana na kurukiana,kila mtu hakuamini na kujikuta wote wanalia machozi ya uchungu, walikua na mambo mengi ya kuongea juu ya maisha waliyopitia hapo nyuma mtu na mama yake.
“Ma..ma ya…ngu, sia..mini kama ningekuona tena, niliteseka sana Mama”
Aliongea Catherine kwa uchungu huku akilia machozi, alimtizama mtoto mdogo aliye mshika mama yake na kutaka kuuliza kitu lakini alisita
“Catherine mwanangu, huyu ni mdogo wako”
“Ma…ma”
“Abee”
“sawa usijali, Baba yake ni nani?”
“nitakwambia”
Waliingia ndani ya gari na safari ya kuanza kurudi kupumzika kuanza, Sabrina Alisha ama tayari nyumba safari hii alikua akiishi Tabata bima kisiri sana hakuna mtu aliyejua isipokua ndugu wa karibu.
Ndani ya siku mbili Catherine alishaanza kuzoea mazingira na kurudi katika hali yake ya kawaida baada ya kutuliza akili yake, alimkumbuka mwanaume Enock, hapo ndipo aliposimuliwa na Mama yake kuwa alimfuatilia mpaka Uganda na kushindwa kumpata.
“wachaniende kwake sasa hivi”
“sawa mwanangu”
Alichukua gari ya mama yake na kuliondosha kwa lengo moja tu kumfuata Enock ili amshukuru, ndani ya moyo wake hata yeye alihisi kuna kitu kina msumbua lakini hakujua ni kipi,
alinyoosha mpaka nyumbani kwa Enock asubuhi hiyo na mapema, alivyo fika aliweka gari pembeni na kufungua geti,
Alinyoosha mpaka seblen kitu kilicho mshtua ni picha ya mwanamke wa maji ya kunde zikiwa zimebandikwa ukutani huku nyingine wakiwa wamepiga na Enock,bado alikumbuka mambo mengi waliyo fanya na Enock ndani ya nyumba hiyo, ilimkumbusha vitu vingi sana vilivyopita katika maisha yake, kweli alikua mbali kifikra, mwanamke aliye kua pichani bila kuuliza chochote alijua tu ni mwanamke wa Enock.
“Dada samahani nikusaidie nini?”
Sauti ya kike ndiyo ilimshtua katika ndimbwi la mawazo alivyokua amesimama, mwanamke aliyesimama mbele ndiyo huyo aliyemuona pichani.
“naomba nionane na Enock”
“wewe ni nani yake?”
“mwambie Catherine”
“Catherine yupi, wa wa….”
“baby funguo zangu za gari utazikuta chumbani, nilikua naomba nitumie gari yako ala….”
Enock aliyekua anatokea chumbani anashusha ngazi huku akirekebisha tai yake vizuri hakuamini mwananamke aliyesimama mbele yake kuwa ni Catherine, alibaki ameganda kama barafu huku bado mkono wake ukiwa kooni mwake, mapigo ya moyo yanamdunda kwa kasi,
Mapigo yake ya moyo yalizidi kumwenda kasi kungekua kuna kipimo cha mapigo ya moyo basi kingeonesha moyo wake una dunda mara mia mbili kwa dakika moja! Mwanamke aliye simama mbele yake bado alibaki kumshangaa,mwanamke ambae alihangaika kumpata kwa siku nyingi sana akijitolea muhanga na kusafiri mpaka nchini Uganda ili kumkomboa , mwanamke ambaye aliyefanya mpaka wawindane na baba yake mzazi kutaka kuuwana,mwanamke huyo huyo alimtoa bikra yake,mwanamke ambaye alidhani amekufa miezi kadhaa iliyopita,
Bado alikua haelewi ni kitu gani kinatokea alimtizama Naomi mchumba wake na kurudisha tena macho yake kwa catherine, hata Naomi nayeye alishindwa kuelewa kwanini mchumba wake ameganda kama barafu anahema juu juu hata yeye alijua kuna kitu kinaendelea picha ilionesha.
“Enock mpenzi upo sawa?”
Aliuliza mchumba wake
“Catherine, hapana sitaki kuamini”
Badala ya kumjibu mchumba wake alimuongelesha Catherine, sio Enock tu peke yake hata Catherine mapigo yake ya moyo yalimwenda kasi na kukumbuka vitu vingi vilivyopita katika maisha yake,
hakusema lolote lile na kuanza kuondoka zake pale pale.
“unaenda wapi Enock?”
Alihoji Naomi alivyomuona mchumba wake nayeye anataka kutoka nje,alitanda mbele yake kwa hasira na jazba zote.
“embu nipishe”
“sitaki, unaenda wapi?”
