BIKRA YANGU (49)

0
Mwandishi: Emmanuel F. Kway

SEHEMU YA AROBAINI NA TISA
ILIPOISHIA...
Hayo ndiyo maneno aliyo sema Sabrina akimuangalia mwanae hakika hata yeye aliridhia binti yake aolewe na Enock aliona ni kijana mkarimu sana kupita yoyote Yule ambaye aliyewahi kujuana nao kabla.

SASA ENDELEA...
Lakini ndani ya moyo wa Catherine pia alimpenda Enock ila kuna nafsi nyingine ilikua nzito kukubaliana na uamuzi anaotaka kuutoa wakati huo, alishusha pumzi na kumtizama Enock machoni mwake ambaye alikua akilia bado kajikunja,

alimuinua taratibu na kutabasamu kisha kumkumbatia.

“nime kusamehe, nakupenda sana Enock”

Katika maisha yake hakudhani kuwa atakuja kukutana tena na Catherine alijua kisha kufa tayari aliona ni kama yupo kwenye njozi ,maisha waliyopitia alistaili kwanza amshukuru Mungu, hakuna alichowaza zaidi ya kitu ndoa kubwa ndani ya akili yake.

“Catherine,naomba uwe mke wangu,nataka tufunge ndoa mwezi ujao”

Alitamka Enock

“Enock bado mapema”

“hapana mpenzi sitaki kukukosa tena”

Ilikua ni furaha kwa wawili hao kukutana tena kuwa wapenzi. Maisha aliyopitia Catherine ndiyo yaliyo muumiza kichwa chake wanaume mbali mbali waliokua wakimuingilia kimwili wakimchezesha filamu za ngono ndiko kitu pekee kilichokua kina mtesa ndani ya mtima wake,lakini hakutaka kumwambia Enock wakati huo wa furaha yao ilibidi kwanza watulie ili aweze kumuelezea wakiwa hata kitandani wanasherekea matunda ya kurudiana na kufungua ukurasa wao mpya wa mapenzi.

“gandeni ivyo ivyo”

Sauti ya jitu lenye misuli ndilo lililowashtua na wote kumgeukia, waliingia ndani watu watatu na kutabasamu.

“ha ha ha ha ha bora tumewakuta wote watatu kazi yetu itakua rahisi, tuanze kumuuwa nani kati yenu?”
Jitu lingine lilitokea, Enock alishajua teyari watu hao walitumwa na baba yake mzazi mzee Mwasha, na bado vita inaendelea,

Hata kwa Sabrina na Catherine walikua wanawaza kitu kimoja, walishangaa kumuona Catherine akiwasogelea.
“niueni Mimi wa kwanza”

Alisema Catherine akimsogelea mtu mmoja wao aliyekua na bastola mkononi mwake akijiamini sana, alikumbuka mafunzo yote ya kupambana na adui yoyote Yule akiwa nchini Kongo,alimkumbuka baba Abushiri na kutambua kuwa sasa huo ndio mtihani wa kuthihirisha kuwa amekwisha wiva kwa kupambana,aliwatizama watu wote watatu kwa zamu na taratibu kusogeza mguu wake nyuma tayari kwa kupambana na maadui hao waliokua mbele yake wanataka kuutoa uhai wake..

Catherine Ramsey Kidhirwa alisha windwa mara nyingi sana kuuwawa sio yeye tu alitakiwa awuwawe, bali ni watu wengine wawili Mama yake mzazi na Mpenzi wake Enock ambaye alitoka kumsamehe muda mchache uliopita, watu waliokua mbele yao wamewazunguka ili kuwauwa walitumwa na Mzee Mwasha aliyekua amejificha huko kisiwani Zanzibar kijiji cha Dore!,

Kila mtu hofu ili mtanda isipokua kwa Catherine ambaye alikua na mahesabu yake kichwani aliona kofi linakuja usawa wake na kuinama kidogo, bastola iliyokua imeshikwa na jambazi aliyekua mbele yake aliipiga teke kisha kumvuta jambazi mwingine na kumpiga kifuti sehemu zake za siri, kitendo cha dakika mbili tu majambazi walikua chini kila mtu anaugulia maumivu sehemu tofauti ya mwili wake, hawakuamini kama mwana mke kawaweka chini,kawazidi nguvu.

Enock na Mama yake mzazi hata wao walistaajabu kushuhudia kitendo kilichotokea mbele yao Catherine kuwapiga wanaume watatu tena kiujasiri,

kweli hakua Catherine waliyemjua miaka michache iliyo pita hapo nyuma,

Majambazi hao walijizoa zoa na kuondoka zao wakiwa hawaamini kilichotokea, hapo ndipo Catherine alipo pata nafasi ya kuwahadithia jinsi alivyo fundishwa jinsi ya kupigana.

Siku zilizidi kukatika huku Enock akizidi kumuonesha mapenzi mengi sana Catherine aliamini kuwa ndiye mwana mke wa maisha yake hapo baadaye, ilikua ni lazima amfate Naomi amueleze ukweli wa mambo, ilikua ni lazima ayaweke mambo wazi, ilikua ni lazima ampe historia fupi juu ya mapenzi yake na Catherine japo alimjua mwanamke huyo angekasirika na kuchukua hatua yoyote mbaya sababu tu 

Alisha muuwa Heather ili afunge ndoa na Enock,haikua kazi rahisi kumfuata na kumueleza ili hitajika akili ya ziada hakua na imani kabisa kama Naomi angemuelewa sababu alijua ni jinsi gani mwanamke huyo alikua ni mkorofi na m-babe sana ingawa alikua mwanamke ila alikua ni mwepesi wa kukasirika sana na sio mwelewa!.

“Mpenzi!”

Aliita Enock usiku wakiwa chumbani mwao kitandani.

“Bee mume wangu mtarajiwa!”

“unanipenda?”

“nakupenda sana, na sijui kitu gani kitakuja kututenganisha Mume wangu”

“nikuombe kitu kimoja Mpenzi?”

“bila shaka!”

Hapo ndipo Enock alipo anza kumuhadithia historia fupi kuhusu Catherine tangu walipoanza mapenzi yao na kudhani wenda alikufa kwenye vita vilivyotokea Congo, maneno hayo haya kumfurahisha hata kidogo mwanamke huyo ambaye muda mchache alikua anawaza ndoa kisha anaambiwa habari za Catherine, alimtizama Enock kwa macho makali na kukunja uso wake, Alisha waalika marafiki zake na kujitamba juu ya harusi yake kubwa itakayozungumziwa na watu wengi sana.

“hivi ni mwanamke gani ambaye utamueleza huo upuuzi unaonieleza akubali, wewe una umwa wewe Enock,oooooh! Eti Catherine nilijua amekufa sasa hivi yupo hai nataka kumrudia, MPUUZI WEWE, HUNA AKILI HATA KIDOGO, yaani sijawahi kuona mwanaume ambaye hamnazo kama wewe, mwenyewe kwa nye** zako ulinitongoza alafu leo unaniambia mashudu yako. UTANIOA nakwambia”

Enock alitegemea majibu kama hayo kutoka kwa Naomi alivuta pumzi ndefu sana na kumtizama mwanamke huyo ambaye alikua bado anabwabwaja sana maneno mengi yaliyoendana na mdomo wake mpana kiasi.

“na kesho kutwa nataka univalishe ile pete ya uchumba uliyo nihaidi”

Alimalizia Naomi huku akiji funika shuka gubi gubi akiwa bado anaongea akiwa ndani ya shuka, haikuwa kazi rahisi kukubali yale yaliyozungumzwa na Enock.

“eti ooh Catherine mimi nampenda tume toka mbali mjinga wewe, usiniletee upuuzi, mimi sio wa kujaribiwa jaribiwa ovyo!”

Naomi bado alizidi kuongea huku akibana pua zake akiyaiga yale aliyokua akiongea Enock,bado alisisitiza kuhusu ndoa yake ambayo teyari aliwaalika marafiki zake kutokea mikoani na wafanya kazi wenzake.

Usiku huo ulipita, hatimaye kukucha!

Jioni ilifika ya siku nyingine bado Enock alikua na mawazo mengi kupita maelezo akili yake ili elemewa na msongo wa mawazo mengi, juu ya wanawake wawili waliokua wanamtesa, Naomi na Catherine!

Alimpenda Catherine sana na muda wowote ule alitaka afunge nae ndoa awe mke wake kisha baadaye amsomeshe hata nje ya nchi ikiwezekana ampeleke OXFORD chuo kikuu alichomalizia masomo yake, ila Naomi ndiye alikua kikwazo kikubwa, Alisha jaribu kukaa nae kistaarabu lakini alishindwa, ilibidi 

Aende nae taratibu sana sababu alimtishia kuwa atamshtaki kuwa yeye ndiye aliyemuagiza aende na sumu wodi ya vichaa na amuuwe Heather, habari izo ndizo zilimfanya aogope sana, kwani alijua sheria ingembana mpaka kujua ukweli angesota sana gerezani, ni kweli alikua katika wakati mgumu mno.

“ndio ivyo chagua moja, twende wote gerezani au unioe?”

Aliuliza Naomi ilikua ni sawa kuvaa bomu na kujitoa muanga wote wakaozee gerezani kuliko kum-shuhudia Enock anafunga ndoa.

“Naomi?”

“Ndio jina langu unasemaje?”

“Mbona unakua ivyo?”

“Nakuwaje? Kama nilivyokwambia usipoangalia tutaenda wote gerezani, mimi naenda utanikuta nyumbani”

Enock alichoka kabisa na kuweka kichwa chake juu ya meza ofisini kwake na kulegeza tai yake kooni, alishindwa ni kitu gani akifanye kwa wakati huo, siku hiyo jioni aliona ni bora aende kumueleza mshenga wake Anderson Peter kila kitu kilichokua kinaendelea ili amuombe ushauri ni kitu gani akifanye juu ya wanawake hao wawili.

“umesema kuwa Naomi ndiye alimuuwa Heather?”

“ndio Anderson”

“kwani wewe ulikua hujui?”

“nilikua najua sana kusema ukweli wa Mungu”

“hapo una kazi ngumu blazza, kuwa makini sana, cha kufanya nipe siku mbili tatu nitajua cha kufanya”

“nitashukuru sana, maana kichwa changu kimechoka hapa sana, silali usiku ndugu yangu!”

Aliona ni bora amuelezee kila kitu rafiki yake aliyemuamini sana kupita mtu yoyote Yule.

Naomi Alisha mfuatilia Catherine mpaka sehemu anayoishi kutokana na wivu wa mapenzi aliokua nao bado alitaka kula nae sahani moja, maneno aliyo ambiwa kuhusiana na mwanamke huyo aliyekiri kuwa ni mrembo kupita yeye yalijenga chuki sana ndani ya moyo wake, alijua ndiye yeye tu anaye fanya mambo ya ndoa yake ya Kwame ilikua ni lazima afanye jambo, mchana wa siku hiyo aliweka gari yake tabata bima pembeni ya nyumba anayoishi Catherine na kushuka ndani ya gari aligonga geti na kufunguliwa na mlinzi.

“nime mkuta Catherine?”

Aliuliza Naomi akiwa na miwani ya jua machoni mwake.

“ndio yupo pita ndani, yupo seblen”

Jibu hilo tu ndilo lilimfanya atembee haraka haraka mlangoni na kuufungua mlango na kumkuta Catherine akiwa na mama yake wamekaa seblen wakiwa na mtoto mdogo christopher!.

“sina haja ya kujitambulisha nafikiri unanijua?”

Alianza kuongea Naomi bila ya salamu

“nakufahamu, mchumba wake na Enock!”

“ahaa umejibu vizuri!, sasa nisikilize wewe Malaya wa Dar es salaam uliye kubuhu, naomba iwe mwanzo na mwisho kuzungumza na Enock umesha nielewa, Enock ni mume wangu mtarajiwa, tunaenda kufunga ndoa kama keshakudanganya atakuoa sahau! Tena sahau, UMKOME Malaya wewe, sijamaliza kukwambia kitu kingine, nimesha zaa nae watoto wawili tayari najua kakuficha”

Naomi alizidi kutoa maneno machafu na kumfanya Catherine aumie moyoni mwake hakika yalikua ni maneno makali sana yenye uzito mno, alijikuta anashindwa kuvumilia na kuanza kububujikwa na machozi yaliyofanya mashavu yake yalowane..

Enock na Catherine walisha patana tayari na kurudiana, sasa hivi ni mtu na mpenzi wake ndoa ndiyo iliyokua ikisubiriwa, historia fupi yenye kusisimua waliyopitia katika maisha yao ndiyo iliyowaunganisha, hata wewe ungeisikia ungewaonea sana huruma visa vingi sana vilijitokeza miaka michache iliyopita katika mahusiano yao na mikasa vile vile mpaka walipofikia siku hiyo!

Hata Enock kuchukiana na Baba yake mzazi mzee Mwasha na kupigana risasi kisa mwanamke huyo mrembo ambaye alikua tishio mbele ya macho ya wanaume,ingawa walipatana ila kikwazo kilikua ni kimoja tu mwanamke aliyeitwa Naomi ambaye alikua ni mchumba wake na Enock, alimpata kutokana na kudhani wenda Catherine alifariki katika vita na fujo zilizotokea nchini Kongo, alidiriki kufanya mauaji na kumuuwa mwanamke Heather kisa yeye aolewe na tajiri Enock aliyetoka ng’ambo.

Mambo yanakua magumu tena baada ya Catherine kutokea na ndoto zake kuzimika kama mshumaa, hapo ndipo alipo funga safari Mpaka tabata Bima na kuanza kumtukana Catherine mbele ya Mama yake mzazi.

“umenisikia Malaya,umkome sawa!”

Alizidi kuropoka Naomi

“Lakini binti mbona una kua sio mstaarabu, unakuja kwa watu na kuanza kutoa kauli chafu”
Alidakia Mama Catherine

“Mama tafadhali, naomba umkanye mwanao mimi naenda ila akiendelea kitakachompata tusije tukalaumiana kabisa hapo baadaye, nadhani nimeeleweka mkanye mwanao”

Alimaliza Naomi na kuondoka zake. Catherine alibaki akilia machozi asijue cha kufanya matusi aliyo tukanwa hakika yalikua mazito sana mama yake ndiye pekee aliyeenda na kumbembeleza ili asiendelee kulia,

KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)