“nipishe moja”
“sipishi”
“nipishe mbili”
“sipishi!”
“Ebwana nipishe bwana tat..”
Naomi alijikuta yupo juu ya kochi baada ya kusukumumizwa, hata yeye alishangaa kuona hali aliyokua nayo Enock. Alimshuhudia akitoka nje huku akiita jina Catherine.
“Catherine Catherine!”
Enock Alizidi kuita huku akiwa nyuma nyuma ana kimbia alivyotoka getini alishuhudia Verosa inazunguka na kutoka kasi ndani akiwepo Catherine anaendesha, aliitambua gari hiyo ilikua ni ya mama yake, alirudi ndani ya geti na yeye kuwasha gari, alifungua geti na kuanza safari ya kumfukuzia mpaka tabata bima nyumbani kwa Mama yake mzazi na kushuka ndani ya gari,
Mzee Mwasha bado alikua na kinyongo na watu watatu rohoni mwake, alishaweka hali ya chuki tangu mwanzo, swala alilolianza ilikua ni lazima alimalize na kuishi kwa amani Catherine, Enock na Sabrina ilikua ni lazima wauwawe.
alikua ni mtu wa kujificha sasa alishajua kuwa Catherine amerudi na yupo hai ilikua ni lazima amuuwe kivyoyote vile, kila siku iendayo kwa Mungu huwa tuma vijana wake wafanye uchunguzi juu ya Enock ili wammalize lakini kikwazo kilikua ni kimoja tu, alikua akitembea na walinzi kila kukicha na kila wakati,makazi yake aliya hamishia Zanzibar kijiji cha DORE huko ndipo alipokua amejificha lakini dunia ni kijiji alishajua nini kinaendelea Dar es salaam juu ya watu anaowatafuta, vijana wake ndiyo waliokua wakimpa taarifa zote.
Hakuna habari iliyo mfurahisha kama alivyo sikia kuwa Enock asubuhi katoka mbio mbio bila ya walinzi wake, hapo ndipo alipo toa kauli kuwa wamfuatilie kisha wamuuwe,
Walikua wakilifuatilia gari lake Marced Benz nyuma nyuma mpaka lilipopaki katika nyumba iliyopo tabata bima.
“Catherine”
Aliita Enock akitia huruma baada ya kuingia ndani mwa Sabrina kama mshale bila ya kubisha hodi
“jamani kuna nini?”
Alihoji Mama Catherine
“Mama nampenda sana Catherine nime kuja kumuomba msamaha ili tuyamalize, nime furahi kumuona akiwa hai”
“hapana hunipendi mimi nawewe hatuwezi kuwa pamoja tena sahau Enock, una mwanamke wako teyari”
Alijibu Catherine akiwa amesimama bado
“usiseme ivyo Catherine usiseme ivyo tafadhali, haujui kilichotokea mimi na mama yako tuliteseka kukutafuta, nilijitolea maisha yangu kufa kwa ajili yako mpenzi wangu, naomba sahau yote yaliyo pita tugange yajayo”
“siwezi kusahau, nitasahau vipi kirahisi?, kisa wewe nilitaka kufa, hapana siwezi, napenda tu kukushukuru uliokoa maisha yangu basi ila kwa unachotaka sahau”
Sabrina aliyekua pembeni yao alibaki kimnya akiwatizama alikua ni kama anaangalia maigizo au tamthilia sababu walipokezana kuongea, alimuonea sana Huruma Enock laiti angelikua Catherine ange mkubalia mara moja Enock sababu alielewa ni jinsi gani kijana huyo alivyoteseka juu ya maisha ya binti yake hata yeye alilielewa hilo,
Bila kuamini alimshuhudia Enock akienda chini na kupiga magoti huku akilia machozi kama mtoto mdogo akizidi kuomba msamaha sana,jambo hilo lilimgusa sana moyoni mwake na kuamua kuingilia kati.
“Catherine”
Alimuita mwanae
“Abee Mama”
“naomba umsamehe”
“Mama!...”
“nakuomba mwanangu, binadamu huwa tunajifunza kupitia makosa Enock na mimi tuliteseka sana kwa ajili yako, aliniadithia kila kitu kuhusu wewe na yeye, alinihadithia kila kitu kuhusu mke wake jinsi alivyomuendea kwa waganga, haikuwa akili yake, kwa niaba yangu naomba msamehe”
Hayo ndiyo maneno aliyo sema Sabrina akimuangalia mwanae hakika hata yeye aliridhia binti yake aolewe na Enock aliona ni kijana mkarimu sana kupita yoyote Yule ambaye aliyewahi kujuana nao kabla.
KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA